Ulaya ya Magharibi

Ulaya ya Magharibi ni sehemu ya magharibi ya bara la Ulaya. Kuna maelezo ya kutofautiana ni nchi zipi ambazo ni sehemu ya kanda hili. Maelezo hutofautiana kutokana na njia mbalimbali za kuangalia sehemu hiyo: kwa maana ya kijiografia, kihistoria, kisiasa au kiutamaduni.

CIA Western-Europe-map2
Ulaya ya Magharibi kijiografia kufuatana na CIA-Factbook (njano); njano nyeupe: Ulaya ya Kusini-Magharibi

Kanda la kijiografia

Kama kanda la kijiografia ni mara nyingi nchi zifuatazo zinazohesabiwa kuwa Ulaya ya Magharibi:

Location-Europe-UNsubregions, Kosovo as part of Serbia
Ulaya ya Magharibi kufuatana na mpangilio wa Umoja wa Mataifa (buluu nyeupe);
Buluu nyeusi: Ulaya ya Kaskazini
Kijani: Ulaya ya Kusini
Nyekundu: Ulaya ya Mashariki

Mpangilio wa Umoja wa Mataifa

Umoja wa Mataifa umepanga kanda hili tofauti hasa kwa kuhesabu Ufalme wa Muungano upande wa Ulaya ya Kaskazini lakini kuingiza Ujerumani, Austria na Uswisi ambazo zinahesabiwa mara nyingi kama sehemu ya Ulaya ya Kati; ila tu mpangilio wa UM hauna Ulaya ya Kati.

Iron Curtain Final
Ulaya ya Magharibi kisiasa wakati wa Vita Baridi
Buluu: Ulaya ya Magharibi (NATO)
Kijivu: Nchi zisizofungamana na upande wowote
Nyekundu: Ulaya ya Mashariki (upande wa Umoja wa Kisovyeti)

Ulaya ya Magharibi kihistoria katika karne ya 20

Wakati wa "vita baridi" Ulaya ya Magharibi ilimaanisha mara nyingi nchi zote za Ulaya zilizofungamana na upande wa magharibi yaani Marekani na NATO dhidi nchi za kikomunisti zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti.

1054

Makala hii inahusu mwaka 1054 BK (Baada ya Kristo).

Baada ya Kristo

Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: BK) ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani.

Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK.

Daniel Arap Moi

Daniel Toroitich arap Moi (amezaliwa 2 Septemba 1924) alikuwa Rais wa Kenya kutoka mwaka 1978 mpaka 2002.

Enzi ya kati

Enzi ya Kati (pia: Zama za Kati; kwa Kiingereza: "Middle Ages", pia "mediaevo" au "medievo") ni kipindi cha katikati cha historia ya Ulaya katika mgawanyo wa “zama” tatu: ustaarabu wa

Zama za Kale,

Zama za Kati, na

Wakati wa Kisasaama:

Enzi ya Kale,

Enzi ya Kati na

Enzi ya Kisasa.Hata kama ugawaji huo umetokana na mazingira ya Ulaya tu, hutumiwa pia kwa maeneo mengine ya dunia. Wataalamu wengi huamini ya kwamba haufai sana kidunia lakini hadi sasa hakuna mpangilio mwingine kwa dunia yote unaoeleweka kirahisi hivi.

Kwa kawaida, Zama za Kati za Ulaya Magharibi huhesabiwa toka mwisho wa Dola la Roma Magharibi (karne ya 5) hadi kuanza kwa falme za kitaifa, mwanzo wa uvumbuzi wa ng’ambo ya Ulaya, kipindi cha mwamko-sanaa, na Matengenezo ya Waprotestanti kuanzia mwaka 1517.

Mabadiliko hayo yalionesha mwanzo wa kipindi cha Zama za Kisasa ambacho kilitangulia mapinduzi ya viwanda.

Historia ya Kroatia

Historia ya Kroatia inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Kroatia.

