Nasaba

Nasaba ikitumiwa kwenye masomo ya historia au siasa inataja ufuatano wa watawala hasa wafalme katika familia moja. Mtoto wa mfalme huwa mfalme tena na kadhalika.

Neno laweza kutaja pia kipindi cha historia ambako familia fulani ilitawala.

Kati ya nasaba za kifalme za leo ni hasa nasaba ya Matenno wa Japani iliyodumu muda mrefu. Tangu Tenno wa kwanza ni watawala 125 wanaohesabiwa katika familia hiyohiyo hadi Kaisari au Tenno Akihito wa leo.

Nasaba nyingine inyojulikana duniani ni Windsor na malkia Elizabeth II wa Uingereza ni wa nne katika nasaba hii nchini Uingereza.

Katika Afrika familia ya wafalme wa Uswazi iko kati ya nasaba za kale zinazoendelea kutawala. Nasaba ya Suleimani iliyotawala Ethiopia tangu 1270 BK ilipinduliwa katika mapinduzi ya 1974.

Historia ya Misri ya Kale hupangwa kufuatana na nasaba 33 za mafarao wake hadi malkia Kleopatra.

Historia ya Misri

Historia ya Misri inahusu eneo la Afrika Kaskazini ambalo wakazi wake leo wanaunda Jamhuri ya Misri.

Nchi hiyo ni kati ya vitovu vya ustaarabu wa binadamu, na kwa sababu hiyo inavutia watalii wengi.

Historia ya Misri inaweza kugawiwa katika vipindi vifuatavyo:

Misri kabla ya hati ya maandishiMisri ya Kale

Kipindi cha nasaba za kale za Misri karne ya 31 hadi 27 KK

Ufalme mkongwe wa Misri karne ya 27 hadi 22 KK

Kipindi cha kwanza cha kati karne ya 22 hadi 21 KK

Ufalme wa kati wa Misri karne ya 21 hadi 17 KK

Kipindi cha kati mwaka 1640-1570 KK hivi

Ufalme mpya wa Misri mwaka 1570-1070 KK

Kipindi cha tatu cha kati na mwaka 1070-664 KK

Mwishoni mwa kipindi cha Misri ya kale

Nasaba ya ishirini na saba ya Misri mwaka 664-525 KK

Akemenidi ya Misri mwaka 525-332 KKMisri ya Ugiriki na Roma

Misri ya Ptolemi 332-30 KK

Misri ya Rumi mwaka 30 KK hadi 395 BK

Misri ya Bizantaini mwaka 395-645Misri ya Uislamu

Misri ya Uarabu 639-1250

Misri ya Mamuluki mwaka 1250-1517

Misri ya Otomani mwaka 1517-1805Misri ya kisasa

Misri chini ya utawala wa nasaba ya Muhammad Ali mwaka 1805-1882

Misri ya Kisasa tangu mwaka 1882

Jamhuri ya Watu wa China

China (pia: Uchina, Sina; kirefu: Jamhuri ya Watu wa China) ni nchi kubwa ya Asia ya Mashariki ambayo ndiyo nchi yenye watu wengi kuliko zote duniani.

China imepakana na Vietnam, Laos, Myanmar, India, Bhutan, Nepal, Pakistan, Afghanistan, Tajikistan, Kyrgyzstan, Kazakhstan, Urusi, Mongolia, Korea ya Kaskazini.

Kuna pwani ndefu kwenye Bahari ya Kusini ya China na Bahari ya Mashariki ya China ambazo ni bahari ya kando ya Pasifiki.

China kuna makabila 56 tofauti. Wahan ndio kabila kubwa zaidi nchini China kwa idadi ya watu ikiwa na asilimia 92.

Lugha rasmi ni Kichina cha Mandarin kinachotumiwa na asilimia 70 za wananchi.

Siasa inatawaliwa na chama cha kikomunisti.

Mji mkuu ni Beijing lakini Shanghai ndio mji mkubwa zaidi.

Hong Kong iliyokuwa koloni la Uingereza na Macau iliyokuwa koloni la Ureno ni maeneo ya China yenye utawala wa pekee.

Taiwan na visiwa vingine vya Jamhuri ya China vinatazamwa na serikali ya Beijing kuwa majimbo yake lakini vimekuwa kama nchi ya pekee tangu mwaka 1949.

