Kamusi elezo

Kamusi elezo (pia: ensiklopedia) ni kitabu kinachojaribu kukusanya ujuzi wote wa binadamu.

Siku hizi, Wikipedia ni kamusi elezo kubwa zaidi duniani. Zamani (kabla ya kuja kwa Wikipedia) Encyclopedia Britannica ilikuwa kati ya kamusi elezo kubwa zaidi.

Katika historia zilikuwepo majaribio mbalimbali ya kukusanya ujuzi wote wa dunia. Mfano bora wa kale ni kamusi ya Yongle kutoka China iliyotungwa na wataalamu 2000 katika karne ya 14 na kuandikwa kwa mkono katika vitabu 1100.

Lakini kamusi elezo au ensiklopedia zimekuwa na athari kubwa sana tangu Johannes Gutenberg na kupatikana kwa uchapaji wa vitabu ulioshusha kabisa bei ya vitabu kwa watu wengi.

Ensiklopedia ya kwanza ya kisasa iliyokuwa na athira kubwa sana ilikuwa "Encyclopédie ou Dictionnaire raisonné des sciences, des arts et des métiers" iliyokusanywa na Denis Diderot pamoja na Jean Baptiste le Rond d’Alembert pamoja na waandishi zaidi ya 130 katika karne ya 18 huko Ufaransa. Kamusi elezo hili likawa kati ya vyanzo vya harakati ya Zama za Mwangaza.

Books-aj.svg aj ashton 01.svg Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kamusi elezo kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
UBN Encyclopaedia Britannica
Encyclopedia Britannica ilikuwa kamusi elezo mashuhuri zaidi duniani hadi kuja kwa Wikipedia.
Catholic Encyclopedia

Catholic Encyclopedia, au Old Catholic Encyclopedia au Original Catholic Encyclopedia, ni kamusi elezo ya Kiingereza kutoka Marekani ambayo inafafanua vidahizo kuhusu Kanisa Katoliki.

Gombo la kwanza lilitolewa mnamo Machi 1907. . Toleo hili linapatikana katika intaneti kwa wasomaji wote.

Encyclopedia Britannica

Encyclopædia Britannica ni kamusi elezo kubwa na moja kati ya kamusi elezo iliyo-maarufu zaidi. Inaandikwa kwa lugha ya Kiingereza. Kamusi elezo hii huchapishwa na kampuni binafsi ya Encyclopaedia Britannica, Inc. Awali ilikuwa ikichapishwa kwenye karatasi tu, lakini hivi karibuni imepanuka na kuwa na dijiti, au matoleo ya kompyuta vilevile. Kamusi elezo hii imegawanyika katika vitabu vingi sana. Makala za kwenye vitabu zimepangwa kwa mtindo wa kialfabeti. Kumekuwa na matoleo yake ambayo ni kwa ajili ya watoto vilevile. Hii ni kamusi elezo kubwa sana ya kuchapishwa. Kamusi elezo iliyo-kubwa ziadi ni Wikipedia. Watu wengi huhesabia kwamba ni kamusi elezo bora, kwa sababu ipo sahihi na ina mambo mengi.

Kamusi elezo hii awali ilikuwa ndogo sana, toleo la kwanza lilikuwa na vitabu vitatu na ilitolewa mnamo mwaka wa 1768. Polepole likawa kubwa zaidi. Toleo jipya, toleo la 15, sasa lina vitabu takriban 29, jumlisha vitabu viwili ambavyo ni faharasa. Pia imemjulisha kitabu cha ziada kiitwacho Propaedia, kwa ajili ya kuainisha ufahamu. Vitabu 29 vimeumba Macropaedia na Micropaedia. Macropædia ni kikubwa kuliko vingine, chenye makala yenye maelezo zaidi ambazo pia zaweza kuwa na kurasa 300, -metengenezwa kwa vitabu 17, wakati Micropædia ni kidogo ambacho kawaida huwa na makala fupi na maneno machache chini ya 750. Micropædia hutumika kwa ajili ya kutazama kwa haraka zaidi, lakini iwapo utahitaji habari zaidi basi inakubidi utumie Macropædia. Kila kitabu kimoja ni kikubwa sana, zaidi ya kurasa 1,000 kwa kitabu. Kuna vitabu vya mwaka. Kila mwaka, kitabu kimechapishwa kuhusu matukio ya mwaka huo.

