Stani

Stani ni elementi. Namba atomia yake ni 50 kwenye mfumo radidia na uzani atomia ni 118.710. Jina ni neno la kilatini stannum kwa metali hii.

Ni metali laini sana yenye rangi ya kifedha-kijivu. Huyeyuka mapema kwenye kiwango cha halijoto cha 505 °C. Hupatikana hasa kama oksidi katika mitapo.

Stani (stannum; kiing. tin)
Vipande vya stani
Vipande vya stani
Jina la Elementi Stani (stannum; kiing. tin)
Alama Sn
Namba atomia 50
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 118.710
Valensi 2, 8, 18, 18, 4
Densiti 7.31 g/cm³
Kiwango cha kuyeyuka 505.08 K (231.93 °C)
Kiwango cha kuchemka 2875 K (2602 °C)
Asilimia za ganda la dunia 3 · 10-3 %
Hali maada mango
Mengineyo Stani kwa mazingira ya wastani ina alotropi mbili au maumbo mawili yaani stani nyeupe na stani kijivu

Matumizi ya kihistoria

Katika historia ilikuwa kati ya metali za kwanza zilizotumiwa na binadamu katika teknolojia. Bronzi ambayo ni aloi ya shaba na stani ilikuwa metali ya kwanza ya vifaa vya kazi na silaha katika nchi nyingi kabla ya teknolojia ya chuma. Mahitaji ya stani yalikuwa sababu muhimu kwa Waroma kuvamia Britania penye migodi muhimu ya stani katika rasi ya Cornwall.

Matumizi ya kisasa

Matumizi ya stani duniani ni takriban tani 300,000 kwa mwaka.

Theluthi moja ya mahitaji ni kwa ajili ya aloi za lihamu kwa kazi za kulehemia. Matumizi haya yamezidi kuwa muhimu kutokana mahitaji makubwa ya kompyuta na vifaa vya elektroniki.

Stani haioksidiki kirahisi hewani na hujiunga na chuma. Hivyo theluthi nyingine ya mahitaji ya stani ni kama koti kwa mabati ya chuma au kwa bati za kopo ni kinga dhidi ya kutu.

Aloi

Aloi ni mchanganyiko wa elementi mbili au zaidi mwenye tabia ya kimetali; angalau elementi moja ndani yake ni metali pia.

Zatengenezwa kwa njia ya:

1) Kuyeyusha metali

2) Kuichanganya katika hali ya kiowevu pamoja nyongeza zote

3) Kupoza yote hadi imekuwa imara

Mifano ya aloi zinazotumiwa sana ni kama vile:

shaba nyeupe kutokana na 35% zinki na 65% shaba - yatumiwa kwa vyombo vya muziki na mapambo mengi

bronzi kutokana na 87% shaba na 13% stani - yatumiwa kwa parafujo, vyuma vya mashua

feleji kutokana na chuma pamoja na bati, nikeli na kaboni

Bronzi

Bronzi (pia: shaba nyeusi) ni aloi ya metali. Kiasi kikubwa ndani yake ni shaba (70-90%) na metali nyingine ndani yake ni stani (takriban 10-30%).

Bujumbura

Bujumbura, ni mji mkuu wa Burundi unaokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 300,000. Mji upo kaskazini mashariki mwa Ziwa Tanganyika, na ni mji mkubwa zaidi Burundi, kitovu cha mawasiliano na uchumi nchini humo.

Bujumbura ni mji pekee Burundi ambao una bandari ya kupakia mali na bidhaa mbalimbali za kuuza nje, kama vile kahawa, pamba, ngozi na madini ya stani.

Elementi za kikemia

Elementi ya Kikemia ni dutu yenye tabia maalumu isiyotenganishwa kuwa dutu tofauti kwa mbinu za Kemia. Elementi tupu ina aina moja ya atomi tu ndani yake.

Johannes Gutenberg

Johannes Gensfleisch zur Laden zum Gutenberg, anayejulikana kifupi kama Johannes Gutenberg, (mnamo 1398 - 3 Februari 1468) alikuwa fundi dhahabu na mvumbuzi kutoka Ujerumani anayekumbukwa hasa kama mbuni wa uchapaji vitabu kwa herufi za kusogezeka.

Alitengeneza mashine ya kwanza ya kuchapa vitabu, alibuni aloi ya kufaa kwa herufi alizotumia katika mashine hii pamoja na wino.

Alitengeneza pia kifaa kilichomwezesha kusubu herufi za metali haraka.

Katanga

Katanga (au Shaba, 1971-1997) ilikuwa jimbo la kusini-mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mji mkuu ulikuwa Lubumbashi (iliyoitwa Elizabethville hadi 1966). Eneo lake lilikuwa km² 496.871 na wakazi 4,125,000.

