Ufalme wa Italia

Ufalme wa Italia (kwa Kiitaliaː Regno d'Italia) ni jina rasmi la nchi ya Italia miaka 1861-1946, yaani tangu rasi hiyo ilipounganishwa kwa kiasi kikubwa chini ya ukoo wa Savoia hadi wananchi walipopiga kura na kuamua iwe jamhuri.

Miaka hiyo Italia ilishiriki vita mbalimbali ili kukamilisha umoja wa rasi na kuteka maeneo mengine.

Baada ya kufaulu kwanza, vita vikuu vya pili vilimalizika kwa Italia kushindwa na kunyang'anywa maeneo mengi, hata ya rasi yake.

Italian empire 1940
Dola la Italia mwaka 1940.

Wafalme

 • Vittorio Emanuele II (1861–1878)
 • Umberto I (1878–1900)
 • Vittorio Emanuele III (1900–1946)
 • Umberto II (1946)

Marejeo

 • Ashley, Susan A. Making Liberalism Work: The Italian Experience, 1860–1914 (2003) excerpt and text search
 • Baran'ski, Zygmunt G. & Rebecca J. West (2001). The Cambridge companion to modern Italian culture, Cambridge: Cambridge University Press, ISBN 0-521-55034-3.
 • Barclay, Glen St. J. 1973. The Rise and Fall of the New Roman Empire. London: Sidgwick & Jackson.
 • Bosworth, Richard J. B. 1983. Italy and the Approach of the First World War. London: The Macmillan
 • Bosworth, Richard J. B. 2007. Mussolini's Italy: Life Under the Fascist Dictatorship, 1915–1945 excerpt and text search
 • Clark, Martin. 1996. Modern Italy: 1871–1995. (2nd ed. Longman)
 • Coppa, Frank J. (1970). "Economic and Ethical Liberalism in Conflict: The extraordinary liberalism of Giovanni Giolitti", Journal of Modern History (1970) 42#2 pp 191–215 in JSTOR
 • Coppa, Frank J. (1971) Planning, Protectionism, and Politics in Liberal Italy: Economics and Politics in the Giolittian Age online edition
 • Davis, John A., ed. 2000, Italy in the Nineteenth Century: 1796–1900 Oxford University Press. online edition
 • de Grazia, Victoria. 1981. The Culture of Consent: Mass Organizations of Leisure in Fascist Italy.
 • de Grazia, Victoria. 1993. How Fascism Ruled Women: Italy, 1922–1945 excerpt and text search
 • De Grand, Alexander J. (2001). The hunchback's tailor: Giovanni Giolitti and liberal Italy from the challenge of mass politics to the rise of fascism, 1882–1922, Greenwood. online edition; excderpt and text search
 • Duggan, Christopher (2008). The Force of Destiny: A History of Italy Since 1796, Houghton Mifflin Harcourt, text search
 • Gentile, Emilio. 2003. The Struggle For Modernity: Nationalism, Futurism and Fascism. Westport, CT: Praeger.
 • Gilmour, David. 2011. The Pursuit of Italy: A History of a Land, Its Regions, and Their Peoples excerpt and text search
 • Hughes, Robert. 2011. Rome: A Cultural, Visual, and Personal History
 • Killinger, Charles L. (2002). The history of Italy, Westport (CT): Greenwood Press, text search
 • Pauley, Bruce F. 2003. Hitler, Stalin, and Mussolini: Totalitarianism in the Twentieth Century. Wheeling: Harlan Davidson
 • Pollard, John F. 1985. The Vatican and Italian Fascism, 1929–32. Cambridge, USA: Cambridge University Press.
 • Salomone, A. William. 1945. Italy in the Giolittian Era: Italian Democracy in the Making, 1900–1914
 • Sarti, Roland (2004). Italy: A Reference Guide from the Renaissance to the Present, New York: Facts on File text search
 • Sarti, Roland. 1974. The Ax Within: Italian Fascism in Action. New York: New Viewpoints.
 • Seton-Watson, Christopher (1967). Italy from Liberalism to Fascism, 1870–1925, New York: Taylor & Francis, text search
 • Smith, Dennis Mack. 1997. Modern Italy; A Political History. Ann Arbor: The University of Michigan Press.
 • Thayer, John A. 1964. Italy and the Great War. Madison and Milwaukee: University of Wisconsin Press.

Historiografia

 • Albanese, Giulia. "Reconsidering the March on Rome," European History Quarterly (2012) 42#3 pp 403–421.
 • Keserich, Charles. "The Fiftieth Year of the" March on Rome": Recent Interpretations of Fascism." History Teacher (1972) 6#1 pp: 135-142 in JSTOR.

Vyanzo

 • Mussolini, Benito. 1935. Fascism: Doctrine and Institutions. Rome: Ardita Publishers.

Viungo vya nje

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ufalme wa Italia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Firenze

Firenze (Kiing. Florence) ni mji katika Italia na makao makuu ya mkoa wa Toscana. Kati ya 1865 hadi 1870 ilikuwa pia mji mkuu wa Ufalme wa Italia. Mji uko kando la mto Arno. Idadi ya wakazi ni mnano 400,000 na pamoja na rundiko la mji ni takriban 600,000.

