Rasi ya Iberia

Rasi ya Iberia ni kati ya rasi kubwa za Ulaya ikiwa na eneo la km² 582,860. Iko kusini magharibi mwa Ulaya ikipakana na Bahari Atlantiki upande wa kaskazini na magharibi, halafu Bahari Mediteranea upande wa kusini na mashariki.

Milima ya Pirenei ni mpaka kati ya rasi na Ufaransa (Ulaya ya magharibi).

Iberia ni jina la kale tangu zamani za Waroma wa Kale.

España y Portugal
Rasi ya Iberia jinsi inavyoonekana kutoka anga ya nje

Nchi na maeneo

Kwenye rasi kuna nchi zifuatazo:

  • Hispania ni nchi kubwa kwenye rasi
  • Ureno iko upande wa magharibi
  • Andorra ni nchi ndogo sana katika milima ya Pirenei kati ya Hispania na Ufaransa
  • Gibraltar ni eneo ndogo la Uingereza katika ncha ya kusini inayotazamana na Afrika.
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Iberia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Al-Andalus

Al-Andalus (Ar.: الأندلس) ilikuwa jina la Kiarabu kwa sehemu za Rasi ya Iberia (Hispania na Ureno wa leo) zilizotawaliwa kwa karne kadhaa na Waislamu kati ya miaka 711 and 1492.Kisiasa ilikuwa chini ya falme na watawala mbalimbali kwanza chini ya Wamuawiya, halafu Ukhalifa wa Cordoba (929-1031) na baadaye chini ya milki mbalimbali hasa Wamurabitun (Almoravi)(1073-1147) na Wamuwahidun (Almohad) (1125-1269) kutoka Moroko.

Kwa historia yake yote Al-Andalus ilikuwa kando ya milki za Wakristo katika kaskazini zilizokuwa mwanzoni chini ya nguvu ya Waislamu. Lakini polepole walijipatia uhuru wao wakaanza urudisha utawala wa kiislamu nyuma na kutwaa maeneo makubwa kutoka kwao. Tangu kuanguka kwa Cordoba mwaka 1236 emirati wa Granada ilikuwa dola la mwisho la Kiislamu la Hispania hadi ilikamatwa mwaka 1492 na malkia Isabella na ii ilikuwa mwisho wa watawala waislamu katika rasi ya Iberia.

Alcabideche

Alcabideche ni mji wa mkoa wa Lisbon nchini Ureno.

Algueirão-Mem Martins

Algueirão-Mem Martins ni mji wa mkoa wa Lisbon nchini Ureno.

Andalusia

Andalusia (Kihispania: Andalucía) ni jimbo la kujitawala (Kihisp.: comunidade autónoma) la Hispania katika kusini ya rasi ya Iberia. Mji mkuu ni Sevilla. Katika historia ni sehemu ya Hispania iliyotwaliwa na kutawaliwa kwa karne kadhaa na Waarabu Waislamu.

Catalonia

Catalonia ni jumuiya ya kujitegemea nchini Hispania upande wa kaskazini-mashariki mwa Rasi ya Iberia, iliyochagua kuwa taifa huru, lakini serikali kuu ya Hispania imezuia kabisa.

Imepakana na Ufaransa na Andorra kwa upande wa kaskazini, Bahari ya Mediteranea kwa upande wa mashariki na Valencia kwa upande wa kusini. Lugha rasmi ni Kikatalani, Kihispania, na lugha ya Aranese ya Occitan.

Catalonia ina ya mikoa minne: Barcelona, Girona, Lleida, na Tarragona.

Mji mkuu na mkubwa zaidi ni Barcelona, manispaa ya pili ya Hispania na msingi wa eneo la mijini saba zaidi katika Umoja wa Ulaya.

