Mashariki ya Kati

Mashariki ya Kati (kwa Kiingereza Middle East) ni namna ya kutaja sehemu kubwa ya Asia ya Magharibi pamoja na Afrika ya kaskazini-mashariki, hasa Misri.

Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa humo:

Nchi hizo zinatajwa pamoja kwa sababu zina historia ya pamoja na utamaduni wa karibu.

MapRegionMiddleEast+Turkey
Mashariki ya Kati pamoja na Uturuki.

Matatizo ya jina hili

Jina "Mashariki ya Kati" limesambazwa kutokana na kawaida ya Kiingereza na kutafsiriwa katika lugha mbalimbali. Lina matatizo kadhaa yanayotakiwa kujulikana hata tukiendelea kulitumia:

 • kuna namna mbalimbali za kutaja nchi za ziada zinazohesabiwa humo au la (kwa mfano: wengine huhesabu pia nchi za Asia ya Kati kama vile Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan n.k.)
 • jina ni tamko la Kiulaya: nchi hizi ziko upande wa mashariki kwa mtu aliyeko Ulaya. Kutoka Uswahilini ingekuwa zaidi "Kaskazini ya Kati"
 • matumizi ya jina yamebadilika: zamani Kiingereza pamoja na lugha nyingine za Ulaya kilitofautisha kati ya
  • "Mashariki ya Karibu" (Near East),
  • "Mashariki ya Kati" (Middle East) na
  • "Mashariki ya Mbali" (Far East)

kikimaanisha

Lugha mbalimbali za Ulaya Bara kama Kijerumani zinaendelea kutumia majina hayo matatu vile. Pia wataalamu wa historia kwa Kiingereza hupendelea kutofautisha kati ya "Mashariki ya Karibu" na "Mashariki ya Kati".

Historia ya Mashariki ya Kati

Kitovu cha ustaarabu

Jerusalem kotel mosque
Ukuta wa maombolezo na Kuba ya Mwamba mjini Yerusalemu ni mahali patakatifu wa Wayahudi na Waislamu kandokando

Nchi zinazoitwa kwa Kiingereza "Mashariki ya Kati" ziko kwenye eneo la dunia ambako watu na tamaduni za Asia, Afrika na Ulaya hukutana.

Ni pia mahali ambako Bahari Hindi na Mediteranea zinakaribiana ambazo zote mbili zilikuwa njia za usafiri wa mbali tangu kale.

Pamoja na mahali pa kubadilishana bidhaa na teknolojia, eneo hili lilikutanisha pia mawazo, falsafa na dini. Hadi leo Mashariki ya Kati ni kitovu cha kiroho cha dini za Uzoroasta, Uyahudi, Ukristo na Uislamu.

Idadi kubwa ya aina za kwanza za ustaarabu duniani zilianza hapa kama vile Mesopotamia (Sumeri, Akkad, Assyria, Babeli) na Misri ya Kale, zikifuatwa na zile za Uajemi, Ugiriki wa Kale, Israeli ya Kale, Finisia na nyingine.

Muhtasari wa historia ya utawala

Eneo lote liliunganishwa mara ya kwanza chini ya Milki ya Ashuru, halafu na milki ya pili ya Babeli iliyofuatwa na milki ya Uajemi na utawala wa Aleksander Mkuu.

Baadaye eneo liligawiwa hasa kati ya milki mbalimbali za Uajemi na Dola la Roma hadi uenezi wa Waarabu Waislamu na kuundwa kwa milki ya khalifa.

Tangu mwaka 1512 Mashariki ya Kati karibu yote ilikuwa chini ya utawala wa Milki ya Osmani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia.

Ugawaji wa Milki ya Osmani

Mashariki ya Kati ya kisasa ilianza kutokea baada ya vita hiyo. Ufaransa na Ufalme wa Maungano zilishinda Milki ya Osmani zikagawana maeneo yake ya nje ya Uturuki. Ugawaji huu ulithibitishwa na Shirikisho la Mataifa, hivyo maeneo ya Syria, Lebanoni, Palestina (baadaye Israeli na Yordani) na Iraki yalikabidhiwa kwa nchi hizo mbili za Ulaya kama maeneo ya kudhaminiwa kwa masharti ya kuyaandaa maeneo haya kuwa nchi huru baadaye.

