Konsonanti

Konsonanti ni sauti za lugha ambazo katika Kiswahili zatajwa kwa herufi B, Ch, D, F, G, H, J, K, L, M, N, P, Q, R, S, T, V, W, Y na Z

Kwa sauti hizo hewa haiondoki mdomoni moja kwa moja lakini mwendo wake ni pamoja na sauti za pembeni kwa kutumia shingo, ulimi au meno.

Hii ni tofauti na sauti za vokali kama A, E, I, O na U. Hizi ni sauti tupu ambako hewa huondoka mdomoni bila kikwazo au sauti za pembeni.

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Konsonanti kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Abjadi

Abjad ni jina la mwandiko wa lugha ya Kiarabu na pia jina la kundi la miandiko inayotumia muundo wa kuandika konsonanti za neno lakini kuacha vokali.

Abugida

Abugida (kutoka Ge‘ez አቡጊዳ ’abugida) ni muundo wa mwandiko mwenye alama kwa silabi yaani konsonanti pamoja na vokali. Ni mwandiko wa kawaida kwa lugha za Ethiopia na Uhindi ya Kaskazini.

Jina latokana na herufi nne za kwanza ya mwandiko wa Ge'ez ambayo ni lugha ya kale ya Ethiopia.

Tofauti yake na alfabeti kama mwandiko wa Kilatini ni ya kwamba hapa kuna alama za pekee kwa vokali na konsonanti zinazounganishwa kufuatana na mahitaji ya lugha. Tofauti na miandiko ya abjadi kama Kiarabu au Kiebrania ni ya kwamba abjadi mara nyingi haziandiki vokali.

Kwa mfano wa mwandiko wa Devanagari ya Kihindi kuna alama ya क ambayo ni "k" na pia silabi "ka". Kwa kuongeza mstari mdogo juu silabi mpya ya के ke inapatikana. Ule mstari mdogo unaomaanisha "e" haupatikani peke yake bali pamoja na alama ya konsonanti pekee.

Kutoka alama ल "l" / "la" kuna uwezekano wa kupata alama kwa ला lā, लि li, ली lĪ, लु lu, लू lū, ले le, लै lai, लो lo na लौ lau.

Alfabeti

Alfabeti ni kiasi cha alama zinazotumiwa kuandika sauti za lugha fulani. Alama hizi hupatikana kama orodha kwa ufuatano uliokubaliwa, kwa mfano katika Kiswahili: "a, b, ch, d, dh, e, f, g, gh, h, i, j, k, kh, l, m, n, ny, ng', o, p, r, s, sh, u, t, th, v,w, y, z".

Jina la "alfabeti" hutokana na mwandiko wa Kigiriki ambamo herufi mbili za kwanza ni α "alfa" na β "beta".

Alfabeti ni mtindo wa mwandiko uliosambaa duniani kote. Kwa lugha nyingi imechukua nafasi ya miandiko ya awali.

Alfabeti huonyesha sauti si maneno kamili - hii ni tofauti na mwandiko kama Kichina wenye alama kwa ajili ya neno lote.

Alfabeti ya Kilatini

Alfabeti ya Kilatini (pia: Alfabeti ya Kirumi) inatumiwa kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano kwenye ukurasa huu wa wikipedia.

Fonolojia

Fonolojia (hasa huitwa Sarufi Matamshi) ni tawi la sayansi ya isimu. Inashughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa irabu na konsonanti.

Ala za sauti (vipashio vya utamkaji) zinatumika katika utamkaji wa fonimu (vitamkwa) za lugha husika. Mkondo wa hewa wakati wa utamkaji. Kuwepo na kutokuwepo kwa mguno wakati wa utamkaji (ghuna/sighuna).

Utanzu huu hushughulikia kanuni zinazotawala uchambuzi wa mfumo wa sauti, yaani, sauti kutamkwaje na wapi katika kinywa cha mwanadamu.

Matokeo ya uchunguzi wa kifonolojia yana umuhimu katika kubuni alfabeti.

Dhana ya fonolojia inajipambanua vizuri zaidi ikifasiliwa kwa kutofautishwa na fonetiki. Wakati fonetiki ni taaluma inayochunguza sauti zitamkwazo na binadamu bila kuzihusisha na lugha yoyote, fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kimwera na Kinyaturu. Kwa ufupi, fonetiki huchunguza sauti zote zitamkwazo na binadamu; fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi.

Hivyo, fonetiki huchunguza sauti nyingi kadiri iwezekanavyo, lakini fonolojia huchunguza sauti chache tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Mathalani, mfumo wa sauti wa lugha ya Kiswahili una sauti thelathini tu (irabu tano na konsonanti ishirini na tano).

