Manispaa

Manispaa (ing. municipality) ni mji mwenye kiwango fulani ya kujitawala katika shughuli zake.

Madaraka haya ni pamoja na haki ya kutawaliwa na serikali ya kimahali iliyochaguliwa na watu wa manisipaa (badala ya kusimamiwa na mwakilishi wa serikali kuu), kuamulia na kukusanya kodi fulani katika eneo la manisipaa na kupanga makisio yake yenyewe.

Manispaa za Tanzania

Nchini Tanzania manispaa ni mji mwenye wakazi zaidi ya 100,000 hadi 500,000.

Katika muundo wa utawala manispaa za Tanzania zinahesabiwa kama wilaya. Serikali ya manisipaa huitwa Halmashauri ya manispaa (Municipal Council).

Manisipaa za Tanzania ni Bukoba, Dodoma, Iringa, Kigoma, Lindi, Morogoro, Moshi, Mtwara, Musoma, Shinyanga, Singida, Songea, Sumbawanga, Tabora.

Halafu kuna masisipaa tano ambazo ni sehemu ya majiji mawili.

Aweil (jimbo)

Aweil State ni mojawapo kati ya majimbo 32 yanayounda Sudan Kusini.

Imegawanyika katika kaunti 8: Buonchai County, Ajak County, Kongdek County, Ajuet County, Chimel County, Mayom Wel County, Barmayen County na Aroyo County, mbali na manispaa ya Aweil.

Aweil East (jimbo)

Aweil State (pia: Abiem State) ni mojawapo kati ya majimbo 32 yanayounda Sudan Kusini.

Imegawanyika katika kaunti 8: Wunlung County, Malualbaai County, Warguet County, Yargot County, Madhol County, Mangok County, Baac County na Mangar-Tong County., mbali na manispaa za Malualkon na Majok Yinh Thiou.

Garissa

Garissa ni mji nchini Kenya ulio makao makuu ya kaunti ya Garissa.

Wakazi walikuwa 119,696 wakati wa sensa ya mwaka 2009.

Mto Tana hupitia eneo la manispaa.

Wakazi walio wengi ni Wasomali kiutamaduni pamoja na raia wa Somalia waliohamia hapa kutokana na hali ya vita nchini kwao. Kundi kubwa la wenyeji ni wa ukoo wa Waogaden.

Kaunti ya Busia

Kaunti ya Busia ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Makao makuu yako Busia.

Shughuli kuu ya kiuchumi ni biashara na nchi jirani ya Uganda, pamoja na mji wa Busia kituo cha mpakani.

Mbali na mji, uchumi wa wilaya hutegemea sana uvuvi na kilimo, mazao msingi yakiwa pamoja na mihogo, mtama, viazi vitamu, maharagwe, na mahindi.

Wilaya ya Busia ni makao ya kabila la Waluhya nchini Kenya ambao wanapatikana hasa katika sehemu za Magharibi mwa Kenya. Wilaya hii ilikuwa na wakazi 370,608 (1999, sensa).

Wilaya ya Busia ina maeneo bunge manne:

Eneo bunge la Nambale

Eneo bunge la Butula

Eneo bunge la Funyula

Eneo bunge la Budalangi

Kigoma-Ujiji

Kigoma Ujiji ni manispaa katika Mkoa wa Kigoma nchini Tanzania na makao makuu ya mkoa huo yenye msimbo wa posta 47100. Inaunganisha miji ya kihistoria ya Ujiji na Kigoma. Manispaa hii ilikuwa na wakazi wapatao 215,458 wakati wa sensa ya mwaka 2012.Kigoma na Ujiji iko kando ya Ziwa Tanganyika, magharibi mwa Tanzania.

Kyebitembe

Kyebitembe ni kata ya Wilaya ya Muleba katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35529 .

Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 25,460 waishio humo.Kata hii imepakana na ziwa Burigi. Pia hifadhi ya Mbuga ya Wanyama ya Burigi inapatikana ndani ya kata hii.

Ni mwendo wa saa 3.5 kwa usafiri wa Hiace kutoka kata ya Kyebitembe mpaka stendi ya mkoa iliyo ndani ya Manispaa ya mji wa Bukoba.

