Mlolongo wa Kitume

Mlolongo wa Kitume (kwa Kiebrania האפיפיור הירושה, kwa Kigiriki Αποστολική διαδοχή) ni jambo linalodaiwa na imani ya baadhi ya madhehebu ya Ukristo, ya kwamba ni lazima viongozi wa Kanisa washiriki mamlaka ya Mitume wa Yesu katika mlolongo usiokatika wa kuwekewa mikono na maaskofu katika kuwapatia daraja takatifu.

Imani hiyo inatiwa maanani hasa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki, lakini pia Waanglikana na wengineo.

Kwao, maaskofu wa leo ni waandamizi wa wale wa jana na juzi hata kurudia kwa wale waliowekewa mikono na mitume wenyewe katika karne ya 1.

Mlolongo huo unahakikisha uhalali wa mamlaka yao katika kufundisha, kutakasa na kuongoza.

Kwa madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti, suala la mikono si la lazima, kwani kwao ni muhimu zaidi kuendeleza mafundisho ya mitume.

Consécration-de-Déodat
Mlolongo wa Kitume unasadikiwa kupitia tendo la maaskofu kumwekea mtu mikono kichwani na kumuombea katika kumpatia daraja takatifu.

Vyanzo na viungo vya nje

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mlolongo wa Kitume kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Jimbo Kuu la Nyeri

Jimbo Kuu la Nyeri ni mojawapo kati ya majimbo 26 ya Kanisa Katoliki nchini Kenya.

Ni makao makuu ya kanda ya Kanisa ambayo inaundwa nalo na majimbo ya Embu, Maralal, Marsabit, Meru, Muranga na Nyahururu.

Mwaka 2004 lilikuwa na waamini 476.870 kati ya wakazi 790.327, waliogawanyika katika parokia 28.

Kwa sasa linaongozwa na askofu mkuu Peter J. Kairo.

Justino de Jacobis

Justino de Jacobis (San Fele, Potenza, Italia, 9 Oktoba 1800 - Eidale, Massawa, 31 Julai 1860) alikuwa mtawa wa Shirika la Misheni (Wavinsenti), halafu askofu na mmisionari nchini Ethiopia na Eritrea.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu tangu tarehe 26 Oktoba 1975. Hata Wakristo wengine na Waislamu wanatembelea kaburi lake kwa heshima.Sikukuu yake ni tarehe 31 Julai.

Kanisa la Kilatini

Kanisa la Kilatini (wakati mwingine "Kanisa la Kiroma") ni moja ya madhehebu yanayounda Kanisa Katoliki. Ndiyo kubwa kuliko yote (97% za waumini wote), likiwa na Wakristo zaidi ya bilioni 1 duniani kote.

Mengine ni Makanisa Katoliki ya Mashariki (3%) yanayofuata mapokeo na hasa liturujia kama ya Waorthodoksi lakini yakiwa na ushirika kamili na Papa wa Roma ambaye ndiye mkuu wa Kanisa la Kilatini, pamoja na kwamba ni pia mkuu wa Kanisa Katoliki lote.

Jina linatokana na kwamba kwa karne nyingi lugha pekee iliyotumika katika ibada zake ilikuwa Kilatini.

Kanisa hilo lote upande wa sheria linafuata Mkusanyo wa sheria za Kanisa, kumbe upande wa liturujia wengi wa waamini wake wanafuata mapokeo ya Kanisa la Roma, lakini wengine wanafuata mapokeo ya Ambrosi wa Milano, au yale ya Lyon, Braga, Toledo na ya mashirika mbalimbali ya kitawa (k.mf. Wakartusi na Wadominiko).

Hivi karibuni waamini waliotokea madhehebu ya Anglikana wameruhusiwa kuendelea kutumia baadhi ya matini yake katika ibada wakiwa sasa ndani ya Kanisa la Kilatini.

Kardinali

Kardinali ni cheo kimojawapo cha juu katika Kanisa Katoliki, hasa Kanisa la Kilatini, lakini si daraja takatifu.

Kigango

Kigango ni sehemu ya parokia ambayo hupata huduma kutoka kwa paroko na mapadri wenzake badala ya kuwa na padri mkazi.

Mara nyingi kina kanisa lake ambamo ibada zinafanyika kawaida kutokana na umbali wa kanisa la parokia.

Katika kigango zinapatikana jumuia ndogondogo za Kikristo zinazounganisha familia kadhaa.

Liturujia ya Braga

Liturujia ya Braga ni liturujia maalumu inayotumika tangu karne ya 6 hasa katika jimbo kuu la Braga (Ureno).