Jenasi

Jenasi (kutoka Kigiriki Γένος genos / Kilatini genus "nasaba, ukoo, familia, aina") ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi unaopanga viumbehai (mimea, wanyama) katika vikundi kulingana na nasaba zao.

Jenasi moja huwa na spishi ndani yake. Jenasi kwa pamoja hupangwa katika familia.

Katika jina la Kisayansi la kiumbehai ni lazima kutaja jenasi. Kwa mfano paka anaitwa "Felis silvestris catus". Felis ni jina la jenasi. Jenasi huandikwa kwa herufi kubwa.

Kaisari Wilhelm II

Kaisari Wilhelm II (kwa jina kamili Friedrich Wilhelm Viktor Albert von Hohenzollern; * 27 Januari 1859 – + 4 Juni 1941) alikuwa mfalme wa mwisho wa Prussia na kaisari wa mwisho wa Ujerumani kuanzia 1888 to 1918.

Alizaliwa kama mtoto wa mfalme mteule Friedrich III na mjukuu wa Kaisari Wilhelm I. Babake alikufa baada ya utawala mfupi wa siku 99 pekee hivyo Wilhelm II akawa mfalme na kaisari akiwa na umri wa miaka 29. Mwanzoni alitawala pamoja na chansella Otto von Bismarck lakini baada miezi michache alifarakana naye na kumwachisha.

Wataalamu wanaona ya kwamba alikuwa na wajibu kubwa kwa kutokea kwa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya kupinduliwa wakati wa upinduzi wa Ujerumani wa 1918 alihamia Uholanzi alipokufa na kuzikwa kwa sababu hakutaka kuzikwa katika Ujerumani isiyo na utaratibu wa kifalme.

Lugha za Kibantu

Lugha za Kibantu ni kundi la lugha ambalo ni tawi la lugha za Niger-Kongo.

Lugha za Kibantu huzungumzwa hasa katika nchi za Nigeria, Kamerun, Guinea ya Ikweta, Gabon, Jamhuri ya Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Tanzania, Komori, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Angola, Namibia, Botswana, Lesotho, Swaziland na Afrika ya Kusini.

Uenezi huo unaonyesha kwamba kundi la lugha za Kibantu ni kubwa kabisa barani Afrika, na idadi ya wanaozitumia ni takriban watu milioni 310.

Neno Bantu, maana yake ni watu katika lugha nyingi za kundi hilo. Shina lake ni -ntu, na kiambishi awali cha ba- kinaonyesha uwingi wa viumbehai. Kwa sababu hiyo, mtaalamu Wilhelm Heinrich Immanuel Bleek (aliyeishi tangu mwaka 1827 hadi 1875) alitumia neno hilo kwa kurejea kundi la lugha hizo. Bleek alilinganisha sarufi za lugha mbalimbali za Kibantu, na baadaye Carl Meinhof alimfuata katika utafiti huo.

Kuna mamia ya lugha za Kibantu; wataalamu wengine wanahesabu 300, wengine wanahesabu 600. Mtaalamu Malcolm Guthrie aliziainisha kulingana na maeneo ya kijiografia. Kila eneo limepata herufi yake — A, B, C, D, E, F, G, H, K, L, M, N, P, R na S — na ndani ya kila eneo kuna tarakimu tena. Pia, Guthrie alichunguza lugha ya nasaba ambayo ni chanzo cha lugha zote za Kibantu.

Mfalme

Mfalme ni mtawala wa kiume juu ya nchi katika utaratibu wa ufalme. Kwa kawaida amerithi cheo chake kutoka mzazi wake aliyekuwa mfalme pia. Lakini kuna pia wafalme waliochaguliwa au kuteuliwa kwa namna nyingine hasa kama mfalme aliyetangulia alikufa bila mrithi.

Utawala wa kifalme ilikuwa hali ya kawaida katika nchi nyingi za dunia kwa muda mrefu.

Mwanamke anayeshika nafasi ya mfalme huitwa "malkia".

Kama cheo kinaendelea katika ukoo mmoja kutoka mababa kwa watoto wao familia hii huitwa nasaba.

Ming (nasaba)

Nasaba ya Ming ilitawala China kati ya 1368 na 1644.

Watawala wa Ming walichukua nafasi ya makaisari wenye asilia ya Mongolia wakafuatwa na nasaba yenye asili ya Manchuria.

