Utanzu

Utanzu (yaani tawi) ni aina fulani ya kazi ya fasihi.

Tanzu kuu za fasihi andishi ni: riwaya, tamthiliya, shairi, insha, novela na hadithi fupi.

Marejeo

  • Wamitila, K.W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia, Nairobi: Focus Books.
Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utanzu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Bunilizi ya kinjozi

Bunilizi ya kinjozi (au bunilizi ya kifantasia) ni utanzu fulani wa fasihi andishi. Katika bunilizi hiyo mwandishi anatumia matukio au wahusika wasio wa kawaida.

Mifano ya bunilizi ya kinjozi katika fasihi ya Kiingereza ni: "A Midsummer Night's Dream" (Ndoto ya Usiku Mmoja) ya William Shakespeare, "Gulliver's Travels" (Safari za Guliveri) ya Jonathan Swift, na "The Lord of the Rings" (Bwana wa Mapete) ya J.R.R. Tolkien.

Bunilizi ya kinjozi hutofautishwa na bunilizi ya kisayansi kwa vile haisifu mambo ya teknolojia bali inatumia maajabu na viumbe vya visasili.

Fasihi

Fasihi (kutoka neno la Kiarabu فصاحة fasaha kwa maana ulumbi) ni utanzu (tawi) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe kwa hadhira husika. Ni ufundi wa kuwasilisha mawazo au ujumbe ulio katika fikra za binadamu.

Vipengele vinavyounda fani ya fasihi ni kama ifuatavyo: fani ni umbo la nje la kazi ya fasihi; maudhui ni umbo lake la ndani.

Fasihi simulizi

Fasihi simulizi ni kazi ya sanaa inayotumia mdomo (tofauti na maandishi kama kwenye fasihi andishi) kama njia kuu maalum ya kufikisha ujumbe. Ni sehemu ya msingi ya utamaduni, na vipengele vyake vingi vinafanya kazi kama katika fasihi kwa jumla.

Katika jamii isiyo na uandishi ni wazi kuwa hakuna fasihi andishi. Hata hivyo kila jamii ina hazina ya mapokeo yapokelewayo mdomo kwa mdomo—kwa mfano utenzi, ngano au nyimbo za jadi—hivyo vyote ni sehemu za fasihi simulizi.

Hata jamii ijuayo kusoma na kuandika inaendelea kuwa na fasihi simulizi, hasa nyumbani, k.m. katika kuwasimulia watoto hadithi. Lakini mara nyingi fasihi simulizi ya jamii ijuayo kusoma na kuandika ni tofauti sana na fasihi simulizi ya jamii isiyo na uandishi, kwa vile imeathiriwa na ujuzi wa kusoma na kuandika, na mitindo ya masimulizi yake haiendi sambamba na mitindo ya masimulizi yasiyoathiriwa na uandishi.

Fasihi ya Kiafrika

Fasihi ya Kiafrika inamaanisha maandiko kuhusu na kutoka Afrika. Kama Yusufu George anavyodokeza katika ukurasa wa kwanza wa sura yake kuhusu Fasihi ya Afrika katika kitabu "Understanding Contemporary Africa", ' wakati mtizamo wa fasihi ya Ulaya kwa ujumla inahusu herufi zilizoandikwa, dhana ya Afrika inahusisha pia fasihi simulizi.

Kama anavyoendelea kuandika, wakati maoni ya Ulaya kuhusu fasihi yalisisitiza mgawanyo wa sanaa na maudhui, mwamko wa Afrika unajumuisha:

"Fasihi" inaweza pia kuashiria matumizi ya maneno kisanaa kwa ajili ya sanaa pekee. Bila kukana jukumu muhimu la somo la sanaa katika Afrika, tunapaswa kukumbuka kwamba, tangu jadi, Waafrika huwa hawatenganishi sanaa na kufundisha. Badala ya kuandika au kuimba kwa sababu ya uzuri uliomo, waandishi wa Afrika, kwa kufuata fasihi simulizi, hutumia uzuri kusaidia kuwasiliana ukweli na taarifa muhimu na jamii. Hakika, kitu huchukuliwa kizuri kwa sababu ya ukweli kinachoonyesha na jamii kinachosaidia kujenga.

Fonolojia

Fonolojia (hasa huitwa Sarufi Matamshi) ni tawi la sayansi ya isimu. Inashughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa irabu na konsonanti.

