Kiarabu

Kiarabu (ar.: العَرَبِيَّة‎‎, al-ʻarabiyyah, kwa kirefu al-luġatu al-ʿarabiyya ) ni lugha ya Kisemiti inayotumiwa na watu milioni 206 kama lugha ya kwanza[1] na milioni 246 wa ziada kama lugha ya pili. Ilhali kuna lahaja nyingi, Kiarabu sanifu (ar. الفصحى fuṣḥā) ni lugha rasmi ya nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ya Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa. Kuna pia matumizi kama lugha ya kidini katika Uislamu.

Hivyo Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani ikisomwa kwa viwango tofauti na mamilioni ya waumini Waislamu wakielekea kujifunza na kuelewa kitabu cha Korani. Kama lugha ya kidini ina athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofautitofauti walio Waislamu.

Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno), ufasaha mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau.

Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo, mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafudhi.

Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isitetereke wala kubadilika na kupotea kama lugha nyingine nyingi, leo, baada ya miaka zaidi ya elfu, imebaki thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoandikwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbalimbali zinazotumika na Waarabu wa sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi hayo yaendelee kufahamika milele.

Leo, Kiarabu ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina, Kihindi, Kihispania, Kiingereza na Kibengali.

Umuhimu wa lugha hii unazidi kukua kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Afrika, Asia na Ulaya) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini).

Arabic speaking world
Ramani inaonyesha nchi ambako Kiarabu ni lugha rasmi pekee (kijani) au lugha rasmi pamoja na lugha nyingine (buluu).
Arabic Text
"al-`arabiyya" - "Kiarabu"

Asili ya lugha ya Kiarabu

Kiarabu, pamoja na lugha ya Kiebrania (ya Uyahudi) na Kiaramu (ya Mashariki ya Kati) na Kiamhari (ya Ethiopia) zinatokana na asili moja ya lugha ya Kisemiti. Kuna lugha nyingi vile vile ambazo zinatokana na asili hii, kama Kiashuri, Kifinisia, Kibabili na kadhalika. Baadhi ya hizi lugha zimekufa au kuwa na wazungumzaji wachache, na kwa hiyo umuhimu wake umekuwa si mkubwa kama ulivyo umuhimu wa lugha ya Kiarabu.

Aina za Kiarabu

Kuna aina tatu kubwa za lugha hii ya Kiarabu:

 • Kiarabu Fasihi ambacho kilikuwa kikitumika zama za Ujahili kabla ya kuja Uislamu, na kuendelea kutumika baada ya kuja Uislamu katika Qurani na Sunnah za Mtume Muhammad,
 • Kiarabu Mamboleo ambacho kinatumika katika maandishi na mazungumzo rasmi baina ya Waarabu wote kwa jumla, na
 • Kiarabu Lahaja ambacho kinatumika na watu maalumu katika sehemu fulani za nchi au vijiji, na ni lugha ya mahali tu, kama vile Kiyemeni au Kimasri au Kishami au Kimaghribi, na lugha hizi au lahaja hizi zinakuwa zinatofautiana sana baina yake katika misamiati na matumizi.

Kiarabu fasihi

Kiarabu ni lugha ya zamani sana (tarehe yake inarudi nyuma zaidi ya miaka 2000), nayo pamoja na lugha nyinginezo za Kisemiti zilikuwa zikitumika katika nchi za Mashariki ya Kati. Kiarabu Fasihi ilianza kuwa na nguvu zaidi baada ya kuteremshwa Qurani kwa lugha hiyo na kuhifadhiwa Hadithi za Mtume Muhammad na kuwa ndio chanzo cha lugha zote nyinginezo za Kiarabu zilizokuweko wakati huo.

Fasihi ya Kiarabu isiyo na tabia ya kidini ilikuwa hasa Ushairi. Washairi kama Abu Nuwas, Omar Khayyam, Hafiz, ibn Qayyim al-Jawziyyah wanakumbukwa hadi leo. Masimulizi kama Alfu Lela U Lela hayakuwa fasihi yenyewe, hata kama yamepata umaarufu katika nchi za Ulaya.

