Ukomunisti

Ukomunisti ni njia ya kisiasa ya kufikiri na dhana ya jinsi gani jamii inapaswa kufanya kazi na kupanga mambo yake.

Ukomunisti ni aina ya ushoshalisti ambao unasema haipaswi kuwa na tofauti za matabaka katika jamii.

Ukomunisti unasema watu wa kila sehemu ya dunia wanapaswa kumiliki zana, viwanda, na mashamba ambayo yanatumiwa kuzalishia bidhaa na vyakula. Mchakato huu wa kijamii hujulikana kama umiliki wa kawaida. Katika jumuia ya wakomunisti, hakuna mali binafsi.

Mwanzo wa mafundisho haya uko kwenye maandiko ya Karl Marx na Friedrich Engels tangu kutolewa kwa "Ilani ya Kikomunisti" mwaka 1847[1].

Hammer sickle clean
Nyundo na Mundu, ni alama ya ukomunisti, nguvu ya wafanyakazi.

Falsafa

Communist-manifesto
Ilani ya Kikomunisti

Kwa mujibu wa waandishi na wafikiri wa Ukomunisti, lengo la Ukomunisti ni wafanyakazi kuchukua udhibiti wa viwanda na biashara na kusimamia uchumi kidemokrasia.

Baada ya wafanyakazi wa serikali kuimarisha maslahi yao wangeweza polepole kuleta zana zote za uzalishaji chini ya udhibiti wao, mpaka hapo mfumo wa bila matabaka na hali ya kutokuwa na serikali katika jamii imeumbwa.

Hili ni wazo la kizamani, lakini limeanza kuwa maarufu baada ya Mapinduzi ya Ufaransa na harakati nyingine maarufu za huko Ulaya mwanzoni mwa miaka ya 1800.

Pamoja na hoja ya kufikia hali ya usawa bila utawala kati ya wanadamu wanaitikadi wa ukomunsti waliona ni lazima kuwa na kipindi cha udikteta ambako wakomunisti wanashika utawala na kukandamiza upinzani dhidi ya mabadiliko waliyoona ya lazima kufikia shabaha yao.

Vladimir Lenin alipanua nadharia ya ukomunisti akidai lazima kuwa na chama cha kikomunisti kinachopanga mapinduzi na kushika utawala katika kipindi alichoita "udikteta wa wafanyakazi".

Viungo vya Nje

  Bendera ya Benin

  Bendera ya Benin ilianzishwa Desemba 1958 wakati koloni ya Kifaransa ya Dahomey ilipopewa madaraka ya kujitawala. Mwaka 1960 Dahomey ikapata uhuru wa kitaifa ikaendelea na bendera ileile.

  Baada ya mapinduzi ya Mathieu Kérékou jina la Dahomey lilibadilishwa kuwa Benin. Kufuatana na itikadi mpya ya Umarx bendera ilibadilishwa kuwa kijani (kwa ajili ya wakulima) yenye nyota nyekundu (kwa ajili ya ujamaa na mapinduzi).

  Baada ya mwisho wa ukomunisti bendera ya awali ilirudishwa tangu Agosti 1990.

  Bendera huonyesha rangi za Umoja wa Afrika yaani zilezile kama bendera ya Ethiopia na nchi mbalimbali za Kiafrika.

  Chama cha kikomunisti

  Chama cha kikomunisti ni chama cha kisiasa kinacholenga kufikisha jamii katika hali ya ukomunisti yaani jamii bila matabaka ya matajiri na maskini na bila watu wenye mali nyingi kuliko wengine. Katika nadharia hali hii ya ukomunisti imedhaniwa kuwa bila utawala wa watu juu ya wengine lakini nadharia hii inadai pia ya kwamba kuna kipindi cha mpito ambako chama cha kikomunisti kinatawala kwa namna ya kidikteta hadi mabaki ya utaratibu wa kale yamekwisha ambayo yanaweza kuzuia au kuchelewesha maendeleo ya kuelekea ukomunisti.

  Vyama vya Wakomunisti vilifaulu kushika serikali katika Urusi tangu 1917, katika Umoja wa Kisovyeti tangu mnamo 1920 / 1924 halafu katika nchi za Ulaya ya Mashariki tangu 1945 / 46. Katika China, Korea ya Kaskazini na Vietnam ya Kaskazini Wakomunisti walitawala tangu mnamo 1948 /49. Vyama mbalimbali katika nchi kadhaa za Afrika vilifuata mtindo wa Wakomunisti kwa namna fulani na kushika utawala kwa miaka kadhaa.