Maeneo kadhaa kwenye rasi ya Uarabuni yalibaki huru baada ya kuondoka kwa jeshi la Osmani hadi mwaka 1918:

 • Chifu Ibn Saud wa Riyad alishinda vita baina ya makabila ya Uarabuni ya kati akaweza kuvamia na kutawala maeneo ya Najd na Hejaz na mwaka 1932 alitangaza Ufalme wa Uarabuni wa Saudia
 • Katika Yemen Imamu Yahya Muhamad wa kundi la Zaidiya alivamia velayat ya Yemen ya Kiosmani na kutangaza Ufalme wa Yemen

Uhuru ulifika kwa ngazi mbalimbali na tofauti kwa kila nchi.

Maeneo ya kudhaminiwa kwa Uingereza:

 • Iraki ilikubaliwa kuwa mwanachama wa Shirikisho la Mataifa mwaka 1932 ingawa hali halisi ilikuwa nchi lindwa chini ya athira ya Uingereza hadi mwaka 1958.
 • Palestina ng'ambo ya mto Yordani (Transjordan) ilipata serikali ya kujitawala kama nchi lindwa chini ya Uingereza tangu mwaka 1922, halafu uhuru kamili mwaka 1946 kwa jina la Transjordani, halafu Yordani tu
 • Israeli ilikubaliwa na Umoja wa Mataifa kuwa nchi huru mwaka 1948.
 • Azimio lilelile lililenga kuanzisha pia dola la Kiarabu la Palestina lakini, kutokana na vita iliyoanza mara moja, hii haikutokea, maeneo yaliyotarajiwa kuwa Palestina yalivamiwa na Israeli, Yordani na Misri. Tangu mwaka 1993 kuna Mamlaka ya Kitaifa ya Palestina yenye viwango tofauti vya utawala juu ya sehemu za maeneo ya Palestina asilia zilizo chini ya usimamizi wa kijeshi wa Israel.

Maeneo ya kudhaminiwa kwa Ufaransa:

Maeneo mengine baada ya Vita Kuu ya Kwanza

Katika nchi kadhaa zilizokuwa nje ya Milki ya Osmani Uingereza ilikuwa na athira kubwa na hali halisi nchi hizo zilikuwa nchi lindwa kabla na baada ya Vita Kuu ya Kwanza

 • Misri ilikuwa rasmi sehemu ya Milki ya Osmani lakini hali halisi ilisimamiwa na Uingereza hasa kwa shabaha ya kusimamia mfereji wa Suez. Mwaka 1914 ilitangazwa kuwa nchi lindwa chini ya Uingereza; tangazo la uhuru la mwaka 1922 bado liliacha athira kubwa kwa Uingereza. Tangu mwaka 1952 Misri imepata uhuru kamili, na tangu hapo ilitawala pia mfereji wa Suez.
 • Omani ilikuwa eneo lililogawiwa kati ya Sultani wa Maskat na Imamu wa Ibadiya mnamo 1890. Maskat ilikubali kuwa eneo lindwa chini ya Uingereza ikapata msaada wa jeshi la Uingereza dhidi ya Saudia na baadaye kuvamia na kutawala pia maeneo ya imamu mwaka 1957. Mkataba wa mwaka 1951 ulitangaza uhuru wa Omani, lakini hali halisi athira ya Uingereza ulikuwa na nguvu hadi miaka ya 1990.
 • Kuwait ilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza tangu mwaka 1899 na Waingereza walitetea hali yake ya pekee dhidi ya Waosmani na baadaye dhidi ya Saudia. Ilipata uhuru mwaka 1961.
 • Maeneo ya Falme za Kiarabu pamoja na Qatar na Bahrain yalikuwa nyumbani kwa makabila madogo na chifu zao. Tangu mwaka 1820 walikuwa na mikataba na Uingereza walipoahidi kuachana na uharamia na kupokea ulinzi wa Uingereza. Ulinzi huu ulizuia uvamizi wa Saudia katika karne ya 20. Tangu mwaka 1971 madola hayo madogo yalipata uhuru. Saba kati yake yaliungana kuwa Falme za Kiarabu.

Ugunduzi wa mafuta

Dammam No. 7 on March 4, 1938
Mafuta ya petroli jinsi ilivyotoka nje kwa nguvu mara ya kwanza 4 Machi 1938 nchini Saudia
BrennendeOelquellenKuwait1991
Chemchemi za mafuta ziliwaka katika vita ya Iraq dhidi Kuwait 1991
Tankers at the Iraqi Al Basra Oil Terminal in the Northern Arabian Gulf
Meli za kubeba mafuta ni kama mshipa wa damu ya uchuimi wa dunia (hapa bandari ya mafuta ya Basra, Iraq)

Hadi Vita Kuu ya Kwanza mataifa yote katika eneo la Ghuba ya Uajemi yalikuwa dhaifu, bila uchumi imara na bila uwezo wa kijeshi. Hasa upande wa Uarabuni watawala wadogo walisimamia miji michache kwenye pwani tu na sehemu kubwa ya watu waliishi katika utaratibu wa kikabila bila kujali serikali.

