Zama za Mawe

Zama za Mawe zilikuwa kipindi kirefu cha historia ya kale ya binadamu. Watu walitumia vifaa vya mawe kwa shughuli zao za kila siku.

Kärnyxa av flinta, Nordisk familjebok
Mawe yaliyochongwa kuwa na kona kali kwa matumizi kama kisu.
Canto tallado talando un arbol
Mtu wa zama za mawe akikata mti.

Utamaduni wa watu kwenye chanzo cha zama za mawe

Mwanzoni watu walidumisha maisha yao kwa kukusanya matunda, mizizi na kuwinda wanyama.

Kwa umbile na akili yake binadamu ana uwezo wa kuwinda wanyama wakubwa kama chakula na kutumia ngozi yao kama mavazi ya kujikinga dhidi ya baridi.

Lakini meno na makucha yake hayafai kupasua ngozi ya mnyama mkubwa au kukata nyama yake vipande-vipande akitaka kubeba windo hadi mahali penye familia yake. Vilevile makucha hayafai sana kuchimba mizizi kwa chakula.

Hapo binadamu aliweza kutumia vitu vinavyopatikana kiasili katika mazingira: jiwe lenye kona kali, tawi la mti lenye ncha kali pamoja na vipande vya mifupa. Hivyo vyote vilisaidia shughuli za kuchimba, kupasua na kukata.[1]

Kuna mabaki mengi ya mawe yaliyochongwa kwa matumizi kama vifaa na mabaki hayo yamekuwa msingi wa jina "zama za mawe". Vifaa hivyo na mabadiliko yake vinaonyesha maendeleo katika maisha ya binadamu na kuongezeka kwa uwezo wake wa kupambana na mazingira yake.

Kwa hiyo ni kipindi cha matumizi ya mawe yaliyochongwa kuwa vifaa baada ya kipindi ambako watu walitumia fimbo tu au mawe katika hali asilia na kabla ya kipindi ambapo watu walielewa namna ya kutumia metali.

Canto tallado 1-Guelmim-Es Semara
Kifaa cha mawe sahili - zama za mawe ya kale
Biface Cintegabelle MHNT PRE 2009.0.201.1 V2
Shoka la mkononi - bapa pande mbili (mwishoni mwa Zama za mawe ya kale) - inaonyeshwa kutoka mitazamo mbalimbali

Vipindi vya zama za mawe

Wataalamu wa akiolojia wametambua ya kwamba vifaa vya mawe vinaonyesha tabia tofautitofauti.

 • Kuna vifaa sahili sana kama jiwe lililogongwa mara moja ili kipande kivunjike na ncha kali ipatikane.
 • Kuna pia vifaa vya mawe vinavyoonyesha maendeleo zaidi; vilifanyiwa kazi kwa siku kadhaa kiangalifu ili kunyoshwa, kung'arishwa na kutobolewa kwa kuweka pini.

Kutokana na tofauti kubwa katika hali ya vifaa vya mawe wataalamu wanaona ya kwamba wanaonyesha historia ndefu ya maendeleo ya teknolojia ya kushughulikia jiwe ambako watu walianza kwa vifaa sahili na kuendelea kujifunza zaidi na kuboresha matokeo ya juhudi zao.

Kwa hiyo wataalamu wengi wanatofautisha:

 • Zama za mawe za kale (pia: Zama za mwanzo za mawe)
 • Zama za mawe za kati (pia: Zama za kati za mawe)
 • Zama za mawe za mwisho (pia: Zama za mwisho za mawe)

Si tofauti katika ubora wa vifaa pekee, lakini kuna pia dalili nyingine zinazoonyesha ya kwamba watu walibadilisha maisha yao, namna ya kujipatia chakula na makazi.

Kila mtu aliweza kugonga jiwe dhidi ya jiwe hadi ncha kali ilipatikana. Lakini mashoka ya mawe yaliyohitaji siku za kazi makinifu yanaonyesha kuwepo kwa jamii iliyokuwa na mafundi wa pekee walioweza kunyosha ufundi wao wakilishwa na wengine ni pia dalili ya biashara iliyofanywa hasa tukikuta vifaa vya jiwe fulani katika maeneo ambako jiwe hili halipatikani kiasili.

