Yerusalemu

Yerusalemu (mara kwa mara pia Kudisi) (kwa Kiebrania ירושלים, Yerushalayim, kwa Kiarabu: القدس, al-Quds) ni mji wa Mashariki ya Kati wenye pande mbili. Kwa upande mmoja ni mji mkuu wa Israel. Kwa upande mwingine Yerusalemu ya mashariki inatazamiwa kuwa mji mkuu wa Palestina, ingawa imetawaliwa na Israel pia tangu 1967. Israel imetangaza tangu mwaka 1980 Yerusalemu yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi za dunia hazikubali azimio hilo, hivyo balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Yerusalemu.

Yerusalemu ina historia ndefu sana.

Yerusalemu
Jerusalem Dome of the rock BW 13

Ukuta wa Maombolezo na Kuba ya Mwamba mjini Yerusalemu
Emblem of Jerusalem
Seal
Flag of Jerusalem
Flag
Jina la Kiebrania יְרוּשָׁלַיִם (Yerushalayim)
Jina la Kiarabu القـُدْس (al-quds);
rasmi: أورشليم القدس
(urshalim-al-quds)
Maana ya Jina Kiebrania: "Urithi wa amani",
Kiarabu: "(Mji) mtakatifu"
Utawala Mji
Wilaya
Wakazi 801,000 (Wayahudi 68%, Waislamu 30%, Wakristo 2%) (2011)
Eneo 126,000  (126 km²)
Meya Zaki al-Ghul
Nir Barkat
Tovuti rasmi www.jerusalem.muni.il

Yerusalemu katika dini

Ni mji muhimu katika dini tatu zinazofuata imani ya Abrahamu, yaani Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Marejeo

  • Cheshin, Amir S.; Bill Hutman and Avi Melamed (1999). Separate and Unequal: the Inside Story of Israeli Rule in East Jerusalem Harvard University Press ISBN 978-0-674-80136-3
  • Cline, Eric (2004) Jerusalem Besieged: From Ancient Canaan to Modern Israel. Ann Arbor: University of Michigan Press ISBN 0-472-11313-5.
  • Collins, Larry, and La Pierre, Dominique (1988). O Jerusalem!. New York: Simon and Schuster ISBN 0-671-66241-4
  • Gold, Dore (2007) The Fight for Jerusalem: Radical Islam, The West, and the Future of the Holy City. International Publishing Company J-M, Ltd. ISBN 978-1-59698-029-7
  • Köchler, Hans (1981) The Legal Aspects of the Palestine Problem with Special Regard to the Question of Jerusalem Vienna: Braumüller ISBN 3-7003-0278-9
  • The Holy Cities: Jerusalem produced by Danae Film Production, distributed by HDH Communications; 2006
  • Wasserstein, Bernard (2002) Divided Jerusalem: The Struggle for the Holy City New Haven and London: Yale University Press. ISBN 0-300-09730-1
  • "Keys to Jerusalem: A Brief Overview", The Royal Islamic Strategic Studies Center, Amman, Jordan, 2010. http://www.rissc.jo/docs/J101-10-10-10.pdf
  • Sebag Montefiore, Simon (2011) Jerusalem: The Biography, London: Weidenfeld and Nicolson, ISBN 978-0-297-85265-0
  • Young, Robb A (2012) Hezekiah in History and Tradition Brill Global Oriental Hotei Publishing, Netherlands

Viungo vya nje

Serikali

Historia

Elimu

Ramani

Dini

BlankAsia Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Yerusalemu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Hekalu la Yerusalemu

Hekalu la Yerusalemu lilikuwa kitovu cha ibada za dini ya Uyahudi wakati wa Israeli ya Kale.

Kwa jumla kulikuwa na majengo mawili yaliyofuatana kwenye mlima wa hekalu mjini Yerusalemu.

Imani ya Kiyahudi inategemea kujengwa kwa hekalu la tatu pamoja na kuja kwa Masiya wakati ujao.

