Magharibi

Magharibi ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande wa machweo ya jua.

Magahribi ni pia neno la kutaja saa ya sala ya jioni ya Waislamu na sala hii yenyewe.

Jina "magharibi" limetokana na neno la Kiarabu مَغْرِب maghrib linalomaanisha sehemu upande wa machweo.

Magharibi kawaida huwa upande wa kushoto kwenye ramani. Tanzania iko upande mwa magharibi ya Bahari Hindi, Burundi iko upande wa magharibi ya Tanzania, na nchi ya Malawi iko upande mwa magharibi ya Msumbiji.

Kwa maana ya kiutamaduni kuna uzoefu kutaja utamaduni wa Ulaya pamoja na Marekani (ambayo ni mtoto wa utamaduni wa Ulaya) kama "magharibi", kinyume chake ni "mashariki" kwa maana ya Asia.

Wakati wa vita baridi magharibi ilikuwa kifupi cha nchi za kibepari zilizofuata mtindo wa demokrasia kinyume na mashariki iliyomaanisha nchi za kikomunisti.

CompassRose16 W
Alama za dira zikionyesha magharibi katika hali ya mkoozo (W = "West" = magharibi)

Tazama pia

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Bahari ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

Mkoa wa Eskişehir

Eskişehir (inatafsiriwa kama: mji wa kale) ni jina la mkoa uliopo mjini kaskazini-magharibi mwa nchi ya Uturuki. Mikoa inayopatikana na mkoa huu ni pamoja na Bilecik kwa upande wa kaskazini-magharibi, Kütahya kwa upande wa magharibi, Afyon kwa upande wa kusini-magharibi, Konya kwa upande wa kusini, Ankara kwa upande wa mashariki, na Bolu kwa upande kaskazini. Mji mkuu wake ni Eskişehir.

Mkoa wa Magharibi (Uganda)

Mkoa wa Magharibi (kwa Kiingereza: Western Region) ni kati ya mikoa minne ya Uganda.

Kwa sasa linaundwa na wilaya 26.

Makao makuu yako Mbarara.

Wakazi ni 8,874,862.

Mto Awach Tende

Mto Awach Tende (au Awach Kusini au Kitare) unapatikana katika kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa Kenya (kwenye ziwa Nyanza).

Maji yake yanaishia katika mto Naili na hatimaye katika Bahari ya Kati.

Mto Engare Siyiapei

Mto Engare Siyiapei unapatikana katika kaunti ya Narok, magharibi mwa Kenya.

Mto Gucha

Mto Gucha unapatikana katika kaunti ya Migori, magharibi mwa Kenya, na unaishia katika ziwa Viktoria, ukichangia hivyo mto Naili na hatimaye Bahari ya Kati.

Mto Kangen

Mto Kangen unapatikana Sudan Kusini, magharibi kidogo kwa Hifadhi ya Taifa ya Boma.

Unaungana na mto Pibor karibu na Pibor. Halafu maji yake yanaingia katika Nile Nyeupe.

Mto Miyombo

Mto Miyombo ni mto wa Tanzania mashariki, unaotiririka hadi kuingia mto Mkata, tawimto wa mto Wami ambao unaishia katika Bahari Hindi magharibi kwa Zanzibar.

Mto Mogunga (Kisii)

Mto Mogunga (Kisii) ni jina la miwili kati ya mito inayopatikana katika kaunti ya Kisii, magharibi mwa Kenya (kwenye ziwa Nyanza).

Maji yake yanaishia katika mto Naili na hatimaye katika Bahari ya Kati.

Mto Momba

Mto Momba ni jina la miwili kati ya mito ya mkoa wa Songwe (Tanzania Kusini Magharibi).

Unatiririka upande wa kusini magharibi na kuishia katika ziwa Rukwa.

Mto Msenguse

Mto Msenguse ni mmojawapo kati ya mito ya Tanzania (upande wa magharibi).

Unatiririka hadi ziwa Tanganyika.

