Wangwa

Wangwa ni eneo la maji lililotengwa na bahari lakini kuna njia kwa maji kuingia na kutoka. Kama wangwa uko kwenye pwani na mito inaishia humo maji yake ni mchanganyiko wa maji ya chumvi na maji matamu. Kama wangwa haupokei maji ya mto na pia kuna njia nyembamba upande wa bahari tu inawezekana maji yake huwa na kiwango cha juu cha chumvi kutokana na uvukizaji.

Nyangwa zinaweza kutokea pale ambapo maji karibu na ufukoni hayana kina kirefu na mtelemko chini ya maji si mkali. Sharti lingine ni kwamba mawimbi ya kugonga ufukoni yasiwe makubwa mno.

Kawaida wangwa unatenganishwa na bahari kwa ulimi mwembamba wa nchi kavu uliojengwa na mkondo wa bahari uliobeba mchanga au matope, au na matope ya mto unaoishia humo. Katika bahari za tropiki matumbawe yanaweza kujenga ulimi huo.

Kuna pia nyangwa ndani ya atolli (kisiwa chenye umbo la mviringo) iliyojengwa na matumbawe na hapo pasipo na mito maji yake ni ya chumvi tu.

Nyangwa ni muhimu katika ekolojia ya bahari. Kuna samaki wengi kwa sababu spishi nyingi zinatega mayai katika nyangwa kwa sababu kina kifupi kinapunguza hatari kwa samaki changa ya kushambuliwa mara moja na samaki wakubwa. Ufuko wa nyangwa za tropiki unajaa mara nyingi miti ya mikoko na kati ya mizizi ya mikoko ni mahali pa spishi nyingi sana za viumbehai.

Nikumaroro Map

Wangwa wa atolli ya Nikumaro katika Pasifiki

Zalewszczecinski.jpeg

Nyangwa kwenye mdomo wa mto Oder karibu na mji wa Stettin, Poland

Chokrak

Wangwa mdogo ambako maji ya bahari yamesukumwa na mawimbi wakati wa dhoruba, bila mdomo wa wazi upande wa bahari

Barhöft, Insel Bock, Bodden (2011-05-21)

Wangwa wa Barhöft kwenye pwani ya Bahari Baltiki

Kivalina Alaska aerial view
Wangwa wa Kivalina (upande wa kushoto) huko Alaska, Marekani umeunganika na bahari.
Abidjan

Abidjan ni mji mkubwa nchini Cote d'Ivoire pia ni mji mkuu hali halisi. Vilevile ni bandari kuu ya nchi kwenye Ghuba ya Guinea ya bahari ya Atlantiki. Abidjan haiko baharini moja kwa moja lakini kwenye wangwa ya Ebrie inayotengwa na bahari kwa kanda nyembamba ya mchanga.

Abidjan imekua haraka kuanzia wakazi 65,000 mwaka 1950 hadi wakazi 3,624,800 mwaka 2000. Ilikuwa pia mji mkuu rasmi kati ya 1934 hadi 1983.

Kuna viwanda vya ngozi, nguo, vyakula na mafuta.

Abidjan ilikuwa kijiji tu hadi mwaka 1904. Wakati ule iliteuliwa kuwa mwanzo wa reli ya kuelekea ndani. Reli ilianzishwa hapa kwa sababu ng'ambo ya wangwa ilikuwepo bandari ndogo ya Port-Bouët. Tangu reli kujengwa Abidjan ilikua haraka. Mwaka 1934 ilitangazwa kuwa mji mkuu wa koloni ya Kifaransa Cote d'Ivoire.

Mwaka 1950 mfereji wa Vridi ilikata kanda la mchanga na kufungua wangwa kwa meli kutoka bahari; wangwa ikawa bandari kubwa yenye usalama mzuri kwa meli, na Abidjan ikawa mji wa bandari iliyosababisha kukua kwa uchumi na kuongezeka kwa watu.

Abidjan kuna chuo kikuu tangu 1964.

Tangu mwanzo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2004 hali ya usalama mjini umeshuka chini sana.

Atolli

Atolli ni kisiwa ambacho ni vipya vya matumbawe inayoonekana juu ya uso wa bahari. Mara nyingi umbo ni kama mviringo na kuna bwawa au wangwa wa maji katikati. Pia ukingo huu wa matumbawe umevunjika mara nyingi hivyo inaonekana kama mviringo wa visiwa vidogo na vyembamba.

Karibu atolli zote za dunia ziko katika Pasifiki na katika Bahari Hindi. Atlantiki ina atolli chache katika bahari ya Karibi.

Brazil

Brazil ni nchi kubwa ya Amerika ya Kusini na pia ni nchi yenye wakazi wengi kushinda nchi zote za bara hilo. Eneo lake ni karibu nusu ya bara lote.

Imepakana na Uruguay, Argentina, Paraguay, Bolivia, Peru, Kolombia, Venezuela, Guyana, Surinam na eneo la Guyana ya Kifaransa.

Brazil ina pwani ndefu kwenye bahari ya Atlantiki.

Mji mkuu ni Brasilia, uliopangwa na kujengwa kati ya 1957 na 1960. Mji mkubwa ni Sao Paulo.

