Parokia


Parokia ni muundo mmojawapo wa zamani sana wa Kanisa Katoliki, ambao umuhimu wake unatokana na kwamba ni sehemu ya jimbo (dayosisi) unapofanyika uchungaji wa kila siku chini ya kasisi anayemwakilisha Askofu.

Kiini cha maisha ya parokia ni adhimisho la Ekaristi siku ya Jumapili, ambapo jumuia nzima ya Kikristo ya eneo husika inakusanyika isikilize Neno la Mungu, imsifu Mungu na Kumega mkate.

Jina

Jina hilo lilianza kutumika katika karne III kutokana na neno la Kigiriki παρоικια (=ujirani) linalotumika katika tafsiri ya Biblia ya Septuaginta kwa maana ya kukaa ugenini.

Katika Sheria za Kanisa Katoliki

Kanuni 515 za Sheria za Kanisa la Kilatini inasema, "Parokia ni jumuia rasmi ya waamini ambayo imeundwa kwa namna ya kudumu ndani ya Kanisa maalumu na imekabidhiwa kichungaji kwa paroko kama mchungaji wake chini ya mamlaka ya Askofu wa jimbo. Ni juu ya Askofu wa jimbo tu kuanzisha, kufuta na kubadilisha parokia; lakini asizianzishe, asizifute wala asizibadilishe sana kabla hajapokea maoni ya Halmashauri ya mapadri. Parokia iliyoundwa kihalali papo hapo ina hadhi ya nafsi ya kisheria".

Katika madhehebu mengine

Mbali ya Kanisa Katoliki, ambalo lina mtandao mkubwa zaidi wa parokia duniani kote, Waorthodoksi, Waanglikana, Walutheri na Wakristo wengine kadhaa wanatumia muundo wa namna hiyo, ingawa mikazo ni tofauti, kulingana na teolojia yao.

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Parokia kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Anthony Banzi

Anthony Banzi (amezaliwa Mangoja, Parokia ya Tawa, Morogoro 28 Oktoba 1946) ni askofu Mkatoliki nchini Tanzania.

Aliwekwa wakfu na Kardinali Polycarp Pengo mwaka 1994. Tangu mwaka huo, ni askofu wa Jimbo la Tanga.

Askofu

Askofu ni mtu mwenye cheo cha juu katika Kanisa. Kwa kawaida huliongoza katika eneo la jimbo dayosisi akisimamia shirika au parokia nyingi.

Chapeli

Kikanisa (kwa Kiingereza Chapel) ni jengo litumiwalo na Wakristo kama mahali pa ibada.

Inaweza kuwa ndani ya taasisi kubwa kama kanisa, chuo, hospitali, ikulu, gereza au chumba cha kuhifadhi maiti au inaweza kuwa imejitenga kabisa, wakati mwingine kwa misingi yake yenyewe. Mpaka Matengenezo ya Kiprotestanti, jengo hilo lilionyesha mahali pa ibada ambapo palitengwa na eneo lililokuwa chini ya jukumu kuu la parokia ya mitaa au mtu yeyote au taasisi. Makanisa mengi makubwa yalikuwa na madhabahu zaidi ya moja au hata moja tu, ambayo kama yangechukua nafasi ya ardhi sawia, yangekuwa kama Chapeli.

Katika Brittany (Ufaransa) kila kijiji kidogo kina chapeli zake chenyewe. Siku hizi nyingi kati ya hizi hutumiwa mara moja tu kwa mwaka, kwa ajili ya mitaa "msamaha" ambayo inaadhimisha mtakatifu ambaye chapeli ni wakfu kwake.Neno Chapeli lina matumizi ya kawaida hasa Uingereza, na hata zaidi katika Wales, kama jengo la ibada liliyotengwa na taasisi, mtu au chini ya jukumu kuu la parokia na katika nchi za [[Scotland] na Ireland makanisa mengi ya Kikatoliki na yale ya Anglikana hujulikana kama chapeli tu.