Katika karne ya enzi za kati Firenze ilikuwa kituo muhimu cha biashara, uchumi na utamaduni katika Ulaya. Ni kati ya miji ambako uchumi wa benki ulijitokeza.

Firenza hutajwa mara nyingi kama chanzo cha kipindi cha "Renaissance" yaani kuzaliwa upya kwa utamaduni wa kale katika Ulaya. Wakati ule ulitawaliwa na familia ya Medici. Mji umepabwa na majengo mazuri sana yanayojaa picha za kupendeza. Wasanii wengi walio muhimu katika utamaduni wa Ulaya waliishi Firenze kama vile Donatello, Botticelli, Michelangelo na Leonardo da Vinci. Pia watu kama mwanafalsafa wa kisiasa Machiavelli, mpelelezi wa Amerika Amerigo Vespucci na mwanasayansi Galileo Galilei waliishi Firenze.

Historia ya Italia

Historia ya Italia inahusu eneo la rasi ya Italia, hasa linalounda leo Jamhuri ya Italia.

Akiolojia imethibitisha uwepo wa Homo neanderthaliensis miaka 200,000 hivi iliyopita. Homo sapiens sapiens alifika miaka 40,000 hivi iliyopita.

Kufikia milenia ya 1 KK wakazi wengi walikuwa wa jamii ya Kizungu na kutumia lugha za Kihindi-Kiulaya.

Peninsula ya Italia iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 KK), lakini hiyo ilipoenea Ulaya kusini na magharibi, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa kama Dola la Roma.

Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa jiji la Roma uliofanywa na Wagermanik (476 BK) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu aliyetawala sehemu ya kaskazini tu.

Juhudi za kuurudisha umoja zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia uliteka sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870) na kubadilika kuwa Ufalme wa Italia wenye makao makuu Roma.

Baada ya vita vikuu vya pili iligeuka Jamhuri yenye katiba inayotia mamlaka kuu mikononi mwa bunge.

Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa ya pamoja (Euro).

Italia

Jamhuri ya Italia (kwa Kiitalia: Repubblica Italiana) ni nchi ya Ulaya Kusini inayoenea katika sehemu kubwa ya Rasi ya Italia na baadhi ya visiwa vya jirani kwenye Bahari ya Kati.

Eneo lake ni km² 302,072.84 ambalo lina wakazi 60,483,973 (31-12-2017): ni nchi ya 23 duniani kwa wingi wa watu, lakini ya 8 au 9 kwa uchumi.

Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia. Nchi huru mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia pande zote ni San Marino na Vatikano.

Makao makuu ni jiji la Roma, lenye umuhimu mkubwa katika historia ya dunia nzima.

Mapatano ya Laterano

Mapatano ya Laterano kati ya Ufalme wa Italia na Ukulu mtakatifu yanaitwa hivyo kwa sababu yalisainiwa katika jumba la Laterano tarehe 11 Februari 1929.

Lengo lake lilikuwa kumaliza suala la Roma lililovuruga Italia tangu mwaka 1870, nchi hiyo ilipoteka mji huo uliotawaliwa na Mapapa kwa karne nyingi.

Kwa mapatano hayo, Papa alikubali mji ubaki mikononi mwa Ufalme, isipokuwa mtaa wa Vatikano na majengo mengine machache. Ndivyo ilivyoundwa na kukubalika kimataifa nchi huru ya Mji wa Vatikani iliyomwezesha Papa kuwa huru katika kuongoza Kanisa Katoliki duniani kote.

Mapatano hayo yaliheshimika hata baada ya serikali ya Ufashisti kuanguka, Italia kugeuka Jamhuri na katiba mpya kutungwa. Tena hiyo ilijumlisha mapatano hayo ndani yake.

Milano

Milano (pia Milan) ni mji mkubwa wa Italia ya kaskazini mwenye wakazi milioni 1.3. Rundiko la mji lina wakazi milioni 7.5. Ni mji mkuu wa eneo la Lombardia na kitovu cha uchumi na utamaduni.

Papa

Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa (samaki)

Papa (neno la mkopo kutoka Kilatini lakini lenye asili ya Kigiriki, πάππας, pappas, jina ambalo mtoto anamuitia baba yake)ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.

Roma

Roma (pia: Rumi) ndio mji mkuu ("Roma Capitale") wa Jamhuri ya Italia.

Uko katika makutano ya mito ya Tiber na Aniene karibu na Bahari ya Mediteranea.

Roma una wakazi milioni 2,870,336 katika eneo la km² 1,287.36.

Ndani ya mji wa Roma lipo eneo la mji wa Vatikano ambao ni nchi ya kujitawala chini ya Papa wa Kanisa Katoliki.

Taji

Taji (kwa Kiingereza "crown") ni mfano wa bangili ambalo linavaliwa kichwani na baadhi ya viongozi, kama vile mfalme na askofu katika matukio fulani muhimu.

Linamaanisha mamlaka yake.

Kadiri ya Injili, kwa dhihaka Yesu alivikwa taji la miba ambalo lilimtia uchungu na maumivu makali siku ya Ijumaa kuu.

Pengine watawa wa kike wanavalishwa taji la nadhiri katika sikukuu zao.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.