Kilatini

Kilatini ni lugha ya kihistoria ambayo siku hizi haina tena wasemaji kama lugha ya kwanza, lakini bado hufundishwa katika shule na vyuo na hata kutumiwa kama lugha ya pili. Ilikuwa pia lugha ya kimataifa ya elimu na istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kilatini.

Kilatini kilikuwa lugha hai takriban kati ya miaka 500 KK na 600 BK na baadaye lahaja zake mbalimbali ziliendelea na kukomaa kuwa lugha za pekee zinazojulikana kama lugha za Kirumi.

Kilatini ni pia jina la mwandiko au aina ya herufi (alfabeti ya Kilatini) inayotumika kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano ukurasa huu wa Wikipedia.

Kilikuwa

Hadi leo ni

Map-Romance Language World
Ramani ya uenezaji wa lugha za Kirumi za leo zilizotokana na Kilatini

.

Kilatini ina athira kubwa katika lugha ya sayansi na elimu. Hadi leo hufundishwa mashuleni hasa Ulaya.

Kiswahili kimerithi maneno yenye asili ya Kilatini hasa kupitia Kiingereza kilichopokea karibu asilimia hamsini ya maneno yake yote kutoka Kilatini kupitia hasa Kifaransa. Maneno mengine ya Kilatini yameingia Kiswahili kupitia Kireno, Kifaransa n.k.

Kilatini huendelezwa na kukuzwa na wapenzi wa lugha. Kuna misamiati ya "Kilatini cha Kisasa" yenye maneno kwa ajili ya mitambo ya kisasa, mtandao n.k. Wikipedia ya Kilatini ilifikia makala zaidi ya 130,000 kwenye mwaka 2019.

Systema Naturae cover
Systema Naturae ni kitabu maarufu kilichoandikwa manmo 1735 kwa Kilatini na Carl Linnaeus ni msingi wa uainishaji wa kisayansi wa mimea na wanyama hadi leo

Tazama pia

Viungo vya nje

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kilatini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Alfabeti ya Kilatini

Alfabeti ya Kilatini (pia: Alfabeti ya Kirumi) inatumiwa kwa lugha nyingi duniani. Hata Kiswahili huandikwa siku hizi kwa herufi za Kilatini kama kwa mfano kwenye ukurasa huu wa wikipedia.

Baada ya Kristo

Baada ya kuzaliwa kwake Yesu Kristo (kifupi: BK) ni namna ya kutaja miaka ambayo imekuwa njia ya kuhesabu miaka inayotumika zaidi duniani.

Kila mwaka huhesabiwa kuanzia ule uliodhaniwa kuwa mwaka wa kuzaliwa kwake Yesu Kristo. Miaka iliyotangulia kuzaliwa kwake Yesu huitwa Kabla ya Kuzaliwa kwake Yesu Kristo au kifupi: KK.

Bahari ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

Familia

Familia (kutoka Kilatini "familia") ni kundi la watu wanaokaa pamoja kama baba, mama na watoto. Kikundi hiki mara yingi ni sehemu ya kundi kubwa zaidi la ukoo unaounganisha watu wenye asili katika uzazi wa pamoja.

Jenasi

Jenasi (kutoka Kigiriki Γένος genos / Kilatini genus "nasaba, ukoo, familia, aina") ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi unaopanga viumbehai (mimea, wanyama) katika vikundi kulingana na nasaba zao.

Jenasi moja huwa na spishi ndani yake. Jenasi kwa pamoja hupangwa katika familia.

Katika jina la Kisayansi la kiumbehai ni lazima kutaja jenasi. Kwa mfano paka anaitwa "Felis silvestris catus". Felis ni jina la jenasi. Jenasi huandikwa kwa herufi kubwa.

Kaizari

Kaizari ni cheo cha mfalme mkuu. Neno la Kiswahili limetokana na lugha ya Kijerumani "Kaiser", lakini asili yake ni Kilatini "Caesar".