Pia ndani ya kata hii kuna sekondari moja ambayo ni Shule ya Sekondari Kanyeranyere na shule 8 za msingi ambazo ni Nyamilanda, Kanyeranyere, Kabungo, Kyebitembe, Kyabishagao, Nyanjubi, Kagasha na Kasindaga.

Meru, Kenya

Meru ni mji wa Kenya mashariki ambao ni makao makuu ya Kaunti ya Meru na mji wa nane kwa ukubwa nchini Kenya.

Meru imeunda baraza la manispaa lenye wakazi 240,900.

Meru iko pande za Mto Kathita, katika mteremko wa kaskazini mashariki wa Mlima Kenya.

Mji huu uko umbali wa maili tano kaskazini mwa ikweta, urefu wa futi 5000, katika eneo la mchanganyiko wa misitu mahali wazi, miji midogo, vijiji, mashamba vijijini na wengi wa wakazi ni wa Ameru.

Unaweza kufikia mji huu ukitumia barabara ya lami, kwa vyovyote vile kama kutoka kusini kuzunguka upande wa mashariki wa Mlima Kenya, kupitia Embu, au kutoka katika eneo la kaskazini magharibi kuzunguka magharibi na kaskazini wa Mlima Kenya, kupitia Nanyuki na Timau.

Kaunti ya Meru ni mahali pa kuzuru Ili kutembelea eneo za kuhifahia wanyama ambazo ni Samburu na Buffalo Springs Lewa Downs, ambazo ziko mbali kiasi kaskazini mwa Meru, pamoja na Samburu na Buffalo Springs kupitia Isiolo, na Hifadhi ya Taifa ya Meru, katika kaskazini mwa Meru, kupitia Maua katika vilima vya Nyambeni.

Meru ni mji wa biashara, kilimo na elimu kaskazini ymw Kenya. Mji huu una mabenki na hoteli, masoko na vituo vya usafirishaji. Kahawa, chai, mbao, ng'ombe, maziwa, maharagwe ya "Kifaransa" na bidhaa nyingine nyingi hutoka katika Kaunti ya Meru. Pia kuna shule za msingi na sekondari, zikiwa pamoja na Shule kuu ya sekondari ya Meru na shule ya wasichana ya kaaga, ambazo ni baadhi ya chuo zinazoongoza katika taasisi za elimu ya sekondari Kenya. Chuo kikuu cha Emory ina ubia na Shule kuu ya sekondari ya Meru katika kusidiana na kompyuta, vitabu, na vifaa vya sayansi katika kumbukumbu ya George Brumley. Pia kuna shule za Ufundi. Taasisi ya ufundi Meru na Chuo cha Teknolojia ya Meru ambazo ndizo kuu. Pia, kuna vyuo vya ualimu na chuo kikuu cha Kenya Methodist University kinachojulikana kama KEMU.

Ni eneo muhimu la uzalizaji wa kahawa. inakuzwa na wengi wa wakulima wadogo, nakukuzwa chini ya kivuli. Mazao ya kahawa katika eneo la Meru huja mara mbili kwa mwaka, sawa n misimu miwili ya mvua, lakini mazao kuu katika Meru inakuja katika wakati tofauti kwa kiasi fulani kuliko mahali pengine nchini Kenya, kutokana na tofauti ya hali ya hewa kwenye kaskazini wa miteremko ya mlima Kenya na vilima vya Nyambenene. pia hukuzwa katika miinuko iliyo juu katika mchanga wa volkeno katika wilaya hii. Kahawa hii inatayarishwa na vyama vya ushirika vya wakulima wa kahawa ambavyo ni wenyewe viwanda vilivyo karibu na wakulima.

Meru ndio eneo kuu la ukuzaji wa Miraa (Khat) nchini Kenya. Wakulima wengi wanapendelea kuzalisha miraa kwa kuwa ina faida kubwa kifedha.

Makumbusho ya Taifa ya Meru yako katika mji.

Mikoa ya Kenya

Mikoa ya Kenya (kwa Kiingereza "Provinces of Kenya") ilikuwa mgawanyo wa kiutawala kwenye ngazi ya juu nchini Kenya. Taifa liligawanywa katika mikoa minane (tazama ramani). Mikoa hii iligawanywa katika wilaya 46 ambazo ziligawanywa zaidi katika tarafa 262. Tarafa ziligawanywa katika lokesheni 2427, na kisha lokesheni ndogo 6612 Kila mkoa ulisimamiwa na Mkuu wa Mkoa (PC).