Makala za kwenye Britannica ni kwa ajili ya watu wazima walio-elimika, si kwa ajili ya watoto, na imeandikwa na wahariri takriban 100 na wachangiaji wataalamu zaidi ya 4,000. Watu wengi hudhania ni kamusi elezo bora, lakini Wikipedia bado inabaki kuwa maarufu kwa kuwa matumizi yake ni bure. Britannica ni kamusi elezo ya kale kwa lugha ya Kiingereza mpaka sasa. Ilianza kuchapishwa kwa mara ya kwanza kunako mwaka kati ya 1768 na 1771 huko mjini Edinburgh, Uskoti na kukua kwa umaarufu mkubwa, ikiwa na toleo lake la tatu mnamo 1801 ikiwa imeongeza vitabu 21.

Ukubwa wa vitabu vya Britannica karibia vyote vinafanana kwa takriban miaka 70, ikiwa na maneno yapatayo milioni 40 ikiwa ni nusu ya mada zilizopo ndani ya vitabu vyenyewe. Kamusi elezo hii awali ilikuwa ikimilikiwa na Uingereza. Kwa sasa inamilikiwa na Marekani, lakini bado inaandikwa kwa Kiingereza cha Uingereza. Muda wa ziada, kamusi elezo hii imekuwa na kipindi kigumu cha upatikanaji wa fedha, kitu ambacho kamusi elezo nyingi huzikumba.

Wikipedia

Wikipedia ni kamusi elezo huru ya lugha nyingi katika mtandao wa wavuti. Inalenga kukusanya elimu nyingi iwezekanavyo na kuisambaza kwa njia ya intaneti.

Inatumia taratibu za wikiwiki. Ni bure kabisa, na inaweza kusomwa, kuandikwa, na kuhaririwa na mtu yeyote, popote pale. Yaani kila mtu anaweza kuchangia makala akiwa na uhuru wa kuboresha makala zilizopo kwa kuzihariri.

Kamusi hii inajengwa kwa utaratibu huria ambao unategemea falsafa ya ushirikiano ambako watu wengi hushirikiana kwa kujitolea bila kupokea malipo yoyote.

Falsafa hii inaonekana katika vuguvugu la programu huria ya tarakilishi, mikutano huria, demokrasia huria, n.k.

Wikipedia inaweza kusomwa pia nje ya mtandao kwa kutumia programu huria ya Kiwix.

Wikipedia ya Kiajemi

Wikipedia ya Kiajemi (Kiajemi: ویکی‌پدیا، دانشنامهٔ آزاد, Vikipedia, Daneshname-ye Azad maana yake Wikipedia, Kamusi Elezo Huru) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiajemi. Toleo la Wikipedia kwa lugha ya Kiajemi, lilianzishwa mnamo mwezi wa Januari katika mwaka wa 2004. Ilipita idadi ya makala 1,000 mnamo tar. 16 Desemba 2004 (26 Adhar 1383 Hsh) na lengo la makala 10,000 lilifikiwa kunako tar. 18 Februari 2006. Na kwa tar. 6 Mei 2009, imekuwa na makala 60,083.

Wikipedia ya Kiajemi ilianzishwa kwa juhudi za Roozbeh Pournader na wachangiaji.

Wikipedia ya Kialbania

Wikipedia ya Albania (Kialbania: Wikipedia shqip) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kialbania. Wikipedia hii, ilianzishwa mnamo tar. 12 Oktoba 2003. Na kwa tar. 22 Aprili 2008, Wikipedia hii imevuka idadi ya makala zaidi ya 20,000na ni Wikipedia ya 52 kwa ukubwa wa hesabu ya wingi wa makala.

