Kiamhari

Kiamhari ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa nchini Ethiopia.

Chart of Amharic fidels[1][2]
[ə] u i a e [ɨ] o
p
t
k
x
b
d
g
p’
t’
tʃ’
k’
ʔ
s’
f
s
ʃ
h
z
ʒ
m
n
ɲ
w
l
j
r

Viungo vya nje

Tanbihi

  1. (1996) "Ethiopic Writing", The World's Writing Systems. Oxford University Press, Inc, 573. ISBN 978-0-19-507993-7.
  2. Principles and Specification for Mnemonic Ethiopic Keyboards. Iliwekwa mnamo 25 March 2016.
Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiamhari kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi cha Watu wa Ethiopia

Chama cha Mapinduzi cha Kidemokrasi cha Watu wa Ethiopia (Kiamhari: የኢትዮጵያ ሕዝቦች አብዮታዊ ዲሞክራሲያዊ ግንባር Yä-Ityopya Həzbočč Abyotawi Demokrasiyawi Gənbar, kifupi Ih'adeg, Ing: Ethiopian People's Revolutionary Democratic Front; EPRDF) ni chama cha kisiasa ambacho ni chama tawala cha Ethiopia tangu mapinduzi ya 1991.

Chama hiki ni maungano ya vyama 4 vya kieneo ambayo ni Umoja wa Kidemokrasia wa Watu wa Oromo (Oromo Peoples' Democratic Organization), Harakati ya Kidemokrasia ya Kitaifa ya Amhara (Amhara National Democratic Movement), South Ethiopian Peoples' Democratic Front na Tigrayan Peoples' Liberation Front.

Kiongozi wa chama hiki alikuwa Meles Zenawi aliyeendelea kuwa kiongozi wa kitaifa wa Ethiopia tangu ushindi wa mapinduzi.

EPRDF ilishinda kila uchaguzi tangu 1991. Wapinzani wanadai ya kwamba chama kilitumia mbinu zisizo halali na kubadilisha matokeo ya kweli mara kwa mara pamoja kupeleka wapinzani wengi gerezani.

Tangu uchaguzi wa mwaka 2010 EPRDF imeshika nafasi 499 katika jumla la wabunge 546.

Dire Dawa

Dire Dawa (kwa Kiamhari: ድሬ ዳዋ) ni mji nchini Ethiopia. Ina cheo cha mji wa kujitawala (ras gez astedader) kama jimbo la Ethiopia.

Idadi ya wakazi wake ni takriban 607,321.

Habari

Habari (kutoka Kiarabu) ni mawasiliano ya maarifa kuhusu matukio ambayo huwasilishwa kwa watu kwa maneno ya kinywa, kwa maandishi kama vile magazeti, kwa matangazo ya masafa marefu kama vile redio au runinga, kwa intaneti n.k.

Neno hili linaweza kutumiwa pia katika sayansi kwa mawasiliano ya habari (kwa Kiingereza information, si news) kati ya seli za mwili, kwa mfano kati ya mkono na ubongo, kwa njia ya neva.

Israel

Kwa maana mbalimbali za jina Israeli katika Biblia tazama Israeli (maana)

Israel (kwa Kiebrania: מדינת ישראל - Medinat Yisra'el; kwa Kiarabu: دَوْلَةْ إِسْرَائِيل - dawlat Isrā'īl) ni nchi ya Mashariki ya Kati kwenye mwambao wa mashariki wa Mediteranea.

Imepakana na Lebanon, Syria, Yordani, Misri na maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya serikali ya Palestina.

Jimbo la Afar

Jimbo la Afar (kwa Kiamhari: አፋር) ni moja ya majimbo 11 ya kujitawala ya Ethiopia.

Idadi ya wakazi wake ni takriban 1.389.004.

Makao makuu ni Asayita.

Jimbo la Amhara

Jimbo la Amhara (kwa Kiamhari: አማራ) ni moja ya majimbo kumi na moja ya kujitawala ya Ethiopia, inayojumuisha hasa watu wa kabila la Waamhara. Hapo awali ulijulikana kama Jimbo 3.

