Kitabu cha Yoshua

Kitabu cha Yoshua ni cha sita kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na vya Agano la Kale katika Biblia ya Ukristo.

Kitabu hicho chenye sura 24 kinatupasha habari za uvamizi wa nchi takatifu ambao Waisraeli waliufanya chini ya Yoshua, ambaye ni mfano wa Yesu (hata jina lao kwa Kiyahudi ni moja, linalotafsiriwa “Mungu anaokoa”): ndiye aliyewaingiza watu katika nchi ya ahadi, si Musa.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

JoshuaSun Martin
Yoshua akiagiza jua lisimame juu ya bonde la Gibeon alivyochorwa na John Martin.

Mazingira

Kitabu cha Yoshua kinahusika zaidi na Waisraeli walipoteka nchi ya Kanaani na nchi hiyo ilivyogawiwa kati ya makabila yake 12.

Tangu wakati wa Ibrahimu, Mungu alikuwa ameahidi kwamba Kanaani ingekuwa mali ya Waisraeli (Mwa 13:14-17), lakini karne kadhaa zilipita mpaka Waisraeli walipokuwa taifa kubwa la kutosha kwa kuteka na kumiliki nchi hiyo.

Taifa la Israeli lilikua na kuongezeka hasa katika nchi ya Misri, na wakati ulipowadia, Musa aliwaongoza watu hao kutoka Misri kuelekea Kanaani (Kut 3:7-10; 12:40-41). Lakini watu walipofika karibu, ambapo wangeweza kuandaa mashambulio, waliwaogopa Wakanaani wakamwasi Mungu. Kwa ukaidi wao, watu walikataa kumtegemea Mungu na kuingia Kanaani, isipokuwa viongozi wawili, yaani Yoshua na Kalebu. Mungu akawaadhibu jangwani mpaka walipokufa watu wazima wote (waliokuwa na miaka 20 na kuzidi, isipokuwa Yoshua na Kalebu) na kizazi kipya kilipokuwa na nguvu ya kutosha (Hes 14:28-35).

Wakati huo, miaka 40 baada ya wazazi wao kuondoka Misri, watu wa kizazi kile kipya walikuwa tayari kuingia Kanaani. Kambi yao kubwa ilikuwa mashariki mwa Mto Yordani kukabili Yeriko (Hes 22:1). Musa alikuwa amekufa tangu muda mfupi (Kumb 34:1-5), na Yoshua alipewa jukumu la kuwaongoza Waisraeli baada ya kifo cha Musa kwenye miaka 1210-1200 hivi KK (Kum 34:9; Yos 1:1-2).

Kiongozi mpya wa Israeli

Yoshua alizaliwa na kukulia Misri, lakini miaka ya taabu huko ilimsaidia kujenga tabia, uwezo na imani ya kumtegemea Mungu ambayo siku moja itamfanya awe mtu wa maana sana katika taifa lake.

Muda mfupi baada ya Waisraeli kuondoka Misri, Yoshua alionyesha uwezo wake wa kuongoza alipokusanya kwa haraka sana jeshi dogo na kuwafukuza wachokozi Waamaleki (Kut 17:8-16).

Waisraeli walipofika Mlima Sinai, Yoshua alikuwa msaidizi maalumu wa Musa. Yeye peke yake alifuatana naye alipokwea mlima, ambapo Musa alikutana na Mungu katika wingu, lakini Yoshua alibaki nje (Kut 24:13).

Vile vile Yoshua hakutoka katika hema ambamo Musa alikutana na Mungu (Kut 33:11; taz. Hes 11:28).

Siku moja, Waisraeli walipomwasi Mungu jangwani, Yoshua alionyesha imani yake yenye ujasiri ambapo yeye na Kalebu walisimama imara kinyume cha wenzao wote (Hes 14:9).

Imani yake ya kumtegemea Mungu ilimpa uvumilivu na kumlinda asije akachukuliwa na tamaa ya ubinafsi ya kutaka makuu. Hakuwa na kijicho dhidi ya Musa kuwa kiongozi wa Israeli, bali alijaribu kumtetea watu wengine walipojaribu kushambulia daraja yake ya pekee (Hes 11:26-30).

