Wimbo Ulio Bora

Wimbo Ulio Bora (kwa Kiebrania שיר השירים, Shir ha-Shirim), ni kitabu kimojawapo cha Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Utunzi wake

Ingawa mapokeo yanamtaja mfalme Solomoni kama mtunzi, wataalamu wanaona ni kazi ya mwandishi wa karne ya 4 KK aliyekusanya nyimbo mbalimbali za mapenzi.

Aina ya uandishi

Ni kati ya vitabu vya kishairi na vya pekee zaidi katika Biblia, kwa kuwa kinaimba mahaba ya wapenzi wawili, ambao wanatafsiriwa kama wawakilishi wa Mwenyezi Mungu na taifa lake, kadiri ya moja kati ya mafundisho makuu ya ufunuo, linalotokana na nabii Hosea.

Ndio ujumbe wa kitabu: upendo kati ya mume na mke unaweza na kutakiwa kufanana na ule kati ya Yesu Kristo na Kanisa lake.

Maneno ya bibiarusi (Wim 8:6-7)

"Nitie kama muhuri moyoni mwako,

kama muhuri juu ya mkono wako;

kwa maana upendo una nguvu kama mauti,

na wivu ni mkali kama ahera.

Mwako wake ni mwako wa moto,

na miali yake ni miali ya Bwana.

Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,

wala mito haiwezi kuuzamisha.

Kama mtu angetoa badala ya upendo mali yote ya nyumbani mwake,

angedharauliwa kabisa".

Viungo vya nje

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Bible.malmesbury.arp.jpg Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wimbo Ulio Bora kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Bernardo wa Clairvaux

Bernardo wa Clairvaux (Fontaine-lès-Dijon, Ufaransa, 1090 - Ville-sous-la-Ferté, Ufaransa, 20 Agosti 1153) alikuwa padri, abati na mwenezaji mkuu wa urekebisho wa Citeaux wa shirika la Benedikto wa Nursia.

Aliitwa “Babu wa mwisho” kwa sababu alitetea na kustawisha teolojia ya mababu wa Kanisa wakati wa kujitokeza teolojia mpya ya shule.

Ndiye mtu muhimu zaidi wa karne ya 12 katika Kanisa Katoliki, ambalo linamheshimu kama mtakatifu (alivyotangazwa na Papa Alexander III mwaka 1174) na mwalimu wa Kanisa (alivyotangazwa na Papa Pius VIII mwaka 1830).

Ni msimamizi wa wakulima.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 20 Agosti.

Gregori wa Narek

Gregori wa Narek (kwa Kiarmenia Գրիգոր Նարեկացի, Grigor Narekatsi; 951 hivi - 1003 hivi) alikuwa mmonaki na padri wa Armenia maarufu kama mwanafalsafa, mwanateolojia na mtakatifu wa Kanisa la Kitume la Armenia.

Mzaliwa wa familia ya washairi, akiishi katika monasteri ya Narek (Narekavank), ni "mshairi mkuu wa kwanza wa Armenia"."Kitabu cha Sala", ambacho pengine kinajulikana kama "Kitabu cha Maombolezo", ni kati ya maandishi bora ya fasihi ya Kiarmenia na kimetafsiriwa katika lugha nyingi.

Papa Fransisko alimtangaza mwalimu wa Kanisa tarehe 12 Aprili 2015.

Hermoni

Hermoni (kwa Kiarabu: جبل الشيخ, jabal-ash-Shaikh, yaani "mlima wa shehe"; kwa Kiebrania: הר חרמון‎‎, Har Hermon) ni mlima wa Siria na Lebanoni ulio mrefu kuliko yote ya safu ya Lebanoni Ndogo na ya Siria nzima, ukiwa na kimo cha m 2,814 juu ya UB.

Kileleni kuna theluji ya kudumu na ni chanzo cha mto Yordani.

Unatajwa katika Biblia (Zaburi 42; 133:3; Wimbo Ulio Bora 4:8).

Historia ya Wokovu

Kwa jina hilo Wakristo wanamaanisha ufafanuzi wa mpango wa kazi ya Mungu kwa wokovu wa binadamu kadiri ya Biblia.

