Nabii

Neno nabii (kwa Kiebrania נביא nevì, kwa wingi נְבִיאִים nevi'ìm, kwa Kiarabu نبي) linatumika kumtajia binadamu anayesema kwa niaba ya Mungu, hasa kwa kusudi la kuelekeza wenzake wafuate imani na maadili sahihi.

Katika lugha nyingi, mtu huyo anaitwa kwa jina linalotokana na neno la Kigiriki προφήτης [prophētēs], maana yake "anayesema mbele", yaani hadharani (mbele ya wasikilizaji), au kabla ya (jambo kutokea).

Watu wa namna hiyo wanapatikana katika dini nyingi, hususan katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Katika matumizi ya kawaida, neno hilo linatumika hasa kwa mtu ambaye anatabiri jambo, bila ya kujali asili ya maarifa yake.

Jesaja (Michelangelo)
Nabii Isaya. alivyochorwa na Michelangelo katika Cappella Sistina, Vatikani.

Katika Uyahudi

Katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) tunakuta vitabu vingi vinavyojumlishwa katika jina "manabii", kuanzia Yoshua hadi Malaki. Katika Ukristo baadhi ya vitabu hivyo vinahesabiwa kuwa "vitabu vya historia", kumbe kile cha Danieli kinapangwa kati ya "manabii wakuu" pamoja na Isaya, Yeremia na Ezekieli, wakati Wayahudi wanacho kati ya "maandiko (mengine)".

Katika Ukristo

Ukristo unakubali manabii wote wa Agano la Kale, lakini upande wa Agano Jipya ni wachache wanaoitwa hivyo, kwa mfano Agabo anayetajwa katika Matendo ya Mitume.

Kwa jumla ni kwamba Wakristo wote wanahesabiwa kuwa manabii kutokana na wajibu wa kutangaza Neno la Mungu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

Katika Uislamu

Katika Islam mtume Muhammad anapewa nafasi ya pekee kati ya manabii wengi waliotumwa na Mungu kwa binadamu wa nyakati na mahali tofauti. Ndiye anayesadikiwa na Waislamu wengi kuwa nabii wa mwisho na wa kudumu ("mhuri wa manabii" - khātim al-nabiyyīn (Kurani, XXXIII:40).

Uislamu unakubali manabii wa Biblia pamoja na wengine wasiotajwa katika kitabu hicho, kama vile Mwarabu Salih.

Katika dini nyingine

Dini nyingine zinatokana na mafundisho ya mtu anayehesabiwa nabii, kama vile:

Agano Jipya

Agano Jipya ni sehemu ya pili ya Biblia ya Kikristo, ikifuata Agano la Kale: Agano Jipya limefichika katika lile la Kale, na Agano la Kale limedhihirika katika lile Jipya.

Linakusanya vitabu ambavyo Wakristo wote wanaviheshimu kama vitakatifu na vilivyoandikwa baada ya ujio wa Yesu Kristo hadi mwisho wa wakati wa mitume wake.

Vitabu vyake 27 vinaleta habari zake, za mitume wake na za mwanzo wa Kanisa lake.

Vinatakiwa kusomwa kama kilele cha ufunuo wa Mungu kwa binadamu kadiri ya Historia ya Wokovu.

Jina lilitungwa na nabii Yeremia (Yer 31:30) alipotambua kwamba kwa kiasi fulani lile la mlima Sinai lilikuwa na dosari (Eb 8), lakini Mungu kwa uaminifu wake asingeweza kukubali likome tu.

Vitabu vya Agano Jipya ni kama ifuatavyo (Kwa mabano: kifupi cha kawaida kwa kutaja kitabu hiki).

Daudi (Biblia)

Daudi (kwa Kiebrania דוד, Daud, kwa Kiarabu داوُد, Dāwūd) alikuwa mfalme wa pili wa Israeli ya Kale mnamo 1010 KK-970 KK. Alimfuata mfalme Sauli akafuatwa na Suleimani.

Alizaliwa na Yese mjini Bethlehemu mnamo 1040 KK.

Kama kijana alipelekwa kwenye jumba la mfalme Sauli alipopanda ngazi na kuwa kiongozi wa kijeshi.

Kati ya matendo yake yaliyokumbukwa zaidi ni ushindi juu ya Mfilisti Goliathi.