Fungo (familia)

Fungo, paka-zabadi au paka wa zabadi ni wanyama mbua wa ukubwa mdogo hadi wastani katika familia Viverridae. Spishi nyingine huitwa kanu, oyani na binturongi, lakini fungo-miti wa Afrika hana mnasaba sana na fungo na yumo katika familia yake binafsi Nandiniidae. Fungo wanatokea Afrika, Asia na Rasi ya Iberia katika maeneo kama savana, milima na misitu, hususa misitu ya mvua. Hawa ni miongoni mwa wanyama wa asili wa oda Carnivora. Mifupa yao ni takriban sawa na ile ya visukuku vya Eocene hapo ilikuwa miaka milioni 50. Wanafanana na paka wenye pua ndefu na mkia mrefu. Wana kucha zinazoweza kurudiwa ndani, mfupa katika mboo wao na tezi za harufu kando ya mkundu. Ukubwa wao unatofautiana kutoka ule wa oyani (mwili wa sm 30 na uzito wa g 650) hadi fungo wa Afrika (sm 84 na kg 18), lakini binturongi anaweza kuwa kg 25.

Fungo hukiakia usiku na kwa hivyo wana uwezo mzuri sana wa kusikia na kuona, lakini spishi nyingi huonekana mchana pia. Kinyume na uainisho wao katika oda Carnivora wanyama hawa hula vitu vyingi na fungo-miti ni walamimea takriban kabisa. Kwa hivyo chonge zao (meno yaliyochongoka ambayo yatumika kwa kunyafua nyama) zimevia. Kinyaa cha tezi za harufu kinaitwa zabadi na hutumika kwa kuchanganya katika manukato. Angalau zabadi inatengenezwa kwa jinsi ya kikemia sikuhizi, inavunwa kutoka wanyama hata sasa. Katika Afrika fungo hutumika, hususa huko Uhabeshi.

Gibraltar

Gibraltar ni eneo la ng'ambo la Uingereza ambalo linaundwa na rasi ndogo katika bahari ya Mediteranea kwenye ncha ya kusini ya rasi ya Iberia katika Ulaya ya Kusini. Imepakana na Hispania.

Hispania

Hispania (kwa lugha ya wenyewe: España, kwa Kiingereza Spain) ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar.

Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki.

Hispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Hispania.

Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi.

Eneo la nchi ni km² 500,000 nalo lina wakazi 46.733.038 (2018).

Mfalme Felipe VI amevaa taji mwaka 2014, akishika nafasi ya baba yake Juan Carlos I, anayeheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana.

Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba, hivyo kisheria madaraka ya mfalme ni madogo.

Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.

Kanu (mnyama)

Kanu, kala au karasa ni wanyama mbua wadogo wa jenasi Genetta katika familia Viverridae. Kanu mlasamaki aliainishwa katika jenasi Osbornictis lakini wataalamu wameonyesha kama spishi hii ina mnasaba wa karibu na kanu wa jenasi Genetta. Wanyama hawa ni warefu na wembamba wenye mkia mrefu, kichwa kidogo na masikio makubwa. Rangi yao ni nyeupe hadi njano na wana madoa meusi na mkia wenye miviringo. Mkia wao ni mrefu sana: 1-1.5 mara urefu wa mwili. Hiyo inawapa taraju wakisombea miti na kuchupa matawi. Wanatokea Afrika tu isipokuwa kanu madoa-madogo ambaye anatokea Rasi ya Iberia na Mashariki ya Kati pia. Kanu wana tezi kando ya mkundu zinazotoa aina ya zabadi ambayo inanuka sana. Hula wanyama wadogo, mijusi, ndege wadogo, amfibia, wadudu na hata matunda.

Kastilia

Kastilia (kwa Kihispania: Castilla, tamka kas-til-ya; kwa Kiingereza Castille) ni eneo kubwa katikati ya Rasi ya Iberia na nchi ya Hispania.

Kihistoria Ufalme wa Kastilia ulikuwa chanzo muhimu cha Hispania ya baadaye.

