Lugha za Kisemiti

Lugha za Kisemiti ni kundi la lugha zinazozungumzwa na watu milioni 300 hivi katika Asia ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini na Afrika ya Mashariki. Zinahesabiwa kama tawi la lugha za Kiafrika-Kiasia.

Lugha za Kisemiti
Maneneo penye wasemaji wengi wa lugha za Kisemiti

Lugha za Kisemiti leo

Lugha yenye wasemaji wengi ni Kiarabu. Wasemaji wengine wengi ni wale wanaotumia lugha za Ethiopia na Eritrea halafu Israel. Lugha hai za kisemiti ni pamoja na:

Lugha za kihistoria

Kuna idadi kubwa ya lugha za Kisemiti zinazojulikana kama lugha za kihistoria zisizo na wasemaji tena. Kati ya lugha hizi ni lugha za Babeli, Ashur, Kanaan, Moabu, Finisia na kwa jumla lugha za mataifa mengi zinazotajwa katika Biblia.

Abjadi

Abjad ni jina la mwandiko wa lugha ya Kiarabu na pia jina la kundi la miandiko inayotumia muundo wa kuandika konsonanti za neno lakini kuacha vokali.

Afrika ya Mashariki

Afrika ya Mashariki ni sehemu ya bara la Afrika ambayo iko upande wa mashariki, ikipakana na Bahari ya Kihindi.

Kadiri ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Mashariki ina nchi 18 zifuatazo:

Burundi (mji mkuu Bujumbura)

Djibouti (mji mkuu Jibuti (mji))

Eritrea (mji mkuu Asmara)

Ethiopia (mji mkuu Addis Abeba)

Kenya (mji mkuu Nairobi)

Komori (mji mkuu Moroni)

Madagaska (mji mkuu Antananarivo)

Malawi (mji mkuu Lilongwe)

Morisi (mji mkuu Port Louis)

Mozambique (mji mkuu Maputo

Rwanda (mji mkuu Kigali)

Zambia (mji mkuu Lusaka)

Shelisheli (mji mkuu Victoria)

Zimbabwe (mji mkuu Harare)

Somalia (mji mkuu Mogadishu)

Sudan Kusini (mji mkuu Juba)

Tanzania (mji mkuu Dodoma)

Uganda (mji mkuu Kampala)Mayotte na Réunion, zilizokuwa makoloni na sasa ni mikoa ya Ufaransa, zinahesabiwa pia katika orodha hii.Hata hivyo:

Malawi, Zambia na Zimbabwe wakati mwingine zinehesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kusini (zamani zilikuwa pamoja kama Rhodesia ya Kusini, Rhodesia ya Kaskazini na Unyasa katika Shirikisho la Afrika ya Kati)Komori, Morisi, Shelisheli, Mayotte na Réunion ni visiwa vidogo vya Bahari Hindi vinavyohesabiwa kuwa sehemu za Afrika ya Mashariki.

Alfabeti ya Kigiriki

Alfabeti ya Kigiriki ni mwandiko maalumu wa lugha ya Kigiriki. Herufi zake zilitumika pia kama tarakimu na sasa hutumiwa kimataifa kama alama za kisayansi.

B

B ni herufi ya pili katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Beta ya Kigiriki.

Ethiopia

Ethiopia (kwa Kiamhara ኢትዮጵያ Ityopp'ya; kwa Kiswahili pia "Uhabeshi") ni nchi ya Afrika ya Mashariki iliyoko kwenye Pembe ya Afrika.

Nchi zinazopakana na Ethiopia ni Sudan na Sudan Kusini upande wa magharibi, Eritrea na Jibuti kaskazini, Somalia mashariki na Kenya upande wa kusini.

Ni nchi ambayo ina historia ya pekee Afrika na hata duniani kwa ujumla.

Ethiopia ni moja ya nchi mbili za Afrika ambazo hazikutawaliwa na wakoloni wakati walipong’ang’ania Afrika. Nchi nyingine ni Liberia. Kabla ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Ethiopia ilivamiwa na Waitalia (1936) lakini ilipata uhuru wake tena baada ya miaka michache.

Jan Knappert

Dr. Jan Knappert (* 14 Januari 1927 – 30 Mei 2005) alikuwa mwanaisimu kutoka nchi ya Uholanzi mwenye umaarufu wa kimataifa alikuwa mtaalamu hasa wa lugha za Kiswahili na Kiesperanto.

