Solomoni

Mfalme Solomoni kadiri ya Biblia alikuwa mfalme wa tatu na wa mwisho wa Israeli nzima, akitawala kuanzia 970 KK hadi 930 KK hivi.

Konrad Witz 003
Solomoni na malkia wa Saba (mchoro wa Konrad Witz, alias Conradus Sapientis, 1434-1435).

Maisha yake

Ingobertus 001
Solomoni katika ikulu yake (kadiri ya Ingobertus, 880 hivi).

Alikuwa mwana wa Daudi na Bath-Sheba (Betsheba), aliyewahi kuwa mke wa Uria Mhiti.

Daudi alimchagua kuwa mrithi wake kwa sababu alikuwa uthibitisho hai wa msamaha aliopewa na Mungu kwa kuzini na hatimaye kumuua Uria.

Ufalme wake ulitazamwa na Wayahudi kuwa na ustawi usio na mfano, kutokana na hekima yake na amani iliyopatikana wakati wote wa utawala wake.

Ufalme wake uliweza kustawi kuliko ule wa baba yake kutokana na msingi imara aliouweka Daudi. Lakini mwenyewe aliudhoofisha na kusababisha mara baada ya kifo chake utokee utengano kati ya makabila ya Kaskazini na yale ya Kusini.

Kati ya kazi muhimu alizozifanya, mojawapo ni kujenga hekalu la Yerusalemu na kuliweka wakfu kwa sherehe kubwa ya siku saba, ambapo Mungu alionyesha kibali chake kwa kulijaza kwa sura ya wingu (1Fal 8). Polepole hekalu hilo likaja kuwa la pekee hata patakatifu pengine pote pakakatazwa chini ya mfalme Yosia.

Ingawa Solomoni anasifiwa kwa hekima yake, alishindwa kukwepa majivuno na tamaa, akataka kuwapendeza wake zake waliokuwa 700 (mbali na masuria 300), wengi wao Wapagani, hata akawajengea mahali pa kuabudia miungu yao akamchukiza Mungu hata akamtabiria mtoto wake atanyang’anywa sehemu kubwa ya ufalme (1Fal 11:1-13) ikawa hivyo.

Hata hivyo mwishoni aliweza kulaumiwa kwa kuzidisha fahari, hasa upande wa wanawake waliomvuta kwenda kinyume cha imani ya Mungu pekee.

Sala zake

"Nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi"? (1Fal 3:9)

"Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe, mbinguni juu wala duniani chini! Ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako, waendao mbele zako kwa mioyo yao yote". (1Fal 8:23)

Baada ya kifo chake

Kwa sababu hiyo, ufalme ulivunjika pande mbili mara baada ya kifo chake.

Hata hivyo, Wayahudi waliendelea kumuona kama kielelezo cha hekima, wakaandika vitabu kwa kutumia jina lake au kwa kujifananisha naye.

Yesu alijitangaza kuwa mkuu na mwenye hekima kuliko Solomoni.

Marejeo

  • Dever, William G. (2003). Who Were the Early Israelites and Where Did They Come From?. Wm. B. Eerdmans Publishing Company. ISBN 0-8028-0975-8.
  • Finkelstein, Israel; Neil Asher Silberman (2006). David and Solomon: In Search of the Bible's Sacred Kings and the Roots of the Western Tradition. Free Press. ISBN 0-7432-4362-5.
  • Finkelstein, Israel; Neil Asher Silberman (2002). The Bible Unearthed: Archaeology's New Vision. Simon & Schuster. ISBN 978-0-684-86913-1.
  • [2005-12-30] in Thomas E. Levy & Thomas Higham (eds.): The Bible and Radiocarbon Dating: Archaeology, Text and Science. London ; Oakville, CT.: Equinox Publishing (UK). ISBN 978-1-84553-056-3. OCLC 60453952.
  • Dever, William G. (2001). What Did the Biblical Writers Know and When Did They Know It?: What Archaeology Can Tell Us about the Reality of Ancient Israel. Grand Rapids, Mich.: Eerdmans Pub.. ISBN 978-0-8028-4794-2. OCLC 45487499.
  • Kitchen, Kenneth A. (2003). On the reliability of the Old Testament. Grand Rapids, Mich.: Eerdmans. ISBN 0-8028-4960-1.

Viungo vya nje

Hekalu la Yerusalemu

Hekalu la Yerusalemu lilikuwa kitovu cha ibada za dini ya Uyahudi wakati wa Israeli ya Kale.

Kwa jumla kulikuwa na majengo mawili yaliyofuatana kwenye mlima wa hekalu mjini Yerusalemu.

Imani ya Kiyahudi inategemea kujengwa kwa hekalu la tatu pamoja na kuja kwa Masiya wakati ujao.

