Umoja wa Ulaya

Umoja wa Ulaya (kifupisho: EU) ni muungano wa kisiasa na wa kiuchumi wa nchi 28 za Ulaya.

Ulianzishwa mwaka 1991 juu ya msingi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya.

Shabaha kuu zilikuwa kujenga uchumi wa pamoja, kuboresha maisha ya watu wa Ulaya na kuzuia vita kati ya nchi za Ulaya.

Nchi 18 za Umoja huo hutumia pesa moja ya Euro.

Nchi nyingi za Umoja zimepatana kufungua mipaka yao bila vizuizi kwa wakazi wote.

Umoja wa Ulaya
Flag of Europe
EU location
www.europa.eu

Historia

Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ilibadilisha jina lake mwaka 1992 kufuatana na mikataba ya Maastricht kuwa Umoja wa Ulaya.

Nchi wanachama zilipatana kujenga siasa ya pamoja ya kiuchumi, kifedha, kisheria na katika mambo ya nje.

Mapatano ya Schengen ilifungua mipaka ili wakazi wa nchi hizo waweze kusafiri bila pasipoti wala vibali.

Nchi 10 tena zilijiunga na Umoja wa Ulaya mwaka 2004. Mbili zaidi ziliingia 2007 na Kroatia mwaka 2103.

Quai d'Orsay

Quai d'Orsay (Brussels)

Eurotower in Frankfurt

Euro Tower (Frankfurt)

Donald Tusk - 2017 (35494428931) (cropped)

Donald Tusk (2017)

Cecilia Malmström (cropped)

Cecilia Malmström

Wakazi

Jumla ya wakazi ni milioni 507.4 (2013). Kuna miji 16 yenye watu zaidi ya milioni moja kila mmojawapo, kuanzia London na Paris ambayo inazidi milioni 10.

Upande wa lugha, lugha rasmi ni 24, lakini lugha inayotumika zaidi ni Kiingereza, kinachoweza kuzungumzwa na 51% za wakazi wote, ingawa ni lugha ya kwanza ya 13% tu. Lugha nyingine ambazo ni za kwanza kwa wananchi wengi ni: Kijerumani (16%), Kiitalia (13%) na Kifaransa (12%). Pia kuna lugha 150 hivi za kieneo.

Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo (72%), hasa Wakatoliki (48%), Waprotestanti 12% na Waorthodoksi 8%. Waislamu ni 2%. Wengine hawana dini au ni Wakanamungu.

Uhuru wa kuhama

Kila mtu mwenye uraia wa nchi ya Umoja anaruhusiwa kuhamia nchi yoyote nyingine na kufanya kazi au biashara huko bila vibali vya pekee.

Vilevile bidhaa zote zinazotengenezwa kote katika Umoja wa Ulaya zinaweza kuuzwa katika kila nchi. Hii ni sababu ya kuwa na sheria za pamoja zinazotawala masharti ya bidhaa na uzalishaji.

Vyombo vya Umoja

Halmashauri ya Ulaya

Halmashauri hii ni mkutano wa viongozi wa serikali za nchi wanachama. Wanakutana mara mbili kwa mwaka na kutoa maazimo muhimu.

Nafasi ya uraisi hubadilika kila baada ya miezi 6. Ufini ilishika uraisi kati ya Julai 2006 hadi Desemba 2006, ikafuatiliwa na Ujerumani tangu Januari hadi Juni 2007.

Baraza za mawaziri

Katika baraza hizi mawaziri ya Kilimo, Sheria, Mambo ya Nje hukutana na kupanga siasa ya pamoja.

Kamati ya Ulaya

Hii ni kamati ya utawala inayotekeleza maazimio ya Halmashauri na bunge. Kuna makamishna 24 na mwenyekiti. Inaelekea kuwa serikali lakini haina madaraka ya serikali bado.

