Uhamisho wa Babeli

Uhamisho wa Babeli unamaanisha kipindi cha Wayahudi kulazimishwa na Wababuloni kuishi ugenini hasa baada ya Yerusalemu kutekwa na kuangamizwa na mfalme Nebukadreza II.

Tissot The Flight of the Prisoners
James Tissot, Mateka Kuhama.

Matukio

Wayahudi walipelekwa uhamishoni kwa awamu tatu: 597 KK, 586 KK na 582 KK. Ingawa wengine tena walikimbilia Misri, baadhi waliweza kubaki nchini Yuda.

Uwezekano wa kurudi ulipatikana tena Babuloni yenyewe ilipotekwa na Koreshi Mkuu, mfalme wa Uajemi (539 KK). Huyo aliwaruhusu warudi kwao na kujenga upya hekalu la Yerusalemu.

Hata hivyo waliokubali hawakuwa wengi, nao walirudi vilevile kwa awamu. Kati yao kulikuwa na asilimia ya makuhani na Walawi kuliko kawaida, kutokana na uhusiano wao na ibada hekaluni.

Wayahudi wengine waliona maisha huko Mesopotamia yamekuwa na maendeleo kuliko yale ya awali nchini kwao.

Maana ya kidini

Vitabu mbalimbali vya Biblia vinahusika na matukio hayo kama ifuatavyo.

Utabiri wake unapatikana hasa katika kitabu cha Yeremia, lakini pia katika Kitabu cha Ezekieli, bila kusahau Kumbukumbu la Sheria ambamo Musa alihimiza Waisraeli kushika masharti ya Agano la Mlima Sinai ili wapate baraka na kukwepa laana.

Uchungu uliofuata unaelezwa kishairi na Kitabu cha Maombolezo.

Sababu zinafafanuliwa hasa na Vitabu vya Wafalme, Mambo ya Nyakati, Kitabu cha Ezra na Kitabu cha Nehemia.

Vyote vinalaumu dhambi kama chanzo cha maangamizi hayo.

Hata hivyo vinatia tumaini kwa kusisitiza uaminifu wa Mungu ambao ni wa milele.

Viungo vya nje

Ramani

Vitabu

Bible.malmesbury.arp.jpg Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uhamisho wa Babeli kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
587 KK

Makala hii inahusu mwaka 587 KK (kabla ya Kristo).

Babeli

Babeli ulikuwa mji wa kale katika Mesopotamia, muhimu kwa karne nyingi kama mji mkuu wa milki zilizotawala maeneo makubwa ya Mashariki ya Kati.

Inatajwa mara nyingi katika Biblia, hasa kwa jina la Babuloni.

Maghofu yake hupatikana karibu na mji wa kisasa wa Al Hillah (Irak) kando ya mto Frati km 90 kusini kwa Baghdad.

Hekalu

Hekalu ni jengo la dini mbalimbali, lakini si zote.

Nyingine zinaita maabadi yao kwa majina tofauti, kutokana na mtazamo wa msingi.

Kwa mfano katika Uislamu jengo la ibada linaitwa msikiti.

Isaya III

Isaya III ni jina lililobuniwa na wataalamu wa Biblia ili kumtaja mwandishi asiyejulikana wa sura 56-66 za kitabu cha Isaya, ingawa wengine wanadhani ni waandishi zaidi ya mmoja.

Sura hizo zinakadiriwa kuwa ziliandikwa baada ya uhamisho wa Babeli (500 hivi K.K.) na zinawakaribisha watu wa mataifa yote kujiunga na Israeli katika kumuabudu Mungu pekee.

Kiini chake ni 61:1-3.

Karne ya 6 KK

Karne ya 6 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 600 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 501 KK.

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Esta

Kitabu cha Esta (jina lake huandikwa pia Ester na "Esther") ni kitabu cha Biblia ya Kiebrania, na hivyo pia cha Agano la Kale, ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo. Kiliandikwa kwanza kwa Kiebrania.

Tafsiri ya kitabu cha Esta inavyopatikana katika Septuaginta imeongezewa sana; nyongeza hizo za Kigiriki zinahesabiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kuwa sehemu za kitabu yenye uvuvio wa Roho Mtakatifu ingawa si sehemu za hadithi asili. Ni katika nyongeza hizo tu kwamba Mungu anatajwa na mtazamo wa imani unajitokeza.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Ezra

Kitabu cha Ezra kinapatikana katika Biblia ya Kikristo katika Agano la Kale.

Kiasili kiliandikwa kwa lugha ya Kiebrania lakini kuna pia sehemu fupi za Kiaramu.

Andiko la Ezra lilitunzwa katika Biblia ya Kiebrania pamoja na Nehemia kama kitabu kimoja lakini kimegawiwa baadaye kuwa vitabu viwili ambavyo Vulgata inavitaja kama "Esdras I" na "Esdras II".

Kitabu kinasimulia habari za Wayahudi chini ya utawala wa Waajemi.

Mwaka 587 KK mfalme wa Babeli alikuwa amevamia mji wa Yerusalemu, kubomoa hekalu la Sulemani na kumaliza ufalme wa Yuda. Wakazi walipelekwa Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli. Tangu wakati huo Waisraeli kwa kawaida walijulikana kuwa Wayahudi. Lakini, kwa kuwa utengano wa Israeli haukuendelea, majina hayo mawili, pamoja na jina la Waebrania, yaliweza kutumiwa kwa watu walewale (Yer 34:9; Yn 1:19, 47; 2 Kor 11:22; Gal 2:14).