Kanisa la Kilatini

Kanisa la Kilatini (wakati mwingine "Kanisa la Kiroma") ni moja ya madhehebu yanayounda Kanisa Katoliki. Ndiyo kubwa kuliko yote (97% za waumini wote), likiwa na Wakristo zaidi ya bilioni 1 duniani kote.

Mengine ni Makanisa Katoliki ya Mashariki (3%) yanayofuata mapokeo na hasa liturujia kama ya Waorthodoksi lakini yakiwa na ushirika kamili na Papa wa Roma ambaye ndiye mkuu wa Kanisa la Kilatini, pamoja na kwamba ni pia mkuu wa Kanisa Katoliki lote.

Jina linatokana na kwamba kwa karne nyingi lugha pekee iliyotumika katika ibada zake ilikuwa Kilatini.

Kanisa hilo lote upande wa sheria linafuata Mkusanyo wa sheria za Kanisa, kumbe upande wa liturujia wengi wa waamini wake wanafuata mapokeo ya Kanisa la Roma, lakini wengine wanafuata mapokeo ya Ambrosi wa Milano, au yale ya Lyon, Braga, Toledo na ya mashirika mbalimbali ya kitawa (k.mf. Wakartusi na Wadominiko).

Hivi karibuni waamini waliotokea madhehebu ya Anglikana wameruhusiwa kuendelea kutumia baadhi ya matini yake katika ibada wakiwa sasa ndani ya Kanisa la Kilatini.

Kigiriki

Kigiriki (pia: Kiyunani) ni lugha ya Kihindi-Kiulaya inayotumiwa hasa nchini Ugiriki. Maandishi yake yamejulikana tangu miaka 3500 iliyopita. Hakuna lugha nyingine duniani inayozungumzwa hadi leo yenye historia ndefu kuliko hii, isipokuwa Kichina.

Kigiriki ni muhimu sana kwa utamaduni wa kisasa kwa sababu ya kutoa michango mingi kwa lugha ya sayansi, teknolojia na utamaduni. Fikra nyingi muhimu zilionekana mara ya kwanza kwa Kigiriki na falsafa iliyojadiliwa na kuandikwa kwa lugha hii. Istilahi nyingi za kisayansi zimetoka katika Kigiriki.

Alfabeti ya Kigiriki ilikuwa msingi wa alfabeti nyingine mbili, za Kilatini na Kikirili, pia kwa miandiko ya abijadi kama herufi za Kiarabu au za Kiebrania. Kiswahili huandikwa leo kwa herufi za Kilatini.

Kati ya maandiko muhimu ya Kigiriki ni yale ya wanafalsafa kama Plato na Aristoteles na pia baadhi ya maandiko ya Biblia ya Kikristo (Agano Jipya pamoja na Deuterokanoni), mbali ya tafsiri ya kwanza ya Biblia ya Kiebrania maarufu kwa jina la Septuaginta (karne ya 2 KK).

Kati ya karne ya 3 KK hadi karne ya 6 BK Kigiriki kilikuwa lugha ya kimataifa katika eneo kubwa la kandokando ya bahari ya Mediteranea pamoja na Mashariki ya Kati.

Lugha imeendelea kubadilika kisarufi, kimatamshi na pia kimsamiati. Hivyo Kigiriki cha kale kimekwisha, hakizungumzwi tena na watu, lakini bado kinafundishwa katika shule na vyuo vingi, hasa Ulaya.

Leo hii katika nchi ya Ugiriki kuna lugha ya Kigiriki Kipya kinachoendela kuandikwa kwa herufi zilezile.

Liturujia ya Kilatini

Liturujia ya Kilatini ni aina ya liturujia ya Ukristo iliyoenea upande wa magharibi wa Dola la Roma ambapo ilitumika lugha ya Kilatini.

Liturujia hiyo ilistawi Ulaya magharibi na Afrika kaskazini.

Polepole liturujia ya Roma, mji mkuu wa Walatini uliotawala dola hilo, ilienea katika maeneo mengi ya Kanisa Katoliki, hasa kutokana na juhudi za makusudi za kaisari Karolo Mkuu za kuunganisha mataifa yaliyokuwa chini ya himaya yake.