Waming walijenga muundo wa serikali iliyodumu hadi mapinduzi ya 1911. Mamlaka yote yalikusanywa mkononi wa kaisari. Walihamisha mji mkuu kutoka Nanjing kwenda Beijing na kujenga Mji Haramu.

Misri

Misri (kwa Kiarabu: مصر, Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki ikiwa na eneo la Rasi ya Sinai kwenye bara la Asia pia.

Ni nchi yenye wakazi milioni 90 na mji mkuu Kairo ni kati ya miji mikubwa zaidi duniani.

Ni kati ya nchi za dunia zenye historia ndefu inayojulikana.

Mitholojia ya Kigiriki

Mitholojia ya Kigiriki ni jumla ya elimu ya visasili au mitholojia ya Ugiriki ya Kale, yaani ukusanyaji wa masimulizi na hadithi kuhusu vyanzo, miungu na mashujaa wao. Zilikuwa moja ya sehemu za dini ya Ugiriki ya Kale.

Chanzo chetu kikuu kuhusu imani ya Wagiriki wa kale kabisa ni shairi ya Theogonia iliyotungwa na Hesiodo mnamo mwaka 700 KK.

Nasaba ya Han

Nasaba ya Han (Kichina cha asili: 漢朝 ; Kichina rahisi: 汉朝; Hanyu Pinyin: Hàn cháo; Wade-Giles: Han Ch'au; 206 KK – 220 BK) ilifuata utawala wa nasaba ya Qin, na ilitangulia Dola Tatu katika Uchina. Utawala huu ulianzishwa na familia maarufu iliyofahamika kama Ukoo wa Liu.

Watu wa China huhesabu nasaba ya Han iliyodumu kwa karne nne kuwa moja ya vipindi vikuu katika historia yote ya nchi. Hivyo, watu wa jamii kubwa ya China hujihesabu mpaka leo “watu wa Han”, kwa heshima ya familia ya Han na utawala waliouanzisha.

Nasaba ya Qing

Nasaba ya Qing (Kichina: 清朝; pinyin: Qīng cháo) ilitawala China kati ya 1644 na 1912.

Watawala wa Qing walichukua nafasi ya makaisari wa nasaba ya Ming. Familia ya Qing ilitoka Manchuria na kwa sababu hii huitwa pia "Nasaba ya Manchu".

Orodha ya Makaizari wa Roma

Orodha hii inataja makaisari wa Dola la Roma kuanzia Kaizari Augustus hadi mwisho wa Dola la Roma Magharibi mwaka wa 476.

Orodha ya nasaba za Kichina

Orodha hii inataja nasaba za kifalme za Kichina na vipindi vinginevyo katika historia ya Uchina.

Nasaba ya Xia (2070 KK- 1600 KK)

Nasaba ya Shang (karne ya 16 KK hadi 1046 KK)

Nasaba ya Chou (1046 KK hadi 256 KK)

Nasaba ya Ch'in (221 KK hadi 207 KK)

Nasaba ya Han (202 KK hadi mwaka wa 220)

Wakati wa San-Guo au "Falme Tatu" (kuanzia 220 hadi 280)

Nasaba ya Hsi Chin (kuanzia 266 hadi 316)

Nasaba ya Dong Jin (kuanzia 317 hadi 420)

Uvamizi wa Hsiung-nu (kuanzia 304 hadi 439)

Nasaba ya Wei (kuanzia 386 hadi 534)

Nasaba ya Sui (kuanzia 581 hadi 618)

Nasaba ya Tang (kuanzia 618 hadi 907)

Wakati wa Shih-Kuo au "Falme Kumi" (kuanzia 907 hadi 960)

Nasaba ya Sung (kuanzia 960 hadi 1279)

Nasaba ya Yüan (kuanzia 1215 hadi 1368)

Nasaba ya Ming (kuanzia 1368 hadi 1644)

Nasaba ya Ch'ing (kuanzia 1636 hadi 1912)Baada ya hapo hakuna nasaba ya kifalme tena, kwa sababu China imekuwa jamhuri.

Tenno

Tenno ni cheo cha mfalme au kaisari wa Japani. Kufuatana na katiba ya nchi yeye ni "ishara wa dola na wa umoja wa taifa".

Tenno wa sasa ni Akihito aliyepokea cheo baada ya kifo cha babake Hirohito mwaka 1989.