Mto Nkusi

Mto Nkusi unapatikana magharibi mwa Uganda (wilaya ya Kakumiro na wilaya ya Kibaale).

Maji yake yanaingia katika ziwa Albert. Katikati ya mwendo wake yanachanganyikana na ya mto Kafu kwa sehemu fulani.

Mto Riana

Mto Riana unapatikana katika kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa Kenya (kwenye ziwa Nyanza).

Ni tawimto la mto Gucha ambao unaishia katika ziwa Viktoria, ukichangia hivyo mto Naili na hatimaye katika Bahari ya Kati.

Mto Rufugu

Mto Rufugu ni mmojawapo kati ya mito ya Tanzania (upande wa magharibi).

Unatiririka hadi ziwa Tanganyika.

Mto Yala

Mto Yala unapatikana magharibi mwa Kenya na unaishia katika ziwa Viktoria, ukichangia hivyo mto Naili na hatimaye Bahari ya Kati.

Mto wa Nzoia

Mto wa Nzoia ni mto wa Kenya unaotoka Mlima Elgon na kuwa na urefu wa kilomita 257 (maili 160). Unatiririkia kusini na kisha magharibi hatimaye unaingia katika Ziwa Viktoria karibu na mji wa Port Victoria.

Mto huu ni muhimu kwa maeneo ya Magharibi mwa Kenya, ukipitia kwenye eneo linalokadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya milioni 1.5. Maji yake hutumika kwa umwagiliaji wa mimea mwaka mzima, wakati mafuriko ya kila mwaka ya kuzunguka eneo amana ya Budalang'i husababisha mchanga unaochangia uzalishaji mzuri wa kilimo katika eneo hili.

Kwenye eneo la viwanda lililoko Webuye, mto huingiwa na uchafu mwingi unaotoka kwenye viwanda vya karatasi na sukari katika eneo hilo.

Mto huu una idadi kubwa ya maporomoko ya maji ya kuvutia, na unakisiwa kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme unaotokana na maji.

Pembetatu ya Ilemi

Majiranukta kwenye ramani: 4°59′29″N 35°19′39″E

Pembetatu ya Ilemi ni eneo la kilometa mraba 10,320-14,000 hivi kaskazini magharibi kwa ziwa Turkana (Afrika Mashariki) linalogombaniwa na Sudan Kusini na Kenya mpakani mwa Ethiopia. Kwa sasa inatawaliwa na Kenya.

Tsavo (mto)

Tsavo ni jina la mto mmojawapo wa Kenya kusini ambao unatiririka kutoka magharibi hadi mashariki na uko mpakani mwa mbuga ya kitaifa ya milima ya Chyulu, na hifadhi ya wanyama ya Mkomazi nchini Tanzania.

Chanzo chake ni karibu na mpaka wa Tanzania, mguuni pa mlima Kilimanjaro. Unapita Mbuga wa Wanyama wa Tsavo Mashariki na kuishia katika mto Athi karibu na Maporomoko ya maji ya Lugard. Kuanzia hapa mto huitwa Galana.

Mto Tsavo ulijengewa daraja mara ya kwanza wakati wa reli ya Uganda na daraja lile lilikuwa mahali ambako simba waliua wafanyakazi 135.

Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki ni moja ya hifadhi kubwa na kongwe zaidi nchini Kenya iliyotambaa eneo la kilomita za mraba 11,747. Ilifunguliwa mnamo Aprili1948, na iko karibu na kijiji cha Voi katika Wilaya ya Taita-Taveta. Hifadhi hii imetengwa na sehemu ya magharibi na barabara na reli ya A109. Jina lake linatokana na mto Tsavo.

Ulaya

Ulaya (asili ya jina ni neno la Kiarabu ولاية, wilaayatun; inaitwa pia Uropa) ni bara lenye eneo la km² 10,600,000 tu, lakini wakazi ni milioni 700.

Wengi wenye asili ya Ulaya wakati wa ukoloni walitawanyika duniani, hasa Amerika, wakiathiri kote upande wa lugha, utamaduni na dini.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.