Shaba

Shaba au shaba nyekundu (pia: Kupri au Cupri kama jina la kisayansi) ni elementi yenye namba atomia 29 kwenye mfumo radidia, uzani atomia ni 65.54. Alama yake ni CU.

Katika mazingira ya kawaida ni metali yenye rangi kahawia nyekundu. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1,083 C°.

Ni kati ya metali za kwanza wanadamu walitumia baada ya kutoka katika zama za mawe. Si metali ngumu zana hivyo ilikuwa nyepesi ya kushughulikia kwa wanadamu wa kale.

Ikichanganywa na stani kunatokea aloi ya bronzi ambayo ni ngumu zaidi. Aloi nyingine ni shaba nyeupe, mchanganyo wa shaba nyekundu na zinki.

Wakati mwingine shaba hupatikana kama metali tupu lakini mara nyingi zaidi kama mtapo.

Tabia muhimu ya shaba ni uwezo wake wa kupitisha umeme. Hivyo imekuwa msingi wa teknolojia yote ya umeme hasa nyaya za kila aina.

Siku hizi shaba huchimbwa hasa katika nchi za Chile (Chuquicamata), Marekani, Urusi, Afrika ya Kati ("Copperbelt" - kanda la shaba), Congo-Zaire, Zambia, Kanada na Peru.

Cu,29

Punje ndogo za shaba: shaba inaweza kutokea kwa rangi nyekundunyekundu; ikikaa hewani hubadilika kuwa na rangi ya machungwa mabivu

Cu-Scheibe

Kupri

Cuivre Michigan

Kupri

Shaba au Kupri (cuprum)
Cu-TableImage
Jina la Elementi Shaba au Kupri (cuprum)
Alama Cu
Namba atomia 29
Mfululizo safu Metali
Uzani atomia 65.54
Valensi 2, 8, 18, 1
Kiwango cha kuyeyuka 1357.77 K (1084.62°C)
Kiwango cha kuchemka 2835 K (2562 °C)
Asilimia za ganda la dunia 0.01 %
Hali maada mango
Aloi

Aloi ni mchanganyiko wa elementi mbili au zaidi mwenye tabia ya kimetali; angalau elementi moja ndani yake ni metali pia.

Zatengenezwa kwa njia ya:

1) Kuyeyusha metali

2) Kuichanganya katika hali ya kiowevu pamoja nyongeza zote

3) Kupoza yote hadi imekuwa imara

Mifano ya aloi zinazotumiwa sana ni kama vile:

shaba nyeupe kutokana na 35% zinki na 65% shaba - yatumiwa kwa vyombo vya muziki na mapambo mengi

bronzi kutokana na 87% shaba na 13% stani - yatumiwa kwa parafujo, vyuma vya mashua

feleji kutokana na chuma pamoja na bati, nikeli na kaboni

Botswana

Botswana ni nchi huru iliyoko Kusini mwa Afrika. Jina rasmi ni Jamhuri ya Botswana.

Mji mkuu wa Botswana ni Gaborone.

Bronzi

Bronzi (pia: shaba nyeusi) ni aloi ya metali. Kiasi kikubwa ndani yake ni shaba (70-90%) na metali nyingine ndani yake ni stani (takriban 10-30%).

Historia ya Kupro

Historia ya Kupro inahusu eneo ambalo siku hizi linaunda Jamhuri ya Kupro.

Karne ya 10 KK

Karne ya 10 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 1000 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 901 KK.

Karne ya 8 KK

Karne ya 8 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 800 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 701 KK.

Kasese

Kasese ni mji mkuu wa Wilaya ya Kasese nchini Uganda wenye wakazi wake takriban 66,600. Mji uko magharibi mwa Ziwa George. Awali mji huu ulikua kutokana na uchimbaji wa madini ya shaba katika eneo ka Kilembe, na hapo baadaye uchimbaji wa kobalti. Huu ndio mji mkuu wa Wilaya ya Kasese na makao makuu ya wilaya yapo hapo. Kasese pia ndio mji mkubwa kwenye Mkoa wa Rwenzururu. Makazi ya Charles Mumbere, Omusinga wa Rwenzururu yako katika mji huu.

Kupro

Kupro (pia: Kuprosi, Kipro, Saiprasi, Cyprus) ni nchi ya kisiwani upande wa mashariki wa bahari ya Mediteranea.

Kijiografia ni sehemu ya Asia, lakini kiutamaduni na kisiasa ni sehemu ya Ulaya.

Mji mkuu ni Nikosia.