Alifundisha kwenye vyuo vikuu mbalimbali pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, cha Nairobi, School of Oriental and African Studies katika Chuo Kikuu cha London, hadi kurudi Ulaya bara alipofundisha miaka mingi kwenye Chuo Kikuu cha Leuven.

Alikuwa pia na shahada za uzamili katika Kisanskrit, lugha za Kisemiti (pamoja na Kiebrania, Kiarabu na Uislamu), na lugha za Austronesia (pamoja na Kimalay, Kitagalog, Kihawaii na Kimalagasy)Katika miaka alipokaa Afrika za Mashariki alikusanya muswada nyingi za Kiswahili zilizoandikwa kwa herufi za Kiarabu akatumikia pia kama Katibu wa Kamati ya Kiswahili ya Afrika ya Mashariki.. Alikabidhi mkusanyiko wa muswada za Kiswahili kwa Chuo Kikuu cha London. ambako sehemu imeshapatikana kwa umma kwa njia ya intaneti.

Aliandika mengi na vitabu vingi. Utafiti wake kuhusu Kiswahili ulikazia hasa utamaduni, ushairi na dini ya Waswahili.

Alikusanya orodha ya istilahi za Kiswahili za kutaja nyota, kundinyota na sayari na hivyo kuhifadhi elimu ya vizazi Waswahili waliokuwa mabaharia na kuvuka bahari katika jahazi zao, ambayo ni elimu inayoanza kupotea haraka kutokana na mabadiliko ya teknolojia na ubaharia..

Akiunganisha elimu yake ya lugha mbalimbali alitunga Kamusi ya Esperanto-Kiswahili akatafsiri pia utenzi wa kitaifa ya Kifini (unaoitwa Kalevala) kwa Kiswahili.

Kiamhari

Kiamhari ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa nchini Ethiopia.

Kiarabu

Kiarabu (ar.: العَرَبِيَّة‎‎, al-ʻarabiyyah, kwa kirefu al-luġatu al-ʿarabiyya ) ni lugha ya Kisemiti inayotumiwa na watu milioni 206 kama lugha ya kwanza na milioni 246 wa ziada kama lugha ya pili. Ilhali kuna lahaja nyingi, Kiarabu sanifu (ar. الفصحى fuṣḥā) ni lugha rasmi ya nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ya Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa. Kuna pia matumizi kama lugha ya kidini katika Uislamu.

Hivyo Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani ikisomwa kwa viwango tofauti na mamilioni ya waumini Waislamu wakielekea kujifunza na kuelewa kitabu cha Korani. Kama lugha ya kidini ina athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofautitofauti walio Waislamu.

Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno), ufasaha mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau.

Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo, mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafudhi.

Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isitetereke wala kubadilika na kupotea kama lugha nyingine nyingi, leo, baada ya miaka zaidi ya elfu, imebaki thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoandikwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbalimbali zinazotumika na Waarabu wa sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi hayo yaendelee kufahamika milele.

Leo, Kiarabu ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina, Kihindi, Kihispania, Kiingereza na Kibengali.

Umuhimu wa lugha hii unazidi kukua kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Afrika, Asia na Ulaya) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini).

Kiaramu

Kiaramu ni mojawapo kati ya lugha za Kisemiti ambazo zinapangwa kati ya lugha za Afrika-Asia pamoja na Kiebrania na nyinginezo.

Inatumika tangu miaka 3,000 iliyopita. Ndiyo lugha aliyoitumia Yesu pamoja na Wayahudi wengi wa wakati wake.

Sehemu chache za Biblia ziliandikwa kwa lugha hiyo wakati ilipokuwa imeenea zaidi kwenye Mashariki ya Kati hata Kiaramu cha Kale kikawa lugha rasmi ya utawala katika Milki ya Uajemi.

Baada ya Aleksander Mkuu wasemaji wa Kiaramu walitawaliwa na watu wa ustaarabu wa Kigiriki. Katika miji mikubwa Kigiriki kilikuwa lugha kuu. Baada ya uenezaji wa Ukristo lugha hiyo iliendelea ikajulikana zaidi kama "Kisiria".

Hata baada ya uenezi wa Uislamu Kisiria kiliendelea kupanuka na vitabu vingi viliandikwa kwa lugha hiyo. Hata hivyo polepole wasemaji wengi wa Kisiria walianza kutumia Kiarabu, hasa wale waliogeukia Uislamu.

Pamoja na hayo watu 445,000 hivi wanaitumia hata leo, hasa nchini Syria, Iraq na Uturuki. Karibu wote ni Wakristo.

