Mwandiko wa Kiebrania

Mwandiko wa Kiebrania ni mwandiko au alfabeti ya lugha ya Kiebrania ya kale na ya kisasa, pia ya Kiaramu ya Biblia na ya Talmudi.

Kuna pia lugha nyingine za Kiyahudi kama Kiyiddish na Kiladino zilizoandikwa kwa kutumia mwandiko huu.

Alefbet ivri
Alfabeti ya Kiebrania

Herufi

Mwandiko huu unafuata mfumo wa abjadi yaani herufi zake zinaonyesha konsonanti pekee. Kuna herufi 22 na hakuna tofauti kati ya herufi kubwa na ndogo (kama vile A-a, B-b) lakini herufi kadhaa zina umbo tofauti kama zinaandikwa katikati au mwishoni mwa neno. Alama za א ה ו י zinaweza pia kuonyesha vokali ndefu. Vinginevyo kuna nukta zinazoweza kuandikwa juu au chini ya herufi za konsonanti kwa kuonyesha vokali.

Herufi tatu za ב bet, כ kaf na פ pe zinaweza kuonyesha sauti mbili tofauti, ama kwa matamshi laini au magumu. Hapo Bet inaweza kuwa na matamshi ya B au V, Kaf kama K au Kh na Pe kama P au F. Tofauti inaweza kuonyeshwa kwa kuweka nukta katikati ya herufi kwa kutofautisha namna hizi mbili. Mfano : b בּ / v ב .

Mwelekeo wa mwandiko ni kutoka kulia kwenda kushoto, sawa na Kiarabu na kinyume cha mwandiko wetu wa Kilatini.

Alef Bet/Vet Gimel Dalet He Waw Zayin Khet Tet Yod Kaf
א ב ג ד ה ו ז ח ט י כ
ך
Lamed Mem Nun Samekh Ayin Pe/Fe Tsadeh Qof Resh Shin/Sin Taw
ל מ נ ס ע פ צ ק ר ש ת
ם ן ף ץ

Historia

Asili ya mwandiko wa Kiebrania ni alfabeti ya Kifinisia. Tangu karne ya 10 KK herufi za Kifinisia zilizobadilishwa kiasi zilitumiwa kuandika Kiebrania cha kale[1]. Mwandiko huu ulitumiwa wakati wa falme za Israeli na Yudah. Baada ya uhamisho wa Babeli Wayahudi walianza kutumia namna ya mwandiko wa Kiaramu (uliotoka pia kutoka Kifinisia).

Mwandiko huo uliendelea kutumiwa kwa kuandika Kiebrania katika karne nyingi ambazo Wayahudi waliishi ugenini nje ya nchi yao ya asili. Katika karne zile Kiebrania kilikuwa lugha ya kidini na ya kitaalamu lakini haikuwa tena lugha ya kwanza.

Katika karne ya 19 na ya 20 Kiebrania kilikuwa na aina ya ufufuko kama lugha ya kila siku katika harakati ya Uzayuni na hasa tangu kuundwa kwa nchi ya Israeli.

Herufi kama namba

Herufi zilitumiwa pia kama namba ingawa hii si kawaida tena katika Kiebrania cha kisasa.

Herufi Maana ya namba Herufi Maana ya namba Herufi Maana ya namba
א 1 י 10 ק 100
ב 2 כ 20 ר 200
ג 3 ל 30 ש 300
ד 4 מ 40 ת 400
ה 5 נ 50 ך 500
ו 6 ס 60 ם 600
ז 7 ע 70 ן 700
ח 8 פ 80 ף 800
ט 9 צ 90 ץ 900

Marejeo

  1. Old Hebrew

Kujisomea

Viungo vya nje

Baobonye za Kiebrania kwenye Intaneti

Kapernaumu

Kapernaumu (pia Kafarnaumu, kwa Kiebrania כְּפַר נַחוּם, Kfar Nahum, yaani "Kijiji cha Nahum") ilikuwa kijiji cha uvuvi upande wa kaskazini wa Ziwa Galilaya kilichoanzishwa wakati wa ufalme wa ukoo wa Wahasmonei (karne ya 2 KK).Kilikuwa na wakazi 1,500 hivi na masinagogi mawili. Nyumba iliyogeuzwa kuwa kanisa inasemekana ilikuwa ya Mtume Petro.

Kijiji kiliachwa mahame katika karne ya 11 BK. This includes the re-establishment of the village during the Early Islamic period soon after the 749 earthquake.

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.