Baadaye Mtaguso wa Trento ulizidi kudai Wakatoliki wa magharibi wafuate wote liturujia ya Roma, isipokuwa kama liturujia yao maalumu yaliendelea zaidi ya miaka 200.

Hivyo baadhi ya liturujia nyingine za Kilatini zimedumu mpaka leo, kama vile liturujia ya Ambrosi kandokando ya Milano (Italia), liturujia ya Kimozarabu hasa huko Toledo (Hispania), liturujia ya Braga huko Ureno na kidogo liturujia ya Lyon huko Ufaransa.

Pia baadhi ya mashirika ya kitawa yanatunza liturujia za pekee.

Liturujia ya Lyon

Liturujia ya Lyon (kwa Kilatini: ritus Lugdunensis) ni liturujia mojawapo ya Kanisa la Kilatini ambayo imeendelea kutumika katika jimbo kuu la Lyon (Ufaransa) tangu karne ya 9 hadi leo, ingawa kwa kuzidi kufifia, hasa baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano.

Mnyama

Wanyama (jina la kisayansi ni animalia na hutoka katika Kilatini) ni viumbehai wasio mmea, kuvu, bakteria, protista au arkea. Vile vile tunaweza kusema wanyama ni viumbehai wanaotegemea chakula kutoka sehemu nyingine: wao hawana uwezo wa kujitengenezea chakula chao wenyewe kupitia usanisinuru (nishati ya jua) lakini kutoka kwa viumbehai vingine ama wanyama wengine au mimea.

Kufuatana na aina ya chakula tunatofautisha hasa wanaokula mimea wanaoitwa walamani au walamea (kwa Kiingereza: herbivorous) na wanaokula nyama wanaoitwa walanyama au wagwizi (ing. carnivorous). Kuna pia walavyote (ing. omnivorous) wanaoweza kula kila kitu, ama mimea ama wanyama wengine (ing. omnivorous).

Wanyama wanahitaji oksijeni kwa kupumua.

Wanyama walio wengi hutembea yaani hubadilisha mahali wanapokaa, kwa hiyo wanahitaji milango ya maarifa.

Sayansi inayochunguza wanyama huitwa zuolojia, ambayo ni tawi la biolojia.

Aina za wanyama ni nyingi sana. Mara nyingi aina zao zinatofautishwa kama ni wanyama wenye seli nyingi (metazoa) au seli moja (protozoa) tu.

Kuna wanyama wanaoishi peke yao, katika vikundi na jamii. Mfano wa wanyama wanaoishi peke yao ni kifaru au nyoka. Wanajumuika kwa tendo la kuzaa pekee. Mfano wa wanyama wa jumuiya ni simba wanaokaa na kuwinda pamoja. Ushirikiano unasaidia kupata chakula bora. Mfano wa wanyama katika jamii ni nyuki na wadudu wengine.

Upande wa mwili hata binadamu ni mnyama na kimaumbile anahesabiwa kati ya mamalia.

Binadamu hutofautisha mara nyingi

Wanyama wa pori au wanyamapori

Wanyama wa kufugwa au Mifugo

Wanyama wa nyumbani (Wanyama-kipenzi)ingawa lugha hii hutumiwa tu kwa wanyama wakubwa zaidi, kwa kawaida wenye uti wa mgongo (kwa Kilatini: Chordata).

Namba za Kiroma

Namba za Kiroma (kwa Kiingereza: Roman numerals) ni mfumo wa tarakimu kwa kuandika namba jinsi ulivyokuwa kawaida wakati wa Roma ya Kale na katika mwandiko wa Kilatini. Mfumo huu unaendelea kutumika hadi leo kwa namba za pekee, hasa katika muundo wa orodha ambako mgawanyo ni wa ngazi mbalimbali. Ni kawaida kwa kutofautisha watu wenye jina lilelile, kwa mfano wafalme au mapapa: Malkia Elizabeth II (= wa pili) au Papa Benedikto XVI (= wa kumi na sita).

