Kiaramu

Kiaramu ni mojawapo kati ya lugha za Kisemiti ambazo zinapangwa kati ya lugha za Afrika-Asia pamoja na Kiebrania na nyinginezo.

Inatumika tangu miaka 3,000 iliyopita. Ndiyo lugha aliyoitumia Yesu pamoja na Wayahudi wengi wa wakati wake.

Sehemu chache za Biblia ziliandikwa kwa lugha hiyo wakati ilipokuwa imeenea zaidi kwenye Mashariki ya Kati hata Kiaramu cha Kale kikawa lugha rasmi ya utawala katika Milki ya Uajemi.

Baada ya Aleksander Mkuu wasemaji wa Kiaramu walitawaliwa na watu wa ustaarabu wa Kigiriki. Katika miji mikubwa Kigiriki kilikuwa lugha kuu. Baada ya uenezaji wa Ukristo lugha hiyo iliendelea ikajulikana zaidi kama "Kisiria".

Hata baada ya uenezi wa Uislamu Kisiria kiliendelea kupanuka na vitabu vingi viliandikwa kwa lugha hiyo. Hata hivyo polepole wasemaji wengi wa Kisiria walianza kutumia Kiarabu, hasa wale waliogeukia Uislamu.

Pamoja na hayo watu 445,000 hivi wanaitumia hata leo, hasa nchini Syria, Iraq na Uturuki. Karibu wote ni Wakristo.

Viungo vya nje

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiaramu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Abati

Abati (pia "abate") ni cheo cha mkuu wa monasteri yenye wamonaki wengiwengi (kwa kawaida 12 na zaidi) hasa katika Kanisa Katoliki.

Jina linatokana na Kilatini abbas, mkoko kutoka Kiaramu אבא (Abba, yaani "baba"). Kiongozi wa monasteri ya kike anaitwa pengine abesi.

Nchini Tanzania Wabenedikto wana maabati katima monasteri za Peramiho, Ndanda, Hanga na Mvimwa.

Maabati wachache wanapewa daraja takatifu ya askofu kwa kuwa monasteri yao ina jukumu la uchungaji kwa waamini wa eneo fulani (abasia ya kijimbo), kama ilivyokuwa kwa wale wa Peramiho na Ndanda wakati wa umisionari.

Biblia ya Kiebrania

Biblia ya Kiebrania ni namna mojawapo ya kutaja vitabu vitakatifu vya Uyahudi vinavyoitwa na Wayahudi wenyewe "Tanakh". Ndivyo vinavyounda pia sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo na kuitwa na Wakristo "Agano la Kale" (vikiwa pamoja na Deuterokanoni au vikiwa peke yake).

Vitabu hivyo, vilivyoandikwa kwa Kiebrania na sehemu ndogo kwa Kiaramu, vinaheshimiwa pia na Wakristo wakiamini ya kwamba ufunuo wa vitabu hivyo ulikuwa hatua ya kwanza iliyokamilishwa baadaye na hatua ya pili au "Agano Jipya" kwa ujio wa Yesu Kristo.

Kuna madhehebu na wataalamu wanaopendelea kuviita vitabu hivyo kwa jina la Biblia ya Kiebrania ili wasisitize usawa wa vitabu vilivyofunuliwa au wasionekane wanavikosea heshima vitabu ambavyo kwa Wayahudi si jambo la "kale".

Hivyo kichwa cha Kilatini "Biblia Hebraica" limekuwa jina la kawaida kwa matoleo ya kitaalamu ya maandiko haya.

Hata hivyo majina "Agano la Kale" na "Agano Jipya" yanapatikana katika Biblia yenyewe (taz. hasa Eb 8).

Efrem wa Syria

Efrem wa Siria (kwa Kiaramu: ܐܦܪܝܡ ܣܘܪܝܝܐ, Aphrêm Sûryāyâ; kwa Kiarabu أفرام السرياني; kwa Kigiriki: Ἐφραίμ ὁ Σῦρος, Ephraim Syros; kwa Kilatini: Ephraem Syrus) (Nisibi, leo nchini Uturuki, 306 hivi - Edesa, leo nchini Uturuki, 9 Juni 373), alikuwa mtawa na shemasi, mwanateolojia na mwanashairi pamoja.