Ketubimu

Ketubimu (כתובים, Ketuvim, wingi wa ketuv, ambalo ni sawa na Kiarabu/ Kiswahili "kitab/kitabu") ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya Biblia ya Kiebrania (תנ״ך, Tanakh, kifupisho kinachounganisha herufi tatu "T" - "N" - "Kh" ambazo ni mianzo ya maneno matatu ya Kiebrania yanayotaja sehemu tatu ndani ya Biblia ya Kiebrania: Torati, Neviim, Ketuvim).

Vitabu hivi hugawanywa katika kundi za:

vitabu vya kihistoria kama vile Ezra, Nehemiah na Mambo ya Nyakati.

vitabu vya hekima kama vile Ayubu, Mhubiri na Mithali.

vitabu vya kishairi kama vile Zaburi, Maombolezo na Wimbo Ulio Bora.

vitabu vingine kama vile Ruthu, Estha na Danieli.

Kitabu cha Ezra

Kitabu cha Ezra kinapatikana katika Biblia ya Kikristo katika Agano la Kale.

Kiasili kiliandikwa kwa lugha ya Kiebrania lakini kuna pia sehemu fupi za Kiaramu.

Andiko la Ezra lilitunzwa katika Biblia ya Kiebrania pamoja na Nehemia kama kitabu kimoja lakini kimegawiwa baadaye kuwa vitabu viwili ambavyo Vulgata inavitaja kama "Esdras I" na "Esdras II".

Kitabu kinasimulia habari za Wayahudi chini ya utawala wa Waajemi.

Mwaka 587 KK mfalme wa Babeli alikuwa amevamia mji wa Yerusalemu, kubomoa hekalu la Sulemani na kumaliza ufalme wa Yuda. Wakazi walipelekwa Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli. Tangu wakati huo Waisraeli kwa kawaida walijulikana kuwa Wayahudi. Lakini, kwa kuwa utengano wa Israeli haukuendelea, majina hayo mawili, pamoja na jina la Waebrania, yaliweza kutumiwa kwa watu walewale (Yer 34:9; Yn 1:19, 47; 2 Kor 11:22; Gal 2:14).

Mwaka 539 KK Waajemi chini ya mfalme Koreshi walivamia Babeli ambayo ikawa jimbo la milki ya Uajemi. Koreshi aliwaruhusu Wayahudi kadhaa warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu.

Habari hizi na zilizofuata zinasimuliwa katika vitabu vya Ezra na Nehemia.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mapenzi

Mapenzi ni neno la Kiswahili linalojumlisha idadi kadhaa ya hisia, kuanzia mahaba, pendo hata upendo wa Kimungu.

Ni kwamba kitenzi "kupenda" kinaweza kurejelea aina za hisia, hali na mitazamo tofautitofauti, kuanzia ridhaa ya jumla ya kitu ("Napenda chakula hiki"), hadi mvuto mkali kati ya binadamu ("Nampenda mume wangu"). Uanuwai wa matumizi na maana, pamoja na utata wa hisia zinazohusika, hufanya kuwe na ugumu katika ufafanuzi, hata kulingana na hali nyingine za kihisia.

Kidhahania, mapenzi kwa kawaida yanarejelea hisia za ndani, zisizoelezeka, za kudumu kwa mtu mwingine. Hata hivyo, maelezo haya finyu pia yanashirikisha hisia tofauti, kutoka hamu na urafiki wa kimahaba hadi ukaribu wa kihisia wa kifamilia na kitaamuli, usioelekea kabisa ngono na hata umoja wa kina au ibada ya upendo wa kidini. Mapenzi katika aina zake mbalimbali husimamia mafungamano kati ya binadamu na, kutokana na umuhimu wake mkuu katika saikolojia, ni mojawapo ya maudhui yanayopatikana sana katika sanaa.

Orodha ya vitabu vya Biblia

Vitabu vya Biblia ya Kikristo vilivyoorodheshwa hapa chini ni vile 66 tu vinavyotambuliwa na Wakristo wote. Zingatia lakini kwamba walio wengi, hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki, katika Biblia wanavyoitumia wana vitabu vingine 7 vinavyoitwa Deuterokanoni, navyo vyote vimo katika Agano la Kale: Yoshua Bin Sira, Kitabu cha Hekima, Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo, Kitabu cha pili cha Wamakabayo, Tobiti, Yudithi, Baruku.

