Samaria

Samaria (kwa Kiebrania שומרון, Shomron; kwa Kiarabu السامرة, as-Sāmirah), ni eneo la milimamilima katikati ya nchi inayoitwa Israeli au Palestina. Jina "Samaria" linatokana na lile la mji mkuu wa Ufalme wa Israeli.[1]

Kadiri ya 1Fal 16:24, jina la mji huo lilitokana na lile la Shemer, aliyemuuzia mfalme Omri eneo kwa ajili ya kuuanzisha kama makao makuu (884 KK hivi) badala ya Tirza.

Palestine under the Persians Smith 1915
Samaria (kijani) ndani ya Palestina, chini ya Waajemi.
גבעות יצהר
Vilima vya Samaria, 2011.
Dothan, where Joseph was sold by his brethren American Colony, Jerusalem
Dothan, ambapo kadiri ya Kitabu cha Mwanzo, Yosefu (babu) aliuzwa na kaka zake.

Historia

Kadiri ya Biblia, Waisraeli waliteka eneo hilo la Kanaani na kulikabidhi kwa kabila la Yosefu.

Eneo lilitekwa na Waashuru mwaka 722 KK hivi, nao wakahamisha wakazi wake wengi hadi Mesopotamia. Badala yao waliletwa wengine kutoka huko. Ndiyo sababu wakazi wa eneo hilo wakaja kuwa wa mchanganyiko wakapewa jina jipya: "Wasamaria".

Baadaye lilitawaliwa na mataifa mbalimbali, kama vile Babuloni, Uajemi, Ugiriki wa kale, Dola la Roma, Bizanti, Waarabu, Wazungu wa vita vya msalaba, Waturuki na hatimaye Waingereza.[2]

Tanbihi

 1. Harvard Expedition to Samaria, 1908–1910, Harvard University
 2. Harvard Expedition to Samaria, 1908–1910, Harvard University

Marejeo

 • Rainey, A. F. (November 1988). "Toward a Precise Date for the Samaria Ostraca". Bulletin of the American Schools of Oriental Research 272 (272): 69–74.
   .
 • Stager, L. E. (February–May 1990). "Shemer's Estate". Bulletin of the American Schools of Oriental Research 277/278 (277): 93–107.
   .
 • Becking, B. (1992). The Fall of Samaria: An Historical and Archaeological Study. Leiden; New York: E. J. Brill. ISBN 90-04-09633-7.
 • Franklin, N. (2003). "The Tombs of the Kings of Israel". Zeitschrift des Deutschen Palästina-Vereins 119 (1): 1–11.
 • Franklin, N. (2004). "Samaria: from the Bedrock to the Omride Palace". Levant 36: 189–202.
 • Tappy, R. E. (2206). “The Provenance of the Unpublished Ivories from Samaria,” Pp. 637–56 in “I Will Speak the Riddles of Ancient Times” (Ps 78:2b): Archaeological and Historical Studies in Honor of Amihai Mazar on the Occasion of his Sixtieth Birthday, A. M. Maeir and P. de Miroschedji, eds. Winona Lake, IN: Eisenbrauns.
 • Tappy, R. E. (2007). “The Final Years of Israelite Samaria: Toward a Dialogue between Texts and Archaeology,” Pp. 258–79 in Up to the Gates of Ekron: Essays on the Archaeology and History of the Eastern Mediterranean in Honor of Seymour Gitin, S. White Crawford, A. Ben-Tor, J. P. Dessel, W. G. Dever, A. Mazar, and J. Aviram, eds. Jerusalem: The W. F. Albright Institute of Archaeological Research and the Israel Exploration Society.

Viungo vya nje

Majiranukta kwenye ramani: 32°08′35″N 35°15′38″E / 32.14306°N 35.26062°E

Al-Qaeda

Al-Qaeda (pengine imeandikwa al-Qaida; kutoka Kiarabu al-qa'idah, "msingi") ni kikundi cha Kiislamu kilichoanzishwa kati ya Agosti 1988 na mwanzoni mwa 1990. Ni mtandao wa kimataifa usio na msingi katika taifa fulani na kundi la wanaharakati wa Sunni wanaotoa wito wa jihad kwa ulimwengu mzima.