Nchini Uingereza Kanisa la Anglikana limewekwa na sheria ya kitaifa kama dini rasmi. Huko, kutokana na kupanda kwa umaarufu wa chapeli katika karne ya 19, wakati wa sensa ya mwaka 1851 watu zaidi walihudhuria chapeli, angalau kupunguza gharama zao wenyewe, badala ya makanisa ya Kianglikana.

Chapeli ni la kimadhehebu kawaida, lakini inaweza kuwa yasiyo ya kimadhehebu. Hayo ya mwisho ni maarufu kama sehemu za taasisi zisizo za kidini kama vile hospitali au gereza.

Chapeli zilizojengwa kama sehemu ya kanisa kubwa ni takatifu na hutengwa kwa kusudi au matumizi maalum: kwa mfano, kanisa kuu na makanisa makubwa huwa na "Lady Chapel", kwa heshima ya Bikira Maria; makanisa ya kiparokia huenda yakawa na "Lady Chapel" upande mmoja, na "chapeli ya Sakramenti" ambapo ekaristi inatunzwa kwa madhumuni ya kuchukua Ushirika Mtakatifu kwa wagonjwa na kwa wasioweza kutoka nyumbani. Pia katika baadhi ya madhehebu ya Kikristo, kwa madhumuni ya ibada.

Mkusanyo wa sheria za Kanisa la Kilatini, katika sheria za chapeli (kitaalamu inaitwa "oratory") unasema ni jengo au sehemu yake iliyowekwa wakfu kwa maadhimisho, hasa Misa, ambayo si kanisa la [parokia]]. Hii inaweza kuwa chapeli binafsi (kwa matumizi ya mtu mmoja au kikundi, kwa mfano kwa ajili ya askofu au jumuia fulani); au semi-oratory, ambayo nusu inapatikana kwa umma kwa ujumla (kama chapeli ya seminari ambayo inakaribisha wageni kwa huduma), au oratory umma (kwa mfano, chapeli ya hospitali au ya chuo kikuu).

Goribe

Goribe ni kata ya Wilaya ya Rorya katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31312. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9,915 waishio humo.Ina shule moja ya sekondari. Kuna zahanati mbili za Panyakoo na Tatwe. Kuna Parokia ya Kikatoliki iliyoanzishwa na wamisionari wa Maryknoll mwaka 1959.

Hananasif

Hananasif ni jina la kata ya Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam

,Tanzania yenye postikodi namba 14109

. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 37,115 waishio humo.Katika kata hiyo inapatikana shule ya secondary ya Hananasif na kanisa katoliki parokia ya mt.Ana Hananasif

Jimbo Katoliki la Musoma

Jimbo Katoliki la Musoma (kwa Kilatini "Dioecesis Musomensis") ni mojawapo kati ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.

Eneo lake ni la kilometa mraba 25,150 (Mkoa wa Mara isipokuwa wilaya ya Bunda na parokia mbili katika wilaya ya Musoma vijijini) na lina wakazi 1,040,000, ambao kati yao Wakatoliki ni 215,000 (20.7 %). Parokia ziko 30.

Kikanisa linahusiana na Jimbo Kuu la Mwanza.

Askofu wake ni Michael George Mabuga Msonganzila na makao yake ni Musoma mjini. Kanisa kuu limejengwa kwa heshima ya Mtume Paulo.

Anasaidiwa na mapadri 58, ambao kati yao 38 ni wanajimbo na 20 ni watawa. Kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 3,707. Pia kuna mabruda 12 na masista 200.

Kanisa la Asiria

Kanisa la Asiria, jina lake rasmi ni Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume la Asiria la Mashariki,(kwa Kiaramu ܥܕܬܐ ܩܕܝܫܬܐ ܘܫܠܝܚܝܬܐ ܩܬܘܠܝܩܝ ܕܡܕܢܚܐ ܕܐܬܘܪܝܐ, ʻIttā Qaddishtā w-Shlikhāitā Qattoliqi d-Madnĕkhā d-Āturāyē), ni Kanisa la Waashuru ambalo kihistoria lilikuwa na kiini chake katika Mesopotamia ya kaskazini.

Kutoka huko wamisionari wake katika milenia ya 1 walieneza Ukristo hadi China, India na Indonesia.