Mungu alimchagua Yoshua awe kiongozi wa taifa baada ya Musa, lakini alionyesha wazi kwamba Yoshua asingekuwa na mamlaka kubwa sawa sawa na Musa, kwa kuwa baada ya kufa kwake, uongozi wa kiraia na ule wa kiroho ukawa juu ya watu tofauti. Tangu wakati huo kawaida ilikuwa kwamba, kiongozi wa kiraia alipata maagizo ya Mungu kwa njia ya kuhani mkuu (Hes 27:18-23).

Hata hivyo, Yoshua alikuwa mtu aliyemwelewa Mungu. Uzoefu wake kama kiongozi wa kiroho, mtawala wa kiraia na mkuu wa jeshi ulimfaa sana kuwaongoza Waisraeli katika nchi yao mpya na katika wakati mpya uliowakabili (Kumb 31:7, 14, 23; 34:9).

Mtindo wa Kitabu cha Yoshua

Kitabu cha Yoshua kimepata jina lake kutokana na mtu ambaye habari zake zimesimuliwa zaidi humo, lakini hakimtaji mwandishi wake.

Inawezekana kwamba mwandishi alipata habari kutokana na kumbukumbu ambazo Yoshua mwenyewe aliziandika (Yos 24:25-26) na vitabu vingine vya historia vya wakati ule (Yos 10:13) na ripoti za kikabila na za kitaifa kuhusu mahali, koo na matukio mbalimbali (Yos 18:8-9).

Ingawa kitabu kinaeleza utekaji wa nchi ya Kanaani, hakitoi orodha ya kinaganaga kuhusu matukio yote ya historia. Vita vya kuteka Kanaani vilichukua muda mrefu (Yos 11:18) usiopungua miaka mitano (Yos 14:7, 10), lakini mwandishi alitaja baadhi ya vita virefu katika mistari michache tu, na mambo mengine yasiyokuwa na maana sana ya kivita aliyaandika kirefu.

Sababu ya tofauti hizo katika masimulizi ni kwamba, madhumuni maalumu ya mwandishi hayakuwa kuandika kinaganaga kuhusu vita na siasa, bali alitaka kuonyesha kazi ya Mungu na watu wake. Mwandishi alikuwa mhubiri kuliko mwandishi wa ripoti na orodha mbalimbali tu. Alikuwa nabii kuliko mwandishi wa historia.

Kwa Waisraeli kazi ya kwanza ya nabii haikuwa kutabiri mambo ya usoni, bali kuwajulisha watu mapenzi ya Mungu (Isa 1:18-20; Yer 1:7,9; Amo 3:7-8; taz. Kut 4:10-16; 7:1-2). Wao waliona historia yao kama ufunuo wa matendo ya Mungu, na kwa sababu hiyo kitabu hiki na vingine kadhaa vya Biblia tunavyoviona vya historia, Waisraeli waliviita vya unabii. Waandishi wengi wa historia katika Israeli walikuwa manabii (1 Nya 29:29; 2 Nya 9:29; 12:15).

Waisraeli waligawanya vitabu vyao vya unabii katika sehemu mbili zilizoitwa Vitabu vya Unabii wa Awali (Yoshua, Waamuzi, Samweli na Vitabu vya Wafalme), na Vitabu vya Unabii wa Baadaye (kitabu cha Isaya, kitabu cha Yeremia, kitabu cha Ezekieli na vitabu 12 vya manabii wadogo). Katika vitabu vya Unabii wa Awali, Mungu alidhihirisha makusudi yake kwa njia ya historia ya Waisraeli, na kwa kweli mataifa yote yalikuwa chini ya utawala wake mkuu. Katika vitabu vya Unabii wa Baadaye, Mungu alidhihirisha makusudi yake zaidi kwa njia ya maneno ya wasemaji wake.

Kwa sababu ya namna hiyo ya pekee ya Waisraeli kutazama historia, mwandishi wa kitabu cha Yoshua hakujaribu kuorodhesha kila tukio lililotokea wakati ule, wala hakuandika katika utaratibu maalumu wa mfululizo wa matukio. Zaidi alichagua na kupanga mambo yake kadiri ya kusudi lake kuu la unabii. Alitaka kuwasaidia watu wamjue Mungu zaidi, akishughulika na matukio yale yaliyokuwa na maana kubwa katika uhusiano wa taifa na Mungu wake.