Maeneo ya Kroatia yalikuwa sehemu ya Illyria wakati wa Dola la Roma na kutawaliwa kama mikoa ya dola hilo.

Mnamo mwaka 395 Dola la Roma liligawiwa katika sehemu ya magharibi na sehemu ya mashariki. Sehemu hizo mbili ziliendela baadaye kwa namna mbili tofauti.

Kuanzia mwaka 600 makabila ya Waslavoni walianza kuingia na kukaa. Wakroatia waliunda utemi wao wa kwanza. Kroatia ilikuwa upande wa magharibi wa mstari wa mwaka 395, hivyo chini ya athira ya Kanisa Katoliki, ikaendelea kuwa sehemu ya utamaduni wa Ulaya ya magharibi. Kumbe Waslavoni wa jirani wanaotumia lugha ileile waliishi chini ya athira ya Bizanti na Kanisa la Kiorthodoksi, hivyo kuendelea kama sehemu ya Ulaya ya Mashariki na kuitwa Waserbia.

Mtemi Tomislav (910–928) alichukua cheo cha mfalme mwaka 925. Huo Ufalme wa Kroatia uliendelea hadi mwaka 1102. Wakati ule mfalme wa mwisho hakuwa tena wa watoto na mfalme wa Hungaria alichaguliwa kuwa mfalme wa Kroatia pia. Maungano hayo na Hungaria yaliendelea kwa karne nyingi.

Tangu maungano wa Hungaria na Austria ni Kaisari wa Austria aliyekuwa na cheo cha mfalme wa Krotia hadi vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918).

Mwaka 1918 Dola la Austria liliporomoka. Waslavoni wa Kusini waliamua kuunda ufalme wa pamoja kwa jina la Yugoslavia. Kroatia ilikuwa sehemu ya Yugoslavia kuanzia 1918; kwanza katika ufalme wa Yugoslavia, halafu katika jamhuri ya kisoshalisti ya Yugoslavia hadi 1991.

Miaka 1990 / 1991 Yugoslavia iliporomoka na majimbo yake zilitafuta uhuru kama nchi za kujitegemea.

Kroatia ilikuwa kati ya majimbo ya Yugoslavia na ilipata uhuru wake mwaka 1991.

Imejiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Julai 2013.

Kalenda ya Gregori

Kalenda ya Gregori ni kalenda ambayo leo inatumiwa zaidi kimataifa. Jina limetokana na Papa Gregori XIII aliyeamua kutumia kalenda hiyo tangu tar. 15 Februari 1582 badala ya Kalenda ya Juliasi.

Kroatia

Kroatia (pia Korasia, kwa Kikroatia: Republika Hrvatska) ni nchi ya Ulaya ya kusini-mashariki. Imepakana na Slovenia, Hungaria, Serbia, Bosnia na Herzegovina na Montenegro.

Ng'ambo ya kidaka cha Adria iko Italia.

Mji mkuu ni Zagreb.

Kroatia ilikuwa kati ya majimbo ya Yugoslavia na ilipata uhuru wake mwaka 1991.

Imejiunga na Umoja wa Ulaya tarehe 1 Julai 2013.

Mapatano ya Warshawa

-Mapatano ya Warshawa ni tofauti na mkataba wa Warshawa kuhusu usafiri wa kimataifa kwa ndege-

Mapatano ya Warshawa ilikuwa jina la maungano ya kijeshi ya Umoja wa Kisovyeti na nchi 7 za Ulaya wakati wa vita baridi baada ya 1945. Jina rasmi ilikuwa "Mapatano juu ya urafiki, ushirikiano na kupeana usaidizi" na ilitiwa sahihi 1955 mjini Warshawa.

Ilikuwa jibu la Umoja wa Kisovyeti dhidi ya kuundwa kwa NATO upande wa Marekani na nchi za Ulaya ya Magharibi. Ilikwisha pamoja na mwisho wa vita baridi ikaondolewa rasmi 1991.