Matukio mbalimbali yamepunguza idadi ya waamini wake hadi kufikia sasa 400,000 hivi.

Ni kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki, lakini halina ushirika na Kanisa lingine lolote la kundi hilo wala la aina nyingine yoyote, ingawa kuna mapatano ya kiasi hasa na Kanisa Katoliki kupitia Kanisa la Wakaldayo ambalo linachanga nayo asili moja.

Linaongozwa na Patriarki wake, kwanzia mwaka 2015 Mar Gewardis III anayeishi Erbil, Iraq.

Chini yake kuna maaskofu wakuu, maaskofu, mapadri na mashemasi wanaotumikia majimbo na parokia katika nchi zote za Mashariki ya Kati na Kaukazi, India, Amerika Kaskazini, Oceania na Ulaya.

Upande wa teolojia, Kanisa hilo linafuata mafundisho yaliyotetewa na Patriarki Nestori wa Konstantinopoli hadi akatengwa na Kanisa Katoliki katika Mtaguso wa Efeso (431).

Kinyala

Kinyala ni jina la kata ya Wilaya ya Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,871 walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53535.

Kinyala inakaliwa na makabila makubwa mawili ambayo ni Wanyakyusa na Wasafwa.

Kata ya Kinyala ina shule 13 za msingi ambazo ni Igogwe, Lukata, Kakala, Isumba, Igembe, Kipande, Songwe, Ikukisya, Kisoko, Swaya, Isebelo, Malangali na Ishinga. Kuna pia shule za sekondari 3 ambazo ni Kinyala na Ziwa Ngosi ambazo ni za serikali na sekondari ya binafsi ya Lubala.

Kwa upande wa afya pia kuna hospitali kubwa moja ya Igogwe Hospital inayomilikiwa na Kanisa Katoliki parokia ya Igogwe.

Kiroka

Kiroka ni kata ya Wilaya ya Morogoro Vijijini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67204. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 21,853 walioishi humo.

Kati yao walio wengi ni Waluguru wanaofuata dini ya Uislamu, lakini walau asilimia 10 ni Wakristo, hasa wa Kanisa Katoliki (parokia ya Mtakatifu Kizito ya Jimbo Katoliki la Morogoro).

Kazi kubwa ya wananchi ni kilimo, hasa cha matunda mbalimbali.

Liturujia ya Canterbury

Liturujia ya Canterbury ni madhehebu yanayoendeleza mambo bora ya Anglikana ndani ya Kanisa la Kilatini.

Mwaka 2011 na 2012 Papa Benedikto XVI alianzisha majimbo matatu kwa Waanglikana walioamua kujiunga na Kanisa Katoliki kama makundi.

La kwanza lilianzishwa kwa wale wa Uingereza na Wales (lakini pia Uskoti), la pili kwa wale wa Marekani (baadaye liliongezewa wale wa Kanada), la tatu kwa wale wa Australia (halafu pia Japani). Jumla ya waamini ni 12,200, ambao wanazidi kuongezeka haraka chini ya mapadri 162, wengi wao wakiwa na ndoa.

Kila mojawapo linaongozwa na padri mwenye ndoa aliyewahi kuwa askofu wa Kianglikana, isipokuwa lile la Marekani ambalo limepewa askofu wa kwanza ambaye ni mseja.

Kabla ya hapo kulikuwa na parokia tu za namna hiyo huko Marekani na Kanada, zikifuata hati maalumu ya Papa Yohane Paulo II ya tarehe 20 Juni 1980,Tarehe 9 Desemba 2009, Benedikto XVI alitoa hati Anglicanorum Coetibus, iliyoweka taratibu za uanzishaji wa majimbo yasiyopakana na majimbo ya kawaida ya Kilatini kwa Wakristo wa namna hiyo, na kufikia mwisho wa mwaka 2015 parokia zote zilizoanzishwa kabla ya hapo isipokuwa 2 zimejiunga na jimbo la Kimarekani. Mkutano maalumu kwa ajili hiyo ulifanyika tarehe 8-10 Novemba 2012.