Habari za kitabu chenyewe

Mara baada ya kushika uongozi, Yoshua alituma wapelelezi nchini; huko Yeriko, mji wa zamani kuliko yote ya dunia, walisaidiwa na Rahabu, kahaba aliyeamini kuwa ushindi utakuwa wa Mungu wa Israeli (Yos 2): kwa hiyo akaokolewa pamoja na ndugu zake, tena akajaliwa kuwa bibi wa babu wa mfalme Daudi, hata akatajwa na Injili kama bibi wa Yesu Kristo (Math 1:5-6), halafu akachukuliwa kama mfano wa imani (Eb 11:31) na wa matendo mema (Yak 2:25).

Kadiri ya kitabu hicho, Yoshua aliwavusha Waisraeli pakavu kati ya mto wa Yordani (Yos 3-4) na hivyo akawaingiza katika nchi takatifu. Hapo ikawabidi kwanza wafunge tena agano na Mungu kwa kutahiriwa wanaume wote na kwa kuadhimisha Pasaka ambapo kwa mara ya kwanza walikula mazao ya nchi hiyo waliyoahidiwa: ndio mwisho wa mana na wa kipindi cha jangwani (Yos 5:1-12). Hata sisi tutaacha kula mkate toka mbinguni tutakapoingia pale tulipoahidiwa.

Baada ya matendo hayo ya kidini Mungu alimtokea Yoshua kama amiri jeshi wa Israeli ili kumhakikishia kwamba mwenyewe ataongoza mambo, hivyo Yoshua amtegemee akijisikia chombo chake tu (Yos 5:13-15). Ni rahisi kwa kila binadamu aliyeshika uongozi kujisikia mwenyewe na hivyo kuacha kumtegemea Mungu. Kumbe Yoshua kwa kupokea ujumbe huo akaweza kushinda watu wenye maboma, nguvu na silaha kali kuliko Waisraeli.

Kwamba hiyo ni nguvu ya Mungu inaonekana wazi hasa katika simulizi la kuteka Yeriko (Yos 6:1-21): huko Waisraeli walifanya maandamano ya ibada mpaka kuta za mji zikaanguka. Vita vyetu vya kiroho na vya kitume vitegemee hasa sala.

Baada ya vita vingi Yoshua akayagawia makabila 12 ya Israeli nchi yote, ikiwa ni pamoja na sehemu zilizobaki chini ya wenyeji (Yos 12:1-13:14).

Huko Shekemu aliwadai wote wachague kumtumikia YHWH au miungu mingine, akisisitiza ugumu wa kumtumikia sawasawa Mungu aliye mtakatifu na mwenye wivu kwa watu wake. Lakini wao walikubali kwa moyo wote kumtumikia Mungu tu, wakasimamisha jiwe kubwa kama kumbukumbu (Yos 24:1-28).

Kabla hajafa Yoshua akawaita Waisraeli wote ili kuwaimarisha katika imani na umoja kwa kuwakumbusha maajabu waliyotendewa na Mungu na kwa kuwahimiza wamuonyeshe shukrani (Yos 23). Kukumbuka ni jambo muhimu ili tuishi kwa imani bila ya kudanganywa na maisha yanayosahaulisha kwa urahisi mambo ya Kimungu.

Muhtasari

1:1-5:15 Kuingia Kanaani

6:1-12:24 Kuteka nchi

13:1-22:34 Kugawanya nchi

23:1-24:33 Yoshua anaaga

Viungo vya Nje

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Bible.malmesbury.arp.jpg Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Yoshua kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Agano la Kale

Agano la Kale ni mkusanyo wa vitabu vya sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo inayotumiwa na waumini wa Ukristo duniani kote. Pengine mkusanyo huu unagawanywa katika makundi kadiri ya mada au mtindo: sheria, historia, ushairi na unabii, ambayo ni tofauti kiasi na kawaida ya Tanakh ya Uyahudi wa leo.

Vitabu vyote vya Agano la Kale viliandikwa kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Kwa mujibu wa wanahistoria wa Biblia, vitabu vya Agano la Kale viliandikwa kati ya karne ya 11 KK na karne ya 1 KK.

Divai

Divai (kutoka Kifaransa du vin) ni kileo kinachotengenezwa kwa majimaji ya zabibu.

Pengine inaitwa pia: mvinyo (kutoka Kireno vinho), ingawa jina hilo linaweza kutumika kwa vileo vikali zaidi.

Inawezekana kutumia pia majimaji ya matunda mengine ili kupata kinywaji cha kufanana ingawa watu wengine hawapendi kukiita "divai".

Kitabu cha Yoshua bin Sira

Kitabu cha Yoshua bin Sira ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Mwandishi alikuwa Myahudi wa Yerusalemu aliyetunga kitabu chake kwa Kiebrania mnamo miaka 196 KK - 175 KK huko Aleksandria (Misri).