Inahusiana na aina nyingine za liturujia ya Kilatini, kama vile liturujia ya Toledo na liturujia ya Roma.

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano, jimbo kuu la Braga limeamua (1971) mapadri waweze kuendelea kwa hiari yao na liturujia hiyo au kutumia ile ya Roma.

Liturujia ya Kilatini

Liturujia ya Kilatini ni aina ya liturujia ya Ukristo iliyoenea upande wa magharibi wa Dola la Roma ambapo ilitumika lugha ya Kilatini.

Liturujia hiyo ilistawi Ulaya magharibi na Afrika kaskazini.

Polepole liturujia ya Roma, mji mkuu wa Walatini uliotawala dola hilo, ilienea katika maeneo mengi ya Kanisa Katoliki, hasa kutokana na juhudi za makusudi za kaisari Karolo Mkuu za kuunganisha mataifa yaliyokuwa chini ya himaya yake.

Baadaye Mtaguso wa Trento ulizidi kudai Wakatoliki wa magharibi wafuate wote liturujia ya Roma, isipokuwa kama liturujia yao maalumu yaliendelea zaidi ya miaka 200.

Hivyo baadhi ya liturujia nyingine za Kilatini zimedumu mpaka leo, kama vile liturujia ya Ambrosi kandokando ya Milano (Italia), liturujia ya Kimozarabu hasa huko Toledo (Hispania), liturujia ya Braga huko Ureno na kidogo liturujia ya Lyon huko Ufaransa.

Pia baadhi ya mashirika ya kitawa yanatunza liturujia za pekee.

Liturujia ya Lyon

Liturujia ya Lyon (kwa Kilatini: ritus Lugdunensis) ni liturujia mojawapo ya Kanisa la Kilatini ambayo imeendelea kutumika katika jimbo kuu la Lyon (Ufaransa) tangu karne ya 9 hadi leo, ingawa kwa kuzidi kufifia, hasa baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano.

Liturujia ya Milano

Liturujia ya Milano ni liturujia maalumu ambayo inatumika katika sehemu kubwa ya jimbo kuu la Milano na katika parokia kadhaa za majimbo ya kandokando (Como, Bergamo, Novara, Lodi) nchini Italia hadi lile la Lugano (Uswisi).

Kesi ya pekee ni parokia ya Pescocostanzo iliyopo katika Italia ya kati.

Kama asili yake anatajwa babu wa Kanisa Ambrosi, aliyekuwa askofu wa jimbo hilo katika sehemu ya mwisho wa karne ya 4. Ndiyo sababu inaitwa pia Liturujia ya Ambrosi.

Baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano liturujia hiyo imeshughulikiwa sana na wachungaji na wataalamu mbalimbali hata kupata uhai mpya.

Ingawa Wakatoliki wa maeneo hayo (milioni 5 hivi) wanafuata liturujia hiyo, upande wa sheria za Kanisa hawatofautiani na wenzao wa Kanisa la Kilatini.

Liturujia ya Roma

Liturujia ya Roma ni liturujia iliyoenea katika sehemu kubwa ya Kanisa Katoliki, kutoka makao yake makuu, Roma (Italia).

Kwa asili yake ni liturujia ya Kilatini, ingawa kwa sasa inaadhimishwa katika lugha nyingi duniani kote.

Kilichochangia uenezi huo ni hasa heshima ya Kanisa la Roma na askofu wake, Papa.

Katika baadhi ya nchi, kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baraza la maaskofu limekubaliwa kutamadunisha liturujia hiyo, bila ya kuvunja umoja wake wa msingi.

Liturujia ya Roma isiyo ya kawaida

Liturujia ya Roma isiyo ya kawaida ni taratibu za ibada zinavyotumika katika Kanisa Katoliki kufuatana na mapokeo ya Roma jinsi yalivyokuwa mwaka 1962.

Mabadiliko ya liturujia yaliyofanywa baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano (1962-1965), baadhi yakiwa halali na baadhi kinyume cha sheria za Kanisa, yalisababisha upinzani mkali kutoka kwa wapenzi wa taratibu za awali, ambazo kwa kiasi kikubwa zilipangwa na Papa Pius V baada ya Mtaguso wa Trento na kwa sababu hiyo pengine zinaitwa liturujia ya Trento.

Hatimaye mwaka 2007 Papa Benedikto XVI kwa hati Summorum Pontificum alipanua ruhusa ya kutumia taratibu hizo duniani kote kama namna isiyo ya kawaida ya liturujia ya Roma.

Liturujia ya Toledo

Liturujia ya Toledo (au liturujia ya Kimozarabu, yaani ya kati ya Waarabu) ni liturujia ya pekee inayotumika hasa katika jimbo la Toledo (Hispania) pamoja na liturujia ya Roma.