  Utawala wa vyama vya kikomunisti uliporomoka mnamo 1989 katika nchi nyingi na leo hii (2011) vyama vya kikomunisti vinatawala katika nchi chache pekee kama vile China, Vietnam na Kuba. Lakini havilengi tena kufikia shabaha ya ukomunisti.

  Daniel Arap Moi

  Daniel Toroitich arap Moi (amezaliwa 2 Septemba 1924) alikuwa Rais wa Kenya kutoka mwaka 1978 mpaka 2002.

  Fidel Castro

  Fidel Alejandro Castro Rúz(13 Agosti 1926 - 25 Novemba 2016) alikuwa kiongozi wa Kuba tangu mwaka 1959 hadi 2006 akiwa waziri mkuu hadi 1976 halafu rais wa nchi.

  George H. Bush

  George Herbert Walker Bush ( 12 Juni 1924 - 30 Novemba 2018) alikuwa Rais wa 41 wa Marekani kuanzia mwaka wa 1989 hadi 1993. Kaimu Rais wake alikuwa Dan Quayle.

  Akijulikana kama George Bush aliwahi kuwa mbunge, balozi wa Marekani, mkuu wa mamlaka ya upelelezi CIA na makamu wa rais Ronald Reagan. Alikuwa mwanasiasa wa Chama cha Jamhuri cha Marekani (Republican).

  Kipindi cha urais wa Bush kiliona kuporomoka kwa ukomunisti katika Urusi na Ulaya ya Mashariki na mwisho wa vita baridi. Alitafuta maelewano na viongozi wa Urusi na kukubali maungano ya Ujerumani. Alituma jeshi la Marekani kwenye uvamizi wa Panama mwaka 1989 uliompindua dikteta Manuel Noriega na kwenye vita dhidi ya Irak iliyowahi kushambulia Kuwait.

  Mwana wake George Walker aliingia pia katika siasa akaendelea kuwa rais wa 43 wa Marekani.

  Historia ya Urusi

  Historia ya Urusi inahusu historia ya eneo ambalo leo linaunda nchi inayoitwa Shirikisho la Urusi.

  Itikadi

  Itikadi ni mkusanyiko wa imani unaoshirikiwa na kikundo cha watu fulani.

  Kuna aina kuu mbili za itikadi: itikadi za kisiasa, na itikadi za kiepistemolojia (ni sehemu ya falsafa ambayo inahusu utafiti wa jinsi tunavyojua mambo). Itikadi ya kisiasa ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kimaadili na vipi nchi itaendeshwa. Itikadi za kiepistemolojia ni upangiliaji unaohusu mawazo ya kifalsafa, ulimwengu, na jinsi gani watu wanapaswa kufanya maamuzi.

  Kuna aina nyingi za itikadi. Moja kati ya hizo ni pamoja na Ukomunisti, Usoshalisti, na ubepari ni itikadi kubwa sana za kiuchumi na kisiasa kwa ujumla.

  Karl Marx

  Karl Marx (1818 - 1883) alikuwa mwanafalsafa kutoka nchini Ujerumani ambaye pamoja na Friedrich Engels alianzisha siasa ya ukomunisti.

  Karne ya 19

  Karne ya 19 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1800 na 1900. Kikamilifu kilianza tarehe 1 Januari 1801 na kuishia 31 Desemba 1900.

  Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya binadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu - hali halisi, maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.

  Hata hivyo kipindi hiki cha karne ya 19 kilikuwa kipindi muhimu sana katika historia ya binadamu.

  Kirusi

  Kirusi (русский язык russkii yazik) ni moja kati ya lugha za Kislavoni cha Mashariki yenye wasemaji wengi kati ya lugha zote za Kislavoni. Kirusi huandikwa kwa alfabeti ya Kikyrili.

  Kirusi ni lugha rasmi katika Urusi na pia katika nchi jirani za Belarus, Kazakhstan na Kirgizia. Wasemaji wa Kirusi wako katika nchi zote zilizokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Kuna pia Warusi katika nchi za magharibi kwa sababu wakati wa Ukomunisti kulikuwa na wakimbizi waliotoka nje ya Urusi kwa sababu za kisiasa.