NATO

NATO ni kifupi cha North Atlantic Treaty Organisation (Kifaransa: OTAN, Organisation du Traité de l'Atlantique Nord) au Jumuiya ya Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini ambayo ni ushirikiano wa kujihami ya kambi ya magharibi. Inaunganisha nchi nyingi za Ulaya pamoja na Marekani na Kanada. Nchi wanachama zimeahidi kuteteana kama moja inashambuliwa na nje. Makao makuu yapo Brussels.

NATO ilianzishwa mwaka 1949 wakati wa vita baridi kama maungano ya nchi za Ulaya ya magharibi pamoja na Marekani dhidi ya Umoja wa Kisovyeti na nchi shiriki zake katika Mapatano ya Warshawa. Nchi wanachama wa kwanza walikuwa Marekani, Ubelgiji, Uholanzi, Luxemburg, Ufaransa, Uingereza, Kanada, Ureno, Italia, Norwei, Denmark na Iceland. 1952 Ugiriki na Uturuki zilijiunga pia zikafuatwa na Ujerumani ya Magharibi.

Baada ya mwisho wa vita baridi nchi zilizokuwa chini ya Umoja wa Kisoveti kama sehemu ya kambi ya kikomunisti zilijiunga na NATO kuanzia mwaka 1999. Ndizo Hungaria, Ucheki, Poland (1999), halafu Estonia, Latvia, Lithuania, Slovenia, Slovakia, Bulgaria na Romania (2004).

Kroatia na Albania zimekaribishwa kujiunga na NATO lakini zinapaswa kutimiza masharti kadhaa juu ya demokrasia na utawala ndani ya taifa. Jamhuri ya Masedonia ilikaribishwa pia lakini Ugiriki ilikataza mwaliko hadi Masedonia itapatana juu ya jina lake linalodaiwa na Ugiriki pia.

Orodha ya milima

Orodha ya milima duniani inataja baadhi tu.

Orodha ya milima ya Alpi

Hii orodha ya milima ya Alpi inataja baadhi tu ya milima mirefu zaidi.

Aletschhorn (m 4,193), Uswisi

Allalinhorn (m 4,024), Uswisi

Alphubel (m 4,206), Uswisi

Balmhorn (m 3,699), Uswisi

Piz Bernina (m 4,049), Uswisi, kilele cha juu kabisa katika Alpi ya Mashariki

Bietschhorn (m 3,934), Uswisi

Bishorn (m 4,153), Uswisi

Blüemlisalp (m 3,664), Uswisi

Breithorn (m 4,164), Uswisi - Italia

Piz Corvatsch (m 3,451), Uswisi

Dachstein (m 2,997), wa juu kabisa katika mkoa wa Styria, Austria

Dammastock (m 3,630), Uswisi

Dent Blanche (m 4,356), Uswisi

Dent du Géant (m 4,013), Mont Blanc, Ufaransa

Dent d'Hérens (m 4,171), Italia - Uswisi

Dents du Midi (m 3,257), Uswisi

Diablerets (m 3,210), Uswisi

Dom (m 4,545), Uswisi

Dufourspitze (m 4,634), Uswisi

Eiger (m 3,970), Uswisi

Fiescherhorn (m 4,049), Uswisi

Finsteraarhorn (m 4,274), kilele cha juu cha Bernese Oberland, Uswisi

Gornergrat (m 3,135), Uswisi

Gran Paradiso (m 4,061), Italia

Grand Combin (m 4,314), Uswisi

Grandes Jorasses (m 4,208), Mont-Blanc, Italia - Ufaransa

Grenzgipfel (m 4,618), Uswisi

Großglockner (m 3,797), kilele cha juu kabisa cha Austria

Hochkönig (m 2,938), Austria karibu na Berchtesgaden, Ujerumani

Jungfrau (m 4,158), Uswisi

Piz Kesch (m 3,418), Uswisi

Klein Matterhorn (m 3,883), Uswisi

Koschuta / Karawanks (m 2,135), Austria - Slovenia

Lagginhorn (m 4,010), Uswisi

Lauteraarhorn (m 4,042), Uswisi

Lenzspitze (m 4,294), Uswisi

Liskamm (m 4,527), Uswisi

Marmolada (m 3,343), mlima mrefu wa Dolomiti, Italia

Matterhorn / Monte Cervino (m 4,477), Italia - Uswisi

Mönch (m 4,101), Uswisi

Mont Blanc (m 4,808), Italia - Ufaransa - mlima mkubwa kuliko yote ya Ulaya ya Magharibi