Serikali za wilaya za Kenya zaidi hazikufuata mipaka yna tarafa. Zimejumuishwa kama Mabaraza ya Majiji, Manispaa, Miji au ya Kaunti.

Aina ya tatu ya mgawanyiko ni sehemu za uwakilishi bungeni au majimbo. Sehemu hizi ziligawanywa zaidi katika kata.

Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 ilifuta ngazi ya mikoa. Tangu mwaka 2013 wilaya za Kenya ni ngazi ya kwanza ya mgawanyo wa kiutawala. Kuna wilaya 47 nchini Kenya ambazo ni maeneo ya kujichagulia bunge na serikali ya kieneo.

Mkoa wa Kocaeli

Kocaeli ni mkoa wa Uturuki. Mji wake mkuu ni İzmit, ambao pia huitwa kama jina la mkoa wenyewe la Kocaeli. Mji mkubwa mkoanio hapa kwa sasa ni Gebze. Kodi ya trafiki katika jimbo hili ni 41. Mkoa upo mwishoni kabisa mwa mashariki mwa Bahari ya Marmara, hasa katika eneo la Pwani ya İzmit. Kwa kufuatia kuwa na hali ya hewa nzuri iliyopo katika Pwani ya İzmit, mji una bandari asilia kubwa sana.

Sogn og Fjordane

Sogn og Fjordane ni moja kati ya majimbo ya Norwei. Jimbo hili limepakana na Møre og Romsdal, Oppland, Buskerud, na Hordaland. Makao makuu ya jimbo hili yapo mjini Hermansverk katika manispaa ya Leikanger - wakati mji mkubwa kabisa ni Førde.

Sør-Trøndelag

Sør-Trøndelag ("Trøndelag kusini") ni jimbo nchini Norwei. Jimbo linachangamana na jimbo la Nord-Trøndelag kaskazini, Wilaya ya Jämtland katika Uswidi mashariki na Hedmark, Oppland na Møre og Romsdal kusini. Sør-Trøndelag lina manispaa 25, na eneo ya 18,839 km².

Tonj (jimbo)

Tonj State ni mojawapo kati ya majimbo 32 yanayounda Sudan Kusini.

Imegawanyika katika kaunti 22 (nyingi kuliko jimbo lolote), mbali na manispaa ya Tonj.

Kaunti hizo ni:

Alabek County

Konggor County

Akop County

Awul County

Rualbet County

Lou Paher County

Warrap County

Manloor County

Kirik County

Pagol County

Luanyjang South County

Luanyjang North County

Luanyjang Centre County

Luanyjang East County

Ngapagok County

Jak County

Manyang-Ngok County

Wanhalel County

Thiet County

Vihiga

Vihiga ni mji wa Kenya magharibi ulioko upande wa mashariki wa Msitu Kakamega. Mji huu uko kando ya barabara ya Kisumu na Kakamega na kilomita tano tu kaskazini kwa ikweta.

Vihiga imetoa jina lake kwa kaunti ya Vihiga ambayo makao makuu yake yako Mbale iliyoko katika manispaa ya Vihiga. Manispaa hiyo ina wakazi 118,696 (sensa ya mwaka 2009).

Manispaa ya Vihiga ina wadi sita, mbili kati ya hizo (Central Maragoli na Wamuluma) ziko katika eneo bunge la Vihiga huku nne zilizobaki (Chavakali, Izawa, Lyaduywa na Maragoli Kaskazini) ni sehemu ya eneo bunge la Sabatia. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2002, viti vyote sita vya baraza vililishindwa na National Rainbow Coalition.

Wamaragoli ndio kabila kuu katika eneo hili na mji huu hujulikana pia wakati mwingine kama Maragoli. Watu wanaoishi Vihiga hujitambulisha kimsingi kama "Wamaragoli" na wanazungumza lugha inayoitwa Kimaragoli. Lugha hiyo ni tofauti kabisa kati ya makabila mengine ya Waluhya na ndiyo lugha ya kwanza ya Kiluhya kutumika kutafsiria Biblia. Wengi wa Wamaragoli waliongokea Ukristo ndani ya madhehebu ya ya Quaker, ambayo bado inafuatilia hadi leo. Watiriki, Waidakho na Wabanyore ndio makabila mengine katika eneo hili.