Madini

Madini (kwa Kiarabu: معدن, ma'adan; kwa Kiingereza: mineral) ni dutu mango inayopatikana duniani kiasili. Madini huwa na tabia maalumu ya kikemia, si mata ogania na mara nyingi huwa na muundo wa fuwele (kristali). Kwa lugha nyingine: Madini ni elementi au kampaundi ya kikemia inayoonyesha umbo la fuwele na ambayo imejitokeza katika mchakato wa kijiolojia.

Kuna takriban madini 4,000 yaliyogunduliwa duniani. Miamba yote yanaundwa na madini na kuna hasa madini 30 yanayounda sehemu kubwa ya miamba duniani. Miamba kwa kawaida huwa na madini mbili au zaidi ndani yake.

Madini yapo kila mahali. Katika mazingira yetu kila jiwe limeundwa na madini. Ardhi ya shamba ina kiwango kikubwa cha madini ni punje za mchanga ambao ni mawe yaliyosagwa. Tukiwasha taa kuna madini kwenye uzi ya kuwaka na umeme umefika kwenye taa kupitia shaba ya waya; na shaba hiyo ni madini. Seli za mwili wetu huhitaji madini na hivyo ni muhimu kwamba chakula chetu kina kiasi kidogo cha madini ya lazima kama chuma au kloridi.

Madini kadhaa hupendwa kama vito (johari, mawe ya thamani) au pia dhahabu.

Madini ni kati ya vitu vigumu vilivo vya kawaida katika Dunia. Ni vitu viundanishavo mawe ya Dunia. Kuna baadhi ya madini huundwa na elementi moja tu. Nyinginezo huundwa na zaidi ya elementi mbili au zaidi.

Metali

Metali (kutoka Kiingereza metal) ni kundi la elementi zenye tabia za pamoja kama vile

zinapitisha umeme kwa urahisi

zinapitisha joto

zinang'aa

ni wayaikaji (zinaweza kubabatizwa kuwa wembamba kama waya au kupinduliwa kabla ya kuvunjika)Kikemia tabia hizo zote zinatokana na muungo metali ya elementi hizo. Kinyume chake simetali kwa kawaida ni kechu kama

mangu, hazing'ai na zinahami (hazipitishi umeme).

Idadi kubwa ya elementi katika mfumo radidia huhesabiwa kati ya metali. Kuna pia elementi zinazoonyesha tabia za kati ya metali na simetali kama vile metaloidi au nusumetali.

Mifano ya metali ni

chuma (feri)

dhahabu (auri)

fedha (ajenti)

natiri

alumini

Michezo ya Olimpiki

Michezo ya Olimpiki ni mashindano makubwa ya michezo mbalimbali duniani inayofanyika kila baada ya miaka minne.

Michezo ya Olimpiki imekuwa na historia ndefu katika vipindi viwili:

Michezo ya Olimpiki ya Kale ilifanyika tangu tarehe isiyojulikana lakini kwa uhakika kuanzia mwaka 776 KK hadi mwaka 393 BK katika mtaa wa mahekalu wa Olimpia kwenye rasi ya Peloponesi nchini Ugiriki.Michezo ya Olimpiki ya Kisasa ya kwanza ilitokea mwaka 1896 mjini Athens (Ugiriki). Mwanzilishi alikuwa Mfaransa Pierre de Coubertin aliyetaka kutumia kielelezo cha michezo ya kale kwa kujenga uhusiano mzuri kati ya vijana wa nchi mbalimbali na kuwapatia nafasi ya kushindana kwenye uwanja wa michezo badala ya uwanja wa vita. Coubertin alianzisha Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (International Olympic Committee - IOC).Michezo hii ya kisasa imeendelea kila baada ya miaka minne isipokuwa 1916, 1940 na 1944 kwa sababu ya Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia.

Michezo ya kisasa hufanyika katika mji tofauti kila safari. Michezo ya 2004 ilifanyika Athens, ya 2008 huko Beijing na ya 2012 London.

Kuna tofauti kati ya michezo ya kiangazi na michezo ya majira ya baridi.

Washindi watatu wa kwanza wa kila mashindano hupewa medali ya dhahabu, fedha au shaba.

Mita

Mita (pia: meta) ni kipimo cha urefu ambacho kimekuwa kipimo sanifu cha kimataifa.

Neno limetokana na Kigiriki μέτρον/métron (kipimo, pia chombo cha kupimia), kwa kupitia Kiingereza "metre, meter".

