Vokali

Vokali ni fonimu au sauti za lugha zinazotajwa kwa herufi za A, E, I, O na U. Kwa jumla ni sauti tupu ambako hewa huondoka mdomoni bila kikwazo au sauti za pembeni.

Herufi zote nyingine ni konsonanti kama B, D, K, L, P, S, W au Z. Kwa sauti hizo si hewa tu inayoondoka mdomoni lakini mwendo wake ni pamoja na sauti za pembeni kwa kutumia shingo, ulimi au meno.

Abjadi

Abjad ni jina la mwandiko wa lugha ya Kiarabu na pia jina la kundi la miandiko inayotumia muundo wa kuandika konsonanti za neno lakini kuacha vokali.

Abugida

Abugida (kutoka Ge‘ez አቡጊዳ ’abugida) ni muundo wa mwandiko mwenye alama kwa silabi yaani konsonanti pamoja na vokali. Ni mwandiko wa kawaida kwa lugha za Ethiopia na Uhindi ya Kaskazini.

Jina latokana na herufi nne za kwanza ya mwandiko wa Ge'ez ambayo ni lugha ya kale ya Ethiopia.

Tofauti yake na alfabeti kama mwandiko wa Kilatini ni ya kwamba hapa kuna alama za pekee kwa vokali na konsonanti zinazounganishwa kufuatana na mahitaji ya lugha. Tofauti na miandiko ya abjadi kama Kiarabu au Kiebrania ni ya kwamba abjadi mara nyingi haziandiki vokali.

Kwa mfano wa mwandiko wa Devanagari ya Kihindi kuna alama ya क ambayo ni "k" na pia silabi "ka". Kwa kuongeza mstari mdogo juu silabi mpya ya के ke inapatikana. Ule mstari mdogo unaomaanisha "e" haupatikani peke yake bali pamoja na alama ya konsonanti pekee.

Kutoka alama ल "l" / "la" kuna uwezekano wa kupata alama kwa ला lā, लि li, ली lĪ, लु lu, लू lū, ले le, लै lai, लो lo na लौ lau.

Alfabeti

Alfabeti ni kiasi cha alama zinazotumiwa kuandika sauti za lugha fulani. Alama hizi hupatikana kama orodha kwa ufuatano uliokubaliwa, kwa mfano katika Kiswahili: "a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, kh, l, m, n, ny, ng', o, p, r, s, sh, u, t, th, v,w, y, z".

Jina la "alfabeti" hutokana na mwandiko wa Kigiriki ambamo herufi mbili za kwanza ni α "alfa" na β "beta".

Alfabeti ni mtindo wa mwandiko uliosambaa duniani kote. Kwa lugha nyingi imechukua nafasi ya miandiko ya awali.

Alfabeti huonyesha sauti si maneno kamili - hii ni tofauti na mwandiko kama Kichina wenye alama kwa ajili ya neno lote.

Alfabeti ya Kigiriki

Alfabeti ya Kigiriki ni mwandiko maalumu wa lugha ya Kigiriki. Herufi zake zilitumika pia kama tarakimu na sasa hutumiwa kimataifa kama alama za kisayansi.

Alfabeti ya Kilatini

Alfabeti ya Kilatini (pia: Alfabeti ya Kirumi) inatumiwa kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano kwenye ukurasa huu wa wikipedia.

E

E ni herufi ya 11 katika katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Epsilon ya alfabeti ya Kigiriki.

Herufi za Kiarabu

Herufi za Kiarabu ni maandishi maalumu ya lugha ya Kiarabu. Nje ya Kiarabu lugha mbalimbali zinaandikwa kwa herufi za Kiarabu, hasa lugha za nchi zenye Waislamu wengi, ingawa herufi hizo zilibuniwa kabla ya dini hiyo kuenea. Kati ya lugha hizo kuna Kiajemi, Kikurdi, Kimalay na Urdu. Pengine katika lugha hizo herufi kadhaa zinaongezwa au kupunguzwa, kulingana na lugha ilivyo.

