Kenda

Kenda ni Kiswahili asilia kwa namba 9. Kwa kawaida inaandikwa 9 lakini IX kwa namba za Kiroma na ٩ kwa zile za Kiarabu.

Vigawo vyake vya namba tasa ni: 3 x 3.

Neno hili ni la asili ya Kibantu. Siku hizi neno "tisa" ambalo ni neno lenye asili ya Kiarabu hutumiwa zaidi kutaja namba 9, pamoja na tisini (tisa mara kumi).

Kamusi za mwanzo na katikati ya karne ya 20 kama M-J SSE zinasema ya kwamba "kenda" iliwahi kutumiwa sawa na "tisa".

Siku hizi matumizi yake imepungua sana.

Mfano wa matumizi yake ni katika jina Mijikenda linalotaja kundi la makabila au koo 9 za Kenya.

Evo9glyph
Mabadiliko katika kuandika tisa.

Marejeo

  • Cecil Balmond, "Number 9, the search for the sigma code" 1998, Prestel 2008, ISBN 3-7913-1933-7, ISBN 978-3-7913-1933-9
E-to-the-i-pi.svg Makala hii kuhusu mambo ya hisabati bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kenda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Arubaini na tisa

Arubaini na tisa au tisa na arubaini au arobaini na tisa au arobaini na kenda ni namba inayoandikwa 49 kwa tarakimu za kawaida na XLIX kwa zile za Kirumi.

Ni namba asilia inayofuata 48 na kutangulia 50.

Vigawo vyake vya namba tasa ni: 7 x 7.

Eneo Bunge la Marakwet East

Marakwet East ni eneo bunge la uchaguzi nchini Kenya. Ni mojawapo wa maeneo bunge mawili katika Wilaya ya Marakwet. Eneo bunge hili lina wadi kumi na moja, zote ambazo huchagua madiwqani katika Baraza la Mji wa Marakwet. Eneo Bunge hili lilianzishwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka wa 1992 likijulikana kama eneo bunge la Kerio East , na kubadilishwa hadi muundu wake wa sasa kwenye uchaguzi wa 1997.

Hamsini na tisa

Hamsini na tisa au tisa na hamsini au hamsini na kenda ni namba inayoandikwa 59 kwa tarakimu za kawaida na LIX kwa zile za Kirumi.

Ni namba asilia inayofuata 58 na kutangulia 60.

59 ni namba tasa.

Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam

Hifadhi ya bahari ya Dar es Salaam inajumlisha maeneo kadhaa kwenye Bahari Hindi karibu na Dar es Salaam, Tanzania. Kwa jumla kuna visiwa tisa visivyokaliwa na watu pamoja na sehemu za bahari kati ya visiwa hivi. Kuna visiwa vinne upande wa kusini wa Dar es Salaam ambavyo ni Bongoyo, Mbudya, Pangavini na Fungu Yasini, halafu vitano upande wa kusini ambavyo ni (Makatumbe, Finda na Kenda). Hifadhi hii inalinda sehemu za matumbawe, za miti ya mikoko na mimea mingine chini ya uso wa maji.

Linah Kilimo

Linah Jebii Kilimo (alizaliwa mnamo 22 Oktoba 1963) ni Mbunge wa kike nchini aliyekuwa anahudumu katika serikali ya Kenya.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2002 alichaguliwa kuwakilisha eneo bunge la Marakwet Mashariki kwa tiketi ya NARC. Wapinzani wake wa kisiasa walikuwa wamepinga kukimbilia kwake kwa kiti cha ubunge kwani msingi wao ulikuwa kwamba Linah hakuwa amepashwa tohara na hivyo basi hakuwa katika hali mwafaka ya kukimbilia ofisi ya umma.

Hata hivyo amefanya kazi kwa ufanisi pamoja na mashirika ya Kiserikali na yasiyo ya Kiserikali (NGO) huku lengo lao kuu likiwa kutokomeza ukeketaji. Pia amefanya kazi kwa ufanisi katika kuleta amani ya kudumu kati ya jamii ya Wapokot na jamii ya Wamarakwet. Jamii ya Wamarakwet na hasa wale wanaotoka katika eneo bunge ya Marakwet Mashariki walikuwa wamevamiwa na kuteswa vibaya sana na mashujaa wa Kipokot ambao walikuwa wezi wa kimabavu na ambao Serikali ya KANU ilikuwa imeshindwa kuwasimamisha licha ya kuwepo kwa Jeshi, Polisi na kijeshi cha polisi katika eneo hilo. Amani hii ilipatikana tu baada ya Serikali ya NARC kuchaguliwa mnamo Desemba mwaka wa 2002. Kama matokeo jamii hizi mbili sasa zinaishi kwa amani na utulivu.