Kugunduliwa mafuta kulibadilisha hali hii katika miaka baada ya vita. Mafuta ya petroli yaligunduliwa mwaka 1908 katika Iran kusini na serikali ya Uingereza ilinunua mara moja hisa nyingi za kampuni ya Anglo-Persian Oil iliyokuwa na mkataba wa kuzalisha mafuta huko.

Vita kuu ya kwanza ya dunia ilionyesha kwa mara ya kwanza umuhimu wa kijeshi ya mafuta.[1].

Mafuta yalibadilisha umuhimu wa Mashariki ya Kati. Mafuta ya petroli yaliendelea kuwa chanzo muhimu zaidi cha nishati katika uchumi wa dunia ya kisasa. Kwa hiyo mataifa na makumpuni makubwa yalianza kuangalia hali ya kisasa ya nchi zenye mafuta. Yalijaribu kuhakikisha ya kwamba wawepo watawala na serikali ambao wawape nafasi nzuri na nafuu ya kupata mafuta kutoka ardhi yao. Vilevile yalijaribu kuzuia nchi nyingine kuingia huko.

Mashindano hayo yaliweka msingi kwa siasa ya nchi hizo za Kiarabu, ambazo zote zilikuwa na watu wachache lakini mafuta mengi, kuwa chini ya athira za nje ilhali mataifa makubwa yalihakikisha kuwepo kwao na mapato makubwa kwa watawala, hivyo pia kuwalinda dhidi ya mabadiliko ya kisiasa na kimapinduzi yaliyoonekana katika nchi nyingine za Mashariki ya Kati zisizo na utajiri wa mafuta.

Nchi ya kwanza iliyopata nafasi ilikuwa Uingereza ikifuatwa na Marekani. Mwaka 1932 kampuni ya Standard Oil ya Kalifornia ikakuta mafuta huko Bahrain ikaendelea kujipatia leseni ya kuyatafuta pia Saudia wakafaulu mwaka 1938.

Utajiri haukuanza kote mara moja; Uajemi (Iran) ilikuwa nchi kubwa ikapata asilimia ndogo ya mapato ya mafuta kufuatana na mikataba ya zamani; upande wa Uarabuni ilichukua muda hadi chemchemi kubwa za mafuta zilipatikana na kuzalisha kwa wingi. Bahrain ilitangulia, Kuwait ilifuata tangu mwaka 1950 hivi, lakini Omani na Falme za Kiarabu zilianza kuzalisha kwa wingi katika miaka ya 1970 pekee.

Mwanzoni uchumi wa mafuta ulikuwa kabisa mikononi mwa makampuni ya nje kwa sababu wenyeji hawakuwa na elimu ya teknolojia na watawala walikosa mapato mengine, hivyo walikubali masharti yoyote. Tangu miaka ya 1960 polepole asilimia ya mapato iliyobaki mikononi mwa serikali iliongezeka, pia zilianza kununua hisa za makampuni yaliyozalisha mafuta katika ardhi yao.

Hadi miaka ya 1990 serikali za nchi za ghuba zilikuwa na hisa nyingi katika makampuni haya yaliyokuwa sasa mali ya taifa au ya familia tajiri za wenyeji.

Mapato kutokana na mafuta yalianza kubadilisha maisha na jamii za nchi zote zinazouza mafuta kwenye soko la dunia. Hasa watawala wa nchi ndogo walikuwa matajiri kupita kiasi, wakaweza kuendelea na mfumo wa utawala wa mfalme asiyebanwa na katiba kwa muda mrefu kwa sababu waliweza kuwagawia wananchi wao sehemu za utajiri wa mafuta.

Wakati wa vita baridi mashindano kati ya magharibi na Umoja wa Kisovyeti yaliendeshwa vikali katika Mashariki ya Kati. Serikali mbalimbali zilichezacheza kati ya pande hizo mbili.