Leo hii imegawiwa katika majimbo ya Kastilia-León, Madrid na Kastilia-La Mancha.

Maghrib

Maghrib (المغرب العربي al-maġrib al-ʿarabī; pia: Maghreb) ni sehemu ya kaskazini-magharibi ya Afrika.

Siku hizi jina linataja nchi za Moroko, Algeria na Tunisia, wakati mwingine pia Mauretania na Sahara Magharibi.

Zamani lilimaanisha tu maeneo kati ya pwani ya Bahari Mediteranea na vilele vya Milima ya Atlas pamoja na sehemu za Rasi ya Iberia (Hispania kusini na Ureno), Malta na Sisilia zilizotawaliwa na Waislamu.

Orodha ya milima

Orodha ya milima duniani inataja baadhi tu.

Orodha ya milima ya Ulaya

Hii Orodha ya milima ya Ulaya inataja baadhi yake tu.

Sesimbra

Sesimbra ni mji wa mkoa wa Lisbon nchini Ureno.

Setúbal

Setúbal ni mji wa mkoa wa Lisbon nchini Ureno.

Ukhalifa wa Cordoba

Ukhalifa wa Cordoba (Ar.خلافة قرطبة‎; Khilāfat Qurṭuba) ilikuwa milki kubwa kilichounganisha Al-Andalus iliyokuwa sehemu ya kiislamu ya Rasi ya Iberia (Ureno na Hispania ya leo) kati ya 929 na 1031. Mji mkuu alikotawala khalifa ilikuwa Cordoba.

Ulaya ya Kusini

Ulaya ya Kusini ni sehemu ya kusini ya bara la Ulaya. Kuna maelezo ya kutofautiana ni nchi zipi ambazo ni sehemu ya kanda hili. Maelezo hutofautiana kutokana na njia mbalimbali za kuangalia sehemu hiyo: kwa maana ya kijiografia, kisiasa au kiutamaduni.

Kwa hakika tamko hili lamaanisha:

Nchi za rasi ya Iberia yaani Hispania, Ureno na Andorra.

Nchi za rasi ya Italia yaani Italia, San Marino na Mji wa Vatikani

Malta

UgirikiKwa kawaida nchi zifuatazo au sehemu zifuatazo za nchi huhesabiwa humo pia:

sehemu za kusini za Ufaransa

sehemu za Uturuki kwenye bara la Ulaya

Kupri hata kama ni sehemu ya Asia kijiografiaMara nyingi pia sehemu ya nchi za Balkani zahesabiwa humo:

Albania

Bosnia na Herzegovina

Kroatia

Montenegro

Masedonia KaskaziniZote zinapakana na Mediteranea isipokuwa Masedonia Kaskazini.

Wakati mwingine Bulgaria huhesabiwa hapa pia.

Ureno

Ureno (kwa Kireno Portugal) ni nchi kwenye pembe ya kusini magharibi kabisa ya Ulaya. Upande wa magharibi na kusini imepakana na Bahari ya Atlantiki, na upande wa mashariki na kaskazini imepakana na Hispania.

Mafunguvisiwa ya Atlantiki ni pia sehemu za Ureno. Visiwa hivyo ni Azori kati ya Ulaya na Amerika na Visiwa vya Madeira vilivyoko katika sehemu ya Afrika ya Atlantiki.

Visiwa vya Baleari

Visiwa vya Baleari (kwa Kikatalunya: Illes Balears) ni funguvisiwa vya bahari ya Kati, karibu na rasi ya Iberia, na ni sehemu ya Ufalme wa Hispania.

Visiwa vikubwa ni vinne: Majorca, Minorca, Ibiza na Formentera. Vingine ni vidogo.

Vile vikubwa vinapata watalii wengi wanaovutiwa na hali ya hewa na pwani.

Wakazi wamehesabiwa kuwa 1,106,049 (2010).

Lugha rasmi ni Kihispania na Kikatalunya.

Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.