Pamoja na matokeo mengine ya utafiti wa akolojia, kama vile mabaki ya makaburi, vyombo vya ufinyanzi, nyumba na vifaa vingine, wataalamu waliweza kupata picha ya undani zaidi kuhusu maisha na jamii ya watu wa zamani zile.

Levallois Preferencial-Animation
Teknolojia ya kupunguza jiwe hadi kupata kisu chembamba - zama za mawe ya kati (Levallois)
Mesa Verde spear and knife
Matumizi ya ncha ya jiwe kwenye mkuki

Vifaa vya mawe

Zama za mawe ya kale

Vifaa vya kwanza vilikuwa mawe yaliyokatwa upande mmoja ili kuwa na kona kali moja. Hatuwezi kujua kwa uhakika tukiona jiwe la aina hii kama kama ilikuwa tokeo la mgongano wa mawe katika mkondo wa maji mtoni au kutokana na kuanguka kwa jiwe kutoka mlimani au kama jiwe limepigwa kwa kusudi kwa jiwe lingine kwa shabaha ya kupata kona kali. Lakini mawe haya yalifaa kutumiwa kwa kukata pia si vigumu kuvitengeneza.

Mifano ya kale kabisa ya mawe yaliyogongwa kwa mawe mengine kwa kusudi la kupata kona kali zimepatikana katika eneo la ziwa Turkana (leo nchini Kenya) yalitegenezwa miaka milioni 3.3 iliyopita[2].

Ngazi iliyofuata ni mawe yaliyofanyiwa kazi zaidi hadi kuwa "shoka la mkononi". Hapo jiwe la kufaa lilipigwa na kupunguzwa pande zote mbili hadi kuwa na bapa pande mbili. Sehemu ya juu ilibaki bila ukali kwa kuishikilia mkononi. Kuna mahali ambako mabaki mengi ya mashoka haya ya mkononi yamepatikana katika hali mbalimbali: mawe yaliyopigwa kiasi, mawe yaliyovunjika vibaya na kutupwa, vipande vidogo vilivyopasuliwa wakati wa kuipa shoka umbo lake na kadhalika. Mahali pale panatazamwa kama karakana au viwanda vya kutengeneza vifaa vya mawe. Mahali mashuhuri katika Afrika ya Mashariki ni bonde la Isimila (karibu na Iringa, Tanzania ya leo).

Zama za mawe ya kati

Kipindi hiki kinatazamwa kilianza miaka 300,000 iliyopita na kudumu hadi miaka 25,000 - 50,000 [3] iliyopita.

Museum Quintana - Neolithische Sichel
Mabamba makali ya mawe yamefungwa katika ubao wa mundu ya kukatia majani au mazao

Kipindi hiki kinaonyesha maendeleo ya teknolojia. Watu walianza kutumia pia vipande vidogo vikali vilivyopatikana wakati wa kupunguza jiwe. Vibanzi vikali vya mawe vilifungwa sasa kwenye pini ya ubao kwa gundi la miti. Kwa njia hii vifaa kama kisu, chusa au mundu vilipatikana. [4]

Matatizo ya lugha ya "zama za mawe"

Zama za mawe zilikuwa vipindi virefu sana cha miaka elfu nyingi. Wataalamu wamegawanya zama hizi kwa vipindi mbalimbali kama Zama za mawe za kale na Zama za mawe za kati. Tofauti hizi zinaonekana kutokana na lakini wataalamu wa siku hizi wanaona ya kwamba mgawanyo huu ulitazama zaidi historia ya Ulaya isiyolingana na historia ya sehemu nyingine za dunia.

Tatizo kuu la mafundisho ni ya kwamba ni kipindi cha teknolojia bila kuangalia pande nyingine za maendeleo ya kibinadamu.