Kutokana na maana hiyo "mita" inataja pia mitambo ya kupima maji, umeme na kadhalika. Hapo matumizi ya Kiswahili yanafanana na ya Kiingereza "metre".

Mtimbwilimbwi

Mtimbwilimbwi ni jina la kata ya Wilaya ya Mtwara Vijijini katika Mkoa wa Mtwara, Tanzania yenye postikodi namba 63227. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,232 waishio humo.Kata ya Mtimbwilimbwi imeundwa na vijiji kama vile; Shaba, Pachani, Mtopwa, Mtimbwilimbwi, Mbambakofi, Nanjedya pamoja na Namisangi.

Nanyuki

Nanyuki ni mji mdogo katikati ya Kenya kaskazini-magharibi chini ya Mlima Kenya mwishoni kwa reli. Mstari wa ikweta unapita katika eneo la mji na Nanyuki ni kituo cha jeshi la anga la Kenya.

Msingi wake umewekwa mwaka 1907 na walowezi Waingereza, ambao dhuria wao bado wanaishi mjini na katika mazingira yake. Sasa Nanyuki ni kituo kuu cha Jeshi la Anga la Kenya. Jeshi la Uingereza linatunza kituo pia na linaendesha mazoezi kila mwaka mlimani na kwa maeneo kame kaskazini. Nanyuki ni katika kaunti ya Laikipia.

Nanyuki ilikuwa na idadi ya watu ya 49,233 mwaka 2009 (). Wakazi wengi huchuma fedha yao kwa kufanya biashara. Maduka mjini hugawia mashamba, ranchi na hifadhi za wanyama katika mazingira mapana. Kwanza maduka mengi yalimilikiwa na Wahindi ambao bado ni kipande kikubwa kiasi cha wakazi. Wakwezi na wabebashanta hutembelea Nanyuki wakienda na kutoka Mlima Kenya kwa njia za Sirimon na Burguret, na watalii wengi wengine hupitia mji. Kwa hiyo Nanyuki una hoteli nyingi ambazo mwongoni mwao kuna Mount Kenya Safari Club, Sportsman’s Arms Hotel, Lion’s Court, Equatorial Hotel, Mount Kenya Paradise Hotel na Joskaki Hotel. Mgahawa wa zamani sana ni Marina ambao bado unapendwa kiasi. Miaka kadhaa iliyopita mgahawa mwingine umefunguliwa kusini kwa Nanyuki ambao umejengwa ndani ya mti mkubwa sana. Unaitwa Trout Tree Restaurant na mvuto mkuu wake ni trauti apikwaye kwa namna mbalimbali. Wateja wanaweza kutembelea pia msimiko wa kufuga trauti chini ya mti.

Hakuna viwanda vikubwa katika Nanyuki. Zamani kiwanda cha nguo kilikuwako huko, Nanyuki Textile Mills. Uongozi wa Kiingereza umepunguka polepole na kiwanda kimefilisika mwaka 1978. Baada ya miaka kiwanda, ambacho kimebaki kizima kwa kadiri, kimenunuliwa na mkazi Mhindi wa Nanyuki. Nguo kiasi inatengenezwa sasa. Pia vilikuwako viwanda vya kupasulia mbao katika Nanyuki. Lakini vimefungika sasa au vinapata riziki kwa shida sana, kwa sababu kukata miti Mlimani Kenya kumepigiwa marufuku takriban kabisa.

Bustani iko kati ya mji na mito miwili, Nanyuki na Liki, inapitia. Ikweta inapitia sehemu ya kusini ya mji. Ukifika Nanyuki barabarani A2 kutoka upande wa kusini unaivuka. Mahali hapa panapendwa sana na watalii ambao wanapigiana picha pale. Kwa kawaida kuna wananchi wanaowaonyesha watalii athari ya kani ya Coriolis. Wanasema kwamba kani hii inasababisha maji yatokayo shimo kuzunguka upande wa kisaa au kinyume saa ukiwa kwa nusudunia ya kaskazini au ya kusini, lakini ni danganyo tu (tazama Coriolis force).

Nanyuki unafikika kwa barabara na kwa ndege. Uwanja wa ndege uko 6.5 km upande wa kusini kwa mji na unapokea ndege ndogo. Ziko huduma za ndege za Air Kenya zinazofaa wafanyabiashara na watalii kwa sababu ya hali mbaya ya barabara kutoka Nairobi. Watalii wanaweza kutembelea hifadhi kadhaa katika ujirani wa Nanyuki, kama Mount Kenya National Park, Sweetwaters Game Reserve, Lewa Wildlife Conservancy, Samburu National Reserve na Shaba National Reserve.