  Watu wengi duniani wamejifunza Kirusi kwa sababu ilikuwa lugha ya kimataifa kati ya nchi zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti. Wanafunzi wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika walipata elimu ya juu kwenye vyuo vikuu vya Umoja wa Kisovyeti kwa lugha ya Kirusi.

  Korea Kaskazini

  Korea ya Kaskazini (jina rasmi: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea) ni nchi ya Asia ya Mashariki iliyoko kwenye nusu ya kaskazini ya rasi ya Korea.

  Imepakana na Korea Kusini, China na Urusi.

  Mji mkuu ni Pyongyang.

  Mapinduzi ya Urusi ya 1917

  Mapinduzi ya Urusi ya 1917 ni namna ya kutaja mfuatano wa mapinduzi mawili katika mwendo wa mwaka 1917 yaliyomaliza ufalme wa miaka 1,000 nchini Urusi na kuanzisha utawala wa ukomunisti kwa miaka 70 iliyofuata.

  Mwaka 1917 uliona mapinduzi mawili katika Urusi:

  mapinduzi ya Februari ambako Tsar alipaswa kujiuzulu na serikali ya muda ilichukua mamlakana

  mapinduzi ya Oktoba ambako serikali ya muda ilifukuzwa na utawala wa kikomunisti ulianza.

  Mapinduzi ya Zanzibar

  Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964 ili kumuondoa madarakani Sultani wa Zanzibar na serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu, na hatimaye kuweka uongozi mikononi mwa Waafrika, ambao ndio wengi visiwani humo (230,000 hivi), kwenye bahari ya Hindi, karibu na pwani ya Tanganyika.

  Usultani wa Zanzibar ulikuwa umepewa na Uingereza uhuru wake mwaka 1963. Kabla ya hapo, Waarabu walikuwa wamefaulu kudumisha katika mfululizo wa chaguzi utawala waliokuwa nao tangu zamani za Zanzibar kuwa chini ya Usultani wa Omani.

  Chama cha Afro-Shirazi Party (ASP), kilichowakilisha hasa Waafrika, kilipoona kwamba bungeni kina viti vichache ingawa kilipata 54% za kura katika uchaguzi wa Julai 1963, kilipatana na chama cha mrengo wa kushoto Umma Party.

  Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP John Okello (1937-1971 ?) kutoka Uganda aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa kisiwa kikuu cha Unguja kushinda polisi wa nchi na kuteka silaha zao. Halafu walielekea Zanzibar Town walipompindua Sultani Jamshid bin Abdullah na serikali yake. Waliokufa katika mapigano wamekadiriwa kuwa 80 hivi tu.

  Kumbe yalifuata kwa siku kadhaa (labda hadi tarehe 20 Januari) maangamizi ya kimbari dhidi ya Waarabu (waliokuwa 50,000 hivi) na Waasia wa Asia Kusini (waliokuwa 20,000 hivi); hakuna hakika kuhusu idadi ya waliouawa: makadirio yanataja kuanzia mamia kadhaa hadi 20,000.

  Kiongozi wa ASP Abeid Karume, asiyekuwa na msimamo mkali akawa rais wa kwanza wa nchi, na wanachama wa Umma party walipewa nafasi serikalini. Kufikia Machi Okello alikuwa ameshawekwa pembeni na kufikia Aprili kikosi chake kimeshanyang'anywa silaha.

  Mwelekeo wa Kikomunisti wa baadhi katika serikali mpya uliogopesha nchi za Magharibi. Kwa kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya athari ya Uingereza, serikali yake iliandaa mipango kadhaa. Hata hivyo, hofu ya kuundwa serikali ya Kikomunisti haikutimia kamwe, na kwa kuwa wananchi wa Uingereza na Marekani waliweza kuhama bila shida, mipango hiyo haikutekelezwa.

  Wakati huo nchi za Kikomunisti za China, Ujerumani Mashariki na Umoja wa Kisovyeti zilianzisha mahusiano ya kirafiki na serikali mpya ya Zanzibar kwa kuitambua rasmi na kwa kutuma washauri.

  Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa Tanzania; vyombo vya habari vilitafsiri muungano huo kuwa juhudi za kuzuia Ukomunisti kugeuza Zanzibar.

  Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu ya taifa zima la Tanzania.

  Mfiadini

  Mfiadini ni binadamu yeyote aliyeuawa kwa ajili ya imani au maadili ya dini aliyoiamini.

  Inasikitisha kwamba katika historia dhuluma nyingi zilifanywa na serikali, viongozi na wafuasi wa dini na madhehebu tofauti, na watu wengine.

  Mfumo wa chama kimoja

  Mfumo wa chama kimoja ni utaratibu wa kisiasa unaoruhusu chama cha kisiasa kimoja tu.

  Mara nyingi mfumo huo umeanzishwa kwa kupiga marufuku vyama vyote vingine. Kuna pia nchi ambako vyama mbalimbali viko, lakini havina nafasi ya kushiriki katika uchaguzi au vinazuiwa kushindana na chama tawala.

  Kihistoria mifumo hii ilitokea katika mazingira ya Ukomunisti, Ujamaa au Ufashisti. Mfumo huu ni karibu na udikteta.

  Papa Yohane Paulo II

  Papa Yohane Paulo II (kwa Kilatini: Ioannes Paulus PP. II; kwa Kiitalia: Giovanni Paolo II; kwa Kipolandi: Jan Paweł II; kwa Kiingereza: John Paul II; 18 Mei 1920 - 2 Aprili 2005) alikuwa papa wa 264 kuanzia 16 Oktoba 1978 hadi kifo chake akidumu katika huduma hiyo kirefu kuliko mapapa wengine wote, isipokuwa Mtume Petro na Papa Pius IX.

  Alimfuata Papa Yohane Paulo I akiwa Papa wa kwanza asiye Mwitalia tangu miaka 455 iliyopita, wakati wa Mholanzi Papa Adrian VI (1522 - 1523), tena papa wa kwanza kutoka Polandi (na makabila yoyote ya Waslavi) katika historia ya Kanisa. Alifuatwa na Papa Benedikto XVI.

  Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Karol Józef Wojtyła (matamshi: ˈkarɔl ˈjuzɛf vɔiˈtɨwa).

  Wengi wanamhesabu kati ya watu walioathiri zaidi karne ya 20, hasa kwa sababu tangu mwanzo wa upapa wake alipambana na Ukomunisti uliotesa nchi yake asili na nyinginezo, akachangia kwa kiasi kikubwa kikomo chake na kusambaratika kwa Urusi.Vilevile alilaumu ubepari wa nchi za magharibi na kudai haki katika jamii zote, akitetea hasa uhai wa binadamu na uhuru wa dini.

  Upande wa dini, aliboresha uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ya Ukristo pamoja na ule na dini mbalimbali, kuanzia Uyahudi, Ubudha, Uislamu.

  Ziara zake 104 kati nchi 129 ulimwenguni kote, mbali na 146 nchini Italia na 317 katika parokia za Roma, zilikusanya mara nyingi umati mkubwa (hadi zaidi ya milioni 4 huko Manila, Ufilipino, mwishoni mwa siku ya kimataifa ya vijana), na kumfanya asafiri kuliko jumla ya mapapa wote waliomtangulia, akiwa mmojawapo kati ya viongozi wa dunia waliosafiri zaidi.

  Papa Wojtyła alitangaza wenye heri 1,340 na watakatifu 483, ili kuwapa Wakristo wa leo vielelezo mbalimbali kwa maisha yao ili walenge utakatifu walioitiwa na Mungu. Idadi hiyo ni kubwa kuliko ile ya waliotangazwa na jumla ya Mapapa wote waliomtangulia walau katika karne tano za mwisho.Alikuwa anaongea lugha mbalimbali, zikiwemo za Kipolandi, Kiitalia, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kiukraina, Kirusi, Kiserbokroatia, Kiesperanto, Kilatini na Kigiriki cha kale.Yohane Paulo II alitangazwa na mwandamizi wake Papa Benedikto XVI kuwa mwenye heri tarehe 1 Mei 2011, halafu Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014.

  Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Oktoba, kulingana na siku ya kuanza rasmi huduma yake ya Kipapa kwa Misa iliyofanyika katika uwanja mbele ya Basilika la Mt. Petro, Vatikani.