Ni maarufu hasa kwa tenzi zake nyingi ajabu kwa lugha ya Kiaramu ambazo zinatumika hadi leo katika liturujia na kutokeza imani kwa namna bora.

Ndiye mwakilishi muhimu zaidi wa Ukristo wa Kisiria.

Kisha kufa akaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu na babu wa Kanisa.

Papa Benedikto XV tarehe 5 Oktoba 1920 alimuongezea sifa ya mwalimu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Juni, siku ya kifo chake kilichotokea Edesa mwaka 373.

Hidekeli

Mto Hidekeli (Kiajemi: tigr, kar.: دجلة, dijla, kituruki/Kikurdi: dicle, Kiaramu: deqlath, Kiebrania: חידקל hidekel) ni mto wa Asia ya magharibi. Pamoja na Frati ni mto mkubwa wa Mesopotamia.

Kalivari

Kalivari au Golgotha ni mahali nje ya Yerusalemu wa zamani panaposadikiwa Yesu alisulubiwa akazikwa.

majina hayo mawili yana maana moja: mahali pa fuvu la kichwa, ambapo paliitwa kutokana na sura ya mwinuko wake.

Jina la pili ni jina la Kiaramu lilivyotoholewa katika Kigiriki (Γολγοθᾶ[ς], Golgotha[s], kutoka golgolta; kwa Kiebrania gulgōleṯ), la kwanza ni tafsiri ya Kilatini (Calvariæ Locus, kutoka ufafanuzi wa neno asili uliotolewa na wainjili Marko na Mathayo: Κρανίου Τόπος, Kraníou Tópos).

Kanisa la Asiria

Kanisa la Asiria, jina lake rasmi ni Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume la Asiria la Mashariki,(kwa Kiaramu ܥܕܬܐ ܩܕܝܫܬܐ ܘܫܠܝܚܝܬܐ ܩܬܘܠܝܩܝ ܕܡܕܢܚܐ ܕܐܬܘܪܝܐ, ʻIttā Qaddishtā w-Shlikhāitā Qattoliqi d-Madnĕkhā d-Āturāyē), ni Kanisa la Waashuru ambalo kihistoria lilikuwa na kiini chake katika Mesopotamia ya kaskazini.

Kutoka huko wamisionari wake katika milenia ya 1 walieneza Ukristo hadi China, India na Indonesia.

Matukio mbalimbali yamepunguza idadi ya waamini wake hadi kufikia sasa 400,000 hivi.

Ni kati ya Makanisa ya Kiorthodoksi ya Mashariki, lakini halina ushirika na Kanisa lingine lolote la kundi hilo wala la aina nyingine yoyote, ingawa kuna mapatano ya kiasi hasa na Kanisa Katoliki kupitia Kanisa la Wakaldayo ambalo linachanga nayo asili moja.

Linaongozwa na Patriarki wake, kwanzia mwaka 2015 Mar Gewardis III anayeishi Erbil, Iraq.

Chini yake kuna maaskofu wakuu, maaskofu, mapadri na mashemasi wanaotumikia majimbo na parokia katika nchi zote za Mashariki ya Kati na Kaukazi, India, Amerika Kaskazini, Oceania na Ulaya.

Upande wa teolojia, Kanisa hilo linafuata mafundisho yaliyotetewa na Patriarki Nestori wa Konstantinopoli hadi akatengwa na Kanisa Katoliki katika Mtaguso wa Efeso (431).

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Danieli

Kitabu cha Danieli ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh yaani Biblia ya Kiebrania ambamo kimo katika kundi la tatu na la mwisho, Ketuvim). Awali kiliandikwa katika lugha mbili: Kiebrania na Kiaramu.