Mont Blanc de Courmayeur (m 4,748), Mont Blanc Massif, Italia - Ufaransa

Mont Blanc du Tacul (m 4,248), Mont Blanc Massif, Ufaransa

Cristallo (mlima) (m 3,199), Dolomiti, karibu na Cortina d'Ampezzo, Italia

Monte Rosa (m 4,634), Italia - Uswisi mlima wa pili katika Ulaya ya Magharibi

Piz Morteratsch (m 3,751), Uswisi

Nadelhorn (m 4,327), Uswisi

Napf (m 1,407), Flysch Alps, Uswisi

Nesthorn (m 3,822), Uswisi

Nordend (m 4,609), Italia - Uswisi

Ober Gabelhorn (m 4,063), Uswisi

Ortler (m 3,902), wa juu katika Trentino-Alto Adige, Italia

Ostspitze (m 4,632), Uswisi

Pelvoux (m 3,946), Ufaransa

Pilatus (m 2,129), karibu Luzern, Uswisi

Rheinwaldhorn (m 3,402), Uswisi

Rigi (m 1,797), unaoelekea Ziwa Luzern, Uswisi

Rimpfischhorn (m 4,199), Uswisi

Piz Palu (m 3,905), Uswisi - Italia

Santis (m 2,502), Uswisi

Schlern (m 2,563), Dolomiti, Trentino-Alto Adige, Italia

Schneeberg (m 2,076), Austria

Schreckhorn (m 4,078), Uswisi

Signalkuppe (m 4,554), Italia - Uswisi

Strahlhorn (m 4,190), Uswisi

Titlis (m 3,239), Urner Alps, Uswisi

Tödi (m 3,620), Glarus Alps, Uswisi

Traunstein (m 1,610), Traunsee, Austria

Triglav (m 2,864), wa juu kabisa katika Slovenia

Untersberg (m 1,973), karibu na mji wa Salzburg, Austria

Weisshorn (m 4,506), Uswisi

Weissmies (m 4,017), Uswisi

Wetterhorn (m 3,701), Uswisi

Wildhorn (m 3,248), Uswisi

Wildspitze (m 3,774), Austria

Wildstrubel (m 3,243), Uswisi

Zinalrothorn (m 4,221), Uswisi

Zugspitze (m 2,962), Austria, wa juu kabisa katika Ujerumani

Zumsteinspitze (m 4,563), Italia - Uswisi

Orodha ya milima ya Ulaya

Hii Orodha ya milima ya Ulaya inataja baadhi yake tu.

Rasi ya Iberia

Rasi ya Iberia ni kati ya rasi kubwa za Ulaya ikiwa na eneo la km² 582,860. Iko kusini magharibi mwa Ulaya ikipakana na Bahari Atlantiki upande wa kaskazini na magharibi, halafu Bahari Mediteranea upande wa kusini na mashariki.

Milima ya Pirenei ni mpaka kati ya rasi na Ufaransa (Ulaya ya magharibi).

Iberia ni jina la kale tangu zamani za Waroma wa Kale.

Ubelgiji

Ubelgiji (België kwa Kiholanzi, Belgique kwa Kifaransa na Belgien kwa Kijerumani) ni ufalme wa Ulaya ya Magharibi. Ni kati ya nchi 6 zilizoanzisha Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ambayo baadaye imekuwa Umoja wa Ulaya.

Imepakana na Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani na Luxemburg.