Jambo lingine la kuzingatia ni vipashio vya kiuchambuzi vya matawi haya mawili. Wakati fonetiki kipashio chake cha msingi ni "foni", fonolojia kipashio chake cha msingi ni "fonimu". Kwa kuzingatia maelezo ya hapo awali, ni wazi kuwa foni ni nyingi zaidi kuliko fonimu, kwa kuwa foni ni kila sauti itamkwayo na binadamu, wakati fonimu ni sauti zile tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha mahususi. Hivyo, kuna fonimu za Kiswahili, za Kiingereza, za Kichina, n.k., lakini foni si za lugha yoyote, wala huwezi kusema kwa uhakika kuna foni ngapi, kwa kuwa bado kuna lugha nyingi duniani ambazo hazijatafitiwa.

Historia ya fonolojia inaweza kuwa imeanza na Ashtadhyayi, sarufi ya Kisanskrit iliyoandikwa na Pāṇini katika karne ya 4 KK. Kwa namna ya pekee Shiva Sutras, nyongeza ya Ashtadhyayi, inaorodhesha fonemi ya lugha hiyo, pamoja na kujadili mofolojia, sintaksia na semantiki.

Herufi za Kiarabu

Herufi za Kiarabu ni maandishi maalumu ya lugha ya Kiarabu. Nje ya Kiarabu lugha mbalimbali zinaandikwa kwa herufi za Kiarabu, hasa lugha za nchi zenye Waislamu wengi, ingawa herufi hizo zilibuniwa kabla ya dini hiyo kuenea. Kati ya lugha hizo kuna Kiajemi, Kikurdi, Kimalay na Urdu. Pengine katika lugha hizo herufi kadhaa zinaongezwa au kupunguzwa, kulingana na lugha ilivyo.

Kihistoria hata Kiswahili na Kituruki ziliwahi kuandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Kuna herufi 28 za Kiarabu zinazoandikwa kutoka kulia kwenda kushoto. Herufi zote isipokuwa sita zinaunganishwa wakati wa kuandika. Kutokana na tabia hiyo kila herufi inaweza kuonekana kwa maumbo tofautitofauti kiasi kutegemeana na mahali pake mwanzoni, katikati au mwishoni mwa neno.

Kwa kawaida maandishi ya Kiarabu ni ya konsonanti tu bila vokali. Vokali zikiandikwa zinaonekana kama mstari au nukta chini au juu ya herufi zinazoanzisha silabi.

Ipsilon

Ipsilon (pia: Ypsilon au kwa Kigiriki Ύψιλον, yaani "i fupi") ni herufi ya ishirini katika alfabeti ya Kigiriki, ikawa baadaye herufi ya ishirini na tano katika alfabeti ya Kilatini.

Asili yake ilikuwa "Waw" ya Kifinisia .

Iliandikwa kama Y ya Kiswahili lakini ilikuwa vokali, si konsonanti. Ipsilon ya Kigiriki ilitaja vokali iliyokuwa kati ya "u" na "i" (kama Kijerumani "ü"); katika Kigiriki cha kisasa ni "i" pekee.

Katika Kigiriki cha Kale ilimaanisha pia namba 400.

Waroma wa Kale waliipokea mara mbili katika alfabeti ya Kilatini:

mwanzoni katika karne za KK kupitia Kietruski kwa umbo la V lililomaanisha mara sauti ya "u" mara ya "w/v".

baada ya kuenea kwa utawala wao hadi Ugiriki katika karne ya 1 KK na kupokea maneno mengi ya Kigiriki.

J

J ni herufi ya 10 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Iota ya alfabeti ya Kigiriki.

Kicheki

Kicheki ni lugha ya Kislavoni katika familia ya lugha za Kislavoni cha Magharibi inayotumiwa nchini Ucheki. Pia kuna wasemaji takriban milioni mbili nje ya Ucheki.

Kicheki ni lugha ya karibu na Kislovakia na Kisorbi. Kinaandikwa kwa alfabeti ya Kilatini.

Wageni hushtuka mara nyingi wakiona maneno bila vokali, kwa mfano sentensi "Strč prst skrz krk". Sababu yake ni kwamba herufi za r na l zinaweza kuhesabiwa kama silabi (utaratibu unaofanana na "m" kama mwanzo wa neno mbele ya konsonanti katika lugha za Kibantu: m-fano, M-swahili).

Sarufi inapanga nomino zote katika jinsia tatu.

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Kige'ez

Kige'ez (kwa maandishi ya Kiamhari: ግዕዝ; matamshi: gē-ĕz) ni lugha ya kale ya Ethiopia iliyozungumzwa zamani za ufalme wa Aksum. Baadaye ilikuwa lugha ya kimaandishi nchini Ethiopia hadi karne ya 19 na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la orthodoksi la Ethiopia.

Huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti za kusini. Hutazamiwa kama lugha mama ya lugha za kisasa kama Kiamhari na Kitigrinya nchini Ethiopia na Eritrea.