Pamoja na makosa yake, Daudi akabaki kielelezo cha mfalme wa Israeli, ambaye awe tofauti na watawala wengine wote kwa kuwa hasa mtumishi mnyenyekevu wa Mungu bila ya kuyumba kwa kuelekea miungu mingine.

Elisha

Elisha (kwa Kiebrania אֱלִישַׁע, Elisha, yaani "Mungu wangu ni wokovu", kwa Kigiriki Ἐλισσαῖος, Elissaios au Ἐλισαιέ, Elisaie, kwa Kiarabu الْيَسَع Elyasaʿ) alikuwa nabii anayetajwa katika Biblia na katika Qur'an.

Historia ya Wokovu

Kwa jina hilo Wakristo wanamaanisha ufafanuzi wa mpango wa kazi ya Mungu kwa wokovu wa binadamu kadiri ya Biblia.

Injili

Injili ni neno la Kiarabu lenye asili ya Kigiriki εὐαγγέλιον, evangelion, linalotafsiriwa Habari Njema, yaani habari ya Yesu Kristo kufa na kufufuka.

Jina hilo linatumika pia kuhusu vitabu vinavyoeleza maisha na mafundisho ya Yesu kufuatana na kile cha Mtakatifu Marko ambacho kwa wataalamu wengi ndiyo Injili iliyowahi kuandikwa (65-70 B.K.)

Kati ya vitabu vyote vya namna hiyo, Ukristo tangu karne ya 2 umekubali vile vinne vya kwanza tu, ambavyo viliandikwa wakati wa Mitume wa Yesu kuwepo duniani.

Hivyo vinashika nafasi ya kwanza katika orodha ya vitabu vya Agano Jipya kama ifuatavyo: Injili ya Mathayo, Injili ya Marko, Injili ya Luka na Injili ya Yohane.

Injili tatu za kwanza zinafanana kwa kiasi kikubwa katika mpangilio, habari na maneno yenyewe; kwa sababu hiyo zinaitwa Injili Ndugu. Kadiri ya wataalamu wengi mfanano unatokana na kwamba Injili ya Marko ilitumiwa na waandishi wa zile nyingine.

Ile ya Mtume Yohane ni ya pekee na inategemea ushahidi wa Mtume huyo ambaye alipendwa zaidi na Yesu akamfuata kiaminifu hadi msalabani.

Vinahesabiwa na Wakristo kuwa moyo wa Maandiko Matakatifu yote (Biblia) yanayotunza ufunuo wa Mungu, kwa kuwa ndivyo shuhuda kuu juu ya Neno aliyefanyika mwili.

Vile vingi vilivyoandikwa kuanzia karne 2 havitumiwi na Kanisa katika kufundisha imani na katika liturujia. Vinaitwa kwa kawaida apokrifa yaani "bandia".

Waislamu wanakiri Injili kuwa iliteremshwa toka mbinguni kwa nabii Isa, lakini hawakubali vitabu 4 vya Wakristo kama vilivyo.

Isa

Isa ni umbo la jina Yesu katika Qurani na pia katika lugha mbalimbali zilizoathiriwa na Uislamu. Ukurasa huu unahusu imani ya Uislamu kumhusu Yesu kadiri ya Kurani.

Kitabu hicho kilichoandikwa miaka 600 hivi baada ya Kristo kina aya 93 zinazomhusu, lakini hakileti mfululizo wa habari za maisha yake wala za mafundisho yake maalumu.

Ingawa Waislamu wanakiri pia vitabu vitakatifu vya Torati, Zaburi na Injili, katika ibada wanatumia Kurani tu na kwa kawaida ndiyo chanzo chao cha habari juu ya watu na matukio ya kabla yake.

Kwao nabii Isa ni mtume anayeaminiwa kuwa mmojawapo wa mfululizo wa mitume na manabii watukufu 124,000 wa Mwenyezi Mungu walioletwa ulimwenguni kuwapasha wanadamu ujumbe wa umoja wake, ili wamuabudu Yeye peke yake akiwa ndiye Muumba na Mruzuku wao hapa duniani.

Mitume na Manabii hao wameletwa katika zama mbalimbali na kwa watu, kaumu na umma mbalimbali, na mfululizo huu ulianza na Adamu, baba wa wanadamu wote, hadi Mtume Muhammad akiwa ndiye wa mwisho.

