Msalaba wa Yesu

Msalaba wa Yesu ni msalaba ule ambao Yesu Kristo alisulubiwa juu yake huko Yerusalemu kwa amri ya Ponsyo Pilato siku ya Ijumaa, labda tarehe 7 Aprili 30 BK.

Tukio hilo, pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndiyo kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi.

Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo.

Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa ya Kikristo, hasa uchoraji na uchongaji.

Cristo crucificado
Mchoro wa Diego Velázquez, Yesu msulubiwa, 1631, Prado (Madrid, Hispania) unaonyesha anwani juu ya kichwa chake.
SabinaCrucify
Kigae cha msalaba - Basilica di Santa Sabina huko Roma (Italia).
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Jesus

Historia

Adhabu hiyo kali ilianza kutumika huko Uajemi na kuenea hadi Dola la Roma ambalo liliitumia hasa katika maeneo ya pembeni na kwa watumwa.

Kadiri ya Injili zote nne, Ponsio Pilato, liwali wa Palestina (26-36), aliamua Yesu aadhibiwe hivyo kulingana na shtaka la viongozi wa Wayahudi waliodai kwamba mtuhumiwa alijitangaza kuwa mfalme na kupinga mamlaka ya Kaisari wa Roma, kwa wakati huo Tiberius, ingawa Pilato alikuwa ametambua shtaka halikuwa la kweli, bali lilitokana na husuda.

Kadiri ya Injili ya Yohane, Pilato mwenyewe alisisitiza kwamba, katika maandishi yaliyotakiwa kuwajulisha watu sababu ya adhabu hiyo, iwekwe wazi kwamba Yesu aliuawa kama mfalme wa Wayahudi, ingawa neno hilo lilichukiza viongozi wa taifa.

Maneno ya ilani hiyo yaliandikwa katika lugha tatu:

Maelezo ya teolojia

Yesu alipokufa, nafsi yake ya Kimungu iliendelea kushikamana na roho na mwili vilivyotengana: kwa hiyo mwili wake uliozikwa haukuweza kuoza kaburini; roho yake ilishukia kuzimu kuwatoa waadilifu waliomtangulia awaingize pamoja naye mbinguni. “Mwili wake aliuawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri” (1Pet 3:19). “Roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu” (Mdo 2:31).

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Msalaba wa Yesu kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Bikira Maria

Maria alikuwa mwanamke Myahudi aliyeishi kati ya karne ya 1 KK na karne ya 1 BK. Mke wa Yosefu, alimzaa Yesu Kristo.

Kwa sababu hiyo na kwa utakatifu wake anapewa heshima ya pekee katika madhehebu mengi ya Ukristo, lakini pia katika Uislamu.

Familia takatifu

Familia takatifu katika Ukristo ni hasa ile iliyoundwa na Mtoto Yesu, Bikira Maria na mtakatifu Yosefu.

Kwa imani ya Wakristo ni kwamba Mungu alipomtuma Mwanae pekee kujifanya mtu hakutaka azaliwe nje ya familia, kwa kuwa hiyo ndiyo mpango wake asili kwa ajili ya watu tangu alipoumba Adamu na Eva akawabariki wazaliane.

Heshima kwa Familia takatifu katika Kanisa Katoliki ilianzishwa rasmi na Fransisko wa Laval, askofu wa kwanza wa New France (Kanada) katika karne ya 17.

Imani

Imani kwa Kiswahili ni neno lenye maana mbalimbali (k.mf. "huruma"), lakini ile kuu inahusiana na kitenzi kuamini, kinachofanana na kusadiki. Hapo ni kukubali ukweli wa jambo lisiloweza kuthibitishwa.

Katika dini msingi wake ni mamlaka ya Mungu aliyeshirikishwa ukweli huo kwa njia ya ufunuo maalumu ili kumsaidia binadamu amjue yeye, ajifahamu pamoja na maisha yake duniani na ahera.

Kwa msingi huo, au wa namna hiyo, mtu anaweza kushikilia jambo bila ya uthibitisho mwingine, ingawa pengine Ukristo unatia maanani pia akili katika ujuzi wa ukweli.