Wakristo wengi wanafuata tafsiri ya Septuaginta yenye nyongeza mbalimbali kwa lugha ya Kigiriki na kukipanga kati ya vitabu vya manabii baada ya Kitabu cha Ezekieli katika Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Kitabu cha Tobiti

Kitabu cha Tobiti ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Nakala zilizopatikana katika mapango ya jumuia ya Waeseni huko Qumran zinaonyesha kuwa kitabu hicho kiliandikwa kwanza kwa Kiaramu miaka 200 KK hivi na kutafsiriwa mapema kwa Kigiriki katika Septuaginta.

Inaonekana kuwa tafsiri ya Kilatini maarufu kwa jina la Vulgata iliyofanywa na Jeromu inategemea andiko asili.

Kitabu hicho kilikubaliwa kama sehemu ya Biblia na mtaguso wa Hippo (393), mtaguso wa Carthago wa mwaka 397 na wa mwaka 419, halafu tena na Mtaguso wa Florence (1442) na Mtaguso wa Trento (1546).

Lakini hakikubaliwi na Wayahudi katika Tanakh, wala na Waprotestanti wengi.

Hadithi hiyo inahusu familia ya kabila la Naftali la taifa la Israeli katika karne ya 7 KK, baada ya uhamisho uliosababishwa na Waashuru.

Lengo lake kuu ni kufundisha maadili bora ya Wayahudi

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Liturujia ya Antiokia

Liturujia ya Antiokia, inayoitwa pia Liturujia ya Siria, ni jina la taratibu za ibada ya Wakristo ambayo ina asili yake katika mji wa Antiokia wa Siria (siku hizi umo katika mipaka ya Uturuki) ambao katika karne ya 1 ulikuwa kituo kikuu cha umisionari wa Kanisa, halafu ukawa na shule ya teolojia muhimu kama ile shindani ya Aleksandria (Misri).

Wanaotumia liturujia hiyo ni hasa Kanisa la Kiorthodoksi la Siria na madhehebu yenye uhusiano naye kihistoria (hasa matawi ya Kanisa la Kiorthodoksi la Kisiria la Malankara kutoka India), na yale yaliyotokana nalo, yakiwa pamoja na Kanisa Katoliki la Kisiria na Kanisa Katoliki la Kimalankara. Kwa kiasi kikubwa liturujia hiyo ni pia ya Kanisa la Wamaroni.

Liturujia ya Mesopotamia

Liturujia ya Mesopotamia ni liturujia maalumu yenye asili katika Mesopotamia ya kale, ambayo kimapokeo inatajwa kama imetokana na Mtume Thoma, na inatumiwa hasa na Wakristo Waashuru na Wakaldayo wa Iraq na nchi za kandokando, pamoja na Wamalabari wa India kusini, wengi wao wakiwa Wakatoliki na waliobaki Waorthodoksi wa Mashariki, ambao wote wametokana na wale waliotengwa na Mtaguso wa Efeso (431).Hata matoleo ya vitabu vya liturujia hiyo kwa kiasi kikubwa yamefanywa na Wakatoliki. Lugha yake hasa ni Kiaramu.

Masiya

Masiya (au Masiha), kutoka Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ mashiakh, maana yake Mpakwamafuta ni jina la heshima ambalo Biblia inampa mfalme au kuhani aliyewekwa wakfu kwa Mungu kwa kupakwa mafuta atende kwa niaba yake kazi ya kusaidia taifa lake hasa kwa kulikomboa.Tofauti na kawaida, Biblia inamtaja kama Masiha hata mfalme Koreshi Mkuu wa Uajemi kwa sababu Mungu alimtumia kutoa Wayahudi katika uhamisho wa Babeli na kuwaruhusu warudi Yerusalemu na kujenga upya hekaluHata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani

Mitume wa Yesu

Mtume wa Yesu Kristo (kwa Kigiriki ἀπόστολος, apóstolos, aliyetumwa), kadiri ya Agano Jipya, ni mmojawapo kati ya wale wanaume 12 ambao Yesu aliwateua mapema akawatuma kuhubiri Ufalme wa Mungu kwanza kwa taifa la Israeli, halafu kwa mataifa yote duniani.

