Lugha za Kiafrika-Kiasia

Lugha za Kiafrika-Kiasia ni familia ya lugha barani Afrika na Asia. Katika familia hiyo kuna lugha zaidi ya 300 zenye wasemaji milioni 350 kati ya Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi, hasa Kiarabu, lakini pia Kihausa, Kioromo, Kiamhara, Kisomali, Kiebrania n.k.

Hamito-Semitic languages
Uenezi wa lugha hizo.

Viungo vya nje

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kiafrika-Kiasia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Afrika

Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara pekee la kushinda Afrika.

Eritrea

Eritrea ni nchi ya Afrika kaskazini-mashariki.

Upande wa Magharibi imepakana na Sudan, upande wa Kusini imepakana na Ethiopia, na Kusini-Mashariki kuna nchi ya Djibouti. Mashariki na Kusini-Mashariki Eritrea ina pwani ndefu ya Bahari ya Shamu. Eneo hili lote hujulikana pia kama Pembe ya Afrika.

Kiaramu

Kiaramu ni mojawapo kati ya lugha za Kisemiti ambazo zinapangwa kati ya lugha za Afrika-Asia pamoja na Kiebrania na nyinginezo.

Inatumika tangu miaka 3,000 iliyopita. Ndiyo lugha aliyoitumia Yesu pamoja na Wayahudi wengi wa wakati wake.

Sehemu chache za Biblia ziliandikwa kwa lugha hiyo wakati ilipokuwa imeenea zaidi kwenye Mashariki ya Kati hata Kiaramu cha Kale kikawa lugha rasmi ya utawala katika Milki ya Uajemi.

Baada ya Aleksander Mkuu wasemaji wa Kiaramu walitawaliwa na watu wa ustaarabu wa Kigiriki. Katika miji mikubwa Kigiriki kilikuwa lugha kuu. Baada ya uenezaji wa Ukristo lugha hiyo iliendelea ikajulikana zaidi kama "Kisiria".

Hata baada ya uenezi wa Uislamu Kisiria kiliendelea kupanuka na vitabu vingi viliandikwa kwa lugha hiyo. Hata hivyo polepole wasemaji wengi wa Kisiria walianza kutumia Kiarabu, hasa wale waliogeukia Uislamu.

Pamoja na hayo watu 445,000 hivi wanaitumia hata leo, hasa nchini Syria, Iraq na Uturuki. Karibu wote ni Wakristo.

Kiiraqw

Kiiraqw ni mojawapo kati ya lugha za Kiafrika-Kiasia. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiiraqw iko katika kundi la lugha za Kikushi.

Inatumika nchini Tanzania na kuzungumzwa hasa na kabila la Wairaqw kaskazini mwa Tanzania kutokana na kuwepo kwao katika mkoa wa Manyara na mkoa wa Arusha kama wenyeji wa karne nyingi.

Baadhi ya watu husema Kiiraqw ni sawa na "Kimbulu", kumbe siyo. Hakuna lugha inayoitwa Kimbulu. Mbulu ni jina la wilaya ambayo ina idadi kubwa ya Wairaqw kuliko eneo lingine lolote nchini Tanzania. Lakini ikumbukwe kuwa Mbulu si eneo pekee wanakopatikana Wairaqw, kitu ambacho kingesababisha watu wengine kuita lugha ya Kiiraqw kuwa Kimbulu.

Mwaka 2001 idadi ya wasemaji wa Kiiraqw imehesabiwa kuwa watu 462,000.

Kimisri

Kimisri ni lugha ya kale ya Misri. Kiliandikwa kwa kutumia hiroglifi.

Kilipoendelea kikaja kuwa lugha ya liturujia ya Kanisa la Misri ambayo inatumika hata leo katika ibada, ila si katika maisha.

Lugha za Afrika

Lugha za Afrika ni zaidi ya 2000.

Baadhi ya lugha hizi zina wasemaji mamilioni kama vile Kiswahili, Kihausa, Kiigbo, au Kiyoruba.

Lugha nyingine zina wasemaji wachache sana hata zinaelekea kupotea.

Lugha za Kikushi

Lugha za Kikushi ni kati ya lugha za Kiafrika-Kiasia. Zinatumika hasa katika Pembe la Afrika na nchi za jirani, kuanzia Misri hadi Tanzania.

Jina linatokana na Kush, mtu wa Biblia anayetajwa kama babu wa makabila ya aina hiyo.

Leo lugha kubwa zaidi katika kundi hilo ni Kioromo (35,000,000), kikifuatwa na Kisomali (18,000,000). Baadhi yake zimeshakufa.