Kadiri ya Mtume Paulo imani ikifuatana na tumaini na upendo ni adili kuu mojawapo, msingi, mzizi na chanzo cha wokovu.

Kalivari

Kalivari au Golgotha ni mahali nje ya Yerusalemu wa zamani panaposadikiwa Yesu alisulubiwa akazikwa.

majina hayo mawili yana maana moja: mahali pa fuvu la kichwa, ambapo paliitwa kutokana na sura ya mwinuko wake.

Jina la pili ni jina la Kiaramu lilivyotoholewa katika Kigiriki (Γολγοθᾶ[ς], Golgotha[s], kutoka golgolta; kwa Kiebrania gulgōleṯ), la kwanza ni tafsiri ya Kilatini (Calvariæ Locus, kutoka ufafanuzi wa neno asili uliotolewa na wainjili Marko na Mathayo: Κρανίου Τόπος, Kraníou Tópos).

Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu

Kanisa la Kaburi na Ufufuo wa Yesu liko mjini Yerusalemu mahali ambako kufuatana na mapokeo ya Ukristo Yesu alisulubiwa, akawekwa kaburini na kufufuka siku ya tatu.

Kanisa hili laitwa "Kanisa la ufufuo" na Wakristo wenyeji Waorthodoksi (Kiarabu: كنيسة القيامة kanisat-al-qiyama) na "Kanisa la Kaburi" kwa lugha nyingi za Ulaya.

Kufuatana na mapokeo ya mahali mwamba wa Golgota uliposimama msalaba wa Yesu na kaburi alikozikwa vyote vilikuwa karibu sana hivyo mahali pote pawili hufunikwa na jengo lilelile.

Majina ya Yesu katika Agano Jipya

Majina ya Yesu katika Agano Jipya ni namna mbalimbali za kumuita kwa heshima na katika jitihada za kuweka wazi yeye ni nani kweli, tena ni nani kwetu sisi binadamu.Pamoja na jina Yesu alilopewa alipotahiriwa siku ya nane baada ya kuzaliwa na Kristo, katika Agano Jipya anaitwa kwa namna nyingine 196kama vile:

Emanueli

Bwana

Neno

Mwana wa Mungu

Mwana wa Adamu

Mwana wa Daudi

Mwanakondoo wa Mungu

Adamu mpya

Mwanga wa ulimwengu

Mfalme wa Wayahudi

Mwalimu

Mwokozi

Mkate wa uzima

Mjumbe wa Agano Jipya

Kuhani mkuu

Nabii

Mfariji (au Mtetezi au Msimamizi)

Alfa na Omega

Nyota ya asubuhi

Masiya

Masiya (au Masiha), kutoka Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ mashiakh, maana yake Mpakwamafuta ni jina la heshima ambalo Biblia inampa mfalme au kuhani aliyewekwa wakfu kwa Mungu kwa kupakwa mafuta atende kwa niaba yake kazi ya kusaidia taifa lake hasa kwa kulikomboa.Tofauti na kawaida, Biblia inamtaja kama Masiha hata mfalme Koreshi Mkuu wa Uajemi kwa sababu Mungu alimtumia kutoa Wayahudi katika uhamisho wa Babeli na kuwaruhusu warudi Yerusalemu na kujenga upya hekaluHata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani

Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu

Mitazamo ya Agano Jipya juu ya Yesu inatofautiana kadiri ya waandishi, lakini bila kuvunja umoja wa imani yuu yake kama Kristo na Mwana wa Mungu.

Mitazamo muhimu zaidi ni ile ya Mtume Paulo na Mtume Yohane, ambao ndio wanateolojia hasa, lakini ipo mingine kama ile ya Injili ya Marko, Injili ya Mathayo, Mwinjili Luka, Waraka kwa Waebrania n.k.

Pengine mwandishi yuleyule anatushirikisha mitazamo tofautitofauti katika vitabu vyake, kwa mfano kutokana na maendeleo ya uelewa wake. Hivyo jinsi Yesu Kristo anavyoonekana katika Waraka kwa Waefeso imeendelea kuliko ilivyo katika Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike ulioandikwa na Paulo yuleyule zaidi ya miaka 10 kabla yake.