Makao makuu yake ni Bahir Dar.

Ziwa kubwa la Ethiopia, Ziwa Tana, liko katika Amhara, na vilevile Mbuga ya Milima Semien, ambayo inajumuisha mlima wa juu nchini Ethiopia, Ras Dashan.

Katika uongozi wa kifalme, Amhara ilikuwa imegawanywa katika mikoa kadhaa (kama Gondar, Gojjam, Begemder na mabadiliko), ambayo ilikuwa ilitawala kwa Ras au Negus mwenyeji. Jimbo la Amhara ilichukua mikoa ya zamani Begemder, Gojjam, na Wollo mwaka 1995.

Jimbo la Benishangul-Gumuz

Jimbo la Benishangul-Gumuz (kwa Kiamhari: ቤንሻንጉል-ጉምዝ) ni moja ya majimbo 11 ya kujitawala ya Ethiopia.

Idadi ya wakazi wake ni takriban 625.000.

Makao makuu ni Asosa.

Jimbo la Gambela

Jimbo la Gambela (kwa Kiamhari: ጋምቤላ) ni moja ya majimbo 11 ya kujitawala ya Ethiopia.

Idadi ya wakazi wake ni takriban 247.000.

Makao makuu ni Gambela.

Jimbo la Harar

Jimbo la Harar (kwa Kiamhari: :ሐረሪ) ni moja ya majimbo 11 ya kujitawala ya Ethiopia.

Idadi ya wakazi wake ni takriban 1.389.004.

Makao makuu ni Harar.

Jimbo la Mataifa ya Kusini, Ethiopia

Jimbo la Mataifa ya Kusini (Kiamhari: ደቡብ ብሔሮች ብሔረሰቦችና ሕዝቦች, Ye-Debub Bəheročč Bəheresebočč-ənna Həzbočč, Ing. "Southern Nations, Nationalities, and Peoples’ Region" SNNPR) ni moja ya majimbo 9 ya kujitawala ya Ethiopia.

Mji mkuu wa jimbo ni Awassa.Jimbo liko katika kusini ya nchi likipakana na Kenya upande wa kusini, Sudan upande wa magharibi na majimbo ya Ethiopia ya Gambela upande wa kaskazini na Oromia upande wa kaskazini, mashariki na kusini-mashariki.

Tofauti na majimbo mengine ya Ethiopia yenye kabila au kundi 1 hasa hapa kuna vikundi vingi vidogo-vidogo kwa jumla 45. Wakazi wengi huishi mashambani ama vijijini au kama wahamiaji katika makambi yao ya kuhama.

Kalenda ya Ethiopia

Kalenda ya Ethiopia (Kiamhari: የኢትዮጵያ ዘመን አቆጣጠር ye'Ityoṗṗya zemen aḳoṭaṭer) ni kalenda rasmi nchini Ethiopia na pia kalenda inayotumiwa na Wakristo walio wengi nchini Eritrea. Asili yake ni kalenda ya Wakopti kwa sababu kanisa la Ethiopia kwa karne nyingi ilikuwa kama mkono wa kanisa la Kikopti la Misri.

Kiarabu

Kiarabu (ar.: العَرَبِيَّة‎‎, al-ʻarabiyyah, kwa kirefu al-luġatu al-ʿarabiyya ) ni lugha ya Kisemiti inayotumiwa na watu milioni 206 kama lugha ya kwanza na milioni 246 wa ziada kama lugha ya pili. Ilhali kuna lahaja nyingi, Kiarabu sanifu (ar. الفصحى fuṣḥā) ni lugha rasmi ya nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ya Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa. Kuna pia matumizi kama lugha ya kidini katika Uislamu.

Hivyo Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani ikisomwa kwa viwango tofauti na mamilioni ya waumini Waislamu wakielekea kujifunza na kuelewa kitabu cha Korani. Kama lugha ya kidini ina athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofautitofauti walio Waislamu.

Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno), ufasaha mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau.

Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo, mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafudhi.

Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isitetereke wala kubadilika na kupotea kama lugha nyingine nyingi, leo, baada ya miaka zaidi ya elfu, imebaki thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoandikwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbalimbali zinazotumika na Waarabu wa sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi hayo yaendelee kufahamika milele.

Leo, Kiarabu ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina, Kihindi, Kihispania, Kiingereza na Kibengali.

Umuhimu wa lugha hii unazidi kukua kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Afrika, Asia na Ulaya) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini).

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Kige'ez

Kige'ez (kwa maandishi ya Kiamhari: ግዕዝ; matamshi: gē-ĕz) ni lugha ya kale ya Ethiopia iliyozungumzwa zamani za ufalme wa Aksum. Baadaye ilikuwa lugha ya kimaandishi nchini Ethiopia hadi karne ya 19 na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la orthodoksi la Ethiopia.

Huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti za kusini. Hutazamiwa kama lugha mama ya lugha za kisasa kama Kiamhari na Kitigrinya nchini Ethiopia na Eritrea.

Maandishi ya Kige'ez ni aina ya abugida yenye herufi 26 za konsonanti na 4 za vokali zinazounganishwa kuwa alama 202 kwa silabi zote zinazowezekana. Mifano ya kwanza inyojulikana ni kutoka karne ya 4 BK.

Kitigrinya

Kitigrinya (pia: Kitigray, Kitigre, Kihabesha) ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa katika Ethiopia (hasa jimbo la Tigray) na Eritrea.

Idadi ya wasemaji ni takriban milioni 5-6. Maandishi yake ni kwa alfabeti ya Kiethiopia. Kitigrinya kimetoka katika lugha ya kale ya Ge'ez iliyokuwa lugha ya nyanda za juu za Ethiopia na hadi leo ni lugha ya liturgia katika kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na Eritrea.

Katika Ethiopia Kitigrinya ni lugha ya tatu inayotumiwa na watu wengi (baada ya Kioromo na Kiamhari). Katika Eritrea ni lugha inayotumiwa zaidi kabisa.

Kitigrinya ( ትግርኛ, tigriññā), pia huandikwa Tigrigna, Tigrina, Tigriña, ni lugha ya pili ambayo huzungumza na watu wa jamii ya Tigray katikati mwa jimbo la Eritrea ambapo lugha hii ni moja kati ya lugha mbili muhimu katika watu wa Eritrea na katika jimbo ya Tigray, nchini Ethiopia. Wazungumzaji wa lugha hii huitwa Watigray ambapo lugha hii kutumika kama lugha maalum miongoni mwao na pia katika vijisehemu vya wahamiaji katika maeneo haya ikiwa ni pamoja na watu wa jamii ya Beta Israel ambao kwa huishi nchini Israeli.

Lugha hii mara nyingi huchanganywa na lugha nyingine ambazo kwa namna fulani hufanana nazo hasa katika matamshi kwa mfano lugha ya Kitigre ambayo lugha hii hutumika katika maeneo ya ukanda wa chini wa Eritrea, hasa kwa upande wa Kaskazini na Magharibi mwa mjii huu ambapo lugha hii hutumika.

Ludwig Krapf

Johann Ludwig Krapf (11 Januari 1810 – 26 Novemba 1881) alikuwa mmisionari wa kwanza wa Uprotestanti nchini Kenya katika karne ya 19 akatunga kamusi ya kwanza ya lugha ya Kiswahili.

Lugha za Kisemiti

Lugha za Kisemiti ni kundi la lugha zinazozungumzwa na watu milioni 300 hivi katika Asia ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini na Afrika ya Mashariki. Zinahesabiwa kama tawi la lugha za Kiafrika-Kiasia.

Ziwa Chew Bahir

Ziwa Chew Bahir (kwa Kiamhari: ጨው ባሕር č̣ew bāhir, "Ziwa ya Chumvi") au Ziwa Istifanos, Stefanie, Basso Naebor na Chuwaha, ni ziwa la Ethiopia kusini, ambalo likijaa linaenea hadi kaskazini mwa Kenya.

Liko mita 573 juu ya usawa wa bahari.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.