Maandishi ya Kige'ez ni aina ya abugida yenye herufi 26 za konsonanti na 4 za vokali zinazounganishwa kuwa alama 202 kwa silabi zote zinazowezekana. Mifano ya kwanza inyojulikana ni kutoka karne ya 4 BK.

Kigeorgia

Kigeorgia (jina la wenyewe: ქართული ენა - kartuli ena) ni lugha rasmi nchini Georgia inazungumzwa na takriban watu milioni 4.5 - 5.

Ni moja kati ya lugha za Kaukazi ya Kusini ina alfabeti yake ya pekee yenye herufi 33 pamoja na 5 nyingine zisizotumika sana.

Lugha ni ya kale imepokea maneno mengi kutoka Kigiriki, Kilatini, Kiajemi, Kiarabu, Kirusi, Kituruki na Kiingereza. Ilianza kuandikwa baada ya Wageorgia kupokea Ukristo katika karne ya 4 BK.

Nje ya nchi ya Georgia lugha hii au lahaja za karibu zajadiliwa katika nchi jirani za Kaukazi, Urusi, Uturuki na Israeli walipohamia Wayhudi Wageorgia wengi.

Majina mengi ya Kigeorgia yanaishia kwa -dze ("mwana") (Georgia ya magharibi) au -shvili ("mtoto") (Georgia ya mashariki). Mifano mashuhuri ya watu wanaojulikana kimataifa ni Josef Stalin (dikteta wa Umoja wa Kisovyeti hadi 1953) na Eduard Shevardnadze (waziri wa mambo ya nje wa mwisho wa Umoja wa Kisovyeti na raisi wa Georgia hadi 2003).

Kigeorgia ina maneno mengi yanayoanza kwa konsonanti mbili, tatu au zaidi kwa mfano:

წყალი (ts'q'ali), "maji"

სწორი, (sts'ori), "sahihi"

რძე , (rdze), "maziwa"

თმა, (tma), "nywele"

მთა, (mta), "mlima"

ცხენი, (tskheni), "farasi"

Kuna maneno mengi yanayoanza kwa konsonanti 3:

თქვენ, (tkven), "ninyi"

მწვანე, (mts'vane), "kibichi"

ცხვირი, (tskhviri), "pua"

ტკბილი, (t'k'bili), "tamu"

ჩრდილოეთი, (črdiloeti), "kaskazini"

Maneno machache huanza kwa konsonanti 4:

მკვლელი, (mk'vleli), "mwuaji"

მთვრალი, (mtvrali), "mlevi"

Neno hili laanza kwa konsonanti 6:

მწვრთნელი, (mts'vrtneli), "mwalimu wa michezo"

neno hili linaanza kwa konsonanti 8:

გვბრდღვნი (gvbrdgvni), "mnatuvuta"

Kigusii

Kigusii ni lugha ya Kibantu nchini Kenya inayozungumzwa na Wakisii. Mwaka wa 2009 idadi ya wasemaji wa Kigusii imehesabiwa kuwa watu 2,205,000. Pia kuna wasemaji 300 tu nchini Tanzania. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kigusii iko katika kundi la E40. Hasa Kigusii huzungumzwa eneo la Kisii ambalo makao yake makuu ni Mji wa Kisii (kati ya Ziwa Victoria na mpaka wa Kenya-Tanzania) katika Mkoa wa Nyanza.

Kislovakia

Kislovakia ni lugha rasmi inayoongelewa nchini Slovakia, nchi iliyopo Mashariki mwa Ulaya. Ni moja kati ya Lugha za Kislavoni, mkusanyiko wa lugha unajumlisha Kirusi, Kipoland na lugha nyingine kadhaa za Mashariki ya Ulaya.

Lugha hii inafanana kabisa na Kicheki, na Wacheki na Wasovakia wanaweza kuelewana vizuri kabisa wakiwa wanazungumza lugha zao. Kipoland na Kisorbia kina fanana kabisa. Kislovakia kinazungumzwa nchini Slovakia na zaidi ya watu milioni 5.

Neno

Neno ni sehemu fupi ya lugha yenye maana. Ni sauti inayotamkwa au kuandikwa pamoja na kutaja jambo fulani.

Neno linaweza kuwa fupi lenye mofimu (yaani sauti inayowakilisha maana fulani) moja tu au kuwa ndefu lenye mofimu mbalimbali. Kwa kawaida ni muunganiko wa silabi kadhaa, zikiwemo konsonanti na vokali.

"Neno" linaweza kumaanisha neno lililosemwa au neno lililoandikwa, au wakati mwingine wazo au barua.