Katika imani hiyo sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu ndani ya hekalu ilikuwa mahali ambapo Mungu mwenyewe aligusa dunia.

Hija

Hija (kutoka Kiarabu حج, Ḥaǧǧ) ni ziara ya kidini yaani ni safari inayofanyika kwa sababu ya dini, ikilenga patakatifu fulani.

Kwa maana ya kiroho, maisha yote ni safari ya kumuelekea Mungu au uzima wa milele n.k.

Sababu ya kwenda mahali maalumu ni tumaini la kuwa karibu zaidi na imani mahali ambako mambo muhimu ya historia ya dini husika yalitokea; mara nyingi pia imani ya kwamba sala itakuwa na nguvu au mafanikio zaidi pale.

Desturi ya kuhiji iko katika dini mbalimbali.

Wahindu huhiji mahali pengi hasa mji wa Benares na mto Ganges.

Uyahudi tangu zamani unatia maanani hasa hija ya kwenda Yerusalemu, iliyokuwa ya lazima katika sikukuu mbalimbali kwa waumini kuanzia umri wa kubalehe; unaendelea hata baada ya hekalu la mji huo kubomolewa kabisa mwaka 70 BK.

Wakristo hasa wa madhehebu ya Kiorthodoksi na Katoliki wanajua hija kwenda Yerusalemu, Roma na mahali pengine.

Waislamu huwa na hajj kutembelea Makka, Washia wanatembela pia makaburi ya maimamu wao huko Najaf, Karbala, Mashhad na penginepo. Mwislamu aliyetimiza safari hii anapokea cheo cha "alhaji" kama sehemu ya jina lake.

Historia ya Wokovu

Kwa jina hilo Wakristo wanamaanisha ufafanuzi wa mpango wa kazi ya Mungu kwa wokovu wa binadamu kadiri ya Biblia.

Israel

Kwa maana mbalimbali za jina Israeli katika Biblia tazama Israeli (maana)

Israel (kwa Kiebrania: מדינת ישראל - Medinat Yisra'el; kwa Kiarabu: دَوْلَةْ إِسْرَائِيل - dawlat Isrā'īl) ni nchi ya Mashariki ya Kati kwenye mwambao wa mashariki wa Mediteranea.

Imepakana na Lebanon, Syria, Yordani, Misri na maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya serikali ya Palestina.

Karne ya 10 KK

Karne ya 10 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 1000 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 901 KK.

Karne ya 6 KK

Karne ya 6 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 600 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 501 KK.

Karne ya 7 KK

Karne ya 7 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 700 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 601 KK.

Kitabu cha Ezra

Kitabu cha Ezra kinapatikana katika Biblia ya Kikristo katika Agano la Kale.

Kiasili kiliandikwa kwa lugha ya Kiebrania lakini kuna pia sehemu fupi za Kiaramu.

Andiko la Ezra lilitunzwa katika Biblia ya Kiebrania pamoja na Nehemia kama kitabu kimoja lakini kimegawiwa baadaye kuwa vitabu viwili ambavyo Vulgata inavitaja kama "Esdras I" na "Esdras II".

Kitabu kinasimulia habari za Wayahudi chini ya utawala wa Waajemi.

Mwaka 587 KK mfalme wa Babeli alikuwa amevamia mji wa Yerusalemu, kubomoa hekalu la Sulemani na kumaliza ufalme wa Yuda. Wakazi walipelekwa Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli. Tangu wakati huo Waisraeli kwa kawaida walijulikana kuwa Wayahudi. Lakini, kwa kuwa utengano wa Israeli haukuendelea, majina hayo mawili, pamoja na jina la Waebrania, yaliweza kutumiwa kwa watu walewale (Yer 34:9; Yn 1:19, 47; 2 Kor 11:22; Gal 2:14).

Mwaka 539 KK Waajemi chini ya mfalme Koreshi walivamia Babeli ambayo ikawa jimbo la milki ya Uajemi. Koreshi aliwaruhusu Wayahudi kadhaa warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu.