Katika imani hiyo sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu ndani ya hekalu ilikuwa mahali ambapo Mungu mwenyewe aligusa dunia.

Historia ya Wokovu

Kwa jina hilo Wakristo wanamaanisha ufafanuzi wa mpango wa kazi ya Mungu kwa wokovu wa binadamu kadiri ya Biblia.

Ithamari

Ithamari (kwa Kiebrania: אִיתָמָר, ʼĪṯāmār au Itamar; maana yake "Baba wa Tamar") katika Biblia ya Kiebrania alikuwa kuhani kama mtoto wa nne na mwisho wa Aroni, kaka wa Musa.

Wazao wake walikuwa makuhani wakuu tangu wakati wa Eli hadi kwa Solomoni.

Mzao wake maarufu zaidi ni nabii Yeremia.

Karne ya 10 KK

Karne ya 10 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 1000 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 901 KK.

Kitabu cha Hagai

Kitabu cha Hagai ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh, yaani Biblia ya Kiebrania. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Hekima

Kitabu cha Hekima au Hekima ya Solomoni ni cha mwisho kuandikwa (miaka 50 hivi KK) katika ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Hupangwa kati ya vitabu vya hekima, kichwa chake kinavyodokezwa.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 22.

Kitabu cha Mhubiri

Mhubiri (pia: Koheleti) ni kimojawapo kati ya vitabu vya hekima vilivyomo katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo. Kwa sababu hiyo kilidhaniwa kimeandikwa na mfalme Solomoni, kielelezo cha hekima katika Biblia.

Kitabu hicho kina sura kumi na mbili na kwa kiasi kikubwa kimeandikwa kwa njia ya ushairi.

Kurani

Kurani (kwa Kiarabu: القرآن, Qur'an) ni kitabu kitukufu cha Uislamu ambacho kinatazamwa na Waislamu kama "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hiki kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya vitabu vya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad.

Mambo ya Nyakati II

Kitabu cha Mambo ya Nyakati katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) kimegawanywa sehemu mbili katika Biblia ya Kikristo na kupangwa katika ya vitabu vya historia.

Sehemu ya pili kinaitwa Kitabu cha pili cha Mambo ya Nyakati kikianzia na habari za mfalme Solomoni.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mshewa

Mshewa ni kata ya Wilaya ya Same katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,154 walioishi humo.

Kata ya Mshewa ina vijiji vya Marindi, Mshewa, Manka na Goma.

Mshewa ina ofisi ya kijiji, shule ya msingi, shamba la kilimo na jengo la kahawa linalomilikiwa na Vuaso Cooperative Union.

Pamoja na kanisa la mtaa KKKT usharika wa Marindi, Mshewa kuna Kanisa la Neno na kanisa la EAGT.

Rehoboamu

Rehoboam (kwa Kiebrania: רְחַבְעָם‬, Rəẖavʻam au Reḥaḇʻām; kwa Kigiriki: Ροβοαμ, Rovoam; kwa Kilatini: Roboam; 970 KK-910 KK hivi) alikuwa mfalme wa nne wa Israeli.

Habari zake zinapatikana katika Biblia (Kitabu cha Kwanza cha Wafalme na kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati).

Alikuwa mtoto na mrithi wa Solomoni, lakini alisababisha uasi wa makabila ya kaskazini yakiongozwa na Yeroboamu I, akajikuta amebaki na yale ya kusini tu.

Mama wa Rehoboam alikuwa si Mwisraeli, bali Mwamoni. Mwenyewe alioa wake 18 na masuria 60 na kupata watoto 88: 28 wa kiume na 60 wa kike.

Rehoboamu alitawala miaka 17 akarithiwa na mwanae Abijah.

Sanduku la agano

Sanduku la Agano (kwa Kiebrania אָרוֹן הַבְּרִית ʾĀrôn Habbərît, kisasa Aron Habrit) au Ushuhuda ni sanduku lililozungumziwa katika Kitabu cha Kutoka 25:10-22.

Kadiri yake lilikuwa na mbao mbili za mawe zilizoandikwa Amri 10 ambazo Musa alipewa na Mungu kama masharti makuu ya Agano kati yake na Israeli.

Inawezekana vilikuwemo pia fimbo la Haruni na mana kidogo, ingawa 2Waf 8:9 inasema wakati wa Solomoni hivyo havikuwemo.

Shilo

Shilo ulikuwa mji wa zamani unaotajwa katika Biblia ya Kiebrania, karibu na Khirbet Seilun, kusini kwa Tirza.Ulikuwa makao ya hekalu lilipotunzwa sanduku la agano kabla ya hilo kutekwa na Wafilisti wakati wa kuhani Eli na hatimaye kuhamishiwa na mfalme Daudi mjini Yerusalemu, ambapo mwanae Solomoni alilijengea hekalu la fahari.