Kwa mfano chuma haikutumiwa huko Amerika hadi karne ya 16 na huko Pasifiki hadi karne ya 17. Hata hivyo jamii za Amerika kama Azteki au Wainka walikuwa na teknolojia nyingine mbalimbali na waliweza kudumisha miji mikubwa kushinda miji ya Ulaya ya wakati ule.

Hata hivyo lugha ya "zama za mawe" imekuwa kawaida duniani na wataalamu wanaendelea kuitumia wakijua kasoro zake kwa sababu hadi hasa hakuna mawazo ya kufaa zaidi.

Canto tallado 2-Guelmim-Es Semara

Kifaa cha jiwe - awamu ya kwanza

Flint hand axe

Shoka la mkononi

Obsidienne biface ethiopie

Shoka la mkononi hali ya juu - kutoka Ethiopia

Agarre de un bifaz

Matumizi ya shoka la mkononi

Haches pierre polie

Mashoka ya mawe yaliyonyoshwa - awamu za baadaye

Museum Pachten, SteinAxt1

Shoka la mawe lenye shimo la pini

Marejeo

 1. Uwezo wa kutumia vitu kama fimbo kama kifaa cha kujipatia chakula umetazamwa pia kwa wanyama kadhaa, kwa mfano ndege na sokwe - linganisha Sokwe wanatengeneza na kutumia vifaa na Matumizi ya vifaa na ndege.
 2. 3.3-million-year-old stone tools from Lomekwi 3, West Turkana, Kenya, katika jarida la Nature 21 May 2015
 3. Katika eneo kubwa la bara Afrika maendeleo yalikuwa tofauti kati ya sehemu mbalimbali. Pamoja na makadirio ya umri ya vifaa vya kale sana hii ni elezo kwa kutaja mwisho wa kipindi hiki kuwa na tofauti ya miaka mielfu kwa bara la Afrika.
 4. • McBrearty, Sally and Alison A. Brooks. 2000. "The revolution that wasn't: A new interpretation of the origin of modern human behaviour" Journal of Human Evolution 39:453–563.

Kujisomea

 • Barham, Lawrence (2008). The First Africans: African Archaeology from the Earliest Toolmakers to Most Recent Foragers, Cambridge World Archaeology. Oxford: Oxford University Press.
 • Belmaker, Miriam (March 2006). Community Structure through Time: 'Ubeidiya, a Lower Pleistocene Site as a Case Study (Thesis). Paleoanthropology Society.
 • Clark, J. Desmond (1970). The Prehistory of Africa, Ancient People and Places, Volume 72. New York; Washington: Praeger Publishers.
 • Deacon, Hilary John (1999). Human beginnings in South Africa: uncovering the secrets of the Stone Age. Walnut Creek, Calif. [u.a.]: Altamira Press.
 • Piccolo, Salvatore (2013). Ancient Stones: The Prehistoric Dolmens of Sicily. Abingdon (UK): Brazen Head Publishing.
 • Rogers, Michael J. (2009). Sourcebook of paleolithic transitions: methods, theories, and interpretations. New York: Springer.
 • Schick, Kathy D.; Nicholas Toth (1993). Making Silent Stones Speak: Human Evolution and the Dawn of Technology. New York: Simon & Schuster. ISBN 0-671-69371-9.
 • Shea, John J. (2010). Out of Africa I: the First Hominin Colonization of Eurasia. Dordrecht; Heidelberg; London; New York: Springer, 47–64.
 • Scarre, Christopher (ed.) (1988). Past Worlds: The Times Atlas of Archaeology. London: Times Books. ISBN 0-7230-0306-8.

Viungo vya Nje

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zama za Mawe kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Bronzi

Bronzi (pia: shaba nyeusi) ni aloi ya metali. Kiasi kikubwa ndani yake ni shaba (70-90%) na metali nyingine ndani yake ni stani (takriban 10-30%).

Cape Town

Cape Town (yaani "Mji wa rasi", kwa Kiafrikaans: Kaapstad; kwa Kixhosa: iKapa) ni mji mkubwa wa tatu wa Afrika Kusini na mmoja kati ya miji mikuu mitatu ya nchi ikiwa ni makao ya Bunge. Pia ni mji mkuu wa jimbo la Rasi Magharibi (Western Cape / Wes-Kaap). Ni sehemu ya Jiji la Cape Town. Eneo lake ni km² 1,644 lenye wakazi 2,375,910 (mwaka 2005).