Habari hizi na zilizofuata zinasimuliwa katika vitabu vya Ezra na Nehemia.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Nehemia

Kitabu cha Nehemia ni kimoja kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Yeremia

Kitabu cha Yeremia ni kimojawapo kati ya vitabu vya kinabii vilivyo virefu zaidi katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania), na kwa hiyo pia katika Agano la Kale ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Masiya

Masiya (au Masiha), kutoka Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ mashiakh, maana yake Mpakwamafuta ni jina la heshima ambalo Biblia inampa mfalme au kuhani aliyewekwa wakfu kwa Mungu kwa kupakwa mafuta atende kwa niaba yake kazi ya kusaidia taifa lake hasa kwa kulikomboa.Tofauti na kawaida, Biblia inamtaja kama Masiha hata mfalme Koreshi Mkuu wa Uajemi kwa sababu Mungu alimtumia kutoa Wayahudi katika uhamisho wa Babeli na kuwaruhusu warudi Yerusalemu na kujenga upya hekaluHata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani

Matendo ya Mitume

Matendo ya Mitume ni kitabu cha Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo chenye sura 28.

Katika orodha ya vitabu 27 vya Agano Jipya kinashika nafasi ya tano baada ya Injili nne.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Msalaba wa Yesu

Msalaba wa Yesu ni msalaba ule ambao Yesu Kristo alisulubiwa juu yake huko Yerusalemu kwa amri ya Ponsyo Pilato siku ya Ijumaa, labda tarehe 7 Aprili 30 BK.

Tukio hilo, pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndiyo kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi.

Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo.

Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa ya Kikristo, hasa uchoraji na uchongaji.

Mtakatifu Paulo

Mtume Paulo (7-67 hivi) ni mmisionari mkuu wa Yesu Kristo katika historia ya Kanisa.

Alitangaza kifo na ufufuko wake katika nchi karibu zote zilizopo kaskazini kwa Bahari ya Kati.

Alimaliza ushuhuda wake kwa Yesu kwa kufia dini yake mjini Roma wakati wa dhuluma iliyoanzishwa na Kaisari Nero.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 29 Juni pamoja na ya Mtume Petro.

Palestina

Palestina (kwa Kiarabu: فلسطين‎ filasṭīn, falasṭīn; kutoka Kilatini: Palaestina; kwa Kiebrania: פלשתינה Palestina) ni jina la eneo lililoko upande wa Mashariki wa Bahari ya Mediteranea kati ya mkingo wa bahari hiyo na mto Yordani.

Sirili wa Yerusalemu

Mtakatifu Sirili wa Yerusalemu (kwa Kigiriki Κύριλλος Α΄ Ἱεροσολύμων) aliishi miaka 315 – 386 au 387. Alikuwa askofu wa mji huo nchini Israeli kuanzia mwaka 348 hadi kifo chake akijihusisha sana na mabishano kuhusu umungu wa Yesu Kristo hata akadhulumiwa na Waario na serikali ya Dola la Roma.

Tangu zamani ametambuliwa kuwa mtakatifu na babu wa Kanisa.

Mwaka 1883 Papa Leo XIII alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 18 Machi.

Upadri

Upadri ni daraja takatifu ya kati ya uongozi wa Kanisa Katoliki na madhehebu mengine kadhaa.

Unatolewa na Askofu kwa kumwekea mtu mikono kichwani na kumuombea ili atoe huduma za kikuhani, hasa kwa kuhubiri rasmi Neno la Mungu, kuadhimisha Ekaristi na sakramenti nyingine na kuongoza jumuia za waamini.

Upadri unatolewa kwa namna ya kudumu, usiweze kurudiwa wala kufutwa.