Mwaka 539 KK Waajemi chini ya mfalme Koreshi walivamia Babeli ambayo ikawa jimbo la milki ya Uajemi. Koreshi aliwaruhusu Wayahudi kadhaa warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu.

Habari hizi na zilizofuata zinasimuliwa katika vitabu vya Ezra na Nehemia.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Hagai

Kitabu cha Hagai ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh, yaani Biblia ya Kiebrania. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Pili cha Wafalme

Kitabu cha pili cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 25.

Kitabu cha Zekaria

Kitabu cha Zekaria ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh, yaani Biblia ya Kiebrania. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mambo ya Nyakati

Mambo ya Nyakati ni jina la maandiko yanayoheshimiwa na dini za Uyahudi na Ukristo kama matakatifu, yaani yenye uvuvio wa Roho Mtakatifu wa Mungu.

Maombolezo (Biblia)

Kitabu cha Maombolezo (kwa Kiebrania איכה, eikha) ni kama nyongeza ya kitabu cha nabii Yeremia katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia katika Agano la Kale iliyo sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kichwa chake kinadokeza kwamba ni mashairi matano ya uchungu kuhusu maangamizi ya Yerusalemu (587 K.K.) na uhamisho wa Babeli uliofuata kwa Wayahudi wengi.

La kwanza, la pili na la nne yanazingatia utaratibu wa kwamba kila mstari unaanza na herufi tofauti kufuatana na alfabeti ya Kiebrania yenye herufi 22.

Katika mashairi hayo matano inaonekana toba halisi iliyotokana na tukio hilo lililotazamwa kuwa adhabu ya Mungu kwa dhambi za taifa lake.

Hatujui yametungwa na nani.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Masiya

Masiya (au Masiha), kutoka Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ mashiakh, maana yake Mpakwamafuta ni jina la heshima ambalo Biblia inampa mfalme au kuhani aliyewekwa wakfu kwa Mungu kwa kupakwa mafuta atende kwa niaba yake kazi ya kusaidia taifa lake hasa kwa kulikomboa.Tofauti na kawaida, Biblia inamtaja kama Masiha hata mfalme Koreshi Mkuu wa Uajemi kwa sababu Mungu alimtumia kutoa Wayahudi katika uhamisho wa Babeli na kuwaruhusu warudi Yerusalemu na kujenga upya hekaluHata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani

Mazingira ya Yesu

Mazingira ya Yesu ni jumla ya mambo ya kijiografia na ya kihistoria yaliotangulia au kuendana na maisha ya Yesu Kristo, akimuathiri kama binadamu katika namna yake ya kuwaza, kusema na kutenda.

Ni muhimu kuyajua ili kumuelewa zaidi mwenyewe, kazi yake na ujumbe wake.

Nabii Hagai

Nabii Hagai (kwa Kiebrania חַגַּי, Ḥaggay au "Hag-i", yaani sikukuu yangu; kwa Kigiriki: Ἀγγαῖος; kwa Kilatini Aggeus) ni mmojawapo kati ya wa manabii wa Israeli, aliyefanya kazi miezi ya mwisho ya mwaka 520 KK tu, akihimiza pamoja na nabii Zekaria ujenzi mpya wa hekalu la Yerusalemu baada ya Wayahudi kurudi toka uhamisho wa Babeli.

Hatimaye kazi ilikamilika na hekalu likatabarukiwa mwaka 515 KK.

Nabii Zekaria

Zekaria (kwa Kiebrania זְכַרְיָה, Zekaria, "YHWH amekumbuka"; kwa Kigiriki Ζαχαρίας, Zakharias; kwa Kilatini Zacharias; kwa Kiarabu زكريا Zakariya' au Zakkariya) alikuwa kuhani wa Israeli, pianabii wa Mungu mjini Yerusalemu kati ya mwaka 520 KK na 518 KK.

Habari zake zinapatikana hasa katika kitabu chake, cha 11 kati ya vile 12 vya Manabii Wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo.

Humo (Zek 1:1) anajitambulisha kama "mwana wa Berakia, mwana wa Iddo", ingawa kitabu cha Ezra (Ezra 5:1 na 6:14) kinamuita tu "mwana wa Iddo".

Kazi ya nabii huyo, iliyoanza wakati uleule alipotabiri nabii Hagai, ni mwanzo wa kipindi cha mwisho cha unabii katika Israeli kabla ya ujio wa Yohane Mbatizaji na Yesu Kristo.

Tofauti na Hagai, Zekaria hakuishia upande wa ujenzi mpya wa hekalu la Yerusalemu, bali alisisitiza pia utakaso wa waamini na ibada zao.

Nebukadreza II

Nebukadreza II alikuwa mfalme wa Babeli katika karne ya 6 KK.

Alitawala sehemu kubwa ya Mashariki ya kati kuanzia mwaka 604 KK mpaka 562 KK.

Ni maarufu hasa kwa sababu aliwahi kuuvunja mji wa Yerusalemu mwaka 587 KK na kuwapeleka sehemu kubwa ya Wayahudi katika uhamisho wa Babeli.

Ndiye aliyejenga bustani za kupendeza katika enzi hizo zinazojulikana kama bustani za kuning'inia za Babeli, ambazo ni moja ya maajabu saba ya dunia.

Yesu

Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).

Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.

Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.