Bunge la Ulaya

European-parliament-brussels-inside
Bunge la Umojwa wa Ulaya huko Brussels.
Tratado de Lisboa 13 12 2007 (08) edited
Picha ya pamoja wakati wa kusaini mkataba wa Lisboa tarehe 13 Desemba 2007.

Bunge la Ulaya lina wabunge 751 wanaochaguliwa na wananchi kila baada ya miaka mitano.

Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya

Umoja Ulaya-2007
Nchi (jina la kienyeji - kifupi)
Austria (Österreich - AT) Bulgaria (Bălgarija - BG) Cyprus (Kypros - CY) Denmark (Danmark - DK) Eire (Éire - IE) Estonia (Eesti - EE) Hispania (España - ES) Hungaria (Magyarország - HU) Italia (Italia - IT) Kroatia (Hrvatska - HR) Latvia (Latvija - LV) Lithuania (Lietuva - LT) Luxemburg (Luxembourg - LU) Malta (Malta - MT) Polonia (Polska - PL) Romania (România - RO) Slovakia (Slovensko - SK) Slovenia (Slovenija - SI) Ubelgiji (België/Belgique - BE) Ucheki (Česká republika - CZ) Ufaransa (France - FR) Ufini (Suomi - FI) Ugiriki (Ellada - GR) Uholanzi (Nederland - NL) Uingereza (United Kingdom - UK) Ujerumani (Deutschland - DE) Ureno (Portugal - PT) Uswidi (Sverige - SE)
Wanaoomba kupokelewa: Masedonia (** - **) Uturuki (Türkiye - TR)

Wanachama tangu 1958 (waanzilishaji)

Wanachama tangu 1973

Mwanachama tangu 1981

Wanachama tangu 1986

Wanachama tangu 1995

Wanachama tangu 2004

Wanachama tangu 2007

Wanachama tangu 2013

Nchi zinazoomba uanachama

Viungo vya Nje

Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Umoja wa Ulaya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Austria

Austria (kwa Kijerumani: Österreich) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani, Ucheki, Slovakia, Hungaria, Slovenia, Italia, Uswisi na Liechtenstein.

Mji mkuu ni Vienna.

Bulgaria

Bulgaria (kwa Kibulgaria: България) - jina rasmi ni Jamhuri ya Bulgaria - ni nchi ya Ulaya kusini - magharibi kwenye rasi ya Balkani.

Imepakana na Bahari Nyeusi, Serbia, Makedonia Kaskazini na Ugiriki.

Ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Eire

Eire (pia: Ireland, Ayalandi; kwa Kiingereza mara nyingi Republic of Ireland) ni nchi ya kisiwani katika funguvisiwa ya Britania ya Ulaya.

Eire ilitawaliwa na Uingereza hadi mwaka 1922. Sehemu ya kaskazini ya kisiwa imebaki kama sehemu ya Ufalme wa Muungano (Uingereza).

Mji mkuu ni Dublin.

Hungaria

Hungaria (kwa Kihungaria Magyarország) ni nchi ya Ulaya ya Kati yenye wakazi milioni 10 wanaozidi kupungua.

Imepakana na Austria, Slovakia, Ukraine, Romania, Serbia, Kroatia na Slovenia.

Mji mkuu ni Budapest. Miji mingine muhimu ni Miskolc, Debrecen, Szeged, Pécs, Győr na Szolnok.

Kihungaria ndiyo lugha rasmi na ya kawaida kwa wananchi.

Wakazi walio wengi (52.9%) ni Wakristo. hasa Wakatoliki (37.4%) na Wakalvini (11.1%).

Italia

Jamhuri ya Italia (kwa Kiitalia: Repubblica Italiana) ni nchi ya Ulaya Kusini inayoenea katika sehemu kubwa ya Rasi ya Italia na baadhi ya visiwa vya jirani kwenye Bahari ya Kati.

Eneo lake ni km² 302,072.84 ambalo lina wakazi 60,483,973 (31-12-2017): ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu, lakini ya 8 au 9 kwa uchumi.

Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia. Nchi huru mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia pande zote ni San Marino na Vatikano.

Makao makuu ni jiji la Roma, lenye umuhimu mkubwa katika historia ya dunia nzima.

Kroatia

Kroatia (pia Korasia, kwa Kikroatia: Republika Hrvatska) ni nchi ya Ulaya ya kusini-mashariki. Imepakana na Slovenia, Hungaria, Serbia, Bosnia na Herzegovina na Montenegro.

Ng'ambo ya kidaka cha Adria iko Italia.

Mji mkuu ni Zagreb.

Kroatia ilikuwa kati ya majimbo ya Yugoslavia na ilipata uhuru wake mwaka 1991.

Imejiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Julai 2013.

Lituanya

Lituanya (au Lituania) ni nchi huru iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Ulaya. Inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Lituania.

Inapakana na Latvia, Belarus, Polandi na Russia.

Ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Mji mkuu wa Lituania ni Vilnius.

Poland

Poland (kwa Kipoland: Polska) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Imepakana na Ujerumani upande wa magharibi, Ucheki na Slovakia upande wa kusini, Ukraine na Belarus upande wa mashariki na Bahari ya Baltiki, Lituanya na Urusi (mkoa wa Kaliningrad Oblast) upande wa kaskazini.

Slovakia

Slovakia (kwa Kislovakia: Slovensko) ni nchi ya Ulaya ya Kati yenye wakazi milioni tano na nusu.

Imepakana na Ucheki, Austria, Poland, Ukraine na Hungaria.

Slovakia imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.

Mji mkubwa na mji mkuu ni Bratislava.

Miji muhimu baada ya Bratislava ni Košice, Banská Bystrica, Žilina, Trenčín, Nitra, Prešov na Trnava.

Wakazi walio wengi wanasema Kislovakia, ambacho ni kati ya lugha za Kislavoni, lakini kieneo kuna pia wasemaji wa Kihungaria, Kibelarus na Kiukraine.

Upande wa dini, 65.8% ni Wakatoliki, 8.9% Waprotestanti. 13.4% wanajitambulisha kama Wakanamungu.

Slovenia

Slovenia ni nchi ya Ulaya ya Kati, mashariki kwa milima ya Alpi.

Imepakana na Italia, ghuba ya Adria ya bahari ya Mediteranea, Kroatia, Hungaria na Austria.

Mji mkuu pia mji mkubwa ni Lyublyana (kwa Kislovenia: Ljubljana).

Ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.

Ubelgiji

Ubelgiji (België kwa Kiholanzi, Belgique kwa Kifaransa na Belgien kwa Kijerumani) ni ufalme wa Ulaya ya Magharibi. Ni kati ya nchi 6 zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ambayo baadaye imekuwa Umoja wa Ulaya.

Imepakana na Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani na Luxemburg.

Ina pwani kwenye Bahari ya Kaskazini.

Mji mkuu ni Brussels.

Ucheki

Ucheki au Chekia au Czechia (kwa Kicheki: Česko) pia Jamhuri ya Kicheki au Jamhuri ya Czech (kwa Kicheki: Česká republika) ni nchi ya Ulaya ya Kati na mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Imepakana na Poland, Ujerumani, Austria na Slovakia.

Mji mkuu ni Praha (Kijer.: Prag; Kiing.: Prague).

Miji mingine mikubwa ni Brno, Ostrava, Zlín, Plzeň, Pardubice, Hradec Králové, České Budějovice, Liberec, Olomouc na Ústí nad Labem.

Tangu zamani nchi imekuwa na kanda za Bohemia, Moravia na Silesia.

Wakazi husema hasa Kicheki ambacho ni lugha ya Kislavoni ya Magharibi.

Ni kati ya nchi ambako dini si muhimu kimaisha. Wakati wa sensa ya mwaka 2011, 45.2% ya wakazi hawakujibu swali husika, na wengine 34.2% walisema hawana dini yoyote. 10.3% walijitambulisha kama Wakatoliki na 0.8% kama Waprotestanti.