Kihistoria hata Kiswahili na Kituruki ziliwahi kuandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Kuna herufi 28 za Kiarabu zinazoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto. Herufi zote isipokuwa sita zinaunganishwa wakati wa kuandika. Kutokana na tabia hiyo kila herufi inaweza kuonekana kwa maumbo tofautitofauti kiasi kutegemeana na mahali pake mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno.

Kwa kawaida maandishi ya Kiarabu ni ya konsonanti tu bila vokali. Vokali zikiandikwa zinaonekana kama mstari au nukta chini au juu ya herufi zinazoanzisha silabi.

Ipsilon

Ipsilon (pia: Ypsilon au kwa Kigiriki Ύψιλον, yaani "i fupi") ni herufi ya ishirini katika alfabeti ya Kigiriki, ikawa baadaye herufi ya ishirini na tano katika alfabeti ya Kilatini.

Asili yake ilikuwa "Waw" ya Kifinisia .

Iliandikwa kama Y ya Kiswahili lakini ilikuwa vokali, si konsonanti. Ipsilon ya Kigiriki ilitaja vokali iliyokuwa kati ya "u" na "i" (kama Kijerumani "ü"); katika Kigiriki cha kisasa ni "i" pekee.

Katika Kigiriki cha Kale ilimaanisha pia namba 400.

Waroma wa Kale waliipokea mara mbili katika alfabeti ya Kilatini:

mwanzoni katika karne za KK kupitia Kietruski kwa umbo la V lililomaanisha mara sauti ya "u" mara ya "w/v".

baada ya kuenea kwa utawala wao hadi Ugiriki katika karne ya 1 KK na kupokea maneno mengi ya Kigiriki.

J

J ni herufi ya 10 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Iota ya alfabeti ya Kigiriki.

Kicheki

Kicheki ni lugha ya Kislavoni katika familia ya lugha za Kislavoni cha Magharibi inayotumiwa nchini Ucheki. Pia kuna wasemaji takriban milioni mbili nje ya Ucheki.

Kicheki ni lugha ya karibu na Kislovakia na Kisorbi. Kinaandikwa kwa alfabeti ya Kilatini.

Wageni hushtuka mara nyingi wakiona maneno bila vokali, kwa mfano sentensi "Strč prst skrz krk". Sababu yake ni kwamba herufi za r na l zinaweza kuhesabiwa kama silabi (utaratibu unaofanana na "m" kama mwanzo wa neno mbele ya konsonanti katika lugha za Kibantu: m-fano, M-swahili).

Sarufi inapanga nomino zote katika jinsia tatu.

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Kige'ez

Kige'ez (kwa maandishi ya Kiamhari: ግዕዝ; matamshi: gē-ĕz) ni lugha ya kale ya Ethiopia iliyozungumzwa zamani za ufalme wa Aksum. Baadaye ilikuwa lugha ya kimaandishi nchini Ethiopia hadi karne ya 19 na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la orthodoksi la Ethiopia.

Huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti za kusini. Hutazamiwa kama lugha mama ya lugha za kisasa kama Kiamhari na Kitigrinya nchini Ethiopia na Eritrea.

Maandishi ya Kige'ez ni aina ya abugida yenye herufi 26 za konsonanti na 4 za vokali zinazounganishwa kuwa alama 202 kwa silabi zote zinazowezekana. Mifano ya kwanza inyojulikana ni kutoka karne ya 4 BK.

Konsonanti

Konsonanti ni sauti za lugha ambazo katika Kiswahili zatajwa kwa herufi B, Ch, D, F, G, H, J, K, L, M, N, P, Q, R, S, T, V, W, Y na Z

Kwa sauti hizo hewa haiondoki mdomoni moja kwa moja lakini mwendo wake ni pamoja na sauti za pembeni kwa kutumia shingo, ulimi au meno.

Hii ni tofauti na sauti za vokali kama A, E, I, O na U.

Hizi ni sauti tupu ambako hewa huondoka mdomoni bila kikwazo au sauti za pembeni.

Neno

Neno ni sehemu fupi ya lugha yenye maana. Ni sauti inayotamkwa au kuandikwa pamoja na kutaja jambo fulani.

Neno linaweza kuwa fupi lenye mofimu (yaani sauti inayowakilisha maana fulani) moja tu au kuwa ndefu lenye mofimu mbalimbali. Kwa kawaida ni muunganiko wa silabi kadhaa, zikiwemo konsonanti na vokali.