Jina la mji limetokana na Rasi ya Tumaini Jema iliyoko karibu na mji upande wa kusini.

Chusa

Chusa ni kifaa kirefu chenye umbo la mkuki kinachotumiwa kwa shughuli za uvuwi na uwindaji wa wanyama wa maji.

Mara nyingi chusa imefungwa kwa kamba inayoruhusu mvuwi kuirudisha pamoja na windo.

Ncha za chusa za samaki kwa kawaida huwa na vipembe vikali vidogo vya kuelekea nyuma. Hivi vinaingia ndani ya mwili wa windo na kuizuia isitoroke.

Chusa zilipatikana tangu zama za mawe. Zamani na kimapokeo zilitengenezwa mara nyingi kwa kutumia ubao au mifupa iliyokatwakatwa kwa kupata vipembe vya kuelekea nyuma. Siku hizi ncha ni za metali.

Chusa zilitumiwa pia kama silaha. Katika michezo ya Roma ya Kale kulikiwa na magladiator walioitwa "wavuwi" waliotumia nyavu na chusa kama silaha zao.

Chusa katika historia

Hifadhi ya Katavi

Hifadhi ya Katavi ni moja ya hifadhi za taifa iliyoundwa mwaka 1974.

Iko juu ya uwanda mpana wa mafuriko magharibi mwa Tanzania katika mkoa wa Katavi na mkoa wa Rukwa. Hifadhi hiyo inazo takribani kilomita za mraba 4,471 (maili za mraba 1,726) katika eneo hilo, ambayo inakuwa ni hifadhi ya tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.

Ni hifadhi ya mbali sana ambayo hutembelewa mara kwa mara kuliko viwanja vingine vya Tanzania. Hifadhi hiyo inahusisha mto Katuma na msimu wa Ziwa Katavi na Ziwa Chada.

Historia ya awali

Historia ya awali ni kipindi kirefu sana cha historia, kikichukua miaka yote tangu binadamu walipotokea duniani mpaka historia andishi ilipoanza (huko Mesopotamia miaka 3,300 hivi KK).Ingawa muda ni mrefu sana na ni wa msingi kwa historia yote iliyofuata, watu hawakuwa wengi kama walivyozidi kuwa kadiri ya maendeleo yao. Maisha yao hayakuwa marefu kutokana na ugumu wa mazingira na utovu wa vifaa na dawa mbalimbali.

Historia ya teknolojia

Historia ya teknolojia ni historia ya ubunifu wa vifaa na mbinu za kutumia vifaa hivi katika uzalishaji wa mahitaji, bidhaa na huduma katika jamii.

Kuna mbinu mbalimbali kupanga historia hii na kutambua ngazi za maendeleo ndani yake.

Isimila

Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania, katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Njia ya kuingia si rahisi kuikuta: ukitokea Iringa iko kabla ya kufikia Tanangozi, upande wa kushoto.

Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa wa Iringa.

Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za Mawe za Kale. Ni katika eneo hilo ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa tangu mwaka 1951.

Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila, ambalo lina mikondo miwili, ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji. Korongo la pembeni lina mmomonyoko wa ardhi ulioacha nguzo za ajabu.

Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zana nyingine na shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.

Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana; kati yake ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na ya twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina tofauti ya viboko.

Kisu

Kisu (maana yake "msu mdogo"; wingi: visu) ni kifaa cha kukata chenye bapa ambalo ni kali angalau upande moja. Kwa kawaida kuna sehemu mbili: bapa kali na shikilio. Siku hizi bapa imetengenezwa kwa metali na shikilio la ubao au plastiki.

Misri

Misri (kwa Kiarabu: مصر, Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki ikiwa na eneo la Rasi ya Sinai kwenye bara la Asia pia.

Ni nchi yenye wakazi milioni 90 na mji mkuu Kairo ni kati ya miji mikubwa zaidi duniani.

