Kisiwa cha Wight

Kisiwa cha Wight kinapatikana kusini kwa Britania. Ni sehemu ya Uingereza.

Kina eneo la kilometa mraba 384 na wakazi 141,000.

England-geo-stub.png Makala hii kuhusu maeneo ya Uingereza bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kisiwa cha Wight kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Charles I wa Uingereza

Charles I (19 Novemba 1600 – 30 Januari 1649) alikuwa mfalme wa Uingereza, Uskoti na Ireland kuanzia tarehe 27 Machi 1625 hadi alipouawa.

Alishindana na bunge lililotaka kupunguza mamlaka yake, ambayo mwenyewe alifikiri alipewa na Mungu na anaweza kuitumia kadiri ya dhamiri yake.

Alizidi kuchukiwa kwa kuongeza kodi bila kibali cha bunge, kwa kuoa mwanamke Mkatoliki na kwa kuunga mkono wakleri wenye mwelekeo wa Kikatoliki kama vile Richard Montagu na William Laud, pamoja na kujaribu kulazimisha Kanisa la Uskoti kufuata taratibu za lile la Anglikana.

Hatimaye vita vilizuka dhidi yake, kwanza vita vya Maaskofu, halafu tangu mwaka 1642 Charles alipigana na mabunge ya Uingereza na Uskoti katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Aliposhindwa na kusalimu amri mwaka 1645, alikataa sharti la kukubali ufalme wa kikatiba. Kisha kutoroka mnamo Novemba 1647 alifungwa tena katika kisiwa cha Wight.

Hatimaye, chini ya utawala wa Oliver Cromwell, mnamo Januari 1649 alihukumiwa kuwa msaliti na kupewa adhabu ya kifo.

Ufalme ulifutwa ikatangazwa jamhuri (Commonwealth of England). Baadaye (1660) ufalme ulirudishwa chini ya mwanae, Charles II wa Uingereza .

Baadhi ya Waanglikana walimuona kama mfiadini na mwaka 1660 walimuingiza katika kalenda ya watakatifu kwa jina la "Mfalme Charles Mfiadini".

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.