Ina pwani kwenye Bahari ya Kaskazini.

Mji mkuu ni Brussels.

Uholanzi

Uholanzi ni nchi ya Ulaya ya Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini.

Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na visiwa vya Aruba, Curaçao na Sint Maarten, mbali ya visiwa vingine vitatu vya Karibi vya Uholanzi.

Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi iko chini ya usawa wa bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.

Ulaya

Ulaya (asili ya jina ni neno la Kiarabu ولاية, wilaayatun; inaitwa pia Uropa) ni bara lenye eneo la km² 10,600,000 tu, lakini wakazi ni milioni 700.

Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa ukoloni walitawanyika duniani, hasa Amerika, wakiathiri kote upande wa lugha, utamaduni na dini.

Ulaya ya Kati

Ulaya ya Kati ni kanda ya bara la Ulaya iliyopo baina ya Ulaya ya Mashariki na Ulaya ya Magharibi.

Katika mpangilio wa Umoja wa Mataifa unaofuata kawaida ya miaka ya Vita baridi hakuna Ulaya ya Kati kwa sababu wakati ule kitovu cha Ulaya kiligawiwa kisiasa kati ya mashariki (Umoja wa Kisovyeti) na magharibi (NATO). Hata hivyo kiutamaduni watu wa sehemu zile hawajisikii kama watu wa Ulaya ya Magharibi wala Mashariki.

Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa kama sehemu za Ulaya ya Kati:

Ujerumani

Austria

Uswisi

Liechtenstein

Slovakia

Ucheki

Poland

Hungaria

SloveniaKihistoria nchi hizi zote ziliwahi kuwa sehemu za madola makubwa ya Dola la Ujerumani na Austria-Hungaria.

Kuna majadiliano kuhusu mipaka ya kanda hili yasiyokwisha bado, kwa mfano swali la nchi za Kibalti kama Latvia.

Urusi

Urusi (kwa Kirusi: Россия, Rossiya) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki na ya Asia.

Kwa eneo ni nchi kubwa kuliko zote duniani, ikiwa na km² 17,075,400.

Urusi imepakana na Norway, Ufini, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland, Belarus, Ukraine, Georgia, Azerbaijan, Kazakhstan, China, Mongolia na Korea ya Kaskazini.

Iko karibu vilevile na maeneo ya Marekani (jimbo la Alaska liko ng'ambo ya mlango wa Bering) na Japani (kisiwa cha Hokkaido kiko ng'ambo ya mlango wa La Pérouse.

Kuna wakazi 144,000,000.

Mji mkuu ni Moscow.

Hadi mwaka 1991 Urusi ilikuwa kiini cha Umoja wa Kisovyeti na kuitwa Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi.

Urusi ilikuwa udikteta chini ya chama cha kikomunisti. Tangu 1990 imekuwa demokrasia.

Muundo wa utawala ni shirikisho la jamhuri chini ya rais mtendaji.

Wabembe

Wabembe ni kabila la watu ambao wanaishi katika nchi zote za Maziwa Makuu ya Afrika.

Wanapatikana kwa wingi Fizi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wanaishi katika nchi tofauti kama: Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia, Burundi, Kongo (Brazzaville) na Mkoa wa Kigoma, Tanzania.

Lugha yao ni Kibembe.

Katika mwaka wa 1991 idadi ya Wabembe ilikuwa 252.000 (Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia). Ila kwa sasa idadi ya Wabembe haijulikani kikamilifu, kufuatana na kusambaratika kwa kabila hiyo kwenye sehemu zote duniani.

Miaka kadhaa iliyopita hadi hivi sasa kuanzia mwaka 2005, inazidi kuonyesha idadi ya Wabembe wengi katika mabara tofauti kama vile: Marekani, Australia, Ulaya ya Magharibi na Ulaya ya Kaskazini.

Pia idadi ya Wabembe wengine inaongezeka katika nchi za Afrika Kusini, Kenya, Zimbabwe, Malawi na Zambia.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.