Isa ni miongoni mwa mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahimilivu wao mkubwa: Manabii Nuhu na Ibrahimu na Musa na Isa na Muhammad. Tena ni miongoni mwa Mitume waliopewa Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kiitwacho Injili. "Masihi Isa bin Mariamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Neno lake tu alilompelekea Mariamu, na ni Roho iliyotoka kwake" (sura ya 4 aya 171). Wakristo wanamuita kwa kawaida Yesu Kristo.

Karne ya 1

Karne ya 1 ilikuwa kipindi cha miaka mia moja kati ya 1 na 100. Kikamilifu kilianza tarehe 1 Januari 1 B.K. na kuishia 31 Desemba 100. Namba zake zinafuata hesabu ya miaka "baada ya Kristo".

Kama kila "karne" ni kipindi kinachohesabiwa kwa hiari ya binadamu kwa sababu ni mgawanyo wa kalenda tu: katika hali halisi maendeleo na mabadiliko makubwa hayafuati migawanyo ya kalenda ya kibinadamu.

Kuna mambo mengi yaliyotokea wakati wa karne hii.

Karne ya 6 KK

Karne ya 6 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 600 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 501 KK.

Karne ya 7 KK

Karne ya 7 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 700 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 601 KK.

Karne ya 8 KK

Karne ya 8 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 800 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 701 KK.

Karne ya 9 KK

Karne ya 9 KK (= kabla ya Kristo) ni kipindi cha miaka mia kuanzia tarehe 1 Januari 900 KK na kuishia tarehe 31 Desemba 801 KK.

Kitabu cha Amosi

Kitabu cha Amosi ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), na kwa hiyo pia ya Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Nahumu

Kitabu cha Nahumu (kwa Kiebrania נחום, Nahum) ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Obadia

Kitabu cha Obadia ni kifupi kuliko vyote vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), na vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Ni cha nne kati ya vitabu 12 vya Manabii Wadogo.

Ni ukurasa mmoja tu wenye aya 21 ulioandikwa na nabii Obadia katika karne VI K.K. dhidi ya Waedomu waliofurahia uhamisho wa ndugu zao Wayahudi waliopelekwa Babuloni mwanzoni mwa karne hiyo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Nabii Eliya

Eliya (kwa Kiebrania אליהו, Eliyahu, maana yake "YHWH ndiye Mungu wangu"; kwa Kiarabu إلياس, Ilyās), alikuwa nabii katika Ufalme wa Kaskazini (Israeli) wakati wa mfalme Ahabu (karne ya 9 KK).

Habari za nabii huyo maarufu sana katika Biblia, na labda katika Qurani pia, zinapatikana hasa katika vitabu vya Wafalme.

Nabii Yeremia

Yeremia (kwa Kiebrania יִרְמְיָהוּ, Yirməyāhū) ni mmojawapo kati ya manabii wakubwa wa Israeli ambao Biblia inatunza kitabu cha ujumbe wao pamoja na habari za maisha yao.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 1 Mei.

Waarabu

Kigezo:Mashaka

Leo duniani kuna watu wengi sana wanaojinasibisha na Waarabu wakiwa wanaishi Bara Arabu au Mashariki ya Kati au kwengineko ulimwenguni. Watu hawa ambao wanatafautiana baina yao kirangi na kimaumbile na kisura wote wanadai kuwa ni Waarabu au asli zao ni za Kiarabu. Walakini, ni nani hasa hawa Waarabu na nini asli yao?

Yesu

Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).

Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.

Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).

Yohane Mbatizaji

Yohane Mbatizaji (7 K.K. - 29 B.K. hivi) alikuwa nabii wa Uyahudi aliyeishi wakati wa Yesu wa Nazareti na kumtangulia miezi tu kuzaliwa, kuanza utume na kuuawa.

Kufuatana na Injili ya Luka sura 1-2 Yohane na Yesu walikuwa ndugu na mama zao walikuwa wazito kwa wakati mmoja.

Habari zake zinapatikana katika Biblia ya Kikristo na katika vitabu vya mwanahistoria Yosefu Flavius.

Anaheshimiwa na Wakristo na Waislamu kama nabii na mtakatifu.

Pengine sikukuu yake muhimu zaidi ni ile ya kuzaliwa (inayoadhimishwa na Kanisa la magharibi tarehe 24 Juni, miezi sita kabla ya Krismasi), lakini ipo pia sikukuu ya kifodini chake.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.