Yakobo Mkubwa

Yakobo, mwana wa Zebedayo na Salome, na kaka wa Mtume Yohane, alikuwa Myahudi wa karne ya 1 aliyepata kuwa mmoja kati ya Mitume wa Yesu muhimu zaidi.

Anaitwa "Mkubwa" ili kumtofautisha na Mtume mwingine mwenye jina hilohilo, Yakobo Mdogo mwana wa Alfayo.

Carlo Crivelli 064
Carlo Crivelli, Yakobo Mkubwa, 1480 hivi, London, Victoria and Albert Museum.
Mitume wa Yesu
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus

Maisha ya awali

Yakobo pamoja na baba na mdogo wake walikuwa wavuvi huko Kafarnaumu kwenye Ziwa la Galilaya.

Wataalamu kadhaa wanadhani walikuwa pia makuhani.

Wito wa utume

Inakadiriwa alikutana na Yesu mwaka 28.

Pamoja na mdogo wake waliitwa na Yesu Boanerghes ("wanangurumo") kutokana na umotomoto wao kitabia.

Pamoja na mitume wengine waliongozana na Yesu Kristo miaka mitatu hivi, ambapo Yakobo alionekana kuwa karibu sana na Yesu na kuchaguliwa naye kushuhudia matukio kadhaa ya pekee (ufufuo wa binti Yairo, kugeuka sura mlimani, kihoro bustanini).

Baada ya ufufuko wa Yesu

Baada ya kifo na ufufuko wa Yesu, Yakobo alishika nafasi ya maana katika jumuia ya kwanza ya Wakristo wa Yerusalemu.

Mwaka 44 hivi aliuawa na mfalme Herode Agripa I kwa upanga (Matendo ya Mitume 12:1-2), wa kwanza kumfia Yesu kati ya Mitume wake.

Heshima yake

Anaheshimiwa na Wakristo wote kama mtakatifu, hasa tarehe 25 Julai huko Santiago de Compostella (Hispania, ambapo wengi wanaamini aliwahi kufika kiutume).

Tazama pia

Marejeo

  • Thenashara, Mitume Kumi na Wawili – tafsiri ya P. A. Bunju – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Ndanda 1984 – ISBN 9976-63-030-1

Viungo vya nje

Saint-stub-icon.jpg Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yakobo Mkubwa kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
25 Julai

Tarehe 25 Julai ni siku ya 206 ya mwaka (ya 207 katika miaka mirefu). Mpaka uishe zinabaki siku 159.

Binti Yairo

Binti Yairo ni maarufu kama msichana aliyefufuliwa na Yesu Kristo kama inavyosimuliwa na Injili ndugu (Mk 5:21–43; Math 9:18–26; Lk 8:40–56).

Yairo, baba yake, alikuwa amemkimbilia Yesu kwa ajili yake.

Walipofika nyumbani walikuta msiba umeshaanza, lakini Yesu alifukuza waombolezaji, akamfufua mtoto huyo wa miaka 12 mbele ya wazazi wake, Petro, Yakobo Mkubwa na Yohane tu.

Hatimaye aliagiza binti apewe chakula.

Egidi mkaapweke

Egidi mkaapweke (kwa Kifaransa Gilles; 650 hivi – 710 hivi) alikuwa mmonaki Mgiriki kutoka Athens, ingawa habari za maisha yake kiini chake ni mikoa ya Provence na Septimania (leo Ufaransa Kusini).

Kaburi lake huko Saint-Gilles-du-Gard limekuwa kituo muhimu cha hija kutoka Arles kwenda Santiago de Compostela kumhesimu mtume Yakobo Mkubwa.

Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Septemba.

Herode Agripa

'Herode Agripa, kwa Kigiriki 'Ἡρώδης Ἀγρίππας, Herodes Agrippas, (10 KK – 44 BK), alikuwa mfalme wa sehemu kubwa ya Palestina katika karne ya 1 kutoka ukoo wa Herode Mkuu, babu yake .

Baba yake alikuwa Aristobulo IV na mama yake Berenike.Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Marcus Julius Agrippa, ambalo alipewa kwa heshima ya mwanasiasa wa Roma Marcus Vipsanius Agrippa.

Alianza kutawala mwaka 41 BK.

Ndiye anayesemwa katika Matendo ya Mitume (Agano Jipya, Biblia ya Kikristo), hasa kama muuaji wa Yakobo Mkubwa muda mfupi kabla hajafa mwenyewe.