Maandishi mengine ya Kiarabu yaliyokuwa muhimu sana ni maandiko ya falsafa na sayansi. Waarabu walitafsiri maandiko ya Wagiriki wa Kale wakaendeleza ujuzi wao. Katika karne zilizopita Ulaya ilipokea sehemu kubwa ya elimu yake kutoka kwa Waarabu kwa njia hiyo.

Tangu karne ya 19 na katika karne ya 20 fasihi ya Kiarabu imepata uamsho mkuu. Khalil Jibran wa Lebanon yuko kati ya washairi wanaosomwa zaidi kimataifa. Nagib Mahfuz wa Misri ni mwandishi Mwarabu wa kwanza aliyepokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 1988.

Viungo vya nje

  Algeria

  Algeria (pia: Aljeria ; kwa Kiarabu: الجزائر al-Jazā’ir; kwa Kiberber: Dzayer, ⴷⵣⴰⵢⴻⵔ) au kwa jina rasmi "Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Algeria" ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na bahari ya Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger, Libya na Tunisia.

  Algeria ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa la Sahara.

  Jina la nchi limetokana na mji mkuu unaoitwa kwa jina lilelile "al-jaza-ir" kama nchi ya leo kwa lugha ya Kiarabu.

  Bahari ya Mediteranea

  Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

  Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

  Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

  Falme za Kiarabu

  Falme za Kiarabu (kwa Kiarabu: الإمارات العربيّة المتّحدة; kwa Kiingereza United Arab Emirates) ni shirikisho la emirati au falme ndogo 7 katika kaskazini-mashariki ya Rasi ya Uarabuni kwenye mwambao wa ghuba ya Uajemi.

  Shirikisho limepakana na Saudia na Omani kwenye nchi kavu; baharini kuna mipaka pia na Katar na Iran.

  Mji mkuu ni Abu Dhabi na mji mkubwa ni Dubai.

  Israel

  Kwa maana mbalimbali za jina Israeli katika Biblia tazama Israeli (maana)

  Israel (kwa Kiebrania: מדינת ישראל - Medinat Yisra'el; kwa Kiarabu: دَوْلَةْ إِسْرَائِيل - dawlat Isrā'īl) ni nchi ya Mashariki ya Kati kwenye mwambao wa mashariki wa Mediteranea.

  Imepakana na Lebanon, Syria, Yordani, Misri na maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya serikali ya Palestina.

  Kaskazini

  Kaskazini ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni ncha ya kaskazini ya dunia. Kinyume chake ni kusini.

  Jina "kaskazini" limetokana na neno la Kiarabu "قيظ qiz" joto na "قيظ قائظ qiz qaez" hali ya hewa lenye joto sana; kutoka sehemu za Zanzibar au Uswahilini kwenda kaskazini kuelekea Somalia joto linaongezeka sana; upepo wa joto latokea huko.

  Kaskazini kawaida huwa juu zaidi kwenye ramani. Kanada ipo kaskazini mwa nchi ya Marekani, Venezuela ipo kaskazini mwa nchi ya Brazil, na Urusi ipo kaskazini mwa nchi ya India. Ncha ya kaskazini ni kaskazini ya mbali unayoweza kwenda.

  Kiswahili

  Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu (30%), lakini sasa ya Kiingereza pia (10%), inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki.

  Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika kufundishia shuleni na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya.

  Magharibi

  Magharibi ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande wa machweo ya jua.

  Magahribi ni pia neno la kutaja saa ya sala ya jioni ya Waislamu na sala hii yenyewe.

  Jina "magharibi" limetokana na neno la Kiarabu مَغْرِب maghrib linalomaanisha sehemu upande wa machweo.

