Tunisia

Tunisia (kirefu Jamhuri ya Tunisia - kwa Kiarabu الجمهرية التونسية, al-Jumhūrīya at-Tūnisīya) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini inayopakana na Bahari ya Mediteranea, Libya na Algeria.

Mji mkuu ni Tunis (wakazi 728 453) ulioko mahali pa Karthago ya kale.

Tunisia sm03
Ramani ya Tunisia

Historia

Tunisia iliwahi kutawaliwa na Wafinikia walioanzisha huko mji wa Karthago.

Baada ya hao kushindwa na Roma ya Kale, ilikuwa jimbo la "Africa" katika Dola la Roma.

Kisha eneo lake likatawaliwa na Wavandali, Waarabu, Wahispania, Waturuki na Wafaransa.

Tarehe 20 Machi 1956 ilipata uhuru.

Watu

Wakazi karibu wote (98%) wanajiita Waarabu na hutumia lugha ya Kiarabu ambacho ndicho lugha rasmi. Hata hivyo damu yao ni mchanganyiko hasa wa ile ya Waberber, Waarabu na Waturuki.

Takriban watu 200,000, hasa kusini, wanaendelea kuzungumza Kiberber ambacho ni lugha asili ya wenyeji lakini Waberber wengi wamezoea kutumia Kiarabu.

Katika elimu na biashara Kifaransa kinatumika pia sana.

Upande wa dini, Uislamu unafuatwa na asilimia 98 za wakazi, nao ndio dini rasmi. Waliobaki ni Wakristo, hasa Wakatoliki, na Wayahudi.

Tazama pia

Viungo vya nje

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tunisia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Afrika

Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.

Algeria

Algeria (pia: Aljeria ; kwa Kiarabu: الجزائر al-Jazā’ir; kwa Kiberber: Dzayer, ⴷⵣⴰⵢⴻⵔ) au kwa jina rasmi "Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Algeria" ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na bahari ya Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger, Libya na Tunisia.

Algeria ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa la Sahara.

Jina la nchi limetokana na mji mkuu unaoitwa kwa jina lilelile "al-jaza-ir" kama nchi ya leo kwa lugha ya Kiarabu.

Bahari ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

Dativus

Dativus wa Abitina alikuwa mmojawapo katika kundi la Wakristo 49 ambao mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, walihukumiwa kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae, mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).

Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.

Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuisi bila ya Bwana").

Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Februari.

Historia ya Tunisia

Historia ya Tunisia inahusu eneo la Afrika Kaskazini ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Tunisia.

Tunisia iliwahi kutawaliwa na Wafinikia walioanzisha huko mji wa Karthago.

Baada ya hao kushindwa na Roma ya Kale, ilikuwa jimbo la "Africa" katika Dola la Roma.

Kisha eneo lake likatawaliwa na Wavandali, Waarabu, Wahispania, Waturuki na Wafaransa.

Tarehe 20 Machi 1956 ilipata uhuru.

Karthago

Karthago (kwa Kilatini Carthago; kwa Kigiriki Καρχηδών Karchēdōn; katika lugha asilia ya Kifinisia Qart-Hadašt, yaani "mji mpya") zaidi ya miaka 2000 iliyopita ulikuwa mji mkubwa katika Afrika ya Kaskazini karibu na Tunis ya leo nchini Tunisia.

Kiarabu

Kiarabu (ar.: العَرَبِيَّة‎‎, al-ʻarabiyyah, kwa kirefu al-luġatu al-ʿarabiyya ) ni lugha ya Kisemiti inayotumiwa na watu milioni 206 kama lugha ya kwanza na milioni 246 wa ziada kama lugha ya pili. Ilhali kuna lahaja nyingi, Kiarabu sanifu (ar. الفصحى fuṣḥā) ni lugha rasmi ya nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ya Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa. Kuna pia matumizi kama lugha ya kidini katika Uislamu.

Hivyo Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani ikisomwa kwa viwango tofauti na mamilioni ya waumini Waislamu wakielekea kujifunza na kuelewa kitabu cha Korani. Kama lugha ya kidini ina athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofautitofauti walio Waislamu.

Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno), ufasaha mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau.

Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo, mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafudhi.

Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isitetereke wala kubadilika na kupotea kama lugha nyingine nyingi, leo, baada ya miaka zaidi ya elfu, imebaki thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoandikwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbalimbali zinazotumika na Waarabu wa sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi hayo yaendelee kufahamika milele.