Lina Kilimo pia amefanikiwa katika kuendeleza eneo bunge la Marakwet Mashariki, kwa kutoa ufadhili kwa shule za mitaa kwa njia ya vitabu, walimu zaidi, mipango ya chakula na hata nguo. Jebii amefanya kazi pamoja na Serikali kuboresha barabara ya kuingia katika eneo bunge hilo kupitia ujenzi wa barabara ya hali ya hewa zote ("all-weather road" kwa lugha ya kimombo) huku nia na lengo kuu likiwa kuweka lami katika barabara hiyo kwa muda usiyokuwa mrefu.

Kilimo Linah ameolewa kwa mhandisi anayehudumu katika Serikali na walijaliwa kuwa na wana watano.

Katika kura ya maoni ya katiba ya Kenya ya mwaka wa 2005, aliunga mkono kupinga katiba hiyo. Pamoja na idadi ya mawaziri wengine, alikuwa mateke nje ya serikali baada ya kura ya maoni, ambayo imeshindwa kupitisha mapendekezo ya katiba aPamoja na idadi ya mawaziri wengine, alifukuzwa kutoka serikalini baada ya kura ya maoni, ambayo ilishindwa kupitisha katiba mpya iliyopendekezwa. mpya. Alijiunga na chama cha Orange Democratic Movement, lakini baadaye alikiondoka chama hicho ilikuunga mkono uchaguzi wa pili wa rais Mwai Kibaki. Hatimaye alikimbilia kiti cha eneo bunge lake kwa tikiti ya chama cha KENDA na kukihifadhi kiti chake cha ubunge.

Lister Elia

Lister Elia ni mwanamuziki, mtunzi wa vitabu, mwalimu wa muziki na mkufunzi wa kituo cha mazoezi kutoka Tanzania, lakini kwa sasa anaishi nchini Japan. Elia alilelewa katika familia ya watu wa dini sana, baba yake akiwa kama kasisi wa Kanisa la Kiangalikana Dayosisi ya Tanganyika Jimbo la Kati. Alikuwa mpenzi sana wa muziki, na kuanza kupiga piano tangu akiwa na umri wa miaka sita. Baadaye alikuja kuhitimu elimu ya muziki kutoka katika chuo cha cha muziki Ruhija huko Bukoba, Tanzania, halafu baadaye kenda kusoma chuo kingine kilichopo mjini Wiesen, nchini Austria. Baada ya kuhamia nchini Japan, alijiandikisha katika chuo kingine cha muziki nchini humo maarufu kama MATE School of Music ili kujiendeleza kimuziki zaidi.Elia alijiunga na bendi ya Orchestra King Kikii Double O, ambayo ilikuwa inamilikiwa na Maestro King Kiki. Baadaye akajiunga na kuwa kiongozi wa bendi ya Benebene Group. Bendi yake ya tatu ilikuwa Orchestra Sambulumaa Band, halafu Orchestra Safari Sound (Ndekule), na mwisho kabisa kwa bendi za Tanzania, ni MK Group, kwa kupiga kinanda kwenye wimbo wa "Maumivu Makali". Mwaka mmoja aliyokaa na bendi ya Sambulumaa alirekodi nyimbo zote za albamu ya kwanza ya bendi, aliondoka katika bendi na kujiunga na Orchestra Safari Sound mnamo 1988. Uhamisho huu ulisimamiwa na Abel Baltazar, hasa kazi yake kubwa ilikuwa kukusanya watu na kuwatia kundini na alikuwa mmoja kati ya viongozi wa Orchestra Safari Sounds. Lister Elia vilevile aliwahi kuishi na kufanya kazi muda mchache jijini Nairobi, Kenya, kabala ya kuhamia mazima nchini Japan.

Huko Nairobi, Elia alipiga piano katika hoteli mbalimbali ikiwa ni pamoja na Jacaranda Hotel, Cassino- Galileo Hall na Tuna Tree Restaurant, Lessa Lassan’s Popolipo na Tchiakatumba. Huko Japan ameungana na rafiki yake wa utotoni maarufu kama Fresh Jumbe, vilevile mwanachama mwenzake wakati yupo Orchestra Safari Sound. Wawili hawa wameunda kundi maarufu kama “The Tanzanites Band-Tokyo. Kazi maarufu ya Lister kwenye kinanda ni pamoja na "Maumivu Makali" na "Mapenzi ya Adhabu" ya MK Group, "Kadiri Mke Wangu" ya Orchestra Sambulumaa,, Mayombo ya "Orchestra Sambulumaa"", na "Mama Happy" (wimbo maarufu), ambao pia alitunga wakati yupo Sambulumaa.