Wikipedia ya Kichina

Wikipedia ya Kichina (Kichina: 中文維基百科/中文维基百科) ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kichina. Wikipedia hii ilianzishwa mnamo mwezi wa Oktoba katika mwaka wa 2002. Wikipedia hii ina makala zaidi ya 250,000 kwa mwezi wa Aprili 2009.

Mtandao huu ulizuiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Ina wasimamizi 87, wakiwemo 29 kutoka China Bara, 18 kutoka Taiwan, na 15 kutoka Hong Kong.

Wikipedia ya Kidenmark

Wikipedia ya Kidenmark ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kidenmark. Wikipedia hii, iliazishwa mnamo tar. 1 Februari katika mwaka wa 2002. Na kwa tar. 28 Desemba 2008, Wikipedia hii imefikisha zaidi ya makala 100,000. Kutokana na Kidenmark kuwa lugha inayoingiliana na Kiswidi na Kinorwei, wasimamizi wa mitandao hushirikiana kwa heshima ya mitandao yao ya Wikipedia kwa kupitia Skanwiki sehemu ya mtando wa Wikimedia mashuhuri kama Meta-Wiki.

Wikipedia ya Kiebrania

Wikipedia ya Kiebrania (Kiebrania: ויקיפדיה: האנציקלופדיה החופשית; inamtamkwa Wikipedia: HaEntziklopedia HaHofshit, wakati Wikipedia inatamkwa na baadhi yao Vikipedia; wikiˈpedia haʔentsikloˈpedia haχofˈʃit) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiebrania. Toleo hili lilianzishwa mnamo mwezi wa Julai katika mwaka wa 2003 na kwa tar. 11 Aprili ya mwaka wa 2009, imefikisha zaidi ya makala 90,000.

Wikipedia ya Kiesperanto

Wikipedia ya Kiesperanto (Kiesperanto: Vikipedio en Esperanto, au esperantlingva Vikipedio) ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kiesperanto. Wikipedia hii, ilianzishwa mnamo mwezi wa Desemba katika mwaka wa 2001, ikiwa kama Wikipedia ya kumi na moja kuanzishwa (ikifuatiwa na Wikipedia ya Kibasque).

Mnamo mwezi wa Juni katika mwaka wa 2008, toleo hili likavuka idadi ya makala 100,000, na kuifanya iwe Wikipedia ya 21 kwa ukubwa wa hesabu ya wingi wa makala na pia ni kubwa wa upande wa lugha ya kuundwa (bila kujumlisha Wikipedia ya Kivolapük ambayo yenyewe ina makala nyingi za mbegu).

Wikipedia ya Kiesperanto, ilianza na makala 139 kutoka katika kamusi elezo ya Enciklopedio Kalblanda ya Stefano Kalb.

Wikipedia ya Kiestonia

Wikipedia ya Kiestonia ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiestonia. Wikipedia hii, ilianzishwa mnamo tar. 24 Julai 2002. Mnamo tar. 20 Januari 2009, imefikisha makala 59,131. Takwimu ya sasa ya Wikipedia kwa Kiestonia, inapatikana hapa.

Wikipedia ya Kihaiti Kreole

Wikipedia ya Kihaiti Kreole ni toileo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kihaiti Kreole. Wikipedia hii, ilianzishwa mnamo mwezi wa Agosti 2004, kwa tar. 21 Januari ya mwaka wa 2009, imefikisha makala 51,000, nakuiifanya liwe toleo la Wikipedia la 38 kwa ukubwa wa wingi wa hesabu ya makala (imeruka kutoka 47 mnamo Agosti 2008). Pia ni moja kati ya Wikipedia chache sana za lugha ya Kikreole.