Kwa niaba ya Papa, Idara ya Ibada ya Kimungu ilipitisha the Book of Divine Worship kwanza kwa muda mwaka 1984, halafu moja kwa moja mwaka 1987. Kuanzia tarehe 29 Novemba 2015 nafasi yake imeshikwa na "Divine Worship: The Missal".

Ibada nyingine kwa ajili ya ndoa na mazishi zilipitishwa na idara hiyo tarehe 22 Juni 2012.

Liturujia ya Milano

Liturujia ya Milano ni liturujia maalumu ambayo inatumika katika sehemu kubwa ya jimbo kuu la Milano na katika parokia kadhaa za majimbo ya kandokando (Como, Bergamo, Novara, Lodi) nchini Italia hadi lile la Lugano (Uswisi).

Kesi ya pekee ni parokia ya Pescocostanzo iliyopo katika Italia ya kati.

Kama asili yake anatajwa babu wa Kanisa Ambrosi, aliyekuwa askofu wa jimbo hilo katika sehemu ya mwisho wa karne ya 4. Ndiyo sababu inaitwa pia Liturujia ya Ambrosi.

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano liturujia hiyo imeshughulikiwa sana na wachungaji na wataalamu mbalimbali hata kupata uhai mpya.

Ingawa Wakatoliki wa maeneo hayo (milioni 5 hivi) wanafuata liturujia hiyo, upande wa sheria za Kanisa hawatofautiani na wenzao wa Kanisa la Kilatini.

Makuburi

Makuburi ni jina la kata ya Wilaya ya Kinondoni katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikodi namba 16106. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ina wakazi wapatao 57,408 waishio humo.Kanisa Katoliki lina parokia huko.

Migoli

Migoli ni mji mdogo kwenye Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51221. Iko mita 700 juu ya usawa wa bahari.

Unapatikana kando ya Bwawa la Mtera ambako wakazi wengi hutegemeza maisha yao katika uvuvi.

Eneo hili lina rutuba lakini mvua ni chache (kwa kawaida haifikii mm. 300 kwa mwaka), hivyo wakazi hawajishughulishi sana na kilimo, hivyo wananunua nafaka kutoka sehemu ambazo zinalimwa kwa wingi, kama vile Ismani tarafani na Mtamba mkoa wa Dodoma.

Kumbe ni eneo maarufu kwa ufugaji, hasa wa ng'ombe na mbuzi, wanaostawi katika mbuga isiyo na malale.

Eneo hili, ambapo inapita barabara kuu ya Afrika kutoka Misri hadi Afrika Kusini (ingawa sehemu hii kati ya Dodoma na Iringa haimalizika kutiwa lami), ni endelevu hasa ukilinganishwa na vijiji vingine vya nchi ya Tanzania, kwa kuwa una huduma nyingi za jamii ambazo zimetokana na juhudi za serikali na wananchi wenyewe.

Wafadhili wa miradi mbalimbali ni kama vile parokia katoliki ya Migoli na makampuni ya mawasiliano kama vile Zain, Tigo, Vodacom na Zantel.

Kijiji asili kilikua sana baada ya serikali kuanza kujenga bwawa la Mtera na kulazimisha watu walioishi bondeni na pembezoni mwa mkondo wa mto Ruaha wasogee ikiwa ni miaka ya 1980. Wazee wa kwanza walioshi katika mitaa miwili ya Migoli na Makonge walikuwa Maulidi Ndilwa, Nyakunga, Simili Magomba, Paulo Magomba, Madekedeke, Kinyaga pamoja na familia zao.

Tangu kuanzishwa kwa Bwawa la Mtera na kijiji cha Migoli, shughuli ya uvuvi ilikikuza sana kijiji cha Migoli ambacho kimekuwa mahali pa biashara yaani watu kutoka makambini (makazi yasiyo rasmi ya uvuvi) walikuwa wakiuzia samaki kwenye kijiji cha Migoli.

Hata hivyo wafanyabiashara wa samaki wamekitumia kijiji cha Migoli kuwa sehemu yao ya kufikia kabla ya kwenda kwenye makambi. Makambi yanayokitegemea kijiji cha Migoli ni Nyegere, Mabati, Maperamengi, Mandela, Kilambakitali, Changalawe na mengine mengi.