Leo, Kiarabu ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina, Kihindi, Kihispania, Kiingereza na Kibengali.

Umuhimu wa lugha hii unazidi kukua kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Afrika, Asia na Ulaya) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini).

Kifaransa

Kifaransa (kwa Kifaransa: français) ni lugha ya Ufaransa (pamoja na maeneo yake ya ng'ambo), Ubelgiji ya Kusini, Uswisi ya Magharibi, Luxemburg na Kanada. Inazungumzwa pia katika nchi nyingi za Afrika kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Senegal, Mali, Shelisheli, Chad, n.k., Asia ya Kusini na Amerika zilizokuwa koloni za Ufaransa.

Libya

Libya ni nchi ya Afrika ya Kaskazini kwenye Bahari ya Mediteraneo, inayopakana na Misri, Sudan, Niger, Chad, Algeria na Tunisia.

Eneo kubwa la nchi ni sehemu ya jangwa la Sahara. Chini yake kuna akiba kubwa ya petroli, ambayo ndiyo utajiri wa nchi.

Miji mikuu ni Tripoli, Benghazi na Misratah.

Maximianus wa Abitina

Maximianus wa Abitina ni jina la mmojawapo katika kundi la Wakristo 49 ambao mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, walihukumiwa kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae, mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).

Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.

Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuisi bila ya Bwana").

Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Februari.

Milki ya Osmani

Milki ya Osmani (pia: Ottomani) ilikuwa dola kubwa lililotawala upande wa mashariki wa Mediteranea pamoja na nchi nyingi za Mashariki ya Kati kati ya karne ya 14 na mwaka 1922.

Milki ilianzishwa na Waturuki Waosmani ikachukua nafasi ya ukhalifa wa Waabbasi na Milki ya Bizanti.

Mji wake mkuu ulikuwa Konstantinopoli (leo: Istanbul) na mtawala wake mkuu alikuwa Sultani wa Waosmani. Imani rasmi ya milki ilikuwa Uislamu hata kama katika maeneo mengi idadi kubwa ya wakazi walikuwa Wakristo.

Tabaka la viongozi wa kisiasa na wa kijeshi walikuwa Waosmani waliokuwa Waturuki pamoja na mchanganyiko wa Waislamu kutoka sehemu zote za milki yao, hasa Balkani. Kwenye uwanja wa uchumi na utawala Waosmani walitumia sana Wakristo Wagiriki na Waarmenia kutokana na elimu yao.

Orodha ya Watakatifu wa Afrika

Hii Orodha ya Watakatifu wa Afrika inataja watu wanaoheshimiwa na Kanisa Katoliki au madhehebu mengine yoyote ya Ukristo kama watakatifu ambao walizaliwa, waliishi au walifariki barani humo (katika mabano mara nyingi inatajwa nchi ya leo).

Sahara

Sahara ni jangwa kubwa kaskazini mwa Afrika. Ni jangwa kubwa kabisa barani, ni la kwanza duniani kati ya majangwa joto na jangwa la tatu kwa ukubwa ulimwenguni baada Bara la Antaktiki na Aktiki.Ina eneo la kilometa za mraba 9,200,000, sawa na eneo la Marekani au karibu sawa na eneo lote ya Ulaya.

Jina lake ni neno la Kiarabu (صحراء, sahra') linalomaananisha "jangwa".

Sahara inafunika sehemu kubwa ya Afrika Kaskazini isipokuwa kanda lenye rutuba kwenye ufuko wa Bahari Mediteranea, milima ya Atlas kwenye Maghreb na bonde la mto Naili huko Misri na Sudan. Inaenea kuanzia Bahari ya Shamu upande wa mashariki hadi Atlantiki upande wa magharibi, na kutoka Mediteranea upande wa kaskazini hadi kanda la Sahel upande wa kusini.

Wataalamu wa jiografia husema Sahara haikuwa hivyo wakati wote. Kutokana na utafiti wa dalili katika udongo na mawe yake eneo la Sahara katika milenia zilizopita lilikuwa na vipindi vya ukame vikifuatana na vipindi vya mvua.

Saturninus wa Abitina

Saturninus wa Abitina alikuwa padri aliyeongoza Wakristo 48 ambao mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, walihukumiwa kufa kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae, mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).

Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.

Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuishi bila ya Bwana").

Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Februari.