Kristolojia inakusanya mitazamo hiyo yote na kujitahidi kuelewa zaidi tena fumbo la Kristo.

Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu

Mitazamo ya Kiyahudi juu ya Yesu ni ya aina mbalimbali, lakini yote haimkubali, la sivyo ingewabidi wahusika wamuamini na kubatizwa badala ya kuendelea na dini yao ambayo viongozi wake walimhukumu ni kafiri anayestahili kuuawa.

Kwa kawaida Wayahudi wanamuona Yesu kama mmojawapo kati ya wengi waliojinadi kuwa Masiya katika nyakati mbalimbali za historia ya taifa lao.Yesu anatazamwa kama yule aliyefaulu zaidi kukubalika, na kwa sababu hiyo, kuleta madhara makubwa kuliko wote.Uyahudi haujawahi kumkubali rasmi Masiya yeyote kuwa ametimiza utabiri wa manabii. Zaidi ya hayo, unaona ibada ya Wakristo kwa Yesu kuwa kinyume cha imani katika Mungu mmoja tu.Katika Karne za Kati, Judah Halevi na Maimonide walimuona Yesu (kama vile Muhammad) kama mtu muhimu katika kuandaa mataifa yote kwa ujio wa Masiya atakayeyafanya yamuabudu Mungu pekee.

Siku hizi kuna wataalamu Wayahudi wanaosema Yesu alikuwa jirani na dini yao kuliko Injili zinavyoonyesha. Mtazamo huo ulianzishwa katika karne ya 18 na Jacob Emden na Moses Mendelssohn.

Mitume wa Yesu

Mtume wa Yesu Kristo (kwa Kigiriki ἀπόστολος, apóstolos, aliyetumwa), kadiri ya Agano Jipya, ni mmojawapo kati ya wale wanaume 12 ambao Yesu aliwateua mapema akawatuma kuhubiri Ufalme wa Mungu kwanza kwa taifa la Israeli, halafu kwa mataifa yote duniani.

Baada ya kifo na ufufuko wake, hao wakawa viongozi wa Kanisa ambalo hadi leo linajitambua kujengwa juu yao.

Habari zao, lakini hasa za Petro, zilianza kuandikwa na Mwinjili Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ambamo baadaye mhusika mkuu ni Mtume Paulo aliyedai kuteuliwa na Yesu Kristo baada ya kufufuka.

Mshumaa wa Pasaka

Mshumaa wa Pasaka au Mshumaa mkuu ni mshumaa maalumu unaotumika katika liturujia ya madhehebu mbalimbali ya Ukristo wa magharibi kama kiwakilishi cha Yesu mfufuka.

Mshumaa mpya wa namna hiyo unabarikiwa na kuwashwa kila mwaka katika kesha la usiku wa Pasaka, halafu unawashwa wakati wa maadhimisho mbalimbali, kama vile yale muhimu zaidi ya Kipindi cha Pasaka (hadi Pentekoste) na hata nje yake, kwa mfano wakati wa ubatizo na mazishi ya Kikristo.

Unatakiwa kuwa mkubwa kuliko mishumaa ya kawaida na uweze kudumu hadi Pasaka ya mwaka unaofuata.

Kwa kawaida unachorwa alama mbalimbali, hasa msalaba wa Yesu na herufi za Kigiriki Alfa na Omega, ambazo ni ya kwanza na ya mwisho katika alfabeti ya lugha hiyo ya Agano Jipya, na hivyo zinamaanisha kuwa Kristo ni mwanzo (asili) na mwisho (lengo) wa ulimwengu wote.

Baada ya kuwashwa kwenye moto wa Pasaka, mshumaa huo unapelekwa kwa maandamano hadi mimbarini, na wakati huo waamini wanawasha kwake mishumaa yao binafsi ili kumaanisha kwamba wameshirikishwa mwanga wa Kristo na kumfuata.