Ala za sauti (vipashio vya utamkaji) zinatumika katika utamkaji wa fonimu (vitamkwa) za lugha husika. Mkondo wa hewa wakati wa utamkaji. Kuwepo na kutokuwepo kwa mguno wakati wa utamkaji (ghuna/sighuna).

Utanzu huu hushughulikia kanuni zinazotawala uchambuzi wa mfumo wa sauti, yaani, sauti kutamkwaje na wapi katika kinywa cha mwanadamu.

Matokeo ya uchunguzi wa kifonolojia yana umuhimu katika kubuni alfabeti.

Dhana ya fonolojia inajipambanua vizuri zaidi ikifasiliwa kwa kutofautishwa na fonetiki. Wakati fonetiki ni taaluma inayochunguza sauti zitamkwazo na binadamu bila kuzihusisha na lugha yoyote, fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kimwera na Kinyaturu. Kwa ufupi, fonetiki huchunguza sauti zote zitamkwazo na binadamu; fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi.

Hivyo, fonetiki huchunguza sauti nyingi kadiri iwezekanavyo, lakini fonolojia huchunguza sauti chache tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Mathalani, mfumo wa sauti wa lugha ya Kiswahili una sauti thelathini tu (irabu tano na konsonanti ishirini na tano).

Jambo lingine la kuzingatia ni vipashio vya kiuchambuzi vya matawi haya mawili. Wakati fonetiki kipashio chake cha msingi ni "foni", fonolojia kipashio chake cha msingi ni "fonimu". Kwa kuzingatia maelezo ya hapo awali, ni wazi kuwa foni ni nyingi zaidi kuliko fonimu, kwa kuwa foni ni kila sauti itamkwayo na binadamu, wakati fonimu ni sauti zile tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha mahususi. Hivyo, kuna fonimu za Kiswahili, za Kiingereza, za Kichina, n.k., lakini foni si za lugha yoyote, wala huwezi kusema kwa uhakika kuna foni ngapi, kwa kuwa bado kuna lugha nyingi duniani ambazo hazijatafitiwa.

Historia ya fonolojia inaweza kuwa imeanza na Ashtadhyayi, sarufi ya Kisanskrit iliyoandikwa na Pāṇini katika karne ya 4 KK. Kwa namna ya pekee Shiva Sutras, nyongeza ya Ashtadhyayi, inaorodhesha fonemi ya lugha hiyo, pamoja na kujadili mofolojia, sintaksia na semantiki.

Maghani

Maghani (au mighani kutoka neno la Kiarabu) ni utanzu wa kifasihi simulizi unaoonyesha matukio ya kijasiri na kishujaa ya mtu au watu katika kipindi fulani cha maisha.

Maigizo

Maigizo ni mpangilio wa maneno unaombatana na utendaji wa wahusika. Wahusika huwa wanaiga mambo ambayo yanafanywa na jamii husika na kuyaonesha mbele ya hadhira. Pia maneno yanayosemwa na wahusika yanalingana na yale ya jamii husika.

Hivyo basi katika sanaa hii hutumika vitendo, misegeo/mijongeo ya mwili na miondoko mbalimbali kwa umbo lenye kuvutia hadhira. Wakati mwingine maigizo huambatana na nyimbo. Utanzu wa maigizo hujumuisha vipera kama vile: matambiko, majigambo, ngonjera, ngoma, vichekesho, michezo ya jukwaani na kadhalika.

Ngonjera

Ngonjera ni aina ya mashairi ya majibizano baina ya pande / watu wawili (2) au zaidi. Aghalabu mazungumzo hayo huwa na mijadala ya malumbano yenye kusudio la kutoa ujumbe maalumu kwa hadhira au jamii husika. Msemaji mmoja huuliza swali katika ubeti mmoja na mwingine hutoa jibu katika ubeti unaofuata na majibizano ya hoja kuendelea hivyo hadi kukamilisha mada ya mjadala husika. Kutokana na sifa hiyo, ndiyo maana kipera cha ngonjera kinapatikana katika utanzu wa ushairi na katika utanzu wa maagizo. Muundo ni sawa kabisa na mashairi.

Nyanja za lugha

Nyanja za lugha ni hasa mbili kuu, ambazo ni:

Sarufi

Fasihi.