Majina ya vitabu yameandikwa hapa kufuatana na tafsiri ya Kiswahili cha kisasa maarufu kama Habari Njema. Kama kuna jina lingine limeongezeka katika mabano.

Papa Gregori I

Papa Gregori I (Roma, Italia, takriban 540 – Roma, 12 Machi 604) alikuwa papa kuanzia 3 Septemba 590 hadi kifo chake.

Alimfuata Papa Pelagio II akafuatwa na Papa Sabinian.

Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Gregorius. Kutokana na umuhimu wake katika historia, hasa ya Kanisa na Italia, aliongezewa lile la Magnus, yaani "Mkuu".

Lakini mwenyewe, aliposikia kuwa Patriarki wa Konstantinopoli alijiita "Patriarki wa ekumene", aliitikia kwa kujiita "Servus servorum Dei" (yaani "Mtumishi wa watumishi wa Mungu"), jina linalotumiwa hata leo na kila Papa. Akijali umoja wa kidugu katika Kanisa lote, yeye aliona unyenyekevu unatakiwa kuwa adili la msingi la kila askofu kama lilivyokuwa kwa Kristo aliyetuosha miguu. Jina hilo alilojichagulia lilidhihirisha kabisa namna yake ya kuishi na kutenda.

Hamu yake ilikuwa kuishi kweli kama mmonaki, akizama daima katika Neno la Mungu, lakini kwa kumpenda alijifunza kuwa mtumishi wa wote katika nyakati za tabu.

Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Mwaka 1298 Papa Bonifasi VIII alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Septemba.

Paradiso

Paradiso (kutoka Kiajemi: پردیس, bustani) ni jina la mahali pa amani kamili palipo tarajio kuu la waumini wa dini mbalimbali.

Dini za Abrahamu zinatumia jina hilo kwa Eden, yaani ulimwengu wa kabla ya dhambi ya asili, na vilevile kwa ule unaotarajiwa kuwepo milele.

Tanakh

Tanakh (תנ״ך) ni jina la Kiebrania la Biblia ya Kiyahudi.

Tanakh ni kifupi kinachounganisha herufi tatu "T" - "N" - "Kh" ambazo ni mianzo ya maneno matatu ya Kiebrania yanayotaja sehemu tatu ndani ya Biblia ya Kiebrania.

1. Torah (תורה) ni Torati au vitabu vitano vya kwanza vinavyoitwa pia "vitabu vya Musa". Mara nyingi vyaitwa pia "sheria" katika imani ya Uyahudi. Hivi ni vitabu vinavyoitwa ama Kitabu cha kwanza, cha pili, cha tatu cha Musa au kwa majina yafuatayo:

Mwanzo, Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu na Kumbukumbu la Torati.

Majina ya Kiebrania ya vitabu hivi ni maneno ya kwanza ya Kiebrania ya kila kitabu: Bereshit (בְּרֵאשִית) yaani mwanzo (Hapo mwanzo..); Shemot (שְמוֹת) yaani majina (Basi majina ya wana wa Israeli...); Wayikra (וַיִּקְרָא) yaani "akaita" (Bwana akamwita Musa...); Bemidbar (בְּמִּדְבַּר) yaani "porini, nyikani" (Bwana akanena na Musa katika bara ya Sinai = nyika ya Sinai...); Devarim (דְּבָרִים) yaani "maneno" (Haya ndiyo maneno...)2. Nevi'im (נביאים) ni manabii yaani maandiko ya maneno na matendo ya manabii katika Uyahudi. Humo huhesabiwa vitabu kama

Yoshua, Waamuzi, Samweli 1, Samweli 2, Wafalme 1 na Wafalme 2

Isaya, Yeremia, Ezekieli na kitabu cha "manabii wadogo" 12 (Hosea, Yoeli, Amosi, Obadia, Yona, Mika, Nahumu, Habakuki, Sefania, Hagai, Zekaria, Malaki)3. Ketuvim (כתובים) ni "maandiko" (Kiebrania "ketuv" ni sawa na Kiarabu/ Kiswahili "kitab/kitabu"). Vitabu hivi hugawanywa katika kundi za

vitabu vya kihistoria kama vile Ezra, Nehemiah na Mambo ya Nyakati .