Liturujia hiyo ilianza katika karne ya 4 na kudumu mpaka leo, ingawa kwa shida, kutokana na uenezi wa liturujia ya Roma, ambayo ni aina kubwa zaidi ya liturujia ya Kilatini.

Liturujia ya Vipindi

Liturujia ya Vipindi ni sala rasmi ya Kanisa kama inavyoadhimishwa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, lakini ni jina hasa la mpangilio unaofuatwa na Kanisa la Roma baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano (kwa Kilatini jina ni Liturgia Horarum).

Kwa njia yake wakleri, watawa na waamini wote wa Yesu wa madhehebu hayo wanaungana naye katika sala yake ya kudumu, na wanasaidiwa kuishi kitakatifu saa zote za siku kwa kumkumbuka Mungu mara kwa mara.

Inaitwa hivyo kwa sababu inafanyika kwa vipindi mbalimbali kadiri ya mwendo wa siku (usiku na mchana): muhimu zaidi ni vipindi vya asubuhi (Masifu ya asubuhi) na jioni (Masifu ya jioni), lakini kuna pia vipindi vya usiku kati au alfajiri (Kipindi cha masomo), mchana (Sala ya kabla ya adhuhuri, Sala ya adhuhuri na Sala ya baada ya adhuhuri) na kabla ya kulala (Sala ya mwisho).

Katika Kanisa la Kilatini hiyo sala ya Kanisa inategemea hasa Biblia ya Kikristo kwa kutumia Zaburi na masomo kutoka kwake.

Matini yake yote yamekusanywa pamoja katika kitabu kimoja ambacho kwa sababu hiyo kilizoeleka kuitwa breviari (yaani: "matini kwa ufupi", badala ya kuzagaa katika vitabu mbalimbali kama zamani).

Mtaguso Mkuu

Mtaguso mkuu ni mkutano mkuu wa maaskofu kutoka pande zote za dunia na waamini wengine kadhaa ambao unafanyika kwa nadra sana katika Ukristo.

Mwalimu wa Kanisa

Mwalimu wa Kanisa ni jina la heshima ambalo kwa nadra Kanisa Katoliki linampa mtakatifu ambaye katika maisha, mafundisho na maandishi yake alionyesha na kueneza mwanga wa pekee katika masuala ya imani, maadili na maisha ya kiroho.

“Tamko la kwamba mtakatifu fulani ni Mwalimu wa Kanisa lote linategemea utambuzi wa karama maalumu ya hekima ambayo alijaliwa na Roho Mtakatifu kwa faida ya Kanisa ikabainishwa na athari njema ya mafundisho yake katika Taifa la Mungu” (Papa Benedikto XVI, Barua ya Kitume ya tarehe 7 Oktoba 2012).

Papa

Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa (samaki)

Papa (neno la mkopo kutoka Kilatini lakini lenye asili ya Kigiriki, πάππας, pappas, jina ambalo mtoto anamuitia baba yake)ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.

Papa Fransisko

Papa Fransisko, S.I. (kwa Kilatini Franciscus, jina la awali Jorge Mario Bergoglio) ni askofu wa Roma, na hivyo pia Papa wa Kanisa Katoliki duniani kote, tangu tarehe 13 Machi 2013.

Amemfuata Papa Benedikto XVI akiwa wa 266 katika orodha ya mapapa.

Ualimu wa kanisa

Ualimu wa Kanisa katika imani ya Wakatoliki linamaanisha mamlaka ya Kanisa, kupitia hasa maaskofu wake, katika kufundisha imani na maadili ili kudumisha, kustawisha na kueneza karne hadi karne hazina ya imani iliyofunuliwa na Mungu hasa katika Yesu Kristo na kukabidhiwa kwa Mitume wake.

Utetezi wa Kanisa Katoliki

Utetezi wa Kanisa Katoliki ni sehemu ya teolojia ya Ukristo inayolenga kutoa hoja za kutetea imani na maisha ya Kanisa Katoliki dhidi ya zile za watu wa madhehebu au dini nyingine au za wale wasio na dini yoyote wanaolenga kuthibitisha kasoro zake ili kukomesha imani katika asili yake ya Kimungu.

Kwa kutaja utetezi wa namna hiyo katika lugha nyingi limetoholewa neno la Kigiriki ἀπολογία, apologia, "utetezi wa sauti, hotuba ya utetezi".

Ni tofauti kidogo na hoja zinaotumiwa na Wakatoliki dhidi ya dini, madhehebu na itikadi nyingine ili kuonyesha vilivyo na kasoro.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.