Halafu mjukuu wake alikitafsiri kwa Kigiriki akitanguliza dibaji. Wakatoliki na Waorthodoksi wanakubali kama Neno la Mungu tafsiri hiyo, si maandiko asili.

Ingawa kitabu hakionyeshi mara moja mpangilio mzuri, kwa kugusagusa mambo mbalimbali, mafundisho yake makuu ni kwamba Hekima, ambayo ni mamoja na Torati, ni sifa maalumu ya Wayahudi;

hao tu wanaweza kumfikia Mungu.

Kitabu kinatoa hasa maadili yanayofanana na yale ya Kitabu cha Mithali.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kumbukumbu la Sheria

Kumbukumbu la Sheria (pia: Kumbukumbu la Torati) ni kitabu cha tano katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na cha Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Papa Damaso I

Papa Damaso I (takriban 304 – 11 Desemba 384) alikuwa papa kuanzia mwezi wa Oktoba 366 hadi kifo chake. Jina lake la kuzaliwa pia lilikuwa Damasus.

Alimfuata Papa Liberius akafuatwa na Papa Siricius.

Mchango wake mkubwa zaidi ni kuthibitisha kanuni ya Biblia kama ilivyo hadi leo katika Kanisa Katoliki.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake ni 11 Desemba.

Rahabu

Rahabu (kwa Kiebrania רָחָב Raẖav au Rāḥāḇ, maana yake "mpana") alikuwa mwanamke wa Yeriko wakati ambapo Waisraeli, wakiongozwa na Yoshua, walivamia nchi ya Kanaani katika karne ya 13 KK.

Kitabu cha Yoshua (2:1-7) kinasimulia jinsi huyo kahaba alivyokaribisha wapelelezi wawili wa Israeli, alivyowaficha wasikamatwe na wenyeji, na alivyowadai wamuapie watamuokoa pamoja na familia yake Mungu atakawapowajalia kuteka mji huo.

Ingawa Rahabu alifanya kazi haramu akasaliti mji wake, anasifiwa na Barua kwa Waebrania (11:31) kwa imani yake iliyomuokoa na kumuingiza katika taifa la Mungu.

Pia anasifiwa na Barua ya Yakobo (2:25) kama kielelezo cha mtu anayetenda mema.

Rahabu (kwa Kigiriki Ῥαχάβ, Rakhab) anatajwa na Injili ya Mathayo (1:5) katika kitabu cha ukoo cha Yesu.

Vitabu vya Unabii wa Awali

Vitabu vya Unabii wa Awali ni vitabu 4 vya Thanak (Biblia ya Kiebrania) ambavyo katika Biblia ya Kikristo vimegawiwa na kuhesabiwa 6.

Ni kwamba Waisraeli waligawanya vitabu vyao vya unabii katika sehemu mbili zilizoitwa Vitabu vya Unabii wa Awali (Kitabu cha Yoshua, Waamuzi, Samweli na Vitabu vya Wafalme), na Vitabu vya Unabii wa Baadaye (kitabu cha Isaya, kitabu cha Yeremia, kitabu cha Ezekieli na vitabu 12 vya manabii wadogo).

Katika vitabu vya Unabii wa Awali, Mungu alidhihirisha makusudi yake kwa njia ya historia ya Waisraeli, na kwa kweli mataifa yote yalikuwa chini ya utawala wake mkuu.

Katika vitabu vya Unabii wa Baadaye, Mungu alidhihirisha makusudi yake zaidi kwa njia ya maneno ya wasemaji wake.

Vitabu vya Unabii wa Baadaye

Vitabu vya Unabii wa Baadaye ni vitabu 4 vya Thanak (Biblia ya Kiebrania) ambavyo katika Biblia ya Kikristo vimegawiwa na kuhesabiwa 15.

Ni kwamba Waisraeli waligawanya vitabu vyao vya unabii katika sehemu mbili zilizoitwa Vitabu vya Unabii wa Awali (Kitabu cha Yoshua, Waamuzi, Samweli na Vitabu vya Wafalme), na Vitabu vya Unabii wa Baadaye (kitabu cha Isaya, kitabu cha Yeremia, kitabu cha Ezekieli na vitabu 12 vya manabii wadogo).

