Zama za Shaba

Zama za Shaba (kwa Kiingereza bronze age) kilikuwa kipindi cha historia ambacho watu walitengeneza vifaa vyao kwa kutumia metali ya shaba na baadaye bronzi yenye mchanganyiko wa metali mbili: vipande tisa vya shaba kwa kipande kimoja cha stani.

Malighafi nyingine, kama mbao na mawe, zilikuwa zikitumika pia kwa zana, lakini shaba ilikuwa nzuri zaidi kwa kukatia na kuchongea, na ilikuwa rahisi sana kuitengenezea umbo la kitu.

Zama hizo za Shaba hazikutokea wakati mmoja kila mahali, kwa sababu makundi tofauti ya watu walianza kutumia shaba kwa vipindi tofauti kabisa. Kwa mfano, Ulaya Magharibi Zama za Shaba ziliisha kunako miaka ya 2000 KK hadi 800 KK. Kumbe upande wa Mashariki ya Kati zilianza takriban miaka elfu moja nyuma.

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zama za Shaba kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Urnenfelder panoply
Moja ya silaha za kawaida za shaba wakati wa Zama za Shaba.
Collier de Penne
Zama za Shaba - Muséum de Toulouse, Ufaransa.
Bangili

Bangili ni pambo la mviringo linalovaliwa mkononi.

Linaweza kuwa la kawaida au la thamani sana.

Kuna ushahidi kwamba lilitumika tangu zama za shaba (kabla ya mwaka 5000 KK).

Erzgebirge

Erzgebirge (jer. tamka erts-ge-bir-ge, milima ya madini, Kicheki Krušné hory) ni safu ya milima iliyopo mpakani wa Ujerumani na Ucheki yenye urefu wa kilomita 150. Upande wa Ujerumani iko katika jimbo la Saksonia, upande wa Ucheki mpakanni wa Bohemia.

Jina latokana na madini yaliyochimbwa katika milima hii hasa fedha kuanzia zama za shaba. Wakati wa karne za kati eneo hili ilikuwa chanzo muhimu cha fedha na pesa ya "Taler" (iliyoitwa "dollar" kwa Kiingereza) ilianzishwa hapa. Tangu karne ya 19 umuhimu wa mogodi imeendelea kupungua.

Milima ya juu ni Klínovec (jer.: Keilberg) yenye kimo cha mita 1,244 na Fichtelberg yenye kimo cha mita 1,215.

Historia ya awali

Historia ya awali ni kipindi kirefu sana cha historia, kikichukua miaka yote tangu binadamu walipotokea duniani mpaka historia andishi ilipoanza (huko Mesopotamia miaka 3,300 hivi KK).Ingawa muda ni mrefu sana na ni wa msingi kwa historia yote iliyofuata, watu hawakuwa wengi kama walivyozidi kuwa kadiri ya maendeleo yao. Maisha yao hayakuwa marefu kutokana na ugumu wa mazingira na utovu wa vifaa na dawa mbalimbali.

Makala za msingi - orodha ya meta Feb 2008

Hii ni tafsiri ya orodha ya Kiingereza ya makala 1,000 za msingi kutoka meta:wikipedia ya Februari 2008.

Sasa (2019) idadi kubwa imetafsiriwa, pia orodha imebadilishwa mara kadhaa. Mapengo ya sasa ni machache, kwenye Septemba 2019 ni yafuatayo: , physical chemistry , conservation of energy , classical mechanics , strong interaction , weak interaction , quantum mechanics , general relativity , mathematical analysis , differential equation , numerical analysis , function , infinity , mathematical proof , set theory , capacitor , inductor , operating system , programming language , Giza Pyramids , video game , Brussels

Pamoja na haya ya juu, inafaa tuangalie sasa orodha ya orodha ya makala 10,000 za msingi kutoka meta:wikipedia. Hapo tumeshapata karibu makala 400, lakini bado kidogo zaidi ya 6,000 zinakosekana. Hata kama si kila mmoja ni mada ya kuvutia sana, bado makala hizi ni kihunzi cha elimu ya msingi! Karibuni kuchangia. Wanaopenda jiografia, basi mtumie orodha ya sehemu yake iliyoswahilishwa kisehemu Mtumiaji:Kipala/10000_list_Geography na jitahidini kumaliza maneno mekundu. Kipala (majadiliano) 22:25, 21 Septemba 2019 (UTC)

Mohenjo-Daro

Mohenjo-Daro ilikuwa mji mkubwa katika utamaduni wa kale wa Harappa kwenye Bonde la Mto Indus. Iko katika jimbo la Sindh, Pakistan ya leo.

Mji ulijengwa mnamo mwaka 2600 KK na kuwa kati ya miji ya kwanza duniani inayojulikana. Mohenjo-Daro ilistawi wakati huohuo kama tamaduni za Misri ya Kale na Mesopotamia.

Mabaki ya mji yamepokewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO.

Ufuaji metali

Ufuaji metali (ing. metallurgy) inamaanisha jumla ya mbinu za kushughulikia metali na elimu yake. Inahusika pia na aloi ambazo ni mchanganyiko wa metali mbalimbali.

Ufuaji metali inaanza kwenye kushuhulikia mtapo yaani mawe yenye madini ya metali na namna ya kutoa metali katika mtapo.

Halafu inaangalia namna ya kuchanganya na kuunganisha metali mbalimbali kuwa aloi na tabia zake.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.