  Magharibi kawaida huwa upande wa kushoto kwenye ramani. Tanzania iko upande mwa magharibi ya Bahari Hindi, Burundi iko upande wa magharibi ya Tanzania, na nchi ya Malawi iko upande mwa magharibi ya Msumbiji.

  Kwa maana ya kiutamaduni kuna uzoefu kutaja utamaduni wa Ulaya pamoja na Marekani (ambayo ni mtoto wa utamaduni wa Ulaya) kama "magharibi", kinyume chake ni "mashariki" kwa maana ya Asia.

  Wakati wa vita baridi magharibi ilikuwa kifupi cha nchi za kibepari zilizofuata mtindo wa demokrasia kinyume na mashariki iliyomaanisha nchi za kikomunisti.

  Mashariki

  Mashariki ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande jua linapochomoza asubuhi.

  Jina "mashariki" limetokana na neno la Kiarabu مشرق mashriq linalomaanisha "mahali jua linapokucha".

  Mashariki kawaida huwa upande wa kulia kwenye ramani. Tanzania ipo mashariki mwa nchi za Kongo, Rwanda na Burundi. Bahari Hindi huwa upande mwa mashariki ya Tanzania na Kenya. Hakuna mwisho wa kuelekea mashariki hadi umezunguka dunia yote.

  Kundi la nchi za Asia magharibi mara nyingi huitwa "Mashariki ya Kati" ambayo ni uzoefu kutoka mtazamo wa Ulaya.

  Majengo ya makanisa mara nyingi hujengwa kutazama upande wa mashariki kwa kukumbuka kufufuka kwa Yesu kulikotokea wakati wa kucha; kwa hiyo altari ya kanisa huwekwa upande wa mashariki wa kanisa na waumini huangalia upande huu.

  Mbili

  Mbili ni namba ambayo inafuata moja na kutangulia tatu. Kwa kawaida inaandikwa 2 lakini II kwa namba za Kiroma na ٢ kwa zile za Kiarabu.

  Misri

  Misri (kwa Kiarabu: مصر, Masr) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Mashariki ikiwa na eneo la Rasi ya Sinai kwenye bara la Asia pia.

  Ni nchi yenye wakazi milioni 90 na mji mkuu Kairo ni kati ya miji mikubwa zaidi duniani.

  Ni kati ya nchi za dunia zenye historia ndefu inayojulikana.

  Mkoa wa Mardin

  Mkoa wa Mardin (Kisyria: ܡܶܪܕܺܝܢ "Merdin" kwa kuhusina na lugha ya Kisemiti Kiarabu: ماردين , Mardīn au "Merdin" ) ni jina la mkoa uliopo nchini Uturuki, wenye wakazi takriban 745 778. Awali idadi ya wakazi ilikuwa 835,173 kunako mwaka wa 2000.

  Mkoa wa Şanlıurfa

  Şanlıurfa (Kisyria: Urhoy, [Kituruki]: urfa, [Kiarabu]: ar-Rûha) ni jina la mkoa uliopo kusini-mashariki ya Anatolia huko nchini Uturuki. Jiji la Şanlıurfa ndiyo mji mkuu wa mkoa ambalo limezaliwa kwa kutokana na ji la mkoa wenyewe. Idadi ya wakazi ni 1,700,352 (makadirio ya 2006).

  Moja

  Moja ni namba ya kwanza na inafuatwa na mbili. Kabla yake kuna sifuri tu. Kwa kawaida inaandikwa 1 lakini I kwa namba za Kiroma na ١ kwa zile za Kiarabu. Namba yoyote ikizidishwa kwa moja inabaki ileile.