Kumbe mwandishi wa Kiyahudi Yosefu Flavio anamsifu na kumuita "Agripa Mkuu".

Kugeuka sura

Yesu kugeuka sura ni sikukuu ya liturujia ya Ukristo inayoadhimisha fumbo la maisha ya Yesu linalosimuliwa katika Agano Jipya, hususan katika Injili Ndugu (Math 17:1–9, Mk 9:2-8, Lk 9:28–36) na katika 2 Pet 1:16–18.

Humo tunasoma kwamba Yesu aliongozana na wanafunzi wake watatu, Mtume Petro, Yakobo Mkubwa na mdogo wake Mtume Yohane, hadi mlima kwa lengo la kusali faraghani.

Huko usiku alianza kung'aa akatokewa na Musa na Eliya waliozungumza naye kuhusu kufariki kwake Yerusalemu.

Kubwa zaidi, Mungu alimshuhudia kuwa Mwana wake mpenzi akawahimiza wanafunzi hao kumsikiliza.Tukio linaheshimiwa hasa na Ukristo wa Mashariki na wamonaki wanaoliona mwaliko wa kutazama utukufu wa Mungu uliofichama katika malimwengu, kumbe kwa sala unadhihirika kwa macho ya imani.

Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu

Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu inatofautiana kadiri ya waandishi, lakini bila kuvunja umoja wa imani yuu yake kama Kristo na Mwana wa Mungu.

Mitazamo muhimu zaidi ni ile ya Mtume Paulo na Mtume Yohane, ambao ndio wanateolojia hasa, lakini ipo mingine kama ile ya Injili ya Marko, Injili ya Mathayo, Mwinjili Luka, Waraka kwa Waebrania n.k.

Pengine mwandishi yuleyule anatushirikisha mitazamo tofautitofauti katika vitabu vyake, kwa mfano kutokana na maendeleo ya uelewa wake. Hivyo jinsi Yesu Kristo anavyoonekana katika Waraka kwa Waefeso imeendelea kuliko ilivyo katika Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike ulioandikwa na Paulo yuleyule zaidi ya miaka 10 kabla yake.

Kristolojia inakusanya mitazamo hiyo yote na kujitahidi kuelewa zaidi tena fumbo la Kristo.

Mitume wa Yesu

Mtume wa Yesu Kristo (kwa Kigiriki ἀπόστολος, apóstolos, aliyetumwa), kadiri ya Agano Jipya, ni mmojawapo kati ya wale wanaume 12 ambao Yesu aliwateua mapema akawatuma kuhubiri Ufalme wa Mungu kwanza kwa taifa la Israeli, halafu kwa mataifa yote duniani.

Baada ya kifo na ufufuko wake, hao wakawa viongozi wa Kanisa ambalo hadi leo linajitambua kujengwa juu yao.

Habari zao, lakini hasa za Petro, zilianza kuandikwa na Mwinjili Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ambamo baadaye mhusika mkuu ni Mtume Paulo aliyedai kuteuliwa na Yesu Kristo baada ya kufufuka.

Mtume Filipo

Filipo (kwa Kigiriki Φίλιππος, Philippos) ni jina la mfuasi wa Yesu Kristo anayeshika nafasi ya tano katika orodha zote nne za Mitume wa Yesu katika Agano Jipya.

Mtume Mathayo

Mathayo (kwa Kiebrania מַתִּתְיָהוּ, Mattityahu au מתי, Mattay, Zawadi ya Mungu; kwa Kigiriki Ματθαῖος, Matthaios) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa hasa kutokana na Injili yenye jina lake. Labda aliitwa pia Lawi.

Mtume Petro

Simoni Petro alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mfuasi wa Yesu Kristo, tena kati ya wandani wake.

Baada ya Yesu, ndiye mtu anayejulikana zaidi katika Injili zote nne.

Katika orodha zote nne za mitume 12 wa Yesu zinazopatikana katika Biblia ya Kikristo anashika nafasi ya kwanza (tofauti na wenzake wengi ambao wanabadilishana nafasi, na kinyume cha Yuda Iskarioti, msaliti anayepewa daima nafasi ya mwisho); isitoshe Math 10:2 inasisitiza nafasi yake hiyo: "Wa kwanza Simoni aliyeitwa Petro".