Historia ya Japani inamkumbuka tenno wa kwanza kabisa aliyekuwa Jimmu mnamo 660 KK. Wataalamu wengine huwa na mashaka lakini wanakubali ya kwamba watawala hawa walikuwepo angalau tangu karne ya 5 BK. Hadi karne ya 19 ikulu yao ilikuwa mjini Kyoto, tangu Meiji iko Tokyo.

Nasaba ya watawala wa Japani ni nasaba ya kale duniani.

Katika historia ndefu matenno walikuwa na madaraka tofautitofauti. Hata kama walitazamiwa kama wakuu wa taifa hali halisi madaraka yao yalikuwa madogo wakati mwingine. Lakini kulikuwa pia na matenno walioamua kabisa juu ya siasa ya nchi kwa mfano Meiji tangu 1868.

Uajemi

Iran - ايران, pia Uajemi (kutokana na Kiarabu العجم- al-'ajam) ni nchi ya Asia ya Magharibi.

Jina rasmi ya nchi ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au Uajemi. Uajemi imejulikana tangu kale kama nchi iliyochangia mengi katika historia ya binadamu.

Imepakana na Afghanistan, Armenia, Azerbaijan, Iraq, Pakistan, Uturuki na Turkmenistan.

Upande wa kusini kuna mwambao wa Ghuba ya Uajemi (Bahari Hindi) na upande wa kaskazini ni mwambao wa Bahari ya Kaspi.

Tehran ni mji mkuu, pia mji mkubwa nchini.

Uislamu nchini Armenia

Uislamu nchini Armenia ulianza milimani au katika nyanda za juu hasa katika kipindi cha karne ya 7.

Waarabu, na baadaye kabila la Wakurdi, walianza kuloea Armenia hasa kwa kufuatia uvamizi wa Waarabu na kucheza nafasi kubwa kiitikadi, kijamii, kiuchumi na kihistoria nchini.Baada ya uvamizi wa Waseljuki katika karne ya 12, elementi za Waturuki hatimaye zikashinda uwepo wa Waarabu na Wakurdi. Kwa kuanzishwa kwa nasaba za Kiajemi kama vile Nasaba ya Safavid, Nasaba ya Afsharid, Nasaba ya Zand na Nasaba ya Qajar, Armenia ikawa kiungo muhimu cha ulimwengu wa Shia ya Kiajemi, huku ikiwa bado inaheshimu uhusiano na uwepo wa Ukristo nchini humo.

Uislamu nchini Zambia

Ujio wa Uislamu nchini Zambia unarudi nyuma kabisa katika karne ya Hijri ya nne wakati Waislamu wanaanzisha imarati katika pwani ya Afrika Mashariki. Katika zama hizo wafanyabiasha wa Kiislamu walipanua biashara zao hadi maeneo ya ndani na kufikia Zambia katika zama za nasaba ya Omani Al Bu Said. Wafanyabiashara Waarabu waliingia Zambia kutoka katika makao yao makuu ya biashara katika pwani ya Tanzania, Malawi na Msumbiji.

Uislamu nchini Zimbabwe

Ujio wa Uislamu nchini Zimbabwe unarudi nyuma kabisa katika karne ya Hijri ya nne wakati Waislamu wanaanzisha imarati katika pwani ya Afrika Mashariki. Katika zama hizo wafanyabiasha wa Kiislamu walipanua biashara zao hadi maeneo ya ndani na kufikia Zambia katika zama za nasaba ya Omani Al Bu Said. .

Wamuawiya

Wamuawiya (Kar. ‏الأمويون‎ al-umawiyyūn) ni jina la nasaba ya makhalifa waliotawala milki kubwa ya Kiislamu kati ya 661 bis 750 BK. Mfululizo huo ulianzishwa na Muawiya ibn Abu Sufyan aliyekuwa gavana Mwislamu mjini Dameski alipoasi dhidi ya khalifa Ali ibn Abi Talib mnamo mwaka 660. Wamuawiya walikuwa nasaba ya kwanza ya Kiislamu ya kutawala. Waliwafuata makhalifa wanne wa kwanza wakafuatwa na nasaba ya Waabbasi. Mkono mmoja wa familia hii iliendelea kutawala huko Hispania hata baada ya mwaka 750.

Mji mkuu wa Wamuawiya ulikuwa Dameski katika Shamu.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.