Waamoni

Amon (kwa Kiebrania עַמּוֹן ʻAmmôn; kwa Kiarabu a=عمّون|t=ʻAmmūn), ni jina la kabila la zamani lililotawala upande wa mashariki wa mto Yordani, leo nchini Yordani.[1][2][3]

Mji muhimu zaidi wa Waamoni ulikuwa Rabbah au Rabbath Ammon, mahali pa Amman ya leo, makao makuu ya Jordan.

Waliabudu hasa Milkom na Molekh (pengine ni majina mawili ya mungu yuleyule).

Kwa mara ya mwisho uwepo wao unatajwa katika kitabu cha karne ya 2.

Rujm Al-Malfouf
Mnara wa Waamoni huko Rujm Al-Malfouf, Amman, Yordani.
Qasralabdfront
Qasr Al Abd ilijengwa na gavana wa Ammon kama mwaka 200 KK.

Tanbihi

  1. Ancient Texts Relating to the Bible: Amman Citadel. University of Southern California. Iliwekwa mnamo 2011-01-11.
  2. MacDonald, Burton; Randall W. Younker (1999). Ancient Ammon. BRILL, 1. ISBN 9004107622, 9789004107625.
  3. Levy, Tom; Øystein S. LaBianca and Randall W. Younker (1998). The archaeology of society in the Holy Land. Continuum International Publishing Group, 399. ISBN 0826469965, 9780826469960.

Viungo vya nje

Lutu

Lutu (kwa Kiebrania לוט - lōṭ; kwa Kiarabu لوط - lūṭ) alikuwa mtoto wa Haran, mdogo wa Abrahamu kadiri ya Biblia na Kurani, ambaye alimfuata kutoka Mesopotamia hadi Kanaani.

Katika Biblia habari zake zinapatikana hasa katika kitabu cha Mwanzo, ambapo sura ya 19 inatuchorea uovu wa watu ambao huko Sodoma ulizidi hata kumdai Mungu alipe kisasi.

Lakini kati yao mwadilifu Lutu akaokolewa, isipokuwa mke wake akaja kuadhibiwa kwa sababu aliangalia nyuma, kinyume cha agizo la Bwana (Lk 17:28-33).

Lutu alikuwa na sifa ya ukarimu maana aliwakaribisha wageni waliokuwa malaika ingawa yeye hakujua; kwa hiyo tusiache kufuata mfano wake huo.

Lutu ndiye baba wa makabila ya Wamoabu na Waamoni, waliokaa upande wa mashariki wa mto Yordani (leo nchini Yordani).

Ufalme

Ufalme ni mfumo wa utawala ambako mfalme, malkia au mtu mwingine aliyerithi cheo chake ni mkuu wa dola. Vyeo vingine vya mkuu katika ufalme ni pamoja na kaisari, shah, tenno, sultani, amiri au mtemi. Kwa kawaida mfalme amerithi cheo chake kutoka kwa babake au mamake kwa hiyo alizaliwa kama mfalme mteule na ataendelea kuwa na cheo hiki hadi kifo chake. Lakini kama mfalme aliyetangulia hakuwa na mrithi inawezekana ya kwamba mfalme mpya amechaguliwa. Mfano wa dola lenye mfumo wa ufalme ambako mkuu anachaguliwa mara kwa mara ni Vatikani ambao Papa ni mkuu wa dola.

Neno ufalme hutumiwa pia kwa kutaja nchi inayotawaliwa na mfalme au malkia, kwa mfano Ufalme wa Maungano, Ufalme wa Uswazi na kadhalika.

Kiwango cha madaraka cha mfalme huwa na tofauti kubwa. Leo hii karibu wafalme wengi wako chini ya katiba ya nchi na mara nyingi wana madaraka machache; nafasi yao ni ya heshima na desturi. Lakini kuna falme kadhaa ambako mfalme bado ana madaraka makubwa habanwi na katiba wala bunge wala serikali kama vile Omani au Saudia.

Waamuzi (Biblia)

Kitabu cha Waamuzi ni cha saba katika orodha ya vitabu vya Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kinaleta mapokeo mbalimbali kuhusu historia ya Israeli kwenye miaka 1200-1025 hivi K.K.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Baada ya makabila 12 ya Waisraeli kugawana nchi takatifu, kila moja likaanza kujitegemea: lakini bila ya umoja hakuna nguvu upande wa dini wala wa siasa.

Upande wa dini, Waisraeli wakaanza kuchanganyikana na wenyeji Wapagani na kufuata utamaduni wao uliostaarabika zaidi, hata wakaabudu miungu yao kwa ukahaba wa kidini na kwa kuitolea sadaka watoto wao.

Kutokana na makosa hayo, Mungu akawaacha wanyanyaswe na makabila mbalimbali.

Mara kwa mara Waisraeli wakamlilia, naye akawainulia mwanamume au mwanamke fulani awashinde maadui na kuwarudishia amani (Amu 2:6-19).

Watu wa namna hiyo wanaitwa “waamuzi” kwa maana ya “watawala”. Majina yao ni: Othniel, Ehud, Shamgar, Debora, Gideoni, Tola, Yair, Yefta, Ibsan, Elon, Abdon, Samsoni.

Habari za waamuzi hao 12 haziwezi kupangwa kitarehe, kwa kuwa hazina dalili zinazotusaidia kujua ipi ilitangulia na ipi ilifuata. Waandishi wenyewe hawakujua mwaka wa matukio hayo, hivyo walikusanya kumbukumbu walizokuwanazo kama kwamba waamuzi walifuatana mmoja baada ya mwingine kuongoza Israeli. Ukweli ni kwamba waliweza kuongoza kwa wakati mmoja huyu huku na huyu huku, kwa kuwa kila mmoja alihusika na eneo fulani tu. Kwa kuwapanga mmoja baada ya mwingine, waandishi waliweza kusisitiza mara 12 kwamba Waisraeli walirudiarudia dhambi, na kwa sababu hiyo walirudiarudia kupewa na Mungu adhabu aliyoitabiri Musa. Lakini fundisho muhimu zaidi ni kwamba Bwana, bila ya kujali ugeugeu wao, daima alikuwa tayari kuwaokoa walipomlilia msaada.

Yefta

Yefta (kwa Kiebrania יפתח‎‎, Yip̄tāḥ) alikuwa mmojawapo kati ya Waamuzi wa Biblia.

Kadiri ya Waamuzi 11-12 alikuwa wa kabila la Manase au wa kabila la Gadi akaongoza Israeli kwa miaka 6.

Alikuwa na mtoto mmoja tu, tena wa kike, lakini alimtoa sadaka kwa Mungu kama shukrani kwa kumpa ushindi vitani dhidi ya Waamoni. Alifanya hivyo ili kutimiza nadhiri aliyoweka kwanza, bila kujua kwamba Torati inakataza sadaka za namna hiyo.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.