Mbali na kazi yake ya muziki, Elia vilevile ni mwalimu wa muziki na mtunzi wa vitabu na hadi sasa keshachapisha vitabu vitabu ikiwa ni pamoja na : The Mystery of Tamko's Death, Jifunze Gitaa na Piano.

Mystic Night Move

Mystic Night Move ni jina la kutaja wimbo uliombwa na kutungwa na msanii wa muziki wa raggae kutoka nchini Ivory Coast - Alpha Blondy.

Mashairi yake anazungumzia kwanini mashujaa weusi wanakufa mapema. Mstari wa kwanza anasema: Naamka asubuhi na Mola anapambazua jua,

Machozi machoni mwangu,

Kwa sababu usiku wa jana nimepata habari za kusikitisha mno,

Nimesikia eti Bob Marley kafa,

Na ninafahamu ya kwamba kwa uwezo wake ipo siku atainuka tena,

Simba wa Zayuni kenda zake,

Kupumzika katika makazi yake ya milele.

Neptun

Kwa elementi ya kikemia nenda Neptuni (elementi), kwa mungu wa Kiroma nenda Neptunus

Neptuni (ing. Neptune) ni sayari ya nane kutoka kwenye Jua na ya nne kwa ukubwa wa kipenyo katika mfumo wa Jua. Masi yake ni mara 17 ya ile ya Dunia. Pamoja na Mshtarii (Jupiter), Zohali (Saturn) na Uranus inahesabiwa kati ya sayari jitu za mfumo wetu.

Neptuni inazunguka Jua kwenye obiti yake katika kipindi cha miaka 164.8 kwa umbali wa kilomita bilioni 4.5 au vizio astronomia 30.

Ogu

Ogu ni jina la mfalme wa Waamori aliyetawala sehemu za Bashani. Ogu anatajwa katika Biblia kwenye vitabu vya Hesabu 21 na Kumbukumbu la Torati 3, kwa kifupi pia katika Zaburi 135:11 na 136:20. Inawezekana ya kwamba kutajwa kwa "Mwamori" katika Amosi 2:9 ni pia kuhusu Ogu.

Out of Time (Heroes)

"Out of Time" ni sehemu ya saba ya msimu wa pili wa tamthilia ya ubunifu wa kisayansi inayorushwa hewani na TV ya NBC - Heroes. Ilianza kurushwa hewani kwa mara ya kwanza mnamo tar. 5 November 5, 2007.

Pluto

Kuhusu matumizi ya jina "Utaridi" kwa sayari hii tazama chini kwa "jina"

Pluto ni sayari kibete inayozunguka jua ng'ambo ya obiti ya Neptuni.

Masi yake ni hasa mwamba na barafu. Kipenyo chake ni km 2,390.

Katika mwendo wake inakata njia ya Neptune kwa sababu njia yake ina umbo la duaradufu kali.

Pwani na Bara ya Afrika Mashariki 1800-1845

Afrika Mashariki katika miaka 1800-1845 ilikuwa na mabadiliko makubwa kama ifuatavyo.

Siti Binti Saad

Siti binti Saad (alizaliwa Fumba, Zanzibari, 1880 akapewa jina la 'Mtumwa' kwa vile alizaliwa kipindi cha utumwa wa Kiarabu. Jina la Siti alipewa na kabaila mmoja wa Kiarabu).

Baba yake bwana Saadi alikuwa ni Mnyamwezi kutoka Tabora na mama yake alikuwa ni Mzigua toka Tanga, lakini wote wawili walizaliwa Zanzibari. Hali ya maisha ya familia yao ilikuwa ni duni sana na walijishughulisha zaidi katika shughuli za kilimo na ufinyanzi kazi ambazo Siti alijifunza na kuzimudu vizuri pia.

Kama Waswahili wasemavyo 'kuzaliwa masikini si kufa masikini' Siti alibarikiwa kuwa na kipaji cha pekee cha uimbaji. Kipaji hiki kilimsaidia sana tangu siku za awali za maisha yake kwani alitumia uimbaji wake kuuza vyungu vya mama yake alivyokuwa akimsaidia kuvitembeza. Siti alipoimba sauti yake iliweza kupaa na kusafiri kwa umbali wa maili nyingi na hii ndio ilikuwa ishara ya watu kujua kwamba vyungu vya kina Mtumwa vinapita leo. Alifananishwa kuwa na mapafu yenye nguvu kama ya simba kutokana na alivyoweza kupaza sauti yake mbali na bila kuachia pumzi.