Ni kati ya nchi za dunia zenye historia ndefu inayojulikana.

Msalaba

Msalaba ni ishara inayotokana na mistari miwili kukutana katikati yake.

Hiyo ni mojawapo kati ya ishara maarufu na ya zamani zaidi duniani kote, katika sanaa, utamaduni na dini, hasa Ukristo unaoheshimu kama ukumbusho wa kifodini cha mwanzilishi wake, Yesu Kristo, aliyekufa kwa njia ya usulubisho.

Msalaba ulikwishatumiwa na Wakristo wa kale sana. Mwanzoni mwa karne ya 3 Tertullianus, katika kitabu "De Corona", alisema kwamba walikuwa na desturi ya kujifanyia ishara hiyo katika paji la uso.

Lakini alama ya msalaba au za kufanana na msalaba zinapatikana pia katika tamaduni mbalimbali tangu kale bila uhusiano wowote na Ukristo.

Misalaba iliyotumiwa kwa adhabu ya mauti iliweza kuwa na maumbo mbalimbali, hata kuwa ubao mmoja tu bila mikono ya kando.

Mseke

Mseke ni jina la kata ya Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51204. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,868 waishio humo.Mseke ina vijiji vya Tanangozi, Wenda, Sadani, Ugwachanya, Makota na Kaning'ombe. Huko Ugwachanya kuna eneo la kihistoria la Isimila penye mabaki mengi ya karahana za kutengeneza zana za mawe wakati wa Zama za Mawe.

Mundu

Mundu ni kifaa kinachotumiwa katika kilimo kwa kukata nyasi na mavuno ya nafaka na mazao mengine.

Mundu kama zana ya kilimo inajulikana tangu zama za mawe.

Katika nchi nyingi za dunia haitumiwi tena sana kwa sababu nafasi yake imechukuliwa na mashine lakini pale ambako kazi ya kilimo inatekelezwa kwa mkono ni mahali pake hadi leo.

Umbo la mundu ni kama kisu kirefu kilichopindwa kama kotama ndefu. Upande wa ndani ya bapa ni kali, upande wa nje ahuna ukali.

Umbo la mundu lilitumiwa pia kama silaha kwa aina za pekee za upanga.

Katika nembo la Austria na pia la Umoja wa Kisovyeti wa zamani mundu ni alama ya wakulima ikionyeshwa pamoja na nyundo kama alama ya wafanyakazi.

Mwamba (jiolojia)

Mwamba katika jiolojia ni namna ya kutaja mawe au zaidi mchanganyiko au mkusanyiko wa mabao ya aina moja au zaidi ya madini ulio imara katika hali asilia. Jiwe ni kipande cha mwamba.

Takriban madini 30 hufanya sehemu kubwa ya miamba ya dunia, ni hasa silikati na kabonati.

Nepal

Nepal ni nchi ya Asia ya Kusini kwenye milima ya Himalaya inayopakana na Uhindi na China.

Mlima Everest ambao ni mlima mkubwa kuliko yote duniani uko Nepal.

Mji mkuu ni Kathmandu.

Ramani ya nyota

Ramani ya nyota ni ramani inayoonyesha nyota zinazoonekana kwenye anga wakati wa usiku. Mkusanyiko wa ramani za nyota katika kitabu kimoja huitwa atlasi ya nyota.

Ramani za nyota za zamani zilionyesha mara nyingi maumbo ya kundinyota jinsi zilivyowazwa katika mitholojia ya mataifa.

Siku hizi ramani za nyota zinapatikana pia kama programu za kompyuta na katika intaneti.

Ramani za nyota zimehifadhiwa katika majengo ya Misri ya Kale tangu zamani, labda pia tangu Zama za Mawe.

Shaba

Shaba au shaba nyekundu (pia: Kupri au Cupri kama jina la kisayansi) ni elementi yenye namba atomia 29 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 65.54. Alama yake ni CU.

Katika mazingira ya kawaida ni metali yenye rangi kahawia nyekundu. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1,083 C°.