Tunis

Tunis (kwa Kiarabu: تونس ) ni mji mkuu wa Tunisia na mji mkubwa nchini ikiwa na wakazi 728,463 (mwaka 2004) ambao pamoja na wakazi wa mitaa ya nje wanafikia jumla ya milioni 1.6.

Mji uko ufukoni mwa Mediteranea, karibu na Karthago ya Kale.

Uislamu nchini Tunisia

Uislamu ni dini rasmi ya dola nchini Tunisia. Imekadiriwa ya kwamba sehemu kubwa ya Watunisia hujisebia kuwa ni Waislamu, japokuwa hapajawahi kuwa na sensa ya jambo hilo. Waumini wengi nchini ni wale wa dhehebu la Sunni wanaofuata mafundisho ya imamu Maliki, lakini idadi ndogo kabisa ni Ibadhi.

Viktoria wa Abitina

Viktoria wa Abitina alikuwa bikira wa Karthago aliyeuawa pamoja na Wakristo wenzake 48 mwaka 304, wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian, kwa kuadhimisha Siku ya Bwana huko Abitinae, mji wa Afrika Kaskazini (leo Tunisia).

Tarehe 24 Februari mwaka 303, Diokletian alikuwa ametangaza hati yake ya kwanza dhidi ya Wakristo, akiagiza uteketezaji wa Biblia na maabadi ya Kikristo katika Dola la Roma lote, pamoja na kukataza Wakristo wasikutane kwa ajili ya ibada.Ingawa Fundanus, askofu wa Abitinae, alikubali kukabidhi maandiko matakatifu ya Kanisa kwa serikali, baadhi ya waamini waliendelea kukutana kwa siri chini ya padri Saturninus. Basi, walikamatwa na kupelekwa na mahakimu wa huko hadi Karthago, makao makuu ya mkoa, kwa ajili ya hukumu.Tarehe 12 Februari gavana Anullinus alisikiliza kesi. Mmoja wa watuhumiwa, Dativus, alikuwa mjumbe wa senati. Ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhojiwa, kuteswa na hatimaye kufa.Saturninus alifuata na kushika msimamo katika kuteswa. Wote walifanya vilevile, wanaume kwa wanawake wakiwemo watoto wake 4.

Kati ya majibu waliyotoa hao wafiadini, moja limetajwa mara nyingi: Emeritus, aliyekuwa mwenyeji wa wenzake, alipoulizwa kwa nini aliwakaribishwa kwa ibada kinyume cha sheria, alijibu: "Sine dominico non possumus" ("Hatuwezi kuishi bila ya Bwana").

Tangu kale wafiadini hao wote wanaheshimiwa kama watakatifu.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 12 Februari.

Wavandali

Wavandali walikuwa kabila kubwa la Kigermanik la mashariki ambao katika karne tano za kwanza BK walihama kutoka sehemu za Poland ya leo hadi Afrika ya Kaskazini wakiunda Ufalme wao katika maeneo ya Algeria na Tunisia ya leo, pamoja na kutawala visiwa vya Mediteraneo magharibi.

Wilaya

Wilaya ni mgawanyo wa kiutawala au eneo lililotengwa kwa ajili ya utawala. Mikoa ya Tanzania na Kenya imegawiwa kwa wilaya.

Asili ya neno ni Kiarabu "ولاية" (wilaayatun - Kituruki: vilayet). Katika Dola la Osmani "vilayet" ilikuwa ngazi ya kwanza ya mgawanyo wa kiutawala ikimaanisha jimbo au mkoa. Mkuu wake au gavana alikuwa na cheo cha "Wali". Neno hili la "wilaya" limepatikana katika nchi nyingi zilizoathiriwa na utamaduni wa Uislamu au lugha ya Kiarabu kama vile Uturuki, Algeria, Tunisia, Oman, Mauritania, Sudan, Malaysia, Indonesia, Afghanistan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan.

Katika Kiarabu cha Kisasa "wilaayatun" inamaanisha pia dola ndani ya shirikisho - kwa mfano madola kama vile Texas ndani ya Marekani.

Katika matumizi ya Kiswahili huko Kenya na Tanzania "wilaya" imekuwa mgawanyo wa ngazi ya pili yaani ni kitengo chini ya ngazi ya kwanza ya mikoa. Vitengo vya wilaya ni tarafa. Na vitengo vya tarafa ni kata zinazoitwa shehia katika Zanzibar na chini yake vijiji au mitaa.

Algeria ni nchi nyingine ambako wilaya inamaanisha ngazi ya pili ya kiutawala.

Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU)

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.