Ufaransa

Ufaransa ni nchi ya Ulaya na mwanachama mwanzilishi wa Umoja wa Ulaya.

Mji mkuu ni Paris.

Eneo lake ni km² 674,843; na idadi ya wakazi ni 63,044,000.

Imepakana na Ubelgiji, Luxemburg, Ujerumani, Uswisi, Italia, Monako, Andorra na Hispania.

Ufaransa ulikuwa kati ya nchi zenye makoloni mengi ikasambaza lugha yake kote duniani na kutunza uhusiano wa pekee na nchi nyingine zinazotumia Kifaransa.

Ufini

Ufini (pia: Finland, Finlendi; kwa Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia iliyoko Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Norwei upande wa kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi.

Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia ambayo watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani, lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Nchi ina wakazi milioni tano unusu tu katika eneo la km² 338,000; hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu.

Mji mkuu ni Helsinki.

Nchi ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa na wa Umoja wa Ulaya.

Ugiriki

Ugiriki (pia: Uyunani; kwa Kigiriki: Ελλάδα, Ellada, au Ελλάς, Ellas) ni nchi ya Ulaya Kusini-Mashariki katika kusini ya rasi ya Balkani.

Imepakana na Albania, Masedonia Kaskazini, Bulgaria na Uturuki.

Upande wa kusini-magharibi na kusini-mashariki kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Mediteranea.

Baharini huko kuna visiwa vingi sana ambavyo ni sehemu za Ugiriki.

Ugiriki ni nchi yenye historia ndefu na maarufu sana, hata inaitwa "nchi mama ya Ulaya".

Lugha ya Kigiriki inaendelea kuandikwa kwa Alfabeti ya Kigiriki inaotumiwa tangu miaka 3000 iliyopita, lakini lugha yenyewe imebadilika. Wagiriki wa leo hawaelewi tena Kigiriki cha Kale moja kwa moja.

Wakazi wengi wanafuata dini ya Ukristo, hasa katika Kanisa la Kiorthodoksi la Kigiriki (97%). 1.3% ni Waislamu.

Ugiriki ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 1981.

Uholanzi

Uholanzi ni nchi ya Ulaya ya Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini.

Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na visiwa vya Aruba, Curaçao na Sint Maarten, mbali ya visiwa vingine vitatu vya Karibi vya Uholanzi.

Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi iko chini ya usawa wa bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.

Ujerumani

Ujerumani (pia: Udachi, kwa Kijerumani: Deutschland) ni nchi ya Ulaya ya Kati.

Imepakana na Denmark, Poland, Ucheki, Austria, Uswisi, Ufaransa, Luxemburg, Ubelgiji na Uholanzi.

Ni nchi yenye watu wengi katika Ulaya, isipokuwa Urusi ina watu zaidi.

Uchumi wa Ujerumani una uwezo mkubwa: ni nchi inayouza bidhaa nyingi nje kushinda mataifa yote ya dunia.

Muundo wake kiutawala ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo 16 ndani yake na kila jimbo lina kiwango cha kujitawala.

Ureno

Ureno (kwa Kireno Portugal) ni nchi kwenye pembe ya kusini magharibi kabisa ya Ulaya. Upande wa magharibi na kusini imepakana na Bahari ya Atlantiki, na upande wa mashariki na kaskazini imepakana na Hispania.

Mafunguvisiwa ya Atlantiki ni pia sehemu za Ureno. Visiwa hivyo ni Azori kati ya Ulaya na Amerika na Visiwa vya Madeira vilivyoko katika sehemu ya Afrika ya Atlantiki.

Uswidi

Uswidi (au: Sweden; Swideni; kwa Kiswidi: "Sverige") ni nchi ya Skandinavia katika Ulaya ya Kaskazini. Imepakana na Ufini (Finland) na Norwei.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.