Kutokana na wakati huo elimu kwa watoto wa kike kutotiliwa mkazo, Siti hakuwahi kwenda shule wala kuhudhuria mafunzo ya Kurani. Hivyo mnamo mwaka 1911 aliona ni bora ahamie mjini ili kubooresha maisha yake zaidi. Ujio wake wa mjini ulikuwa wa neema kwani alikutana na bwana mmoja wa kundi la muziki wa Taarabu la "Nadi Ikhwani Safaa" aliyeitwa Muhsin Ali. Katika kipindi hicho hilo ndilo lilikuwa kundi pekee la muziki wa taarabu lililoanzishwa na Sultani mpenda starehe na anasa bwana Seyyid Barghash Said. Kundi hili lilikuwa ni la wanaume peke yake , wanawake hawakuruhusiwa kujiunga na vikundi vya muziki kwa vile ilikuwa ikichukuliwa kama ni uhuni. Bwana Muhsin alikiona kipaji cha pekee cha Siti na hivyo akajitolea kumfundisha kuimba kwa kufuata vyombo vya muziki na lugha ya kiarabu. Baada ya hapo alikwenda kumtambulisha kwa wanamuziki wenzie wa "Nadi Ikhwani Safaa" ambao bila kusita wakaanza kufanya naye maonyesho mbalimbali katika jamii. Walipata mialiko mingi hasa kutoka kwa Sultani na matajiri wengine wa Kiarabu, pia katika maharusi na sherehe zingine mbalimbali, inasemekana ulifika wakati ambapo sherehe ilishindwa kufana kama Siti binti Saadi hakuwepo kutumbuiza. Siti alikuwa ni moto wa kuotea mbali na jina lake lilivuma kwa haraka sana hadi nje ya mipaka ya nchi na bara la Afrika. Na punde Siti alianza kufananishwa na 'Umm Kulthum', mwimbaji mahiri wa kike aliyetamba wakati huo kutoka Misri.

Kama nilivyosema moto wa Siti ulikuwa si wa kuusogelea karibu, mwaka 1928 kampuni ya kurekodi muziki ya Columbia and His Master's voice yenye makazi yake Mumbai India ilisikia umaarufu wa Siti binti Saadi na hivyo ikamwalika yeye pamoja na kundi lake kwenda kurekodi kwa lugha ya Kiswahili ili kujaribu kama muziki wake utauzika. Kampuni ile haikuweza kuamini jinsi muziki ule ulivyouzika kwa kasi kubwa kwani wastani wa santuri 900 ziliweza kuuzika katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo, na hadi kufikia 1931 santuri 72,000 zilikuwa zimeuzwa. Kutokana na kusambaa kwa santuri hizi, umaarufu wa Siti ulizidi mara dufu watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia walikuwa wakija Zanzibari kuja kumwona. Mambo yalizidi kuwa mazuri kwa Siti hadi ikafikia hatua kampuni ya kurekodi ya Columbia kuamua kujenga studio ya kurekodi muziki palepale Zanzibar maalumu kwa ajili ya Siti binti Saadi.

Hatua hiyo ya hadi kujengewa studio iliwaumiza wengi wenye wivu, hivyo wakaanza kumtungia nyimbo za kumkejeli ili kumshusha na hasa walitumia kigezo kwamba hana uzuri wa sura, nyimbo nyingi ziliimbwa lakini huu ndio uliovuma sana:

Siti binti Saadi kawa mtu lini,

Kaja mjini na kaniki chini,

Kama si sauti angekula nini?Na yeye kwa kujua hila za wabaya wake, akaona isiwe taabu akajibu shambulio namna hii:

Si hoja uzuri,

Na sura jamali,

Kuwa mtukufu,

Na jadi kebeli,

Hasara ya mtu,

Kukosa akili.Kwa kujibu shambulio hilo kwa namna yake aliwafunga midomo wale wote waliokuwa wakifumatafuata. Siti pia alikuwa ni mwanamke wa kwanza mwanaharakati katika kipindi chake, alitetea wanawake na wanyonge kwa ujumla, kwani katika kipindi chake watu matajiri walikuwa wakiwaonea masikini na walipofikishwa mbele ya haki waliweza kutoa hongo na kuachiwa huru halafu wewe uliyeshitaki ndiye unayefungwa.