Shirika la kwanza la Kanisa la Kikristo katika Yerusalemu lilikuwa na wasomi wengi sawa na lile la sinagogi la Uyahudi, lakini lilikuwa na Halmashauri au chuo cha wazee waliowekwa (πρεσβύτεροι, wazee )

Katika Matendo ya Mitume 11:30 na 15: 22 tunaona mfumo wa washirika wa uongozi huko Yerusalemu ingawa unaongozwa na Yakobo Mdogo, askofu wa kwanza wa mji. Katika Matendo 14: 23, Mtume Paulo anaweka wakubwa katika makanisa aliyoanzisha.

Utume wa Yesu

Utume wa Yesu katika Injili, unaanza na ubatizo wake kwa mkono wa Yohane Mbatizaji katika mto Yordani na unakamilika katika mji mtakatifu wa Yerusalemu kwa kifo chake msalabani.Injili ya Luka (3:23) inasema Yesu Kristo alipoanza utume wake alikuwa "na umri wa miaka 30 hivi".Kwa kawaida wataalamu wa Biblia wanakadiria kwamba mwaka wa kubatizwa ulikuwa kati ya 27 na 29 BK na ule wa kuuawa kati ya 30 na 33.Awali Yesu, baada ya kubatizwa na kukaa siku 40 katika jangwa la Yudea, alifanya kazi ya kitume zaidi katika mkoa wa Galilaya, huko alikokulia, akihubiri na kuponya, pamoja na kufukuza pepo wachafu.

Mbali ya hiyo miujiza yake, ni muhimu mwenendo wake wa kukaribiana na watu wa kila aina, bila ubaguzi: tendo lake la kushiriki karamu pamoja na wakosefu lilichukiza wengi, hasa kati ya madhehebu ya Mafarisayo waliokwepa watu hao. Kumbe kwa Yesu lilikuwa dokezo la kwamba Mungu anawaalika wote kutubu na kuingia raha ya ufalme wake.

Wakati huohuo aliita baadhi kumfuata kama wanafunzi katika safari zake. Kati yao aliteua mitume 12 kama mwanzo wa Kanisa lake.Hao aliwaita mitume kwa sababu aliwapeleka kwanza kwa Waisraeli (Math 8) lakini baada ya kufufuka kwa mataifa yote pia (Math 28:16-20).Baada ya kifodini cha Yohane Mbatizaji, Yesu alijiandaa kwenda Yerusalemu kwa mara ya mwisho ili kukamilisha utume wake kwa kujitoa kafara alivyotabiriwa na Yohane: "Huyu ndiye mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu".Safari hiyo ya mwisho ilimchukua tena kwa muda karibu na mahali alipobatizwa.Utume wake wa mwisho mjini Yerusalemu ulianza na tukio la kuingia Yerusalemu kwa shangwe ya Wayahudi walioamini kwamba ndiye Masiya, hasa baada ya muujiza mkuu alioufanya, yaani kumfufua Lazaro wa Bethania kutoka kaburini siku ya nne baada ya kifo. Injili zinasimulia kirefu zaidi habari za hiyo wiki ya mwisho kutokana na umuhimu wake kama kilele cha yote.

Vita za Misalaba

Vita za Misalaba (pia: Vita vya msalaba) vilitokea kati ya mataifa ya Wakristo wa Ulaya na watawala Waislamu wa nchi za Mashariki ya Kati wakati wa karne za 11 hadi 13, hasa kuanzia 1095 hadi 1291 katika jina la dini na kwa baraka za Kanisa Katoliki. Kaisari wa Bizanti aliomba msaada wa Wakristo wa magharibi dhidi ya mashambulio ya Waturuki Waislamu. Hivyo Papa aliwaita mataifa ya Kikatoliki ya Ulaya kuikomboa nchi takatifu. Tangu mwaka 1096 hadi mwaka 1270 kampeni za kijeshi zilianzishwa Ulaya kuelekea Yerusalemu.

Kwa maana nyingine na pana zaidi "vita vya msalaba" vilikuwa jitihada za watawala wa Ulaya kutetea haki za Wakristo wenzao wa nchi hizo, au kujitetea kwa silaha na vita na wakati huohuo kueneza himaya yao pamoja na Ukristo.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.