Kiswahili kilitumiwa kama lugha rasmi.

Jimbo ni maarufu kwa utajiri wake wa madini mbalimbali. Hasa mashariki mwa jimbo ni sehemu ya Kanda la Shaba linaloenea hadi Zambia. Kati ya madini yake ni kobalti, shaba, stani, radiamu, urani na almasi.

Baada ya uhuru wa Kongo mwaka 1960 jimbo lilijitenga na kuwa nchi ya pekee chini ya urais wa Moise Tshombe. Jeshi la UM lilimaliza kipindi hiki kwa nguvu ya kijeshi na kurudisha Katanga kuwa sehemu ya Kongo tena hadi Januari 1963. Katika kipindi hiki kifupi waziri mkuu wa Kongo Patrice Lumumba aliuawa katika Katanga.

Kiutawala Katanga imegawiwa katika sehemu nne kufuatana na mipango ya katiba mpya ya Kongo: Mkoa wa Tanganyika, wa Lomami Juu, wa Lualaba na wa Katanga Juu.

Kigali

Kigali ni mji mkuu wa Rwanda na pia mji mkubwa kuliko mingine yote nchini.

Iko karibu sana na mstari wa ikweta kwenye kimo cha 1400 - 1600 m juu ya UB. Hali ya hewa ni ya wastani hakuna baridi kali wala joto kali.

Kigali ina wakazi 600,000.

Lubumbashi

Lubumbashi (zamani ulijulikana kwa Kifaransa kama Élisabethville na kwa Kiholanzi kama Elizabethstad) ni mji wa pili kwa ukubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani ilijulikana kama Zaire) ukifuata mji mkuu wa taifa wa Kinshasa na ni kitovu cha biashara cha sehemu ya kusini ya nchi.

Mji huu ndio makao makuu ya Mkoa wa Katanga Juu ambao una madini ya shaba na uko karibu na mpaka wa Zambia. Makadirio ya idadi ya watu ni karibu milioni 1.8.

Makala za msingi - orodha ya meta Feb 2008

Hii ni tafsiri ya orodha ya Kiingereza ya makala 1,000 za msingi kutoka meta:wikipedia ya Februari 2008.

Hadi sasa (2019) idadi kubwa imetafsiriwa, pia orodha imebadilishwa mara kadhaa. Mapengo ya sasa ni machache, kwenye Septemba 2019 ni yafuatayo: , physical chemistry , conservation of energy , classical mechanics , strong interaction , weak interaction , quantum mechanics , general relativity , mathematical analysis , differential equation , numerical analysis , function , infinity , mathematical proof , set theory , capacitor , inductor , operating system , programming language , video game

Pamoja na haya ya juu, inafaa tuangalie sasa orodha ya orodha ya makala 10,000 za msingi kutoka meta:wikipedia. Hapo tumeshapata karibu makala 4,000, lakini bado zaidi kidogo ya 6,000 zinakosekana. Hata kama si kila moja ni mada ya kuvutia sana, bado makala hizi ni kiunzi cha elimu ya msingi! Karibuni kuchangia. Wanaopenda jiografia, basi mtumie orodha ya sehemu yake iliyoswahilishwa kisehemu Mtumiaji:Kipala/10000_list_Geography na jitahidini kumaliza maneno mekundu. Kipala (majadiliano) 22:25, 21 Septemba 2019 (UTC)

Metali

Metali (kutoka Kiingereza metal) ni kundi la elementi zenye tabia za pamoja kama vile

zinapitisha umeme kwa urahisi

zinapitisha joto

zinang'aa

ni wayaikaji (zinaweza kubabatizwa kuwa wembamba kama waya au kupinduliwa kabla ya kuvunjika)Kikemia tabia hizo zote zinatokana na muungo metali ya elementi hizo. Kinyume chake simetali kwa kawaida ni kechu kama

mangu, hazing'ai na zinahami (hazipitishi umeme).

Idadi kubwa ya elementi katika mfumo radidia huhesabiwa kati ya metali. Kuna pia elementi zinazoonyesha tabia za kati ya metali na simetali kama vile metaloidi au nusumetali.

Mifano ya metali ni

chuma (feri)

dhahabu (auri)

fedha (ajenti)

natiri

alumini

Mmumunyo

Mmumunyo au myeyusho (kwa Kiingereza solution) ni tokeo la kuchanganya kabisa dutu mbili hadi kupata mchanganyiko wa aina moja usioonyesha sehemu zake. Mfano ni kukoroga sukari katika maji. Hapo sukari haionekani tena imechanganika kabisa na maji.

Kwa lugha ya kemia sukari ni kimumunyika, maji ni kimumunyi (kiyeyushi) na tokeo ni mchanganyiko wa aina moja au mmumunyo,

Mara nyingi kimumunyi ni kiowevu lakini kuna pia mifano mingine.