Hatimaye kijiji kimemegwa na kuzaa kijiji kipya cha Mtera upande wa kaskazini.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Migoli ilikuwa na wakazi wapatao 10,937 waishio humo.Siku hizi barabara inayopita kijijini ikiunganisha Iringa na Dodoma, hivyo pia Cape Town na Kairo, imetiwa lami.

Mwaka wa Kanisa

Mwaka wa Kanisa (pia: mwaka wa liturgia / liturujia) ni mpangilio wa maadhimisho au kalenda inayoratibu majira na sikukuu za Ukristo katika muda wa mwaka mmoja.

Kalenda hii inataja nafasi ya vipindi vya pekee kama vile Majilio (Adventi), Krismasi au Noeli, Kwaresima au Pasaka, pamoja na nafasi ya sikukuu mbalimbali.

Sikukuu kadhaa kama Krismasi zinafuata tarehe za kudumu za kalenda ya jua, lakini nyingine kama Pasaka tarehe zake zinazosogezwa katika kalenda ya kawaida, hasa kwa sababu zinafuata hesabu ya Jumapili, si tarehe katika mwezi fulani.

Mwendo wa vipindi vya liturujia unafanana na ule wa maisha ya binadamu, ambayo yana maadhimisho ya pekee na majira ya kukua na kukomaa kwa utulivu. Vivyo hivyo mwaka wa Kanisa una sikukuu na siku za kawaida, vipindi vya pekee na la.

Sehemu muhimu zaidi ya mwaka huo inategemea Pasaka na Krismasi, sherehe kuu mbili zinazoendesha muda mtakatifu wote, ingawa zimo sikukuu nyingine pia.

Mwanajimbo

Mwanajimbo ni neno linalotumiwa hasa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kuhusu mwamini wake ambaye anategemea jimbo katika shughuli zake za kichungaji au za kiroho kwa jumla.

Kwa namna ya pekee linatumika kuhusu padri au shemasi ambaye ameandikishwa na jimbo kama mmojawapo wa viongozi wake wa kudumu, tofauti na mtawa ambaye ameandikishwa rasmi katika shirika lake.

Pengine katika historia ya Kanisa aina hizo mbili za kleri zilishindana sana upande wa wajibu na haki hasa kuhusu uchungaji katika parokia na makanisa mengine.

Papa Yohane Paulo II

Papa Yohane Paulo II (kwa Kilatini: Ioannes Paulus PP. II; kwa Kiitalia: Giovanni Paolo II; kwa Kipolandi: Jan Paweł II; kwa Kiingereza: John Paul II; 18 Mei 1920 - 2 Aprili 2005) alikuwa papa wa 264 kuanzia 16 Oktoba 1978 hadi kifo chake akidumu katika huduma hiyo kirefu kuliko mapapa wengine wote, isipokuwa Mtume Petro na Papa Pius IX.

Alimfuata Papa Yohane Paulo I akiwa Papa wa kwanza asiye Mwitalia tangu miaka 455 iliyopita, wakati wa Mholanzi Papa Adrian VI (1522 - 1523), tena papa wa kwanza kutoka Polandi (na makabila yoyote ya Waslavi) katika historia ya Kanisa. Alifuatwa na Papa Benedikto XVI.

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Karol Józef Wojtyła (matamshi: ˈkarɔl ˈjuzɛf vɔiˈtɨwa).

Wengi wanamhesabu kati ya watu walioathiri zaidi karne ya 20, hasa kwa sababu tangu mwanzo wa upapa wake alipambana na Ukomunisti uliotesa nchi yake asili na nyinginezo, akachangia kwa kiasi kikubwa kikomo chake na kusambaratika kwa Urusi.Vilevile alilaumu ubepari wa nchi za magharibi na kudai haki katika jamii zote, akitetea hasa uhai wa binadamu na uhuru wa dini.

Upande wa dini, aliboresha uhusiano kati ya Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ya Ukristo pamoja na ule na dini mbalimbali, kuanzia Uyahudi, Ubudha, Uislamu.