"Neno" linaweza kumaanisha neno lililosemwa au neno lililoandikwa, au wakati mwingine wazo au barua.

"Neno tata" kawaida litajumuisha mzizi na maana moja au zaidi maelezo (mwamba, nyekundu, haraka-haraka, kukimbia, kutarajia), au mizizi zaidi ya mmoja kwenye kiwanja (bodi-nyeusi, sanduku la mchanga). Maneno yanaweza kuwekwa pamoja ili kujenga vitu vikubwa vya lugha, kama vile misemo (mwamba mwekundu, kuweka juu), vifungu (nilitupa mwamba), na sentensi (Alitupa mwamba, lakini alikosa).

Leonard Bloomfield alianzisha dhana ya "Aina ndogo za Bure" mnamo 1926. Maneno hufikiriwa kama sehemu ndogo ya maana ya hotuba ambayo inaweza kusimama peke yake. Hii hulinganisha vitengo vya sauti na vitengo vya maana. Walakini, maneno mengine yaliyoandikwa si aina ya bure kabisa.

Wataalamu wanaona neno ni sehemu ya lugha yenye kituo kidogo mbele na nyuma yake, au kwa maandishi jumla ya herufi zenye maana zilizotengwa kwa nafasi nyuma na mbele.

Katika mazungumzo wakati mwingine si rahisi kutofautisha maneno kama ni maneno marefu au maneno mawili. Kwa mfano kuna maneno yaliyobuniwa juzi tu kwa kutaja mambo ya teknolojia na sayansi ambayo yanaunganisha maneno mawili kuwa moja:

garimoshi (gari + moshi) kama kifupi cha "gari la moshi" iliyokuwa kawaida zamani

mawasilianoanga (mawasiliano + anga - "telecommunication")Si wazi mara moja kwa wakilizaji wanaosikia haya mara ya kwanza kama ni neno moja au maneno mawili.

Wataalamu wa lugha hutofautiana aina za maneno kama vile nomino, kitenzi, kivumvishi, kielezi, kiunganishi kiwakilishi na kihisishi

Maneno kwa pamoja yanaunda sentensi yakifuata masharti ya sarufi katika lugha husika.

Silabi

Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambapo sauti za lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

Maneno kufanywa na silabi. Maneno mafupi huwa na silabi 1 pekee. Maneno mengine huwa na silabi zaidi kama 2, 3 au nyingi. Silabi fupi sana inaweza kuwa vokali 1 pekee au konsonanti 1 kama "m" katika "m-to-to".

Kama silabi inaishia kwa konsonanti inaweza kuitwa silabi iliyofungwa, kama inaishia kwa vokali inaweza kuitwa silabi wazi.

Kuna lugha zilizo na silabi nyingi zilizofungwa kama Kiingereza. Kiswahili kinapendelea silabi wazi, lakini "m" na "n" zinaweza kuwa mwishoni kwa silabi au kuwa silabi peke yao. Lugha kama Kijapani takriban hazina silabi za kufungwa.

Mifano ya maneno yenye silabi 1:

tu

naManeno mengi ya Kiswahili huwa na silabi mbili au zaidi:

ne-n-da

ku-ja

shu-le

hi-i

ma-a-na

ra-fi-ki

se-ko-n-da-ri

se-ri-ka-li

i-li-yo-fu-n-gwaKuna lugha zinazotumia mwandiko wa silabi badala ya alfabeti, kwa mfano abugida.

Tahajia

Tahajia (kutoka neno la Kiarabu; pia othografia au orthografia kutoka neno la Kiingereza orthography ambalo lina asili ya Kigiriki) ni utaratibu wa kuandika maneno kwa namna inayokubalika. Kila lugha huwa na kanuni na mapatano jinsi ya kuandika maneno.

U

U ni herufi ya 21 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Ipsilon katika alfabeti ya Kigiriki.

V

V ni herufi ya 22 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni ipsilon katika alfabeti ya Kigiriki.

Y

Y ni herufi ya 25 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Ipsiloni ya alfabeti ya Kigiriki.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.