Kusini

Kusini ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni ncha ya kusini ya dunia. Kinyume chake ni kaskazini.

Jina "kusini" laaminiwa limetokana na neno lenye asili ya Misri ya Kale kwa ajili ya nchi ya Kushi iliyokuwepo upande wa kusini wa Misri katika Nubia (au Sudani ya leo) pamoja na Uarabuni ya Kusini. Jina la Kushi lapatikana pia katika masimulizi ya Biblia likimtaja mmoja wa wana wa Hamu katika kitabu cha Mwanzo 10:16 kama baba wa watu wa Kushi. Hili neno lilitumiwa na mabaharia Waarabu pia kutaja mwelekeo wa kusini na kwa umbo la "kusi" hasa upepo wa kusini. [1]

Ukitazama jua linapochomoza kusini huwa ni upande wa kulia. Kusini kawaida huwa chini zaidi kwenye ramani. Marekani ipo kusini mwa nchi ya Kanada, Tanzania ipo kusini mwa nchi ya Kenya, na Msumbiji ipo kusini mwa nchi ya Tanzania. Ncha ya kusini ni kusini ya mbali unayoweza kwenda.

CompassRose16 S
Alama za dira zikionyesha kusini katika hali ya mkoozo

Tazama pia

Marejeo

  1. linganisha maelezo katika makala "kusini" katika kamusi ya M-J SSE
Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kusini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Afrika Kusini

Afrika Kusini ni nchi kubwa ya Afrika ya Kusini yenye wakazi takriban milioni 54.

Imepakana na Namibia, Botswana, Zimbabwe, Msumbiji na Uswazi. Nchi nzima ya Lesotho iko ndani ya eneo la Afrika Kusini.

Mji mkubwa ni Johannesburg. Majukumu ya mji mkuu yamegawiwa kati ya miji mitatu: Cape Town ni makao ya Bunge, Pretoria ni makao ya Serikali na Bloemfontein ni makao ya Mahakama Kuu.

Bahari ya Hindi

Bahari ya Hindi ni bahari ya tatu kwa ukubwa duniani ikiwa imechukua asilimia 20 ya uso wa dunia na kuzungukwa na mabara manne.

Upande wa kaskazini imepakana na Asia ya Kusini; magharibi imepakana na Ghuba ya Uajemi, Bahari ya Shamu na Afrika; mashariki imepakana na Ghuba ya Malay, visiwa vya Sunda (Indonesia), na Australia; na upande wa kusini imepakana na Bahari ya Kusini.

Bahari hii ni njia muhimu ya usafiri na usafirishaji kwa meli kati ya Asia na Afrika.

Mto Achwa

Mto Achwa (pia Aswa) unapatikana katika wilaya ya Nwoya, kaskazini mwa Uganda. Unaanza nchini Uganda na kuingia katika Nile Nyeupe nchini Sudan Kusini. Hivyo maji yake yanaishia kkatika Bahari ya Kati.

Mto Awach Tende

Mto Awach Tende (au Awach Kusini au Kitare) unapatikana katika kaunti ya Homa Bay, magharibi mwa Kenya (kwenye ziwa Nyanza).

Maji yake yanaishia katika mto Naili na hatimaye katika Bahari ya Kati.

Mto Ewaso Ng'iro wa Kusini

Mto Ewaso Ng'iro wa Kusini unapatikana nchini Kenya na unaishia katika ziwa Natron nchini Tanzania.

Mto Goshi (Kilifi)

Mto Goshi (Kilifi) unapatikana katika kaunti ya Kilifi, kusini mashariki mwa Kenya (eneo la pwani).

Mto Kangen

Mto Kangen unapatikana Sudan Kusini, magharibi kidogo kwa Hifadhi ya Taifa ya Boma.

Unaungana na mto Pibor karibu na Pibor. Halafu maji yake yanaingia katika Nile Nyeupe.

Mto Kidepo

Mto Kidepo unaanza nchini Uganda (wilaya ya Kaabong), unapokea maji ya Mto Narus kilometa 13 baada ya kuingia nchini Sudan Kusini na unaishia katika Nile Nyeupe.

Mto Mbagathi

Mto Mbaghati unapatikana kusini mwa Kenya. Ni tawimto la mto Athi-Galana-Sabaki ambao unaishia katika Bahari ya Hindi.

Mto Momba

Mto Momba ni jina la miwili kati ya mito ya mkoa wa Songwe (Tanzania Kusini Magharibi).

Unatiririka upande wa kusini magharibi na kuishia katika ziwa Rukwa.

Nile

Mto Nile (pia: Naili; kwa Kiarabu: ‏ ,النيل‎ an-nīl) ni mto mkubwa upande wa mashariki ya bara la Afrika. Mara nyingi hutajwa kuwa pia ni mto mrefu kabisa duniani kushinda mto Amazonas. Kutoka Ziwa la Viktoria Nyanza hadi mdomo wake kwenye Bahari ya Mediteranea Nile inavuka nchi za Uganda, Sudan Kusini, Sudan na Misri kwa urefu wa km 6,650.

Beseni la Nile hukusanya maji ya eneo linalojumlisha 10% za eneo la Afrika yote au km² 3,349,000. Takriban watu milioni 250 hukalia beseni hilo.