Mti wa uzima

Mti wa uzima (kwa Kiebrania עֵץ הַֽחַיִּים, Etz haChayim,) ni mfano unaotumiwa na Biblia.Katika kitabu cha Mwanzo, mti wa uzima unapatikana katika mstari 2:9 kama mti uliopandwa na YHWH Elohim (יְהוָה אֱלֹהִים) karibu na mti wa ujuzi wa mema na mabaya (עֵץ הַדַּעַת) "katikati ya bustani ya Eden".Katika 3:24 imeandikwa kwamba baada ya dhambi ya asili kerubi analinda njia inayofikia mti wa uzima.

Kitabu cha Mithali kinatumia jina hilo mara nne (3:18, 11:30, 13:12 na 15:4).

Hatimaye Kitabu cha Ufunuo kinatumia usemi wa Kigiriki ξύλον (τῆς) ζωής, xylon (tēs) zōës, mara nne vilevile (2:7, 22:2, 22:14 na 22:19.

Kwa kawaida Wakristo wamechukua usemi huu kama wa fumbo kwa msalaba wa Yesu.

Mtume Yohane

Yohane mwana wa Zebedayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu, ambaye alipendwa na mwalimu wao kuliko wenzake wote.

Mapokeo ya Kikristo yanamuona kuwa mwandishi wa Injili ya Yohane, wa barua tatu (Waraka wa kwanza wa Yohane, Waraka wa pili wa Yohane, Waraka wa tatu wa Yohane) na wa Kitabu cha Ufunuo.

Mwana wa Daudi

Mwana wa Daudi ni jina la heshima la wanaume waliotokana na vizazi vya mfalme Daudi na hivyo kuhusishwa na ahadi alilopewa na nabii Nathani kwamba ukoo wake utatawala milele (2Sam 7:1-29).

Kwa namna ya pekee jina hilo lilitumika kwa Yesu aliyetambuliwa na wengi kuwa ndiye Masiya aliyetazamiwa, ama wakati wa maisha yake au baada ya kifo chake.

Injili ya Mathayo na Injili ya Luka zinasisitiza haki ya Yesu kuitwa hivyo kwa kuorodhesha vizazi kati ya Daudi na Yosefu, mume wa Bikira Maria, mama yake.

Mwana wa Mungu

"Mwana wa Mungu" ni jina linalotumiwa katika dini mbalimbali ili kusisitiza uhusiano wa mtu fulani na Mungu au mmojawapo wa miungu. Kwa maana hiyo lilitumika hasa kwa ajili ya watawala.

Pengine linamaanisha viumbe vingine, kama vile malaika.

Ufufuko wa Yesu

Ufufuko wa Yesu ndio tukio kuu lililotangazwa daima na Kanisa lake lote kuhusu mwanzilishi wake, Yesu Kristo, kuanzia ushuhuda wa Mitume wa Yesu na maandiko ya Agano Jipya, hususan Injili, hadi leo.

Kadiri ya imani hiyo, siku ya tatu baada ya kuuawa msalabani Ijumaa kuu, Yesu alifufuka mtukufu akiacha kaburi lake na vitambaa vyote vilivyotumika kumzikia.

Tangu Jumapili hiyo na kwa muda wa siku arubaini (kadiri ya Matendo ya Mitume 1:3), yeye aliendelea kuwatokea mara kadhaa wanafunzi wake, hadi alipoonekana nao akipaa mbinguni huku akiwabariki.

Tukio hilo linaadhimishwa kila mwaka kwenye Pasaka ya Kikristo na kila wiki kwenye Dominika.

Kwa Wakristo, ufufuko wa Yesu ndiyo sababu na kielelezo cha ufufuko wa waadilifu wote siku ya kiyama.

Ujio wa pili

Ujio wa pili ni imani ya kwamba Yesu, aliyekuja mara ya kwanza kwa unyenyekevu alipozaliwa na Bikira Maria, atashuka tena toka mbinguni kwa utukufu siku ya kiyama.