Katika vitabu vya Unabii wa Awali, Mungu alidhihirisha makusudi yake kwa njia ya historia ya Waisraeli, na kwa kweli mataifa yote yalikuwa chini ya utawala wake mkuu.

Katika vitabu vya Unabii wa Baadaye, Mungu alidhihirisha makusudi yake zaidi kwa njia ya maneno ya wasemaji wake.

Vitabu vya Wafalme

Katika vitabu vya historia vya Tanakh (Biblia ya Kiebrania), vinavyopatikana pia katika Agano la Kale (sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo), viwili vinafuata kinaganaga habari za wafalme wote wa Israeli waliomfuata mfalme Daudi hadi mwisho wa ufalme wa Yuda.

Vitabu hivyo viwili hapo mwanzo vilikuwa kitabu kimoja, navyo vinaendelea na historia ya Israeli tangu mwisho wa Vitabu vya Samweli. Muda wote unaoelezwa katika vitabu hivi ni kama miaka 400 hivi, kuanzia miaka ya mwisho ya utawala wa Daudi mpaka watu walipopelekwa katika kifungo cha Babeli. Hivyo vinaeleza mgawanyiko wa ufalme katika sehemu mbili, historia yake na jinsi falme hizo mbili zilivyorudi nyuma na kwenda mbali na mapenzi ya Mungu.

Vitabu hivyo viwili vinapitia historia ya Israeli kuanzia mwaka 972 hadi 560 hivi K.K. vikionyesha mwenendo wa kila mfalme upande wa dini, hasa katika kutekeleza maneno ya Kumbukumbu la Torati, ya kwamba Mungu ni mmoja, hivyo hekalu lake liwe moja tu. Kwa kuwa wafalme wote wa kaskazini na karibu wale wote wa kusini walikwenda kinyume, vitabu hivyo vinaanza na ufalme imara na wa fahari ulioweza kumjengea Mungu hekalu la ajabu, kumbe vinaishia na hali mbaya na ya aibu kuliko ilivyokuwa kabla ya Musa, wafalme wakiwa wafungwa Babeli, Waisraeli wote uhamishoni na hekalu lenyewe magofu tu.

Lakini waandishi hawakusimulia hayo ili kutunza kumbukumbu za zamani kama wanavyofanya wanahistoria, bali kwa lengo la kuonyesha tena uaminifu wa Mungu, aliyezidi kutuma manabii wake hata baada ya kuona hawasikilizwi, bali wanadhulumiwa hata kuuawa. Kwa kutegemea uaminifu huo, Wayahudi waliohamishiwa Babeli waliweza kutumaini mwanzo mpya. Hasa manabii wa mwisho wa wakati huo, Yeremia na Ezekieli, waliwatia moyo kuwa Mungu atabadili mioyo yao na kufanya nao Agano Jipya.

Vitabu vya hekima

Miongoni mwa aina za vitabu vya Biblia vipo vile vinavyojulikana kama vitabu vya hekima.

Kati ya vitabu hivyo, Agano la Kale lina Methali , Kitabu cha Yobu, na Mhubiri, ingawa hata baadhi ya Zaburi na sehemu za vitabu vingine pia vinaweza kuhesabiwa kuwa ni maandiko ya hekima. Tena, kati ya Deuterokanoni, Kitabu cha Yoshua bin Sira na Kitabu cha Hekima ni vitabu vya hekima.

Upande wa Agano Jipya, ni hasa Waraka wa Yakobo ulioendeleza mtindo huo wa uandishi.

Yoshua

Yoshua ni kiongozi wa taifa la Israeli linalojulikana hasa kupitia kitabu cha sita kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na vya Agano la Kale katika Biblia ya Ukristo.

Kitabu hicho chenye sura 24 kinatupasha habari za uvamizi wa nchi takatifu ambao Waisraeli waliufanya chini ya Yoshua, ambaye ni mfano wa Yesu (hata jina lao kwa Kiyahudi ni moja, linalotafsiriwa “Mungu anaokoa”): ndiye aliyewaingiza watu katika nchi ya ahadi, si Musa.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Yoshua anaheshimiwa kama mtakatifu na Wayahudi, Wakristo na Waislamu, hasa tarehe 1 Septemba.

Yuda Iskarioti

Yuda Iskarioti (kwa Kiebrania יהודה איש־קריות), Myahudi wa karne ya 1, alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha (Injili ya Mathayo 26:14-16).

Ni tofauti na mtume mwenzake Yuda Tadei.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.