  Tuva

  Tuva (kwa Kirusi: Тыва) ni jina la jamhuri mojawapo ndani ya Shirikisho la Urusi. Iko katika Siberia ya kusini, kwenye kitovu cha kijiografia cha Asia.

  Imepakana na nchi ya Mongolia upande wa kusini na maeneo yafuatayo ya Shirikisho la Urusi: Jamhuri ya Altai, Jamhuri ya Khakassia, mikoa ya Krasnoyarsk Krai, Irkutsk Oblast na Jamhuri ya Buryatia.

  Mji mkuu wake ni Kyzyl.

  Idadi ya wakazi ni 307,930 (sensa ya mwaka 2010).

  Kuanzia 1921 hadi 1944 Tuva ilikuwa nchi huru ya kujitegemea iliyojulikana kwa jina la Tannu Tuva. Mwaka 1944 iliingizwa katika Umoja wa Kisoveti na kuwa sehemu ya Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi, na baada ya anguko la Ukomunisti sehemu ya Shirikisho la Urusi.

  Umaksi

  Umaksi (pia: Umarksi, Umarx, kwa Kiingereza Marxism) ni falsafa ambayo inafuata uyakinifu na inakusudia kuleta maendeleo ya haraka katika jamii kuanzia uchumi unaotazamwa kuwa msingi wa mahusiano yote.

  Lengo kuu ni kuondoa matabaka katika jamii na kuleta usawa katika ya binadamu. Njia ni kuwawezesha wanyonge kudai haki zao kwa kuungana na kuleta mapinduzi dhidi ya wanyonyaji.

  Katikati ya karne ya 19, waanzilishi wa jitihada hizo walikuwa Wajerumani wawili: Karl Marx na Friedrich Engels. Jina Umaksi linatokana na wa kwanza kati yao, Marx.

  Umaksi uliendelezwa na watu mbalimbali hasa katika karne ya 20 kadiri siasa hiyo ilivyozidi kuenea duniani, hadi kuongoza maisha ya theluthi ya binadamu wote. Kati yao, Vladimir Ilich Lenin, Leon Trotsky, Joseph Stalin nchini Urusi na Mao Zedong huko China.

  Baada ya ukomunisti kushindikana Ulaya Mashariki pamoja na Urusi kusambaratika (1989), mvuto wa falsafa hiyo umepungua sana.

  Vladimir Lenin

  Vladimir Ilyich Lenin (Влади́мир Ильи́ч Ле́нин) alikuwa na jina la kiraia Vladimir Ilyich Ulyanov (Влади́мир Ильи́ч Улья́нов) (*10 Aprili (22 Aprili ya kalenda ya Gregori) 1870 - + 21 Januari 1924) alikuwa mwanasiasa nchini Urusi na kiongozi wa chama cha Bolsheviki akaendesha awamu la kikomunisti la Mapinduzi ya Urusi ya 1917 akaanzisha Umoja wa Kisovyeti. Mafundisho yake yalikuwa msingi wa itikadi ya Ulenin.

  Lenin alizaliwa katika familia tajiri katika mji wa Simbirsk, (sasa unaitwa Ulyanovsk), Lenin alianza kupendelea mapinduzi baada ya kaka yake kuuliwa mwaka wa 1887. Alipofukuzwa kutoka Chuo Kikuu cha Kazan kwa maandamano ya kuipinga serikali ya Tsar, alijishughulisha kupata shahada ya sheria katika miaka iliyoufuata.

  Alianza kutumia jina la "Lenin" kama jina la siri alipojiunga na upinzani dhidi ya serikali ya kifalme ya Kirusi. Hakuna uhakika kama alilitumia kama kumbukumbu kwa mlezi wake alipokuwa mtoto au kutokana na mto Lena katika jimbo la Siberia alipohamishwa ufungoni 1897 baada ya kushiriki katika upinzani dhidi ya serikali.

  Lenin aliaga dunia mjini Nizhny Novgorod (Gorki karibu na Moskva) tar. 21 Januari 1924. Maiti yake ilihifadhiwa kwa madawa na kuonyeshwa katika kaburi kubwa kwenye uwanja nyekundu mjini Moskva. Kiongozi aliyemfuata alikuwa Josef Stalin.

  Lugha zingine

  This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
  Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
  Images, videos and audio are available under their respective licenses.