Ziara zake 104 kati nchi 129 ulimwenguni kote, mbali na 146 nchini Italia na 317 katika parokia za Roma, zilikusanya mara nyingi umati mkubwa (hadi zaidi ya milioni 4 huko Manila, Ufilipino, mwishoni mwa siku ya kimataifa ya vijana), na kumfanya asafiri kuliko jumla ya mapapa wote waliomtangulia, akiwa mmojawapo kati ya viongozi wa dunia waliosafiri zaidi.

Papa Wojtyła alitangaza wenye heri 1,340 na watakatifu 483, ili kuwapa Wakristo wa leo vielelezo mbalimbali kwa maisha yao ili walenge utakatifu walioitiwa na Mungu. Idadi hiyo ni kubwa kuliko ile ya waliotangazwa na jumla ya Mapapa wote waliomtangulia walau katika karne tano za mwisho.Alikuwa anaongea lugha mbalimbali, zikiwemo za Kipolandi, Kiitalia, Kifaransa, Kijerumani, Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kiukraina, Kirusi, Kiserbokroatia, Kiesperanto, Kilatini na Kigiriki cha kale.Yohane Paulo II alitangazwa na mwandamizi wake Papa Benedikto XVI kuwa mwenye heri tarehe 1 Mei 2011, halafu Papa Fransisko akamtangaza mtakatifu tarehe 27 Aprili 2014.

Sikukuu yake huadhimishwa kila mwaka tarehe 22 Oktoba, kulingana na siku ya kuanza rasmi huduma yake ya Kipapa kwa Misa iliyofanyika katika uwanja mbele ya Basilika la Mt. Petro, Vatikani.

Peramiho

Peramiho ni kata ya Wilaya ya Songea Vijijini katika Mkoa wa Ruvuma, Tanzania. yenye postikodi namba 57213 .Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 15,031 waishio humo. .

Inajulikana hasa kutokana na abasia ya wamonaki Wakatoliki Wabenedikto.

Abasia hiyo ilianzishwa kama kituo cha umisionari na P. Cassian Spiess O.S.B. aliyefika Peramiho mwaka 1898.

Mnamo mwaka 1931 Peramiho ilifanywa kuwa abasia na pia makao ya jimbo chini ya Abate-Askofu Gallus Steiger O.S.B..

Makao ya jimbo yalihamishiwa Songea mnamo mwaka 1969, na siku hizi kuna majimbo matatu (Jimbo kuu la Songea, Jimbo Katoliki la Njombe na Jimbo Katoliki la Mbinga) yaliyotokana na jimbo la zamani la Peramiho.

Peramiho kuna shule na hospitali nzuri pamoja na monasteri.

Pia ni makao makuu ya parokia ya Peramiho ambayo ina vigango vifuatavyo: Parangu, Lilambo, Likuyu, Mwanamonga, Litowa, Nakahuga, Sinai, Maposeni, Mdunduwalo na Morogoro.

Ukanoni

Ukanoni ni mtindo wa maisha ya kitawa katika kanisa katoliki uliokusudiwa hasa kwa mapadri wa parokia za mjini.

Unovisi

Unovisi ni kipindi cha pekee katika malezi ya mashirika ya kitawa. Ni kama kiini chake, na kwa sababu hiyo sheria za Kanisa zinakiratibu kwa uangalifu mkubwa.

Aliyejisikia wito, kwanza anaandaliwa miaka au walau miezi ili kuziba mapengo ya malezi ya awali katika familia, shule, parokia n.k. hadi akomae zaidi kiutu na Kikristo.

Ndipo anapoanza unovisi ambao kwa kawaida unachukua miaka miwili au walau mmojaWakati huo mhusika anatulia kabisa mbele ya Mungu wake akijaribu maisha ya shirika lake ili kuona kama anayaweza.

Katika hilo ni lazima asaidiwe hasa na mlezi na mafundisho mbalimbali ya kidini: Biblia, liturujia, maisha ya Kiroho, nadhiri n.k.

Akiamua na kukubaliwa, anamaliza unovisi kwa kujitoa kwa Mungu walau kwa mwaka mmoja kabla ya kuweka nadhiri za daima.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.