Al-Qaeda imeweza kushambulia raia na malengo ya kijeshi katika nchi mbalimbali, mashuhuri zaidi ikiwa mashambulio ya 11 Septemba 2001. Serikali ya Marekani iliitikia kwa kuzindua Vita dhidi ya Ugaidi. Kati ya wanachama 3,000 na 4,000 wa mtandao huu wamekamatwa, na maelfu zaidi kuuawa vitani Afghanistan.

Mbinu zao za kushambulia ni pamoja na mashambulizi ya kujitolea mhanga na ulipuaji wa mabomu ya malengo tofauti kwa wakati mmoja. Shughuli zake zinaweza kuhusisha wanachama wa harakati, ambao wamechukua amana ya uaminifu kwa kiongozi (sasa Mmisri Ayman al-Zawahiri), au wengi zaidi "watu binafsi wanaohusishwa na al-Qaeda" ambao wamepitia mafunzo katika moja ya kambi zake nchini Afghanistan au Sudan, bila kuchukuliwa amana yoyote. Wakereketwa wa Al-Qaeda wanaangazia kukatiza kabisa mvuto wa kigeni katika nchi za Kiislamu, na uumbaji wa ahmadiyya mpya ya Kiislamu. Imani ambazo zimeripotiwa ni pamoja na kuwa muungano wa Wakristo na Wayahudi unakusudia kuharibu Uislamu, na kwamba mauaji ya raia wanaopatikana pahali pa mashambulizi yanakubalika katika jihad.

Usimamizi wake falsafa umeelezewa kama "umoja wa uamuzi na madaraka ya utekelezaji mikoani." Kufuatia vita dhidi ya ugaidi, imedhaniwa kwamba uongozi wa al-Qaida "umegawanyika kijiografia", na hili limepelekea "kuibuka kwa uongozi uliogawanywa kikanda" wa makundi yanayotumia jina la al-Qaeda.

Filipo mwinjilisti

Filipo mwinjilisti ni Myahudi wa karne ya 1 anayejulikana hasa kutokana na Matendo ya Mitume.

Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa na Kanisa Katoliki na Anglikana tarehe 11 Oktoba, kumbe katika Makanisa ya Kiorthodoksi ni tarehe 6 Juni.

Historia ya Wokovu

Kwa jina hilo Wakristo wanamaanisha ufafanuzi wa mpango wa kazi ya Mungu kwa wokovu wa binadamu kadiri ya Biblia.

Kristo Mfalme

Kristo Mfalme ni sifa mojawapo ya Yesu katika imani ya Ukristo.

Inahusiana na wazo la Ufalme wa Mungu ambapo Kristo anachorwa kuwa ametawazwa upande wa kuume wa Mungu kama mshiriki wa mamlaka yake juu ya wote na vyote

Kupaa Bwana

Kupaa Bwana ni ukumbusho wa fumbo la Yesu Kristo kupaa katika utukufu wa mbinguni akiwa na mwili wake mzima ambao Ijumaa kuu ulisulubiwa hata akafa akazikwa kabla hajafufuka siku ya tatu (Jumapili) kadiri ya imani ya Ukristo.

Makabila ya Israeli

Makabila 12 ya Israeli (kwa Kiebrania בני ישראל, Bnai Yisraʾel, yaani Wana wa Israeli) waliunda taifa la lugha ya Kisemiti katika Mashariki ya Kati, wakiishi katika sehemu kubwa ya nchi ya Kanaani kati ya karne ya 15 KK na karne ya 6 KK), halafu wakawa wanaitwa Wayahudi na Wasamaria.

Biblia inaeleza kuwa makabila hayo yalitokana na wana wa kiume 12 wa babu Yakobo, bin Isaka na mjukuu wa Abrahamu. Ni Yakobo aliyepewa kwanza jina la Israeli.

Majina ya watoto hao na ya makabila yaliyotokana nao ni: Reubeni (babu), Simeoni (babu), Lawi (babu), Yuda (babu), Dan (babu), Naftali (babu), Gad (babu), Asheri (babu), Isakari (babu), Zebuluni (babu), Yosefu (babu) (wazao waligawanyika katika makabila mawili, kutokana na watoto wake Manase (babu) na Efraim (babu)), Benyamini (babu).