  Nile Nyeupe

  Nile Nyeupe (kwa Kiingereza: White Nile; kwa Kiarabu: النيل الأبيض, an-nīl al-'abyaḍ) ni mto wa Afrika, moja kati ya matawimto makuu ya Nile; la pili linaitwa Nile ya Buluu. Majina hayo yanatokana na rangi ya maji inayosababishwa na udongo uliomo.Kwa usahihi, "Nile Nyeupe" ni mto unaopatikana katika Ziwa No, inapokutana mito Bahr al Jabal na Bahr el Ghazal. Kwa maana pana ni mikondo yote inayotokana na Ziwa Viktoria hadi kuungana na Nile ya Buluu. These Mikondo hiyo inaitwa "Nile ya Viktoria" (kupitia Ziwa Kyoga hadi Ziwa Albert), "Nile ya Albert" (hadi mpaka wa Sudan Kusini) halafu "Nile ya mlimani" au "Bahr-al-Jabal" (hadi Ziwa No). "Nile Nyeupe" inamaanisha pengine hata vyanzo vya Ziwa Viktoria.

  Nne

  Nne (pia: aruba kutoka Kiarabu) ni namba ambayo inafuata tatu na kutangulia tano. Kwa kawaida inaandikwa 4 lakini IV kwa namba za Kiroma na ٤ kwa zile za Kiarabu.

  Vigawo vyake vya namba tasa ni: 2 x 2.

  Somalia

  Somalia, (kwa Kisomali: Soomaaliya; kwa Kiarabu: الصومال, As-Suumaal), ambayo inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Shirikisho ya Somalia, ni nchi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki katika Pembe ya Afrika.

  Kijiografia, imezungukwa upande wa kaskazini-mashariki na Ethiopia na Jibuti, na upande wa magharibi ya kati na Kenya; Ghuba ya Aden nayo iko mashariki.

  Mji mkuu na mji mkubwa zaidi ni Mogadishu (wakazi 2,120,000).

  Tarakimu

  Tarakimu (kutoka Kiarabu رقم raqm) au numerali (kutoka Kilatini numerus, kupitia Kiingereza numeral) ni alama za kimaandishi zinazotumiwa kuandika namba.

  Tunisia

  Tunisia (kirefu Jamhuri ya Tunisia - kwa Kiarabu الجمهرية التونسية, al-Jumhūrīya at-Tūnisīya) ni nchi ya Afrika ya Kaskazini inayopakana na Bahari ya Mediteranea, Libya na Algeria.

  Mji mkuu ni Tunis (wakazi 728 453) ulioko mahali pa Karthago ya kale.

  Wilaya

  Wilaya ni mgawanyo wa kiutawala au eneo lililotengwa kwa ajili ya utawala. Mikoa ya Tanzania na Kenya imegawiwa kwa wilaya.

  Asili ya neno ni Kiarabu "ولاية" (wilaayatun - Kituruki: vilayet). Katika Dola la Osmani "vilayet" ilikuwa ngazi ya kwanza ya mgawanyo wa kiutawala ikimaanisha jimbo au mkoa. Mkuu wake au gavana alikuwa na cheo cha "Wali". Neno hili la "wilaya" limepatikana katika nchi nyingi zilizoathiriwa na utamaduni wa Uislamu au lugha ya Kiarabu kama vile Uturuki, Algeria, Tunisia, Oman, Mauritania, Sudan, Malaysia, Indonesia, Afghanistan, Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan.

  Katika Kiarabu cha Kisasa "wilaayatun" inamaanisha pia dola ndani ya shirikisho - kwa mfano madola kama vile Texas ndani ya Marekani.

  Katika matumizi ya Kiswahili huko Kenya na Tanzania "wilaya" imekuwa mgawanyo wa ngazi ya pili yaani ni kitengo chini ya ngazi ya kwanza ya mikoa. Vitengo vya wilaya ni tarafa. Na vitengo vya tarafa ni kata zinazoitwa shehia katika Zanzibar na chini yake vijiji au mitaa.

  Algeria ni nchi nyingine ambako wilaya inamaanisha ngazi ya pili ya kiutawala.

  Lugha zingine

  This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
  Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
  Images, videos and audio are available under their respective licenses.