Utunzi wake wa wimbo wa Kijiti ulimpatia sifa kubwa kwani ulikuwa ukielezea kisa cha kweli kilichomkuta mwanamke mmoja mgeni kutoka bara, mwanamke huyu alipofika alikutana na Tajiri mmoja ambaye alijifanya amempenda, hivyo akamchukua na kulala naye halafu baadaye akamuua. Tajiri yule alishitakiwa na bahati nzuri walikuwepo mashahidi wawili walioshuhudia tukio lile, lakini kwa vile ni Tajiri alitoa pesa na kesi ikawageukia wale mashahidi na kufungwa.

Siti akatoa wimbo huu:

Tazameni tazameni,

Eti alofanya Kijiti,

Kumchukua mgeni,

Kumcheza foliti,

Kenda naye maguguni,

Kamrejesha maiti.Siti aliendelea kumwambia katika nyimbo zake kwamba asijethubutu kwenda Dar er Salaam kwa maana watu wenye hasira wanamsubiri na wameapa kwa ajili yake.

Siti aliendelea na shughuli yake ya muziki hadi uzeeni, muda mfupi kabla ya kifo chake alikutana na mwandishi maarufu na mwanamashairi Shaaban Robert ambaye alimhoji na kuweza kuandika wasifu wake katika kitabu alichokiita " Wasifu wa Siti binti Saadi." Wasifu huu unaonekana kuwa ndio bora zaidi uliowahi kuandikwa katika fasihi ya Tanzania. Kitabu hiki kinatumika kufundishia shule za sekondari za Tanzania.

Tarehe 8 Julai 1950 Siti binti Saadi alifariki dunia na kuacha pengo kubwa katika fani ya Taarabu. Ingawa pengo hilo haliwezi kuzibika lakini kuna watu wengi walioweza kuibuka na umaarufu wa kuimba taarabu kupitia kwake, mfano hai ni Bi Kidude.

Hata baada ya kifo chake jina lake bado linatumika sana kama kielelezo cha ushujaa wake, Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), kimetumia jina lake kulipa jina gazeti la chama chao "Sauti ya Siti". Hadi leo hii Siti hutumika kama kipimo cha kufundishia uimbaji wa Taarabu. Na anakumbukwa katika historia yake ya kuwa mwanamke wa kwanza Afrika mashariki kurekodi muziki katika santuri.

Uchaguzi wa bunge nchini Kenya, 2007

Uchaguzi wa bunge nchini Kenya ulifanyika kama sehemu ya uchaguzi mkuu wa Kenya mnamo tarehe 27 Desemba 2007; uchaguzi wa rais ulifanyika tarehe hiyo pia.Uchaguzi huu wa ubunge ulifanyika ukiwa huru na wa haki kwa ujumla kinyume na uchaguzi wa rais uligombewa vikali. uchalikuwa huu unazingatiwa kuwa wa ajabu kulungana na idadi ya mabadiliko yaliyoshuhudiwa. Miongoni mwa haya yalikuwa:

Kati ya wabunge 190 waliokuwa wakiondoka ambao walivitetea viti vyao 71 tu ndio walivihifadhi viti vyao.

Mawaziri 20 waliotetea viti vyao walishindwa.

KANU kilikuwa chama rasmi cha upinzani cha mwaka 2002 ambacho baadaye kilijiunga na serikali kilishinda viti 14 peke yake, kwa hivyo kupunguza idadi ya viti vyake kutoka 62.

Wagombea wanawake 15 walichaguliwa ambayo ni idadi kubwa zaidi katika historia ya Kenya (Mnamo 2002 wanawake 9 walikuwa wamechaguliwa)

Uranus

Kuhusu matumizi ya jina Zohali kwa sayari hii tazama kipengele cha "Jina"

Uranus ni sayari ya saba kutoka jua letu.

Wamijikenda

Mijikenda ("miji au makabila tisa": "kenda" ni Kiswahili asilia kwa namba 9) ni jina la kutaja jumla vikundi tisa kwenye pwani ya Kenya. Vikundi hivi wakati mwingine huitwa koo, wakati mwingine makabila. Watazamwa kuwa vikundi ya pekee vinavyoshiriki lugha moja kwa lahaja mbalimbali.

Idadi yao ilikuwa takriban 750,000 mnamo mwaka 1980.

Wapare

Wapare ni kabila kutoka milima ya Pare, Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi ya Tanzania.

Wanakadiriwa kuwa 1,000,000 hivi.

Lugha yao ni Kipare (au Chasu).

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.