Gesi zinaweza kumumunyika katika kiowevu, kwa mfano oksijeni katika maji ambayo ni msingi wa uhai baharini au mtoni. Gesi inamumunyika pia katika gesi nyingine. Hewa kwa mfano ni mchanganyiko wa aina moja; oksijeni na gesi nyingine zimemumunyika katika nitrojeni.

Kiowevu kinaweza kumumunyika katika kiowevu kingine, lakini kuchanganya maji na mafuta hakuleti mchanganyiko wa aina moja, tokeo lake ni kiolei au emalshani (ing. emulsion).

Kuna pia mifano ya mmumunyo kama kimumunyi ni mango. Aloi zote ni mimumunyo ya metali mbili, kwa mfano bronzi ni mmumunyo wa stani iliyomumunika katika shaba. Mmumunyo wa aloi unatokea katika hali kiowevu wakati metali zote mbili zilipashwa moto na kuyeyuka.

Shaba

Shaba au shaba nyekundu (pia: Kupri au Cupri kama jina la kisayansi) ni elementi yenye namba atomia 29 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 65.54. Alama yake ni CU.

Katika mazingira ya kawaida ni metali yenye rangi kahawia nyekundu. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1,083 C°.

Ni kati ya metali za kwanza wanadamu walitumia baada ya kutoka katika zama za mawe. Si metali ngumu zana hivyo ilikuwa nyepesi ya kushughulikia kwa wanadamu wa kale.

Ikichanganywa na stani kunatokea aloi ya bronzi ambayo ni ngumu zaidi. Aloi nyingine ni shaba nyeupe, mchanganyo wa shaba nyekundu na zinki.

Wakati mwingine shaba hupatikana kama metali tupu lakini mara nyingi zaidi kama mtapo.

Tabia muhimu ya shaba ni uwezo wake wa kupitisha umeme. Hivyo imekuwa msingi wa teknolojia yote ya umeme hasa nyaya za kila aina.

Siku hizi shaba huchimbwa hasa katika nchi za Chile (Chuquicamata), Marekani, Urusi, Afrika ya Kati ("Copperbelt" - kanda la shaba), Congo-Zaire, Zambia, Kanada na Peru.

Uchapaji

Uchapaji ni njia ya kunakili maandishi na picha kwa karatasi au loho bapa nyingine, hata kitambaa.

Vitabu na magazeti vinatengenezwa kwa njia ya uchapaji. Hivyo vinaweza kutolewa kirahisi kwa nakala nyingi.

Kabla ya kupatikana kwa uchapaji vitabu, hati na maandiko yote yalinakiliwa kwa mkono pekee. Katika tamaduni mbalimbali waandishi na wanakili walikuwa mabingwa muhimu. Lakini kunakili matini ndefu kama kitabu kulichukua muda mrefu, hata miaka, hivyo vitabu havikupatikana kwa nakala nyingi, pia vilikuwa ghali mno.

Tangu kubuniwa kwa uchapaji maandishi yamepatikana kwa wingi tena kwa bei nafuu. Hii ilisaidia uenezaji wa habari na elimu na kusababisha mapinduzi makuu katika historia ya binadamu.

Ufuaji metali

Ufuaji metali (ing. metallurgy) inamaanisha jumla ya mbinu za kushughulikia metali na elimu yake. Inahusika pia na aloi ambazo ni mchanganyiko wa metali mbalimbali.

Ufuaji metali inaanza kwenye kushuhulikia mtapo yaani mawe yenye madini ya metali na namna ya kutoa metali katika mtapo.

Halafu inaangalia namna ya kuchanganya na kuunganisha metali mbalimbali kuwa aloi na tabia zake.

Zama za Shaba

Zama za Shaba (kwa Kiingereza bronze age) kilikuwa kipindi cha historia ambacho watu walitengeneza vifaa vyao kwa kutumia metali ya shaba na baadaye bronzi yenye mchanganyiko wa metali mbili: vipande tisa vya shaba kwa kipande kimoja cha stani.

Malighafi nyingine, kama mbao na mawe, zilikuwa zikitumika pia kwa zana, lakini shaba ilikuwa nzuri zaidi kwa kukatia na kuchongea, na ilikuwa rahisi sana kuitengenezea umbo la kitu.

Zama hizo za Shaba hazikutokea wakati mmoja kila mahali, kwa sababu makundi tofauti ya watu walianza kutumia shaba kwa vipindi tofauti kabisa. Kwa mfano, Ulaya Magharibi Zama za Shaba ziliisha kunako miaka ya 2000 KK hadi 800 KK. Kumbe upande wa Mashariki ya Kati zilianza takriban miaka elfu moja nyuma.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.