Chamchanga

Chamchanga ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia ya Scolopacidae. Chamchanga tumbo-jeupe huitwa kiulimazi kwa kawaida. Ndege hawa ni weusi au kahawia na weupe, na wana domo refu na miguu mirefu na myembamba. Huonekana kandi ya bahari, viziwa au mito ambapo hukamata wadudu, gegereka hata samaki wadogo. Hutaga mayai 3-5 ardhini mahali majimaji.

Kapa (pwani)

Kapa au wangwa (wengi: nyangwa) ni msitu unaokua katika maji ya chumvi kwenye fuko za bahari za kanda za tropiki na nusutropiki (kati ya latitudo za 25º kaskazini na 25º kusini). Jumla ya maeneo ya kapa duniani kote ilikuwa km² 137,800 (maili za mradi 53,190) katika nchi na maeneo 118 mwaka 2000.

Miti inayokua ndani ya nyangwa, kama mikoko na mikandaa, inaweza kumudu maji yenye chumvi nyingi. Na mizizi yao inaunda matawi yanayomea juu ya matope na kupumua hewa, kwa sababu matope hayana oksijeni ya kutosha. Spishi nyingine zinabebwa juu ya mizizi kama magongo.

Spishi za miti ya kapa zinazotokea Afrika ya Mashariki ni:

Familia Acanthaceae

Avicennia marina, Mchu (Grey mangrove)

Familia Combretaceae

Lumnitzera racemosa, Mkandaa dume (Tonga mangrove)

Familia Lythraceae

Sonneratia alba, Mliana (White mangrove)

Sonneratia caesolaria, Mkoko-mpia (Crabapple mangrove)

Familia Meliaceae

Xylocarpus granatum, Mkomafi (Cannonball mangrove)

Xylocarpus moluccensis, Mkelenge (Moluccan mangrove)

Familia Rhizophoraceae

Bruguiera gymnorrhiza, Mchofi au Mkoko Wimbi (Black mangrove)

Ceriops tagal, Mkandaa (Indian mangrove)

Rhizophora mucronata, Mkoko Magondi (Asiatic mangrove)

Lagos

Lagos ni mji mkubwa wa Nigeria. Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi mwaka 1991.

Ikiwa na wakazi takriban milioni 12 katika eneo la jiji na milioni 15 - 22 katika rundiko la mji ni kati ya miji mikubwa zaidi ya Afrika; inawezekana kwamba idadi ya watu imeshapita ya Kairo, hivyo kuwa jiji lenye watu wengi barani Afrika.

Lagos ilianzishwa kama mji wa bandari uliokua juu ya visiwa vidogo karibu na mdomo wa wangwa wa Lagos unapounganika na Bahari ya Atlantiki.

Bandari ya Lagos iko kati ya bandari muhimu zaidi Afrika.

Mkoko

Mikoko ni aina za miti au vichaka vinavyokua katika maji ya chumvi kwenye fuko za bahari za kanda za tropiki. Miti hii inaainishwa katika jenasi tatu: Bruguiera, Ceriops na Rhizophora katika familia Rhizophoraceae. Pengine jina hili hutumika kwa Theobroma cacao lakini afadhali jina mkakao litumike kwa mti huu.

Takriban 1/3 ya pwani kwenye tropiki huwa na mikoko au miti ingine inayoweza kukua katika maji ya chumvi. Msitu wa mikoko huitwa kapa au wangwa.

Mizizi ya mikoko inaweza kushika matope na hivyo husaidia kukinga pwani na kujenga visiwa.

Nigeria

Nigeria (kwa Kiswahili pia: Nijeria au Naijeria) ni nchi ya Afrika ya Magharibi kwenye pwani ya Bahari Atlantiki.

Imepakana na Benin, Niger, Chad na Kamerun.

Mji mkuu ni Abuja ikitanguliwa na Lagos hadi mwaka 1991.

Nigeria imepata uhuru wake tarehe 1 Oktoba 1960, ikiunganisha maeneo ya koloni la Nigeria na sehemu ya kaskazini ya eneo lindwa la Kamerun ya Kiingereza.

Kwa sasa ni nchi ya Afrika yenye watu wengi na uchumi mkubwa kuliko zote. Kimataifa, ni ya 7 kwa idadi ya watu na ya 20 kwa uchumi.

Orodha ya Ndege wa Afrika ya Mashariki nr. 4

Kwa makusudi ya orodha hii nchi za Afrika ya Mashariki ni Kenya, Uganda na Tanzania.

Tazama orodha ya familia hapa chini.

Wangwa wa Lagos

Wangwa wa Lagos uko nchini Nigeria ukiwa mmojawapo kati ya nyangwa kubwa kwenye pwani ya ghuba ya Guinea. Eneo lake ni takriban km² 6,354.7Ni gimba la maji lenye urefu wa kilomita 60 na upana hadi km 15. Kina cha wastani ni mita 2 pekee. Maji yake ni mchanganyiko wa maji ya bahari na maji ya mito hivyo yana chumvi kidogo tu.

Mito ya Ogun na Osun inaishia hapa.

Ufuko wa wangwa una misitu ya mikoko inayotumika kwa ufugaji wa samaki. Machafuko wa maji ni tatizo kubwa kwa sababu maji machafu kutoka mji na viwanda yanaingia humo bila kusafishwa.

Bandari ya Lagos iko ndani ya wangwa. Beseni zake pamoja na njia ya kuingia baharini vinapaswa kuchimbwa mara kwa mara kwa kutunza kina cha kutosha kwa meli kubwa.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.