Matendo ya Mitume

Matendo ya Mitume ni kitabu cha Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo chenye sura 28.

Katika orodha ya vitabu 27 vya Agano Jipya kinashika nafasi ya tano baada ya Injili nne.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira ya Yesu

Mazingira ya Yesu ni jumla ya mambo ya kijiografia na ya kihistoria yaliotangulia au kuendana na maisha ya Yesu Kristo, akimuathiri kama binadamu katika namna yake ya kuwaza, kusema na kutenda.

Ni muhimu kuyajua ili kumuelewa zaidi mwenyewe, kazi yake na ujumbe wake.

Sanjaranda

Sanjaranda ni jina la kata ya Wilaya ya Manyoni katika Mkoa wa Singida, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,828 waishio humo.

Ufalme wa Israeli

Ufalme wa Israeli unaweza kuhusu falme mbalimbali zilizotokea katika historia ya Israeli, kama vile:

Ufalme wa Muungano chini ya Sauli, Daudi na Solomoni (1050–931 KK)

Ufalme wa Kaskazini (Samaria) chini ya koo mbalimbali (931–722 KK)

Ufalme wa Kusini (Yuda) chini ya warithi wa Solomoni (931–586 KK)

Ufalme wa Wamakabayo (140–37 KK)

Ufalme wa Herode Mkuu (37–4 KK) na warithi wake, wa mwisho wao Agrippa II (hadi 100 hivi BK)

Ukristo

Ukristo (kutoka neno la Kigiriki Χριστός, Khristos, ambalo linatafsiri lile la Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ, linalomaanisha "Mpakwamafuta" ) ni dini inayomwamini Mungu pekee kama alivyofunuliwa kwa Waisraeli katika historia ya wokovu ya Agano la Kale na hasa Yesu Kristo katika [[Agano Jipya]] ambaye ni mwanzilishi wake katika karne ya 1.

Dini hiyo, iliyotokana na ile ya Wayahudi, inalenga kuenea kwa binadamu wote, na kwa sasa ni kubwa kuliko zote duniani, ikiwa na wafuasi 2,400,000,000 (33% kati ya watu 7.274 bilioni), ambao nusu ni waamini wa Kanisa Katoliki na nusu ya pili wamegawanyika kati ya Waorthodoksi (11.9%) na Waprotestanti (38%) wa madhehebu mengi sana.

Karibu wote wanakubali Utatu Mtakatifu, yaani kwamba milele yote Mungu ni nafsi tatu zenye umoja kamili: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni kwa jina lao kwamba mataifa yote wanahimizwa kubatizwa kwa maji, ili kuzaliwa upya, kadiri ya agizo la Yesu ili kuingizwa katika fumbo la Mungu pekee kupitia fumbo la kifo na ufufuko wake mwenyewe.

Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinajulikana kama Biblia. Ndani yake inategemea hasa Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya.

Wakati wa Mababu wa Kanisa misingi ya imani ya Ukristo ilifafanuliwa na Mitaguso ya kiekumeni namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo. Maungamo yao yanakiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu ili kuwaokoa binadamu. Baada ya kuteswa na kuuawa msalabani alizikwa ila akafufuka, siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki mamlaka ya Baba hadi atakaporudi kuhukumu waadilifu na wasiotubu, akiwapa tuzo au adhabu ya milele kadiri ya imani na matendo yao.

Hivyo, kati ya madhehebu ya Ukristo, karibu yote yanamkiri Yesu kuwa kwa pamoja Mungu kweli na mtu kweli: katika umoja na nafsi yake ya Kimungu zinapatikana sasa hali hizo zote mbili.

Yote yanamkiri kuwa Mwokozi wa watu wote, na kuwa ndiye atakayerudi mwishoni mwa dunia kwa hukumu ya wote, ingawa maelezo kuhusu jambo hilo yanatofautiana.