Wikipedia ya Kihungaria

Wikipedia ya Kihungaria (Kihungaria: Magyar Wikipédia) ni toleo la kamusi elezo huru ya Wikipedia kwa lugha ya Kihungaria/Magyar. Wikipedia hii, ilianzishwa mnamo tar. 8 Julai 2003. Wikipedia hii, imefikisha idadi ya makala zaidi ya 100,000 kunako tar. 17 Julai 2008.

Wikipedia ya Kiingereza Rahisi

Wikipedia ya Kiingereza Rahisi au Simple English Wikipedia ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia ambalo limeandikwa kwa Kiingereza Rahisi.

Ilianza mwaka wa 2004. Mnamo Machi 2016, Wikipedia kwa Kiingereza Rahisi ina makala zipatazo 118,000. Makala nyingi za Simple ni fupi kuliko zile za Wikipedia kwa Kiingereza.

Kamusi elezo hiyo ilitakiwa itumike kwa ajili ya watoto, ambao huenda wasiwe na uwezo kuelewa vyema makala za Wikipedia ya Kiingereza, na watu wengine ambao bado wanajifunza Kiingereza.

Wikipedia ya Kilithuania

Wikipedia ya Kilithuania ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kilithuania. Ni huru na kamusi elezo kubwa ya intaneti kwa lugha ya Kilithuania. Toleo hili lilifanya hatua yake ya kwanza mnamo mwaka wa 2003, lakini ilifikisha makala za uhakika kunako mwaka wa 2004. Mnamo tar. 14 Desemba 2005, Wikipedia ya Kilithuania, imefikisha idadi ya makala 10,000 na kunako tar. 26 Februari ya mwaka wa 2006, imefikisha tena kiwango cha makala 40,000. Lengo lipya limefikiwa kunako tar. 1 Agosti 2007 - 50,000. Kwa sasa, Wikipedia ya Kilithuania ina makala zaidi ya 80,000.

Wikipedia ya Kipoland

Wikipedia ya Kipoland (Kipoland: Wikipedia polskojęzyczna) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kipoland. Wikipedia ya Kipoland, ni toleo la tisa la Wikipedia. Ilianzishwa tarehe 26 Septemba 2001.

Mwezi wa Mei 2008 ilifikisha makala zaidi ya 500,000, na kuifanya iwe toleo la nne kwa ukubwa baada ya Wikipedia kwa Kiingereza, Kijerumani, na Kifaransa.

Tarehe 24 Septemba 2013 ilifikia nakala 1,000,000.

Hii ni toleo kubwa la Wikipedia katika orodha ya lugha za Kislavoni kwa idadi ya makala.

Wikipedia ya Kiserbia

Wikipedia ya Kiserbia (Kiserbia: Википедија на српском језику/Vikipedija na srpskom jeziku) ni toleo la kamusi elezo la Wikipedia kwa lugha ya Kiserbia. Ilianzishwa mnamo tar. 16 Februari 2003. Toleo hili, kwa tar. 5 Januari ya mwaka wa 2009, imefikisha zaidi ya makala ya 75,000.

Wikipedia ya Kislovene

Wikipedia ya Kislovene (Kislovene: Slovenska Wikipedija) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kislovene. Iianza kufanyakazi mnamo mwezi wa Machi katika mwaka wa 2002. Mnamo mwezni wa Julai 2007, imefikisha makala 50,000. Na kwa mwezi wa Aprili katika mwaka wa 2009, imefikisha zaidi ya makala 75,000.

Wikipedia ya Kiukraini

Wikipedia ya Kiukraini (Kiukraini: Українська Вікіпедія au Ukrayins’ka Vikipediya) ni toleo la kamusi elezo ya Wikipedia kwa lugha ya Kiukraini. Makala ya kwanza iliandikwa tarehe 30 Januari 2004. Tarehe 28 Machi 2008 imefikisha zaidi ya makala 100,000. Tarehe 9 Septemba 2017 imefikisha makala 722,255 na ndiyo Wikipedia ya 16 kwa ukubwa.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.