Lugha za Kisemiti

Lugha za Kisemiti ni kundi la lugha zinazozungumzwa na watu milioni 300 hivi katika Asia ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini na Afrika ya Mashariki. Zinahesabiwa kama tawi la lugha za Kiafrika-Kiasia.

Orodha ya lugha za Kenya

Kenya ni nchi ya lugha nyingi. Lugha zake za taifa ni Kiswahili na Kiingereza. Kuna jumla ya lugha 62 zinazozungumzwa nchini Kenya (kulingana na Ethnologue), nyingi zikiwa za asili ya Kiafrika na baadhi za asili ya Kiasia na Mashariki ya Kati.

Tamazight

Tamazight ni jina la kundi la lugha zinazotajwa pia kama "lugha za Kiberber" na kuzungumzwa hasa Moroko na Algeria lakini pia kati ya wakazi wa jangwa kubwa la Sahara hadi eneo la Sahel. Ni lugha ya Waberberi wanaoishi kati ya wasemaji wa Kiarabu katika Afrika ya Kaskazini.

Tamazight ni kati ya lugha za Kiafrika-Kiasia. Wasemaji wa Tamazight watazamiwa kuwa wenyeji asilia wa Afrika ya Kaskazini kabla ya kuja kwa Waroma wa Kale au kwa Waarabu.

Tangu uenezaji wa Kiarabu matumizi ya Tamazight imerudi nyuma polepole. Wakazi wengi wa nchi za Afrika ya Kaskazini ni wa asili ya Kiberber lakini kwa kawaida kupotea kwa lugha humaanisha pia upotevu wa tabia ya kuwa Berber. Leo hii wamebaki wasemaji milioni 10 na wengi wao hutumia lugha yao pamoja na Kiarabu au Kifaransa katika maisha ya kila siku.

Utamaduni wa Kiafrika

Utamaduni wa Afrika unajumuisha tamaduni zote ambazo ziliwahi kuweko katika bara la Afrika.

Dhana ya utamaduni wa Afrika nzima ilijadiliwa kwa makini katika miaka ya 1960 na 1970 katika muktadha wa harakati ya Négritude, lakini imepoteza mtindo katika masomo ya Afrika.

Mpasuko mkuu ni kati ya Afrika ya Kaskazini (pamoja na Chad na Pembe la Afrika), ambayo ni sehemu ya ulimwengu wa Kiislamu, na Afrika ya kusini kwa Sahara, ambayo imegawanywa katika idadi kubwa ya tamaduni za kikabila, zikiwemo za Niger-Congo (sanasana za Kibantu), Nilo-Saharan katika maeneo ya Sahara na Sahel na sehemu za Afrika ya Mashariki na Khoisan (wazawa wachache wa Tanzania na Kusini mwa Afrika).

Uenezi mpana wa Kibantu unaojumuisha maeneo ya Afrika ya Magharibi, Afrika ya Mashariki, Afrika ya Kati na vilevile Afrika ya Kusini, ni matokeo ya uenezi wa Wabantu katika milenia ya 1 BK. Utumizi mpana wa Kiswahili kama lingua franca unaonyesha zaidi athari ya Kibantu juu ya utamaduni wa "Afrika nzima".

Waalagwa

Wasi (au Waalagwa) ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa, hasa tarafa ya Kolo katika vijiji kama Kwa Dinu, Mneniya, Hurui n.k. Watu hao wapo pia mkoani Manyara (Babati mjini na Galapo). Kati ya makabila yaliyopo Kondoa linaweza kuwa kabila la pili kwa ukubwa na wingi baada ya Warangi.

Lugha yao ni [[Algwaisa] si Chasi ambayo ni mojawapo ya lugha za Kiafrika-Kiasia, si ya Kibantu, kwani huendana na Kifyomi, Kiiraqw na Kiburunge ambazo zote hizi ni lugha za Kikushi. Kabila hili sehemu zote wanazokaa wenyewe huongea lugha hii na ndiyo asili yao ya wazazi wao waliowakuta.

Waborana

Waborana Oromo (ambao pia huitwa Boran) ni kabila lipatikanalo Kusini mwa Ethiopia, Oromia na Kaskazini mwa Kenya ambao wanajulikana kuwa wafugaji.

Wao ni kundi dogo la Waoromo.

Wanawakilisha nusu ya makundi mawili ya Waoromo asili, nusu nyingine ikiwa Wabarentu. Takribani watu milioni 7 wanajitambulisha kama jamii ya Waborana.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.