Wakazi

Leo hii wakazi wa Mashariki ya kati mara nyingi wanatazamwa kwa jumla kuwa "Waarabu". Hii ni kweli kwa kiasi tu kwa sababu mbili

 • Nchi kadhaa kama Uturuki, Iran na Israel zina wakazi Waarabu wachache tu
 • Kwa jumla eneo hili ni mchanganyiko mkubwa wa makabila mengi na vikundi vingi vyenye lugha, tamaduni na dini tofautitofauti, wakiwemo wahamiaji wengi sana, pengine kuliko wananchi wenyewe.

Ni kweli kwamba idadi kubwa ya wakazi leo hii wanatumia lugha ya Kiarabu. Lugha muhimu katika eneo hili ni:

pamoja na lugha nyingine mbalimbali kama Kiebrania, Kiaramu, Kiarmenia na lugha asili za wahamiaji.

Picha za Miji ya MAshariki ya Kati

Abu Dhabi Skyline from Marina

Abu Dhabi - Falme Arabu (UAE)

Kızılay Square in Ankara, Turkey

Ankara - Uturuki

Haifa street, as seen from the medical city hospital across the tigres

Baghdad - Iraq

Zaitunay Bay, Downtown Beirut, Lebanon

Beirut - Lebanon

Cairo by night

Kairo - Misri

Barada river in Damascus (April 2009)

Dameski - Syria

West Bay Skyline, Doha, State of Qatar

Doha - Qatar

Dubai skyline 2010

Dubai - UAE

Turkey-3019 - Hagia Sophia (2216460729)

Istanbul - Uturuki

Austrian Hospice Jerusalem April 2007

Yerusalemu (Israeli-Palestina)

Kuwait City cropped

Kuwait City - Kuwait

Manama Cityline

Manama - Bahrain

The Holy Mosque in Mecca

Mekka - Saudi Arabia

Bank Of Palestine - Ramallah

Ramallah - Palestina

San'a03 flickr

Sana'a - Yemen

Panorama of Tabriz

Tabriz - Iran

North Tehran Towers

Tehran - Iran

Tel Aviv P5280003

Tel Aviv - Israel

Tanbihi

 1. Uingereza ulitafuta chanzo cha mafuta kisichotawaliwa na mataifa makubwa mengine, maana ulitaka kubadilisha manowari zake kutoka matumizi ya makaa kwenda mafuta, kwa sababu hii iliwapa nafasi ya kusafiri mbali zaidi. Mafuta ya Iran yalikuwa chanzo cha badiliko hilo

Viungo vya nje

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mashariki ya Kati kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Asia ya Magharibi

Asia ya Magharibi (inalingana kwa kiasi kikubwa na jina la Mashariki ya Kati) ni sehemu ya magharibi-kusini ya bara la Asia. Inatajwa kati ya kanda za dunia ya UM.

Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki

Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki (Kiing. Great Rift Valley) ni maumbile ya kijiolojia inayoanza katika Mashariki ya Kati na kuendelea hadi Msumbiji. Ni kati ya maajabu makubwa ya dunia hii. Ufa hii imetokea tangu miaka milioni 35 kutokana na mwendo wa mabamba ya gandunia ya Afrika na Uarabuni. Mwendo huu umesababisha pia farakano ndani ya bamba la Afrika na wataalamu huamini kuwa Afrika ya Mashariki iko katika mwendo wa kuachana na Afrika kwa jumla.

Falme za Kiarabu

Falme za Kiarabu (kwa Kiarabu: الإمارات العربيّة المتّحدة; kwa Kiingereza United Arab Emirates) ni shirikisho la emirati au falme ndogo 7 katika kaskazini-mashariki ya Rasi ya Uarabuni kwenye mwambao wa ghuba ya Uajemi.

Shirikisho limepakana na Saudia na Omani kwenye nchi kavu; baharini kuna mipaka pia na Katar na Iran.

Mji mkuu ni Abu Dhabi na mji mkubwa ni Dubai.

Israel

Kwa maana mbalimbali za jina Israeli katika Biblia tazama Israeli (maana)

Israel (kwa Kiebrania: מדינת ישראל - Medinat Yisra'el; kwa Kiarabu: دَوْلَةْ إِسْرَائِيل - dawlat Isrā'īl) ni nchi ya Mashariki ya Kati kwenye mwambao wa mashariki wa Mediteranea.

Imepakana na Lebanon, Syria, Yordani, Misri na maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya serikali ya Palestina.