Odi Pop

Odi Pop au Gengeton ni mtindo wa muziki maarufu nchini Kenya ambao unatokana na aina mbalimbali za muziki kama Genge, Hip Hop na Reggaeton na kuchanganya ushawishi kutoka kwa muziki wa Reggae na Dancehall, na kujenga kwenye msingi wa mahadi ya Kiafrika.

Unaimbwa kwa njia ya kufoka kwa lugha ya Kiswahili pamoja na ya Sheng. Kuna tanzu kadhaa kutoka kwa tanzu hii (inayojulikana kwa jina la jumla Odi pop) kama vile: Dabonge, Debe na nyinginezo. Muziki huo unaongozwa na vijana wa Kenya na wengi wao wanaandika muziki kama bendi.

Neno Odi Pop lilibuniwa mnamo 2019 na msomi wa mziki na mwanamuziki Dan 'chizi' Aceda, ambaye ni maarufu kwa muziki wa Benga. Alielezea alivyo fikia neno hilo kwenye chapisho la The Elephant: Kwa sababu ya utaratibu wa majina, ninapendekeza neno la pamoja "Odi-pop" kurejelea mitindo yote ya sanaa hii mpya. Ninajua kila kundi lina jina lao la kando kando mfano; Gengetone, mtindo wa Dabonge na kadhalika na ufafanuzi wangu sio kujaribu kufuta hayo. Kwangu huu mtindo wa mziki kimsingi ni pop lakini na sauti ya pamoja (inayotumia mvuto wa hip-hop pamoja na kuchanganya miradi ya mashairi ya Karibiani na yote yamejengwa kwa msingi wa mtungo wa Kiafrika na kuimbwa kwa marudio ya rap na viunzi vya Kiswahili na Sheng). Utaratibu wangu wa kutaja umekopa kutoka K-Pop. Wasanii kama Ethic wamekemea jina Odi pop na wanapendelea istilahi gengeton (wakati mwingine inaandikwa Gengetone ) . Neno Gengeton lina kopa kutoka tanzu mbili za mziki ambazo ni; Genge, utanzu ambao ilikuwa maarufu nchini Kenya katika miaka ya 2000 na utanzu wa Reggaeton.

Semi

Semi ni tungo fupifupi zenye busara na ushauri kwa jamii zenye kutumia lugha ya picha, ishara na tamathali za semi. Utanzu wa semi una vipera kama vile:

Methali

Nahau

Misemo

Mafumbo

Vitendawili

Mizungu

UKUTA

UKUTA (kiferefu chake: Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania) ni jina la kutaja chama kilichoasisiwa na na hayati Mathias Mnyampala mnamo mwaka wa 1965. Lengo kuu la kuanzishwa kwa UKUTA lilikuwa kuendeleza ushairi na matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa ujumla.Chama kilinuia kusimamia madhumuni kama vile;

Kumasisha matumizi ya Kiswahili fasaha katika jamii

Kutoa mingozo ya utungaji bora wa kazi za fasihi kwa watunzi chipukizi

Kuandaa vitabu vya mashairi ya Kiswahili

Kushirikiana na taasisi nyengine za za ukuzaji wa Kiswahili nchini katika kuendeleza lugha ya Kiswahili. Mathalani kupitia semina na makongamano mbalimbali yanayochochea utumizi mkubwa wa Kiswahili.UKUTA ilikubwa na changamoto mbalimbali kama zinavyokubwa taasisi nyengine za Kiswahili katika kutimiza majukumu yake ya kukuza na kueneza matumizi ya lugha ya Kiswahili. Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazohitaji pesa kuzitatua. Ilikuwa lazima ipatikane fedha ili kuweza kutoa machapisho mbalimbali kwa ajili ya semina na makongamano, upungufu wa watalaamu wa fani ya ushairi na kadhalika. Nyengine ilikuwa kupungua kwa utanzu wa ushauri tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Katika kuhakikisha wanafikia malengo, UKUTA iliweza kufanikiwa kuchapisha baadhi ya mashairi kama vile;

(a) Mwaka wa 1997 waliweza kuandika mashairi ya kusifu miaka kumi ya Azimio la Arusha yaliyoitwa Maishairi ya Miaka Kumi ya Azimio la Arusha (UKUTA, 1977) na Ngonjera za UKUTA (1968) kikiwa kama kitabu chao cha kwanza.

(b) Kuandaa na kuendesha makongamano kwa waandishi wachanga ili kuwaelimisha kuhusu mbinu za wa mashairi na ngonjera.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.