"Neno tata" kawaida litajumuisha mzizi na maana moja au zaidi maelezo (mwamba, nyekundu, haraka-haraka, kukimbia, kutarajia), au mizizi zaidi ya mmoja kwenye kiwanja (bodi-nyeusi, sanduku la mchanga). Maneno yanaweza kuwekwa pamoja ili kujenga vitu vikubwa vya lugha, kama vile misemo (mwamba mwekundu, kuweka juu), vifungu (nilitupa mwamba), na sentensi (Alitupa mwamba, lakini alikosa).

Leonard Bloomfield alianzisha dhana ya "Aina ndogo za Bure" mnamo 1926. Maneno hufikiriwa kama sehemu ndogo ya maana ya hotuba ambayo inaweza kusimama peke yake. Hii hulinganisha vitengo vya sauti na vitengo vya maana. Walakini, maneno mengine yaliyoandikwa si aina ya bure kabisa.

Wataalamu wanaona neno ni sehemu ya lugha yenye kituo kidogo mbele na nyuma yake, au kwa maandishi jumla ya herufi zenye maana zilizotengwa kwa nafasi nyuma na mbele.

Katika mazungumzo wakati mwingine si rahisi kutofautisha maneno kama ni maneno marefu au maneno mawili. Kwa mfano kuna maneno yaliyobuniwa juzi tu kwa kutaja mambo ya teknolojia na sayansi ambayo yanaunganisha maneno mawili kuwa moja:

garimoshi (gari + moshi) kama kifupi cha "gari la moshi" iliyokuwa kawaida zamani

mawasilianoanga (mawasiliano + anga - "telecommunication")Si wazi mara moja kwa wakilizaji wanaosikia haya mara ya kwanza kama ni neno moja au maneno mawili.

Wataalamu wa lugha hutofautiana aina za maneno kama vile nomino, kitenzi, kivumvishi, kielezi, kiunganishi kiwakilishi na kihisishi

Maneno kwa pamoja yanaunda sentensi yakifuata masharti ya sarufi katika lugha husika.

Silabi

Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambapo sauti za lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti.

Maneno kufanywa na silabi. Maneno mafupi huwa na silabi 1 pekee. Maneno mengine huwa na silabi zaidi kama 2, 3 au nyingi. Silabi fupi sana inaweza kuwa vokali 1 pekee au konsonanti 1 kama "m" katika "m-to-to".

Kama silabi inaishia kwa konsonanti inaweza kuitwa silabi iliyofungwa, kama inaishia kwa vokali inaweza kuitwa silabi wazi.

Kuna lugha zilizo na silabi nyingi zilizofungwa kama Kiingereza. Kiswahili kinapendelea silabi wazi, lakini "m" na "n" zinaweza kuwa mwishoni kwa silabi au kuwa silabi peke yao. Lugha kama Kijapani takriban hazina silabi za kufungwa.

Mifano ya maneno yenye silabi 1:

tu

naManeno mengi ya Kiswahili huwa na silabi mbili au zaidi:

ne-n-da

ku-ja

shu-le

hi-i

ma-a-na

ra-fi-ki

se-ko-n-da-ri

se-ri-ka-li

i-li-yo-fu-n-gwaKuna lugha zinazotumia mwandiko wa silabi badala ya alfabeti, kwa mfano abugida.

Vokali

Vokali ni fonimu au sauti za lugha zinazotajwa kwa herufi za A, E, I, O na U.

Kwa jumla ni sauti tupu ambako hewa huondoka mdomoni bila kikwazo au sauti za pembeni.

Herufi zote nyingine ni konsonanti kama B, D, K, L, P, S, W au Z. Kwa sauti hizo si hewa tu inayoondoka mdomoni lakini mwendo wake ni pamoja na sauti za pembeni kwa kutumia shingo, ulimi au meno.

Y

Y ni herufi ya 25 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Ipsiloni ya alfabeti ya Kigiriki.

YHWH

YHWH (yaani, “Mimi Ndimi”) ni herufi nne ambazo kwa Kiebrania zinaandikwa יהוה. Ni konsonanti zinazounda jina la Mungu lililo muhimu kuliko yote linalopatikana mara 6,828 hivi katika Biblia ya Kiebrania kuanzia Mwa 2:4.

Jina hilo halipatikani kabisa katika vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Kitabu cha Mhubiri na Kitabu cha Esta.

Wayahudi walizidi kuliheshimu jina hilo hata wakaacha kulitamka wakati wa kulikuta katika Maandiko Matakatifu; badala yake wanasoma אֲדֹנָי, Adonai, yaani Bwana.

Labda kwa sababu hiyo watafsiri wa kwanza wa Biblia kwenda lugha ya Kigiriki (LXX) walilitafsiri Κύριος, Kyurios, yaani Bwana.

Kwa kuzoea hivyo, katika kutoa madondoo ya Agano la Kale, Wakristo wa kwanza walitumia tafsiri hiyohiyo.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.