Vilevile yote yanamchukua kama kielelezo cha utakatifu ambacho - kwa msaada wa Roho Mtakatifu na wa sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe, kuanzia ile ya ubatizo - kiwaongoze ndani ya Kanisa katika maadili yao maalumu, kuanzia unyenyekevu na upole hadi upendo unaowaenea wote, bila kumbagua yeyote, hata adui.

Utume wa Yesu

Utume wa Yesu katika Injili, unaanza na ubatizo wake kwa mkono wa Yohane Mbatizaji katika mto Yordani na unakamilika katika mji mtakatifu wa Yerusalemu kwa kifo chake msalabani.Injili ya Luka (3:23) inasema Yesu Kristo alipoanza utume wake alikuwa "na umri wa miaka 30 hivi".Kwa kawaida wataalamu wa Biblia wanakadiria kwamba mwaka wa kubatizwa ulikuwa kati ya 27 na 29 BK na ule wa kuuawa kati ya 30 na 33.Awali Yesu, baada ya kubatizwa na kukaa siku 40 katika jangwa la Yudea, alifanya kazi ya kitume zaidi katika mkoa wa Galilaya, huko alikokulia, akihubiri na kuponya, pamoja na kufukuza pepo wachafu.

Mbali ya hiyo miujiza yake, ni muhimu mwenendo wake wa kukaribiana na watu wa kila aina, bila ubaguzi: tendo lake la kushiriki karamu pamoja na wakosefu lilichukiza wengi, hasa kati ya madhehebu ya Mafarisayo waliokwepa watu hao. Kumbe kwa Yesu lilikuwa dokezo la kwamba Mungu anawaalika wote kutubu na kuingia raha ya ufalme wake.

Wakati huohuo aliita baadhi kumfuata kama wanafunzi katika safari zake. Kati yao aliteua mitume 12 kama mwanzo wa Kanisa lake.Hao aliwaita mitume kwa sababu aliwapeleka kwanza kwa Waisraeli (Math 8) lakini baada ya kufufuka kwa mataifa yote pia (Math 28:16-20).Baada ya kifodini cha Yohane Mbatizaji, Yesu alijiandaa kwenda Yerusalemu kwa mara ya mwisho ili kukamilisha utume wake kwa kujitoa kafara alivyotabiriwa na Yohane: "Huyu ndiye mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi ya ulimwengu".Safari hiyo ya mwisho ilimchukua tena kwa muda karibu na mahali alipobatizwa.Utume wake wa mwisho mjini Yerusalemu ulianza na tukio la kuingia Yerusalemu kwa shangwe ya Wayahudi walioamini kwamba ndiye Masiya, hasa baada ya muujiza mkuu alioufanya, yaani kumfufua Lazaro wa Bethania kutoka kaburini siku ya nne baada ya kifo. Injili zinasimulia kirefu zaidi habari za hiyo wiki ya mwisho kutokana na umuhimu wake kama kilele cha yote.

Yesu

Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).

Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.

Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).

Yothamu wa Yuda

Yothamu (kwa Kiebrania: יוֹתָם, Yōtam, Yōṯam, "Mungu ni mwadilifu"; kwa Kigiriki: Ιωαθαμ, Ioatham; kwa Kilatini: Joatham) alikuwa mfalme wa Yuda kwa miaka 16, akimrithi baba yake Uzia wa Yuda (2 Fal 15:33 na 2 Nya 27:1) hadi alipoondolewa madarakani na wapinzani na hatimaye kurithiwa na mwanae Ahazi.

Wakati wake walifanya kazi manabii Amosi, Isaya na Mika.

Injili ya Mathayo inamtaja katika orodha ya vizazi vya Yesu.

Yudea

Yudea (kwa Kilatini IVDAEA, kwa Kiebrania יהודה, Yehûḏāh au Yehuda, kwa Kigiriki Ἰουδαία) ni jina la jimbo la Dola la Roma kuanzia mwaka 6 hadi 135 BK.

Iliunganisha Uyahudi wenyewe, Samaria na Idumea chini ya liwali.

Asili ya jina ni kabila la Yuda, ambalo kuanzia karne ya 8 KK lilibaki karibu peke yake kati ya makabila 12 ya Israeli.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.