Kitabu cha Esta

Kitabu cha Esta (jina lake huandikwa pia Ester na "Esther") ni kitabu cha Biblia ya Kiebrania, na hivyo pia cha Agano la Kale, ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo. Kiliandikwa kwanza kwa Kiebrania.

Tafsiri ya kitabu cha Esta inavyopatikana katika Septuaginta imeongezewa sana; nyongeza hizo za Kigiriki zinahesabiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kuwa sehemu za kitabu yenye uvuvio wa Roho Mtakatifu ingawa si sehemu za hadithi asili. Ni katika nyongeza hizo tu kwamba Mungu anatajwa na mtazamo wa imani unajitokeza.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Esther Megillah Italy 1616
Gombo la kitabu cha Esta kwa Kiebrania.
Aert de Gelder 004
Esta na Mardokai, mchoro wa Aert de Gelder.

Wakati wa kuandikwa

Mwandishi wake hajulikani, lakini kufuatana na mapokeo ya Wayahudi, kitabu kiliandikwa takriban mwaka wa 400 KK, muda usio mrefu baada ya matukio kinayoyasimulia. Sababu za mwelekeo huo ni zifuatazo: Sherehe ya Purim ilikuwa husherehekewa kila mwaka wakati wa kuandikwa kwa kitabu, lakini Mfalme Ahasuero hutajwa kama mfalme aliyepita. Ukamilifu wa maelezo kuhusu mila na desturi za dola la Waajemi unadokeza kuwa kitabu kimeandikwa kabla dola hilo halijavamiwa na kuangamizwa na Iskanda Mkuu takriban mwaka wa 330 KK.

Yaliyomo

Kitabu cha Esta kinahusika na wakati wa taifa la Israeli unaojulikana kama wakati wa baada ya Uhamisho wa Babeli. Kinasimulia Wayahudi walivyoishi katika dola la Waajemi. Wayahudi hao walibaki uhamishoni badala ya kurudi kwao hata baada ya Waajemi kuangamiza utawala wa Babuloni mwaka 539 KK, ambapo Mfalme Koreshi alishinda na kuteka Babeli.

Ingawa Koreshi aliwaruhusu Wayahudi waliofungwa warudi katika nchi yao, wengi wao waliamua kubaki Babeli au Uajemi. Wao walihakikishiwa usalama na uhuru fulani katika nchi ya kifungo chao, kwa hiyo hawakutaka kukabiliana na wasiwasi na ugumu wa maisha mapya huko Yerusalemu. Pamoja na watoto wao waliendelea kuongeza mafanikio ya namna mbalimbali, lakini hawakuonyesha nia ya kuimarisha upya dini yao iwe nguvu ya kiroho katika maisha yao ya kitaifa. Hata hivyo, kadiri Wayahudi walivyoendelea kufuata sheria zao za kidini walisumbuliwa sana na wenyeji. Lakini Mungu alikuwa akiendelea bado kuwalinda watu wake, wawe wamemkubali au sivyo, asiruhusu waangamizwe.

Hivyo kitabu kinaeleza hasa jinsi Hamani, waziri mkuu wa mfalme Artashasta, alivyopanga kuwaangamiza Wayahudi wote. Wakati huohuo, malkia wa Uajemi alikuwa Esta, Myahudi. Pamoja na Mordekai, baba mlezi wake, Esta alifaulu kuzuia mipango ya Hamani. Ushindi huo wa Wayahudi ulianzisha sherehe ya Purim ambayo imekuwa sikukuu maarufu ya Wayahudi ikiadhimishwa kabla ya Pasaka.

Wataalamu wengi wanakubaliana kusema hii ni hadithi tu, si habari ilivyotokea katika historia.

Muhtasari wa sehemu ya Kiebrania

1:1-2:23 Kuinuliwa kwa Esta kuwa malkia

3:1-7:10 Mikakati ya kuwaangamiza Wayahudi

8:1-10:3 Shangwe ya Wayahudi

Viungo vya nje

Kitabu cha Esta (kadiri ya Biblia ya Kiebrania) katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Bible.malmesbury.arp.jpg Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Esta kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Agano la Kale

Agano la Kale ni mkusanyo wa vitabu vya sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo inayotumiwa na waumini wa Ukristo duniani kote. Pengine mkusanyo huu unagawanywa katika makundi kadiri ya mada au mtindo: sheria, historia, ushairi na unabii, ambayo ni tofauti kiasi na kawaida ya Tanakh ya Uyahudi wa leo.

Vitabu vyote vya Agano la Kale viliandikwa kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Kwa mujibu wa wanahistoria wa Biblia, vitabu vya Agano la Kale viliandikwa kati ya karne ya 11 KK na karne ya 1 KK.

Deuterokanoni

Vitabu vya deuterokanoni (kutoka Kigiriki "deuteros" = ya pili na "kanon" = orodha) ni maandiko ya Agano la Kale yanayotazamwa na Wakatoliki, na baadhi ya Waorthodoksi na ya Makanisa ya Kale ya Mashariki kama sehemu kamili ya Biblia.

Wayahudi na Waprotestanti wengi huviita apokrifa na kuvitazama kama vitabu vinavyostahili kuheshimiwa lakini si sawa na Biblia yenyewe.

Kitabu cha Ezra

Kitabu cha Ezra kinapatikana katika Biblia ya Kikristo katika Agano la Kale.

Kiasili kiliandikwa kwa lugha ya Kiebrania lakini kuna pia sehemu fupi za Kiaramu.