Baada ya kifo na ufufuko wake, hao wakawa viongozi wa Kanisa ambalo hadi leo linajitambua kujengwa juu yao.

Habari zao, lakini hasa za Petro, zilianza kuandikwa na Mwinjili Luka katika kitabu cha Matendo ya Mitume, ambamo baadaye mhusika mkuu ni Mtume Paulo aliyedai kuteuliwa na Yesu Kristo baada ya kufufuka.

Msalaba wa Yesu

Msalaba wa Yesu ni msalaba ule ambao Yesu Kristo alisulubiwa juu yake huko Yerusalemu kwa amri ya Ponsyo Pilato siku ya Ijumaa, labda tarehe 7 Aprili 30 BK.

Tukio hilo, pamoja na ufufuko wa Yesu unaosadikiwa na Ukristo kutokea siku ya tatu (Jumapili ya Pasaka), ndiyo kiini cha imani ya dini hiyo mpya iliyotokana na ile ya Uyahudi.

Kwa Wakristo fumbo hilo la Pasaka ndilo kilele cha historia ya wokovu inayotangazwa na Biblia ya Kikristo.

Fumbo hilo lilisababisha kazi nyingi za sanaa ya Kikristo, hasa uchoraji na uchongaji.

Mwana wa Mungu

"Mwana wa Mungu" ni jina linalotumiwa katika dini mbalimbali ili kusisitiza uhusiano wa mtu fulani na Mungu au mmojawapo wa miungu. Kwa maana hiyo lilitumika hasa kwa ajili ya watawala.

Pengine linamaanisha viumbe vingine, kama vile malaika.

Saumu

Saumu (kutoka neno la Kiarabu صوم, sawm, linalotokana na Kiaramu ܨܘܡܐ, ṣawmā. Maana yake ni "kujikatalia", kama neno la Kiebrania tsom) ni tendo la kujinyima chakula kwa sababu za kidini, ili kuweka roho huru kutoka utawala wa mwili wake, iweze kuinuka kwa Mungu na kutafakari kwa urahisi zaidi.

Kuna pia malengo mengine ya saumu, kama vile kushikamana na mafukara.

Waashuru

Waashuru (kwa Kiaramu ܣܘܪܝܝܐ) ni kabila la Kisemiti la watu wa Mesopotamia kaskazini, ambao leo kwa kiasi kikubwa wanaishi nje ya nchi yao asili (hasa katika Iraq na Syria za leo, pamoja na maeneo madogo ya Uturuki na Iran), hasa Marekani, Ulaya Magharibi na Australia.Kwa jumla duniani kote wanakadiriwa kuwa kati ya milioni 2 na 4.25. Wengi wao ni Wakristo (hasa Kanisa Katoliki la Wakaldayo na Kanisa la Waashuru la Mashariki), na kwa sababu hiyo wamedhulumiwa na watawala mbalimbali kwa karibu miaka 2000 mfululizo.Waashuru wana historia tukufu upande wa ustaarabu na siasa kwa kuwa walirithi na kueneza utamaduni wa Wasumeri na Waakadi ambao ndio wa kwanza duniani katika mambo mengi.

Hasa dola la Ashuru lilistawi kati ya karne ya 24 KK na karne ya 7 KK liliposhindwa na Wakaldayo wa Babuloni (605 KK).

Biblia inazungumzia mara nyingi habari za dola hilo lililokuwa tishio kwa Waisraeli na mataifa mengi ya Mashariki ya Kati kwa muda mrefu.

Yesu

Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).

Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.

Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).

Yosefu Flavius

Yosefu Flavius (jina la awali יוסף בן מתתיהו, Yosef bin Matityahu, 37-100 BK) alikuwa kuhani Myahudi mwenye kujua Kiaramu, Kiebrania na Kigiriki, aliyejipatia umaarufu kama mwanahistoria.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.