Maji ya mfereji katika Nanyuki ni baina ya maji safi kabisa katika Kenya, kwa sababu maji haya yanatoka mto wa Mlima Kenya. Maji yajiri kwa mifereji chini ya ufadhili wa uvutano kutoka mwanzo mpaka mafereji ya maji machafu.

Taasisi za taaluma ni Nanyuki High School, Brickwoods High School, Nanyuki Primary School, Nkando Primary School k.y.k. Makao makuu ya Kenayodemo (ushirikisho wa vijana na waari) yako mjini hapa.

Sarafu

Sarafu (kar. صرافة badilisha) ni kipande cha metali iliyotolewa na serikali ya nchi kama namna ya pesa. Mara nyingi sarafu ina umbo la duara kama kisahani. Kuna pia sarafu za pembe tatu, pembe nne au pembe zaidi.

Zamani sarafu ilikuwa umbo la kawaida ya pesa. Sarafu za kwanza zinazojulikana dunia zimepatikana kutoka Lydia katika Anatolia ya Magharibi iliyokuwa wakati ule sehemu ya utamaduni wa Wagiriki wa Kale. Sarafu zilitengenezwa hasa kwa kutumia metali ya thamani kama dhahabu na fedha, pia ya shaba na wakati mwingine ya chuma. Thamani ya sarafu ililingana na kiasi fulani cha metali hizi.

Siku hizi sehemu kubwa ya fedha inatolewa kama noti yaani kama karatasi.

Karibu popote duniani sarafu hutumika kwa ajili ya pesa ndogo tu. Isipokuwa sarafu za dhahabu zinatolewa kwa idadi ndogo hasa kwa ajili ya watu wanaopenda kukusanya aina mbalimbali za sarafu zenye thamani ingawa hazitumiki kama pesa ya kulipia.

Shore (Muscicapidae)

Shore, shorwe au sholwe ni ndege wadogo wa nusufamilia Muscicapinae katika familia Muscicapidae. Spishi nyingine zinaitwa chekiro, kidaku au gongo shaba. Spishi kadhaa za familia Pycnonotidae zinaitwa shore pia. Wale wa Muscicapinae wana rangi ya kahawa, kijivu au nyeusi kwa kawaida, lakini spishi nyingine wana rangi kali kama buluu, nyekundu, manjano na machungwa. Shore wanatokea misitu na maeneo mengine yenye miti katika Afrika na Asia. Hula wadudu. Kwa kawaida shore hukaa tawi wakiangalia ujirani. Wakiona mdudu huruka ili kumkamata na kurudi tawi. Hujenga tago lao kwa umbo wa kikombe katika tundu la mti au dhidhi ya shina. Jike huyataga mayai 2-6.

Umeme

Umeme au stima hutokea wakati chaji ya umeme inatiririka. Ni chanzo cha nishati tunayotumia kwa kuendesha mashine na vifaa vingi.

Kiasili neno la Kiswahili "umeme" lilimaanisha mwangaza wa ghafla unaofuatana na radi angani, lakini katika Kiswahili cha kisasa hutumiwa zaidi kwa habari ya kisayansi na ya kitekinolojia inayoelezwa hapa.

Kwa maana ya kisayansi umeme ni neno pana sana linalojumlisha mambo mbalimbali ambayo yote yanahusiana na kuwepo kwa chaji ya umeme.

Upanga

Upanga ni silaha inayoshikwa mkononi kwa ajili ya kukata. Hutengenezwa kwa metali, hasa feleji, ikifanana na kisu ila tu ni kubwa. Hasa kengee yake ni ndefu na mpini wake ni mkubwa kwa sababu mkono wote unahitaji kushika silaha hii.

Mara nyingi kuna chuma cha kupandana kinachokusudiwa kukinga mkono unaoshika upanga. Umbo la upanga ni muhimu kwa mbinu za mapigano.

Kuna aina nyingi za upanga zinazotofautiana hasa katika urefu na pia uzito.

Panga hutengezwa kutokana na malighafi ya shaba na chuma. Panga za kwanza zilitengenezwa na wahunzi (wafua chuma) wa Misri na China wakitumia bronzi. Tangu kupatikana kwa bunduki umuhimu wa upanga umepungua. Katika vita vya silaha za kisasa panga zimepotea kabisa. Lakini katika vita vya wenyewe kwa wenyewe au ghasia ya Kenya ya mwaka 2008 panga zilikuwa silaha muhimu tena.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.