Vihiga pia ni jina la moja ya divisheni ndani yake. Divisheni nyingine ni pamoja na Sabatia, Hamisi, Lwanda na Emuhaya.

Voi

Voi ni mji mkubwa wa Kaunti ya Taita-Taveta, kusini mwa Kenya. Awali ilikuwa kati ya wilaya sita za Mkoa wa Pwani.

Voi inapatikana Magharibi mwa jangwa la Taru, Kusini na Magharibi mwa Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Magharibi iliyo maarufu sana duniani kote.

Wakazi walikuwa 45,483 wakati wa sensa ya mwaka 2009.

Wilaya ya Busia, Kenya

Busia ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Magharibi wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Ilikuwa inapakana na Wilaya ya Kakamega mashariki, Wilaya ya Bungoma kaskazini, Wilaya ya Busia, Uganda upande wa magharibi, na Ziwa Victoria upande wa kusini.

Makao makuu yalikuwa mjini Busia.

Kwa sasa imekuwa kaunti ya Busia.

Shughuli kuu ya kiuchumi ni biashara na nchi jirani ya Uganda, pamoja na mji wa Busia kituo cha mpakani.

Mbali na mji, uchumi wa wilaya hutegemea sana uvuvi na kilimo, mazao msingi yakiwa pamoja na mihogo, mtama, viazi vitamu, maharagwe, na mahindi.

Wilaya ya Busia ni makao ya kabila la Waluhya nchini Kenya ambao wanapatikana hasa katika sehemu za Magharibi mwa Kenya. Wilaya hii ilikuwa na wakazi 370,608 (1999 sensa).

Wilaya ya Busia ina maeneo bunge manne:

Eneo bunge la Nambale

Eneo bunge la Butula

Eneo bunge la Funyula

Eneo bunge la Budalangi

Wilaya ya Ilala

Majiranukta kwenye ramani: 6.824°S 39.249°E / -6.824; 39.249

Wilaya ya Ilala ni wilaya mojawapo ya Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania yenye postikadi namba 12000. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 634,924. Eneo lake ni km² 273.

Ilala yenyewe inahesabiwa kama manispaa ya Ilala ndani ya jiji la Dar es Salaam. Inajumlisha kitovu cha kihistoria cha Dar es Salaam ambako kuna ofisi nyingi za serikali pamoja na makampuni makubwa na maduka. Nafasi ya kitovu chenyewe ni Sanamu ya Askari; mitaa mingine maarufu ni Kariakoo, Buguruni, Kivukoni na kando yake iko Pugu.

Wilaya ya Nyeri

Wilaya ya Nyeri ilikuwa wilaya mojawapo ya mkoa wa Kati wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Makao makuu yalikuwa mjini Nyeri.

Kwa sasa imekuwa kaunti ya Nyeri.

Wilaya hiyo ilikuwa na ukubwa wa eneo la kilomita mraba 3,356 [1] katika maeneo ya kusini mashariki mwa Mlima Kenya.

Ilikuwa na jumla ya wakazi 661,156. Wenyeji ni haswa wa kabila la Wakikuyu.

Wilaya ya Thika

Wilaya ya Thika ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Kati wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).

Makao makuu yalikuwa mjini Thika.

Kwa sasa imekuwa sehemu ya kaunti ya Kiambu.

Wilaya ilipakana na Nairobi upande wa kaskazini mashariki. Idadi ya wakazi ilikuwa 645.713.

Wilaya hasa ni kijiji, lakini wakazi wake wa mjini wanazidi kuongezeka pale mji wa Nairobi inapozidi kupanuka. Wakikuyu ndio waliozaidi kwa idadi wilayani.

Wilaya ina majimbo ya uchaguzi manne:

Eneo bunge la Gatanga (lina Gatanga na Kakuzi divisions)

Eneo bunge la Gatundu Kusini

Eneo bunge la Gatundu Kazkazini

Eneo bunge la Juja

Østfold

Østfold ni jimbo nchini Norwei. Østfold linachangamana nchi ya Uswidi masharakini, jimbo la Akershus kaskazinini na lango la Oslofjorden magharabini. Watu 272,254 wanakaa Østfold.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.