Ukoo wa Yesu

Ukoo wa Yesu unapatikana katika vitabu viwili vya Agano Jipya: Injili ya Mathayo ambayo inaorodhesha vizazi kuanzia Abrahamu hadi kwa Yosefu (mume wa Maria), na Injili ya Luka inayorudi nyuma kuanzia Yosefu hadi kwa Adamu, aliyeumbwa na Mungu mwenyewe.

Injili hizo zote mbili zinasisitiza kwamba Yosefu si mzazi wa Yesu, kwa kuwa Bikira Maria alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Pia zinasisitiza kwamba Yesu ni Mwana wa Daudi, yaani kwa njia ya Yosefu, ambaye kinasaba anatokana na mfalme huyo maarufu wa Agano la Kale, ana haki ya kurithi cheo chake.

Hata hivyo majina mengi ni tofauti katika orodha hizo mbili, kiasi kwamba wataalamu wanatoa maelezo mbalimbali kuhusiana na desturi za Israeli wakati ule, kwa mfano katika kutumia orodha ya vizazi, na kutokana na malengo ya Wainjili hao, ambao wote wawili walitaka kusisitiza kihisabati kwamba Yesu amefika kwa wakati mwafaka uliopangwa na Mungu kwa makini (vizazi 14x3 kadiri ya Mathayo; 7x11 kadiri ya Luka).

Akiwaandikia Wayahudi, mwinjili Mathayo alitaka kusisitiza kwamba Yesu ni Daudi mpya, lakini pia mrithi wa Abrahamu katika kuwa baraka kwa mataifa yote.

Akiwaandikia watu wa mataifa, mwinjili Luka alitaka kuonyesha kwamba Yesu ni mwana wa Adamu, hivyo anahusiana na binadamu wote.

Umwilisho

Umwilisho (kwa Kiingereza "incarnation" kutoka Kilatini "incarnatio") ni neno la teolojia linalotumika kulitaja fumbo la imani ya Ukristo la kwamba Mwana wa Mungu alijifanya binadamu kweli kwa kutwaa roho na hata mwili kama vile vya mtu yeyote.

Mkazo juu ya mwili unatokana na dibaji ya Injili ya Yohane inayosisitiza ajabu la tukio hilo ikisema: "Neno akawa mwili akakaa kwetu" (1:14).

Kwa msingi huo Kanuni ya imani ya Nisea-Konstantinopoli inafundisha kukiri:

Alishuka toka mbinguni kwa ajili yetu sisi wanadamu na kwa ajili ya wokovu wetu, akapata mwili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kwake yeye Bikira Maria akawa mwanadamu.

Umwilisho ulifanyika pale ambapo Maria alikubali wito wa Mungu kwake alivyoletewa na Malaika Gabrieli katika kijiji chake, Nazareti . Habari inasimuliwa hivi (Lk 1:26-38):

26 Mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27 kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu. 28 Akaingia nyumbani kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. 29 Naye akafadhaika sana kwa ajili ya maneno yake, akawaza moyoni, Salamu hii ni ya namna gani? 30 Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu. 31 Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu. 32 Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake. 33 Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho. 34 Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? 35 Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. 36 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; 37 kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. 38 Mariamu akasema, Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema. Kisha malaika akaondoka akaenda zake.

Dini nyingine ziliwahi kusimulia juu ya mungu fulani kuja duniani akionekana kama mtu (kwa mfano Avatar katika Uhindu), lakini umwilisho ni wa pekee kwa kuwa unatokana na imani ya kuwa Yesu tangu alipotungwa tumboni mwa mama yake ni binadamu halisi kama mwingine yeyote, ingawa nafsi yake ni ya milele kama ile ya Mungu Baba na ya Roho Mtakatifu.

Imani hiyo inaongoza kumkiri Yesu kuwa Mungu kweli milele yote na mtu kweli tangu alipotwaa mwili. Kwa sababu hiyo, Wakristo wengi (Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na baadhi ya Waprotestanti) wanamuita Maria "Theotokos" (yaani "Mzazi wa Mungu" au "Mama wa Mungu", kwa maana ni mama aliyemzaa mtu ambaye tangu milele ni Mungu, si kwamba aliweza kumzaa Mungu kama Mungu).

Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Msalaba wa Yesu  • Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.