Kigiriki

Kigiriki (pia: Kiyunani) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya inayotumiwa hasa nchini Ugiriki. Maandishi yake yamejulikana tangu miaka 3500 iliyopita. Hakuna lugha nyingine duniani inayozungumzwa hadi leo yenye historia ndefu kuliko hii, isipokuwa Kichina.

Kigiriki ni muhimu sana kwa utamaduni wa kisasa kwa sababu ya kutoa michango mingi kwa lugha ya sayansi, teknolojia na utamaduni. Fikra nyingi muhimu zilionekana mara ya kwanza kwa Kigiriki na falsafa iliyojadiliwa na kuandikwa kwa lugha hii. Istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kigiriki.

Alfabeti ya Kigiriki ilikuwa msingi wa alfabeti nyingine mbili, za Kilatini na Kikirili, pia kwa miandiko ya abijadi kama herufi za Kiarabu au za Kiebrania. Kiswahili huandikwa leo kwa herufi za Kilatini.

Kati ya maandiko muhimu ya Kigiriki ni yale ya wanafalsafa kama Plato na Aristoteles na pia baadhi ya maandiko ya Biblia ya Kikristo (Agano Jipya pamoja na Deuterokanoni), mbali ya tafsiri ya kwanza ya Biblia ya Kiebrania maarufu kwa jina la Septuaginta (karne ya 2 KK).

Kati ya karne ya 3 KK hadi karne ya 6 BK Kigiriki kilikuwa lugha ya kimataifa katika eneo kubwa la kandokando ya bahari ya Mediteranea pamoja na Mashariki ya Kati.

Lugha imeendelea kubadilika kisarufi, kimatamshi na pia kimsamiati. Hivyo Kigiriki cha kale kimekwisha, hakizungumzwi tena na watu, lakini bado kinafundishwa katika shule na vyuo vingi, hasa Ulaya.

Leo hii katika nchi ya Ugiriki kuna lugha ya Kigiriki Kipya kinachoendela kuandikwa kwa herufi zilezile.

Kilimo

Kilimo ni uzalishaji wa mazao kwenye mashamba.

Kilimo kina maana pana inayojumuisha mifumo ya uzalishaji mimea, ufugaji wa wanyama, na uvuvi wa samaki. Mara nyingi kilimo cha mimea kinaenda sambamba na ufugaji wa wanyama.

Watu hupanda mimea na kuitunza hadi mavuno hasa kwa uzalishaji wa chakula cha binadamu na lishe ya wanyama, lakini pia kwa shabaha ya kupata malighafi mbalimbali zinazotumiwa kwa kutengeneza nguo za watu.

Siku hizi kilimo kinalenga pia nishati ya mimea.

Mtu anayejihusisha na kilimo huitwa mkulima.

Lebanoni

Lebanoni (kwa Kiarabu: لبنان ) ni nchi ndogo ya Mashariki ya Kati katika Asia ya Magharibi kando ya Bahari ya Mediteranea.

Imepakana na Syria na Israel.

Mashariki

Mashariki ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande jua linapochomoza asubuhi.

Jina "mashariki" limetokana na neno la Kiarabu مشرق mashriq linalomaanisha "mahali jua linapokucha".

Mashariki kawaida huwa upande wa kulia kwenye ramani. Tanzania ipo mashariki mwa nchi za Kongo, Rwanda na Burundi. Bahari Hindi huwa upande mwa mashariki ya Tanzania na Kenya. Hakuna mwisho wa kuelekea mashariki hadi umezunguka dunia yote.

Kundi la nchi za Asia magharibi mara nyingi huitwa "Mashariki ya Kati" ambayo ni uzoefu kutoka mtazamo wa Ulaya.

Majengo ya makanisa mara nyingi hujengwa kutazama upande wa mashariki kwa kukumbuka kufufuka kwa Yesu kulikotokea wakati wa kucha; kwa hiyo altari ya kanisa huwekwa upande wa mashariki wa kanisa na waumini huangalia upande huu.

Misri

Misri (kwa Kiarabu: مصر, Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki ikiwa na eneo la Rasi ya Sinai kwenye bara la Asia pia.

Ni nchi yenye wakazi milioni 90 na mji mkuu Kairo ni kati ya miji mikubwa zaidi duniani.

Ni kati ya nchi za dunia zenye historia ndefu inayojulikana.

Omani

Usultani wa Omani (kwa Kiarabu:سلطنة عُمان Saltanat ˤUmān) ni nchi ya Bara Arabu katika Asia ya Magharibi.