Nabii Yeremia alichukua Shilo kama kielelezo cha maangamizi yatakayolipata hekalu la Yerusalemu kutokana na Waisraeli kutokubali ujumbe wa toba aliowaletea kutoka kwa Mungu.

Ufalme wa Israeli

Ufalme wa Israeli unaweza kuhusu falme mbalimbali zilizotokea katika historia ya Israeli, kama vile:

Ufalme wa Muungano chini ya Sauli, Daudi na Solomoni (1050–931 KK)

Ufalme wa Kaskazini (Samaria) chini ya koo mbalimbali (931–722 KK)

Ufalme wa Kusini (Yuda) chini ya warithi wa Solomoni (931–586 KK)

Ufalme wa Wamakabayo (140–37 KK)

Ufalme wa Herode Mkuu (37–4 KK) na warithi wake, wa mwisho wao Agrippa II (hadi 100 hivi BK)

Visiwa vya Solomon

Visiwa vya Solomon ni nchi ya visiwani ya Melanesia katika Bahari ya Pasifiki mashariki kwa Papua Guinea Mpya.

Eneo lake ni visiwa 1000 hivi, vyenye jumla ya km² 28,400 na wakazi wenye idadi ya watu 552,438, wengi wakiwa Wamelanesia, wakiongea lugha 90.

Kati yao 92% ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Anglikana.

Mji mkuu ni Honiara kwenye kisiwa cha Guadalcanal.

Wayahudi

Wayahudi (kwa Kiebrania יְהוּדִים, Yehudim) ni kundi la kikabila na la kidini lenye asili yake katika eneo la Israeli ya Kale (Mashariki ya Karibu). Kabila la Kiyahudi, taifa la Kiyahudi na dini ya Kiyahudi yote yana uhusiano wa karibu sana, kwa sababu Uyahudi ndio dini ya jadi ya watu wa taifa la Kiyahudi

Wanaobadilika kuwa Wayahudi, ambao hadhi yao kama Wayahudi katika kabila la Kiyahudi ni sawa na wale ambao wamezaliwa kuingia kabila hilo, wameingizwa ndani ya kundi la watu wa Kiyahudi tangu jadi.

Katika utamaduni wa Kiyahudi, ukoo unarudi nyuma hadi kwa mababa wa Biblia kama vile Abrahamu, Isaka na Yakobo katika milenia ya 2 KK.

Wayahudi wamefurahia enzi tatu za uruhu wa kisiasa katika nchi yao ya nyumbani, Nchi ya Israel, mara mbili wakati wa historia ya kale, na mara nyingine tena, kuanzia mwaka wa 1948, wakati ambapo taifa la kisasa la Israeli lilipoanzishwa. Enzi ya kwanza ilianza mnamo mwaka wa 1350 hadi 586 KK, na ilijumuisha vipindi vya Mahakimu, Milki iliyoungana na Miliki zilizogawanywa za Israeli na Yudea, na ilisha wakati wa kuharibiwa kwa thehebu la kwanza la Solomoni.

Enzi ya pili ilikuwa kipindi cha Milki ya Hasmonea iliyoanza mnamo mwaka wa 140 hadi mwaka wa 37 KK. Tangu kuharibiwa kwa Thehebu la Kwanza, nchi geni ndizo zimekuwa kama nyumbani kwa Wayahudi wengi wa Dunia. Isipokuwa katika taifa la kisasa la Israeli, Wayahudi ni wachache katika kila nchi wanamoishi, na mara nyingi wameteswa katika kipindi chote cha historia, kusababisha idadi yao kupanda na kushuka katika karne zilizopita.

Wimbo Ulio Bora

Wimbo Ulio Bora (kwa Kiebrania שיר השירים, Shir ha-Shirim), ni kitabu kimojawapo cha Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Yerusalemu

Yerusalemu (mara kwa mara pia Kudisi) (kwa Kiebrania ירושלים, Yerushalayim, kwa Kiarabu: القدس, al-Quds) ni mji wa Mashariki ya Kati wenye pande mbili. Kwa upande mmoja ni mji mkuu wa Israel. Kwa upande mwingine Yerusalemu ya mashariki inatazamiwa kuwa mji mkuu wa Palestina, ingawa imetawaliwa na Israel pia tangu 1967. Israel imetangaza tangu mwaka 1980 Yerusalemu yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi za dunia hazikubali azimio hilo, hivyo balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Yerusalemu.

Yerusalemu ina historia ndefu sana.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.