Tangu kale Wakristo wengi, hasa Wakatoliki na Waorthodoksi, wanamheshimu kama mtakatifu, tena kama papa wa kwanza wa Roma hadi kifodini chake kati ya miaka 64 na 67, wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Ukristo iliyoanzishwa na Kaisari Nero.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 29 Juni pamoja na ya Mtume Paulo.

Mtume Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu.

Ili kumtofautisha na mtume mwenzake Simoni Petro anaitwa Mkananayo, yaani Mwenye juhudi kwa ukombozi wa Israeli kutoka ukoloni wa Roma.

Jina lake linapatikana katika orodha zao zote, lakini hatuna habari zake zaidi, isipokuwa masimulizi mbalimbali yasiyo na hakika.

Inasadikika kuwa kaburi lake liko Komani (Georgia).

Mtume Yohane

Yohane mwana wa Zebedayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wenzake wote.

Mapokeo ya Kikristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa barua tatu (Waraka wa kwanza wa Yohane, Waraka wa pili wa Yohane, Waraka wa tatu wa Yohane) na wa Kitabu cha Ufunuo.

Orodha ya Watakatifu Wakristo

Hapa chini wameorodheshwa kwa utaratibu wa alfabeti baadhi ya Watakatifu yaani watu wanaoheshimiwa na Wakristo kama vielelezo vya uadilifu wa Kiinjili.

Orodha hii inaonyesha pia kila mtakatifu huheshimiwa katika madhehebu gani.

Kanisa Katoliki linaheshimu watakatifu na wenye heri zaidi ya elfu kumi, kati yao Mapapa 78.

Katika makanisa ya Kiorthodoksi na ya Waorthodoksi wa Mashariki idadi ni kubwa zaidi kwa vile hakuna kanuni za kutangaza watakatifu kama zile zinazofuatwa na Papa, ambaye amejiwekea mamlaka hiyo tangu Karne za Kati.

Waanglikana walimtangaza mtakatifu mmoja tu (Mfalme Charles I wa Uingereza), lakini wanawatambua watakatifu wengine waliotangazwa kuwa watakatifu kabla ya Matengenezo ya Kiprotestanti, kama wanavyofanya pia Wamethodisti.

Madhehebu hayo na mengineyo yana marehemu wengine ambao bila kutangazwa rasmi wameingizwa katika kalenda ya watakatifu.

Walutheri pia wana watakatifu katika kalenda zao.

Salome (mke wa Zebedayo)

Salome (kwa Kiebrania: שלומית, Shelomit, kutoka mzizi שָׁלוֹם, shalom, yaani amani) alikuwa mke wa Zebedayo na mfuasi wa Yesu Kristo pamoja na wanae Yakobo Mkubwa na Mtume Yohane, waliokuwa marafiki wakuu wa Yesu pamoja na mtume Petro.

Kwa msingi huo alithubutu kumuomba Yesu awape wanae nafasi mbili za kwanza katika ufalme wake ujao.

Anatajwa kati ya wanawake waliosimama chini ya Yesu msalabani (Mk 15:40; Math 27:56) na kati ya wale waliowahi kwenda kaburini Jumapili asubuhi na mapema (Mk 16:1).

Pengine anadhaniwa kuwa na undugu na Bikira Maria, mama wa Yesu.Anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu.

Ukristo

Ukristo (kutoka neno la Kigiriki Χριστός, Khristos, ambalo linatafsiri lile la Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ, linalomaanisha "Mpakwamafuta" ) ni dini inayomwamini Mungu pekee kama alivyofunuliwa kwa Waisraeli katika historia ya wokovu ya Agano la Kale na hasa Yesu Kristo katika [[Agano Jipya]] ambaye ni mwanzilishi wake katika karne ya 1.

Dini hiyo, iliyotokana na ile ya Wayahudi, inalenga kuenea kwa binadamu wote, na kwa sasa ni kubwa kuliko zote duniani, ikiwa na wafuasi 2,400,000,000 (33% kati ya watu 7.274 bilioni), ambao nusu ni waamini wa Kanisa Katoliki na nusu ya pili wamegawanyika kati ya Waorthodoksi (11.9%) na Waprotestanti (38%) wa madhehebu mengi sana.

Karibu wote wanakubali Utatu Mtakatifu, yaani kwamba milele yote Mungu ni nafsi tatu zenye umoja kamili: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni kwa jina lao kwamba mataifa yote wanahimizwa kubatizwa kwa maji, ili kuzaliwa upya, kadiri ya agizo la Yesu ili kuingizwa katika fumbo la Mungu pekee kupitia fumbo la kifo na ufufuko wake mwenyewe.

Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinajulikana kama Biblia. Ndani yake inategemea hasa Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya.

Wakati wa Mababu wa Kanisa misingi ya imani ya Ukristo ilifafanuliwa na Mitaguso ya kiekumeni namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo. Maungamo yao yanakiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu ili kuwaokoa binadamu. Baada ya kuteswa na kuuawa msalabani alizikwa ila akafufuka, siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki mamlaka ya Baba hadi atakaporudi kuhukumu waadilifu na wasiotubu, akiwapa tuzo au adhabu ya milele kadiri ya imani na matendo yao.

Hivyo, kati ya madhehebu ya Ukristo, karibu yote yanamkiri Yesu kuwa kwa pamoja Mungu kweli na mtu kweli: katika umoja na nafsi yake ya Kimungu zinapatikana sasa hali hizo zote mbili.

Yote yanamkiri kuwa Mwokozi wa watu wote, na kuwa ndiye atakayerudi mwishoni mwa dunia kwa hukumu ya wote, ingawa maelezo kuhusu jambo hilo yanatofautiana.

Vilevile yote yanamchukua kama kielelezo cha utakatifu ambacho - kwa msaada wa Roho Mtakatifu na wa sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe, kuanzia ile ya ubatizo - kiwaongoze ndani ya Kanisa katika maadili yao maalumu, kuanzia unyenyekevu na upole hadi upendo unaowaenea wote, bila kumbagua yeyote, hata adui.

Yairo (Injili)

Yairo ni maarufu kama baba wa msichana aliyefufuliwa na Yesu Kristo kama inavyosimuliwa na Injili ndugu (Mk 5:21–43; Math 9:18–26; Lk 8:40–56).

Kiongozi wa sinagogi fulani, alikuwa amemkimbilia kwa imani Yesu kwa ajili ya binti yake.

Walipofika nyumbani walikuta msiba umeshaanza, lakini Yesu alifukuza waombolezaji, akamfufua mtoto huyo wa miaka 12 mbele ya Yairo mwenyewe, mke wake, Petro, Yakobo Mkubwa na Yohane tu.

Hatimaye aliagiza binti apewe chakula.

Yakobo Mdogo

Yakobo Mdogo ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu. Anaitwa hivyo ili kumtofautisha na mtume mwenzake, Yakobo wa Zebedayo.

Katika Injili anaitwa Yakobo wa Alfayo na kutajwa na Injili ya Mathayo 10:3, Injili ya Marko 3:18, Injili ya Luka 6:15, mbali ya Matendo ya Mitume 1:13.

Kutokana na wingi wa Wayahudi waliotumia jina hilo la babu wa taifa la Israeli, ni vigumu kuelewa kama ndiye Yakobo anayetajwa kama mmoja kati ya nguzo za Kanisa la Yerusalemu na kama ndiye anayetajwa kuwa mwandishi wa Waraka wa Yakobo.

Kama ndiye, aliuawa Yerusalemu mwaka 62 kwa himizo la kuhani mkuu Anna II.

Yuda Iskarioti

Yuda Iskarioti (kwa Kiebrania יהודה איש־קריות), Myahudi wa karne ya 1, alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha (Injili ya Mathayo 26:14-16).

Ni tofauti na mtume mwenzake Yuda Tadei.

Zebedayo

Zebedayo (kwa Kigiriki Ζεβεδαῖος, Zebedaios, kutoka Kiebrania זְבַדְיָה, Zvad'yah, yaani Mwingi au Zawadi yangu), kadiri ya Injili zote nne, alikuwa baba wa Mitume wawili wa Yesu Kristo: Yakobo Mkubwa na Yohane.

Injili zinamtaja pia mke wake, Salome, ambaye pia alifuatana na Yesu hadi kifo chake msalabani huko Kalivari, nje kidogo ya ngome ya Yerusalemu.

Zebedayo aliishi kwenye Ziwa Galilaya na kuwa mvuvi mwenye wafanyakazi chini yake (Mk 1:19-20; Math 4:21-22; Lk 5:4)Injili zinamtaja pia katika mistari mingine: Math 10:2; 20:20; 26:37; 27:56; Mk 3:17; 10:35; Lk 5:10 na Yoh 21:2.

Baadhi ya wataalamu wanadhani alikuwa pia kuhani.

Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Msalaba wa Yesu  • Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.