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Kifinisia

Kifinisia ilikuwa lugha ya Kisemiti iliyozungumzwa kati ya 1100 KK hadi takriban 600 BK katika maeneo ya pwani la Kanaani na Shamu ya magharibi ambako leo hii kuna nchi za Israeli, Lebanoni na Syria.

Ilikuwa lugha ya Wafinisia ikaenea pamoja nao katika koloni zao hadi Afrika ya Kaskazini kama Karthago na Hispania.

Kifinisia ilikuwa lugha ya kwanza iliyoandikwa kwa aina ya alfabeti iliyoendelezwa baadaye katika alfabeti ya Kigiriki. Hali halisi mwandiko huu ulikuwa abjadi ukawa mama wa miandiko yote ya Kisemiti (kama herufi za Kiarabu na Kiebrania) na pia wa alfabeti zote zilizofuata alfabeti za Kigiriki na Kilatini.

Kige'ez

Kige'ez (kwa maandishi ya Kiamhari: ግዕዝ; matamshi: gē-ĕz) ni lugha ya kale ya Ethiopia iliyozungumzwa zamani za ufalme wa Aksum. Baadaye ilikuwa lugha ya kimaandishi nchini Ethiopia hadi karne ya 19 na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la orthodoksi la Ethiopia.

Huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti za kusini. Hutazamiwa kama lugha mama ya lugha za kisasa kama Kiamhari na Kitigrinya nchini Ethiopia na Eritrea.

Maandishi ya Kige'ez ni aina ya abugida yenye herufi 26 za konsonanti na 4 za vokali zinazounganishwa kuwa alama 202 kwa silabi zote zinazowezekana. Mifano ya kwanza inyojulikana ni kutoka karne ya 4 BK.

Kimalta

Kimalta ni lugha rasmi kwenye nchi ya kisiwani ya Malta katikati ya Bahari ya Mediteranea. Kimalta huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti ikiwa ni lugha pekee ya familia hiyo katika nchi za Ulaya.

Kimalta ni karibu na Kiarabu cha Tunisia lakini huandikwa kwa alfabeti ya Kilatini. Lugha imepokea maneno mengi kutoka Kiitalia na Kiingereza. Siku hizi takriban nusu ya maneno yana asili ya Kiitalia, na theluthi moja ni Kiarabu. Mengine yameingia kutoka kwa Kiingereza. Misingi ya sarufi ni Kiarabu.

Kitigrinya

Kitigrinya (pia: Kitigray, Kitigre, Kihabesha) ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa katika Ethiopia (hasa jimbo la Tigray) na Eritrea.

Idadi ya wasemaji ni takriban milioni 5-6. Maandishi yake ni kwa alfabeti ya Kiethiopia. Kitigrinya kimetoka katika lugha ya kale ya Ge'ez iliyokuwa lugha ya nyanda za juu za Ethiopia na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na Eritrea.

Katika Ethiopia Kitigrinya ni lugha ya tatu inayotumiwa na watu wengi (baada ya Kioromo na Kiamhari). Katika Eritrea ni lugha inayotumiwa zaidi kabisa.

Kitigrinya ( ትግርኛ, tigriññā), pia huandikwa Tigrigna, Tigrina, Tigriña, ni lugha ya pili ambayo huzungumza na watu wa jamii ya Tigray katikati mwa jimbo la Eritrea ambapo lugha hii ni moja kati ya lugha mbili muhimu katika watu wa Eritrea na katika jimbo ya Tigray, nchini Ethiopia. Wazungumzaji wa lugha hii huitwa Watigray ambapo lugha hii kutumika kama lugha maalum miongoni mwao na pia katika vijisehemu vya wahamiaji katika maeneo haya ikiwa ni pamoja na watu wa jamii ya Beta Israel ambao kwa huishi nchini Israeli.

Lugha hii mara nyingi huchanganywa na lugha nyingine ambazo kwa namna fulani hufanana nazo hasa katika matamshi kwa mfano lugha ya Kitigre ambayo lugha hii hutumika katika maeneo ya ukanda wa chini wa Eritrea, hasa kwa upande wa Kaskazini na Magharibi mwa mjii huu ambapo lugha hii hutumika.

Tarakimu

Tarakimu (kutoka Kiarabu رقم raqm) au numerali (kutoka Kilatini numerus, kupitia Kiingereza numeral) ni alama za kimaandishi zinazotumiwa kuandika namba.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.