Papa

Kwa samaki anayeitwa kwa Kiswahili "papa" tazama papa (samaki)

Papa (neno la mkopo kutoka Kilatini lakini lenye asili ya Kigiriki, πάππας, pappas, jina ambalo mtoto anamuitia baba yake)ni cheo cha kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote. Cheo hicho kinategemea kile cha askofu wa Roma.

Picha

Picha (kutoka neno la Kiingereza "picture", lililotokana na Kilatini "pictura") ni taswira ya kitu fulani ambacho kimechorwa au kutumia vifaa vya elektroniki kuchukua taswira ilivyo.

Siku hizi picha zimeenea kila mahali, na wengi wanapenda sana kuzipiga ili kutunza kumbukumbu zao.

Upigaji picha umekuwa aina mojawapo ya sanaa.

Sakramenti

Sakramenti katika mapokeo na imani ya Ukristo ni ishara na chombo cha neema ya Mungu.

Jina hilo linatokana na neno la Kilatini "sacramentum" linalofanana na lile la Kigiriki "mysterion" (fumbo) .

Ni mafumbo kwa kuwa ishara ya nje (vitendo na vitu vinavyosindikizwa na maneno maalumu) zinamletea mtu neema zisizoonekana.

Wakatoliki wanasadiki zina uwezo huo bila kutegemea utakatifu au sifa nyingine ya mhudumu anayezitoa kwa mwamini. Zinatenda "ex opere operato" (kwa Kilatini "kwa tendo kutendeka").

Kwa ajili hiyo ni lazima sakramenti ziwe zimewekwa na Yesu Kristo ambaye alizikabidhi kwa Kanisa ili liendeleze kazi yake ya kutakasa binadamu wote mahali kote na nyakati zote.

Spishi

Spishi (kutoka Kilatini "species", yaani: aina, maumbile) katika biolojia ni jina la kutaja kundi la wanyama au mimea wa aina moja. Spishi ni kitengo muhimu katika uainishaji wa kisayansi.

Kwa kuhesabiwa katika spishi ileile haitoshi kama viumbe vinafanana sana, ni lazima waweze kuzaliana na kuwa na watoto ambao wanaweza kuzaa tena.

Kwa mfano, farasi na punda ni spishi mbili tofauti zinazoweza kuzaliana lakini watoto wao, wanaoitwa baghala, hawazai tena. Mbwa wote ni spishi moja, hata kama wanaonekana na maumbile tofauti kutokana na historia ya ufugaji wa kuteua sifa kadhaa tu kwa kuzaana. Lakini hata mbwa mkubwa kabisa anaweza kuzaliana na mbwa mdogo na watoto wao wanazaa tena.

Spishi za karibu hupangwa pamoja katika jenasi.

Mfano: mbwa, mbweha, mbweha wa Ethiopia na koyote wa Marekani wote ni spishi mbalimbali za jenasi inayoitwa "Canis".

Taifa

Taifa ni kundi lolote la binadamu lenye utamaduni wake maalumu na mapokeo yake katika historia ya eneo fulani. Mara nyingi umoja wake unategemea pia lugha.

Kila mojawapo lina haki ya kujitambua hivyo na kuhamasisha mshikamano kati ya watu wanaoliunda hata kujipatia uhuru wa kisiasa walau kwa kiasi fulani.

Katika Kilatini linatumika neno natio linalotokana na nasci ("kuzaliwa").

Katika ngazi ya chini tunakuta kundi linaloitwa kabila.

Tarakimu

Tarakimu (kutoka Kiarabu رقم raqm) au numerali (kutoka Kilatini numerus, kupitia Kiingereza numeral) ni alama za kimaandishi zinazotumiwa kuandika namba.

Uswisi

Uswisi ni nchi ya Ulaya isiyo na pwani katika bahari yoyote.

Imepakana na Ujerumani, Ufaransa, Italia, Austria na Liechtenstein.

Jina rasmi ni Confoederatio Helvetica (kwa Kilatini: Shirikisho la Kiswisi).

Majimbo yake 26, ambayo huitwa "kantoni", yanajitawala.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.