vitabu vya hekima kama vile Ayubu, Mhubiri na Mithali.

vitabu vya kishairi kama vile Zaburi, Maombolezo na Wimbo Ulio Bora.

vitabu vingine kama vile Ruthu, Estha na Danieli.Mgawanyo huo wa vitabu ni tofauti kiasi na namna ya kuvipanga katika Biblia ya Kikristo vinamopatikana katika sehemu ya kwanza ambayo inaitwa Agano la Kale na kufuatwa na Agano Jipya lililoandikwa baada ya Yesu ambaye Wakristo wanaamini ndiye Masiya aliyetabiriwa tangu kale.

Hasa Wakristo wanawauliza kaka zao Wayahudi: imekuwaje ufunuo wa Mungu kwao ulisimama tangu miaka zaidi ya 2000 ingawa wao wanamsubiri bado Masiya afike? Je, historia ya wokovu imekatika?

Teresa wa Yesu

Teresa wa Yesu (Avila, Hispania, 28 Machi 1515 - Alba de Tormes, Hispania, usiku wa kuamkia tarehe 15 Oktoba 1582) ni jina la kitawa la Teresa Sánchez de Cepeda Ávila y Ahumada, maarufu pia kama Teresa wa Avila.

Mwanamke halisi, bikira, utu wake ulikomaa: alikuwa na tabia ya kupendeza, uchangamfu na busara sana, uhodari na msimamo, uwezo wa kukubali hali iliyopo kwa kupanga vizuri na kufanikisha mambo.

Ni kati ya watu muhimu zaidi katika ya historia ya Kanisa ya karne ya 16, katika historia ya utawa na katika teolojia ya Kiroho kutokana na urekebisho aliouanzisha katika shirika la Wakarmeli (wanawake na wanaume vilevile) na kutokana na maandishi yake juu ya maisha ya kiroho yanayomfanya mwalimu wa sala aliye bora kuliko wote.

Alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri tarehe 24 Aprili 1614, na Papa Gregori XV kuwa mtakatifu tarehe 12 Machi 1622, na hatimaye na Papa Paulo VI kuwa mwalimu wa Kanisa tarehe 4 Oktoba 1970.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 15 Oktoba.

Vitabu vya hekima

Miongoni mwa aina za vitabu vya Biblia vipo vile vinavyojulikana kama vitabu vya hekima.

Kati ya vitabu hivyo, Agano la Kale lina Methali , Kitabu cha Yobu, na Mhubiri, ingawa hata baadhi ya Zaburi na sehemu za vitabu vingine pia vinaweza kuhesabiwa kuwa ni maandiko ya hekima. Tena, kati ya Deuterokanoni, Kitabu cha Yoshua bin Sira na Kitabu cha Hekima ni vitabu vya hekima.

Upande wa Agano Jipya, ni hasa Waraka wa Yakobo ulioendeleza mtindo huo wa uandishi.

YHWH

YHWH (yaani, “Mimi Ndimi”) ni herufi nne ambazo kwa Kiebrania zinaandikwa יהוה. Ni konsonanti zinazounda jina la Mungu lililo muhimu kuliko yote linalopatikana mara 6,828 hivi katika Biblia ya Kiebrania kuanzia Mwa 2:4.

Jina hilo halipatikani kabisa katika vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Kitabu cha Mhubiri na Kitabu cha Esta.

Wayahudi walizidi kuliheshimu jina hilo hata wakaacha kulitamka wakati wa kulikuta katika Maandiko Matakatifu; badala yake wanasoma אֲדֹנָי, Adonai, yaani Bwana.

Labda kwa sababu hiyo watafsiri wa kwanza wa Biblia kwenda lugha ya Kigiriki (LXX) walilitafsiri Κύριος, Kyurios, yaani Bwana.

Kwa kuzoea hivyo, katika kutoa madondoo ya Agano la Kale, Wakristo wa kwanza walitumia tafsiri hiyohiyo.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.