Kitabu cha Nahumu

Kitabu cha Nahumu (kwa Kiebrania נחום, Nahum) ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Nahum-prophet
Nabii Nahumu katika picha ya Waorthodoksi ya karne XVIII.

Muda

Kitarehe kinashika nafasi kati ya kile cha nabii Mika na kile cha Habakuki.

Mada

Katika kitabu hiki Nabii Nahumu anashangilia kwa ufasaha wa ushairi ujio wa maangamizi ya dola la Waashuru na ya makao yao makuu, Ninawi (612 KK): hivyo adui wa taifa na wa Mungu hatimaye ataadhibiwa.

Mtunzi

Mtunzi anadhaniwa kuwa nabii wa Yerusalemu wakati wa mfalme Yosia wa nchi ya Yuda.

Ufafanuzi

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Viungo vya nje

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Bible.malmesbury.arp.jpg Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Nahumu kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Nabii Nahumu

Nahumu (kwa Kiebrania נחום, yaani "Aliyefarijiwa na Mungu") alikuwa nabii wa Yerusalemu wakati wa mfalme Yosia aliyetawala nchi ya Yuda kati ya mwaka 640 KK na 609 KK.

Mahubiri yake yanatunzwa katika Kitabu cha Nahum ambacho ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kinashangilia kwa ufasaha wa kishairi ujio wa maangamizi ya dola la Waashuru na ya makao yao makuu, Ninawi (612 KK): hivyo adui wa taifa na wa Mungu hatimaye ataadhibiwa.

Kitarehe kinashika nafasi kati ya kile cha nabii Mika na kile cha Habakuki.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.