Imepakana na Maungano ya Falme za Kiarabu, Saudia na Yemen, halafu Bahari Hindi na Ghuba ya Omani.

Utawala wa nchi hufuata muundo wa kifalme usiobanwa na masharti ya katiba.

Mji mkuu ni Maskat (Omani).

Palestina

Palestina (kwa Kiarabu: فلسطين‎ filasṭīn, falasṭīn; kutoka Kilatini: Palaestina; kwa Kiebrania: פלשתינה Palestina) ni jina la eneo lililoko upande wa Mashariki wa Bahari ya Mediteranea kati ya mkingo wa bahari hiyo na mto Yordani.

Qatar

Qatar (kwa Kiarabu: قطر ) ni emirati ndogo wa Uarabuni kwenye rasi ya Qatar ambayo ni sehemu ya rasi kubwa ya Uarabuni.

Imepakana na Saudia upande wa kusini. Mipaka mingine ni ya Ghuba ya Uajemi. Kisiwa cha Bahrain kiko karibu.

Mji mkuu wa Qatar ni Doha.

Saudia

Ufalme wa Uarabuni wa Saudia (المملكة العربية السعودية, al-mamlaka al-'arabiyya as-sa'audiyya ) ni nchi kubwa kati ya nchi za Bara Arabu.

Imepakana na Yordani, Iraq, Kuwait, Qatar, Bahrain, Falme za Kiarabu, Oman na Yemen.

Kuna pwani ya Ghuba la Uajemi upande wa kaskazini-mashariki na Bahari ya Shamu upande wa magharibi.

Syria

Syria au Siria (kwa Kiarabu: سوريا au سورية ) ni nchi ya Mashariki ya Kati au Asia ya Magharibi.

Imepakana na Lebanon, Israel, Yordani, Iraq na Uturuki.

Kuna pwani kwenye bahari ya Mediteranea.

Nchi inatajwa pia kwa jina la "Shamu" katika maandiko ya Kiswahili, ingawa neno hili lamaanisha zaidi eneo la kihistoria ambalo lilikuwa kubwa kuliko Syria ya leo.

Uajemi

Iran - ايران, pia Uajemi (kutokana na Kiarabu العجم- al-'ajam) ni nchi ya Asia ya Magharibi.

Jina rasmi ya nchi ni Jamhuri ya Kiislamu ya Iran au Uajemi. Uajemi imejulikana tangu kale kama nchi iliyochangia mengi katika historia ya binadamu.

Imepakana na Afghanistan, Armenia, Azerbaijan, Iraq, Pakistan, Uturuki na Turkmenistan.

Upande wa kusini kuna mwambao wa Ghuba ya Uajemi (Bahari Hindi) na upande wa kaskazini ni mwambao wa Bahari ya Kaspi.

Tehran ni mji mkuu, pia mji mkubwa nchini.

Uturuki

Uturuki (Jamhuri ya Uturuki; kwa Kituruki: Türkiye Cumhuriyeti) ni nchi ya kimabara kati ya Asia na Ulaya.

Sehemu kubwa iko Asia ya magharibi lakini sehemu ndogo ya eneo lake upande wa magharibi wa Bosporus iko Ulaya.

Waarabu

Kigezo:Mashaka

Leo duniani kuna watu wengi sana wanaojinasibisha na Waarabu wakiwa wanaishi Bara Arabu au Mashariki ya Kati au kwengineko ulimwenguni. Watu hawa ambao wanatafautiana baina yao kirangi na kimaumbile na kisura wote wanadai kuwa ni Waarabu au asli zao ni za Kiarabu. Walakini, ni nani hasa hawa Waarabu na nini asli yao?

Waorthodoksi

Waorthodoksi ni Wakristo wanaofuata mapokeo ya Mitume wa Yesu jinsi yalivyostawi kihistoria katika Ukristo wa Mashariki upande wa mashariki wa Dola la Roma iliyoitwa pia Bizanti na nje ya mipaka yake. Leo hii ni nchi za Ulaya ya Mashariki pamoja na nchi za Mashariki ya Kati ulipoenea baadaye dini ya Uislamu.

Yemen

Yemen (Kiarabu: الجمهورية اليمنية ) ni nchi kusini mwa Bara Arabu.

Imepakana na Omani, Saudia na Bahari Hindi.

Nchi za karibu ng'ambo ya mlango wa bahari wa Bab el Mandeb ni Eritrea, Jibuti na Somalia.

Eneo lake ni pamoja na kisiwa cha Sokotra na visiwa 200 vingine.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.