Andiko la Ezra lilitunzwa katika Biblia ya Kiebrania pamoja na Nehemia kama kitabu kimoja lakini kimegawiwa baadaye kuwa vitabu viwili ambavyo Vulgata inavitaja kama "Esdras I" na "Esdras II".

Kitabu kinasimulia habari za Wayahudi chini ya utawala wa Waajemi.

Mwaka 587 KK mfalme wa Babeli alikuwa amevamia mji wa Yerusalemu, kubomoa hekalu la Sulemani na kumaliza ufalme wa Yuda. Wakazi walipelekwa Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli. Tangu wakati huo Waisraeli kwa kawaida walijulikana kuwa Wayahudi. Lakini, kwa kuwa utengano wa Israeli haukuendelea, majina hayo mawili, pamoja na jina la Waebrania, yaliweza kutumiwa kwa watu walewale (Yer 34:9; Yn 1:19, 47; 2 Kor 11:22; Gal 2:14).

Mwaka 539 KK Waajemi chini ya mfalme Koreshi walivamia Babeli ambayo ikawa jimbo la milki ya Uajemi. Koreshi aliwaruhusu Wayahudi kadhaa warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu.

Habari hizi na zilizofuata zinasimuliwa katika vitabu vya Ezra na Nehemia.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Wamakabayo I

Kitabu cha kwanza cha Wamakabayo ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Kinasimulia jinsi Wayahudi, wakiongozwa na familia ya Wamakabayo, walivyopambana kwanza na mfalme Antioko IV (aliyejiita Antioko Epifane) halafu na Wayunani wengine katika karne ya 2 KK (175-135 KK).

Kitabu si mbali na matukio kinayoyasimulia, kwa kuwa kiliandikwa kati ya mwaka 140 KK na 130 KK kwa lugha ya Kiebrania, ingawa katika lugha hiyo asili hatuna nakala yoyote, bali tuna tafsiri ya Kigiriki tu katika Septuaginta.

Mwandishi wake hajulikani, lakini kitabu kinaonyesha alikuwa Myahudi wa Palestina, alipenda taifa na dini yake ya Uyahudi, na alijua kwa dhati masuala ya teolojia.

Mfalme huyo alijaribu kulazimisha Wayahudi kufuata utamaduni na dini ya Kiyunani, jambo ambalo lilipingwa na waamini waadilifu wakiongozwa na Matathia na wanae Yuda Mmakabayo, Yonathani Mmakabayo na Simoni Mmakabayo.

Tofauti na kitabu cha Tobiti, kitabu cha Yudith na Kitabu cha Esta, kitabu hiki kinajitahidi kusimulia taratibu za habari za historia, ingawa kinasifu ushujaa wa Wayahudi.

Mwandishi hamtaji Mungu, isipokuwa kwa kusema "mbingu"; lakini wapigania uhuru wanategemea sala. Hivyo hatimaye ushindi uliopatikana unahesabiwa ni tunda la msaada wa Mungu.

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Purim

Purim (פּוּרִים, Pûrîm, yaani bahati, kutoka neno pur, kuhusiana na Kiakadi pūru) ni sherehe ya kila mwaka ya Wayahudi.

Inaadhimishwa katika tarehe 14 ya mwezi wa Kiyahudi wa Adar, au tarehe 15 sehemu fulanifulani.

Sikukuu hiyo inafanya ukumbusho wa wokovu wa taifa la Israeli lililokabili maangamizi ya kimbari ya halaiki katika dola la Uajemi.

Kadiri ya Kitabu cha Esta, njama hiyo ilishindikana hasa kwa juhudi wa huyo Esta aliyebahatika kuwa malkia wa dola hilo wakati huo.

Taifa la Mungu

Jina Taifa la Mungu linatumika katika Biblia kumaanisha kwanza taifa la Israeli. Baadaye, Wakristo walilitumia kwa ajili yao katika Agano Jipya kama warithi wa wito wa taifa hilo kupitia Yesu Kristo na Mitume wake 12.

Vitabu vya hekima

Miongoni mwa aina za vitabu vya Biblia vipo vile vinavyojulikana kama vitabu vya hekima.

Kati ya vitabu hivyo, Agano la Kale lina Methali , Kitabu cha Yobu, na Mhubiri, ingawa hata baadhi ya Zaburi na sehemu za vitabu vingine pia vinaweza kuhesabiwa kuwa ni maandiko ya hekima. Tena, kati ya Deuterokanoni, Kitabu cha Yoshua bin Sira na Kitabu cha Hekima ni vitabu vya hekima.

Upande wa Agano Jipya, ni hasa Waraka wa Yakobo ulioendeleza mtindo huo wa uandishi.

YHWH

YHWH (yaani, “Mimi Ndimi”) ni herufi nne ambazo kwa Kiebrania zinaandikwa יהוה. Ni konsonanti zinazounda jina la Mungu lililo muhimu kuliko yote linalopatikana mara 6,828 hivi katika Biblia ya Kiebrania kuanzia Mwa 2:4.

Jina hilo halipatikani kabisa katika vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Kitabu cha Mhubiri na Kitabu cha Esta.

Wayahudi walizidi kuliheshimu jina hilo hata wakaacha kulitamka wakati wa kulikuta katika Maandiko Matakatifu; badala yake wanasoma אֲדֹנָי, Adonai, yaani Bwana.

Labda kwa sababu hiyo watafsiri wa kwanza wa Biblia kwenda lugha ya Kigiriki (LXX) walilitafsiri Κύριος, Kyurios, yaani Bwana.

Kwa kuzoea hivyo, katika kutoa madondoo ya Agano la Kale, Wakristo wa kwanza walitumia tafsiri hiyohiyo.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.