Nile Nyeupe

Nile Nyeupe (kwa Kiingereza: White Nile; kwa Kiarabu: النيل الأبيض, an-nīl al-'abyaḍ) ni mto wa Afrika, moja kati ya matawimto makuu ya Nile; la pili linaitwa Nile ya Buluu. Majina hayo yanatokana na rangi ya maji inayosababishwa na udongo uliomo.Kwa usahihi, "Nile Nyeupe" ni mto unaopatikana katika Ziwa No, inapokutana mito Bahr al Jabal na Bahr el Ghazal. Kwa maana pana ni mikondo yote inayotokana na Ziwa Viktoria hadi kuungana na Nile ya Buluu. These Mikondo hiyo inaitwa "Nile ya Viktoria" (kupitia Ziwa Kyoga hadi Ziwa Albert), "Nile ya Albert" (hadi mpaka wa Sudan Kusini) halafu "Nile ya mlimani" au "Bahr-al-Jabal" (hadi Ziwa No). "Nile Nyeupe" inamaanisha pengine hata vyanzo vya Ziwa Viktoria.

Pembetatu ya Ilemi

Majiranukta kwenye ramani: 4°59′29″N 35°19′39″E

Pembetatu ya Ilemi ni eneo la kilometa mraba 10,320-14,000 hivi kaskazini magharibi kwa ziwa Turkana (Afrika Mashariki) linalogombaniwa na Sudan Kusini na Kenya mpakani mwa Ethiopia. Kwa sasa inatawaliwa na Kenya.

Ruaha Mdogo

Ruaha Mdogo ni mto wa Tanzania Kusini Magharibi (Nyanda za Juu za Kusini) na ni tawimto la Ruaha Mkuu.

Ruaha Mdogo unatokea bonde la Usangu na kuingia katika Ruaha Mkuu karibu na mji wa Iringa.

Baada ya hapo mto huo unapitia Iringa na tambarare ya Kilombero hadi kuishia katika mto Rufiji ambao unamwaga maji mengi katika bahari Hindi.

Rufiji (mto)

Rufiji ni mto mkubwa wa Tanzania. Chanzo kiko Tanzania ya kusini-magharibi katika maungano ya tawimito ya mto Kilombero na mto Luwegu.

Unafikia Bahari Hindi kwa njia ya delta yake takriban km 200 kusini kwa Dar es Salaam karibu na kisiwa cha Mafia. Urefu wa Rufiji ni takriban km 600.

Tawimto mkubwa katika beseni yake ni Ruaha Mkuu.

Mwaka 2005 daraja lilikamilika linalorahisisha usafiri kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Lindi na Mtwara.

Ruhuhu (mto)

Mto Ruhuhu ni mto wa Tanzania Kusini. Chanzo chake kiko katika milima ya Kipengere upande wa kusini wa Njombe ikielekea kwanza kusini-mashariki na baadaye magharibi inapoishia katika Ziwa Nyasa karibu na mji wa Manda.

Mwendo wake una urefu wa kilomita zaidi ya 300. Hivyo ni tawimto mrefu wa Ziwa Nyasa na kutokana na hali hii inahesabiwa kama chanzo cha mto Shire unaopeleka maji ya ziwa kwenda mto Zambezi na Bahari Hindi.

Songwe (Mbeya)

Songwe ni jina la mito miwili ya Tanzania: mmoja uko katika mkoa wa Mbeya, mwingine katika mkoa wa Songwe.

Songwe ya Kusini ina chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya ikielekea kusini na kuishia Ziwa Nyasa. Baada ya kupita Itumba (Ileje) mto ni mpaka kati ya Tanzania na Malawi.

Tabia yake ya kubadilisha-badilisha mwendo wake imesababisha matatizo kati ya nchi jirani kwa sababu mashamba ya watu yamepatikana mara upande mmoja mara upande mwingine wa mpaka wa kimataifa.

Tana (mto)

Tana ni jina la mto mrefu kuliko yote ya Kenya ukiwa na urefu wa takriban km 650.

Chanzo chake ni milima ya Aberdare magharibi kwa Nyeri. Mwanzoni unelekea mashariki, halafu inapinda kuzunguka Mlima Kenya upande wa kusini. Kisha huingia ndani ya mabwawa ya Masinga na Kiambere yaliyotokana na bwawa la Kindaruma. Chini ya bwawa mto huu hugeuka kuelekea kaskazini na kutiririka mpaka wa kaskazini-kusini kati ya kaunti za Meru na Kitui, Bisanadi, Kora na Hifadhi ya wanyama ya Rabole. Ndani ya hifadhi hugeuka kuelekea mashariki, na kisha kusini mashariki.

Kati ya mito inayoingia mto wa Tana kuna mto Thika.

Inapita miji ya Garissa, Hola na Garsen kabla ya kufika Bahari Hindi kwenye Ghuba ya Ungwana.

Uganda

Uganda ni nchi ya Afrika ya Mashariki. Imepakana na Kenya upande wa mashariki, Sudan Kusini upande wa kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi, Rwanda na Tanzania upande wa kusini.

Uganda inamiliki sehemu ya ziwa la Viktoria Nyanza ikipakana huko na Kenya na Tanzania.

Uganda ni nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na wa miundo mingine mbalimbali ya kimataifa.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.