Ni kati ya metali za kwanza wanadamu walitumia baada ya kutoka katika zama za mawe. Si metali ngumu zana hivyo ilikuwa nyepesi ya kushughulikia kwa wanadamu wa kale.

Ikichanganywa na stani kunatokea aloi ya bronzi ambayo ni ngumu zaidi. Aloi nyingine ni shaba nyeupe, mchanganyo wa shaba nyekundu na zinki.

Wakati mwingine shaba hupatikana kama metali tupu lakini mara nyingi zaidi kama mtapo.

Tabia muhimu ya shaba ni uwezo wake wa kupitisha umeme. Hivyo imekuwa msingi wa teknolojia yote ya umeme hasa nyaya za kila aina.

Siku hizi shaba huchimbwa hasa katika nchi za Chile (Chuquicamata), Marekani, Urusi, Afrika ya Kati ("Copperbelt" - kanda la shaba), Congo-Zaire, Zambia, Kanada na Peru.

Silaha

Silaha ni kifaa cha upiganaji dhidi ya wanadamu au wanyama.

Inafaa kumtisha, kumwumiza au kumwua adui au kumletea hasara nyingine inayokusudiwa.

Kusudi la silaha ni matumizi

dhidi wanyama: uwindaji

dhidi ya watu: ama utetezi dhidi ya shambulio au shambulio lenyewe kwenye vita, jinai au fitina

ya kijamii: katika michezo (mashindano ya kufyatulia pinde au bunduki), kama sifa ya cheo au utamaduniKatika historia watu wameweka nguvu nyingi katika maendeleo ya silaha. Kila sayansi na kila teknolojia huangaliwa na watu kwa faida yake katika utengenezaji wa silaha.

Silaha zimepatikana tangu zama za mawe. Upanga, pinde na mshale pamoja na mikuki zilikuwa silaha kwa milenia nyingi lakini ziliboreshwa tena na tena.

Tangu nyakati za kati silaha za moto zilianza kuenea duniani na kuboreka. Bunduki, mzinga na bombomu zilibadilisha uso wa vita. Karne ya 20 iliongeza vifaru na ndege za vita pamoja na viumbe vya sayansi ya kisasa kama silaha za nyuklia.

Usindikaji wa samaki

Usindikaji wa samaki ni mchakato unaohusiana na samaki na bidhaa za samaki wakati hupatikana au kuvunwa halafu hutolewa kwa wateja.

Ingawa neno hilo linamaanisha hasa samaki, kwa mazoea hupanuliwa kuhusisha viumbehai wa majini ambao pia kuvuna kwa madhumuni ya biashara, ikiwa wamepatikana katika uvuvi wa mwitu au kuvunwa kutoka kilimo cha samaki.

Makampuni makubwa ya usindikaji samaki mara nyingi hufanya kazi zao za uvuvi au shughuli za kilimo. Samaki huharibika haraka sana. Shida kuu ya usindikaji wa samaki ni kuzuia samaki kuharibika, na hii inabakia kuwa na wasiwasi mkubwa wakati wa shughuli nyingine za usindikaji.

Usindikaji wa samaki unaweza kugawanywa katika utunzaji wa samaki, ambao ni usindikaji wa awali wa samaki ghafi, na utengenezaji wa bidhaa za samaki.

Mgawanyiko mwingine wa asili ni katika usindikaji wa msingi unaohusishwa na uchujaji na kufungia samaki safi kwa usambazaji katika maduka ya rejareja, na usindikaji wa sekondari unaozalisha bidhaa zilizohifadhiwa katika makopo kwa ajili ya biashara ya rejareja na upishi.

Kuna ushahidi kwamba binadamu wamekuwa wakifanya usindikaji wa samaki tangu zama za mawe.

Xi'an

Xi'an ni makao makuu ya Mkoa wa Shaanxi nchini China. Kwenye mwaka 2011 ilikuwa na wakazi milioni 6. Jiji hilo ni maarufu kwa Jeshi la Matofali lililopatikana ndani ya kaburi la kaisari wa kwanza wa China Qin Shi Huang.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.