Kabonati

Kabonati (kutoka Kiingereza carbonate) ni kampaundi yoyote yenye ioni ya CO32-. Ioni hiyo inafanywa na kaboni na oksijeni.

Kabonati hutokea kama chumvi na esta za asidi kabonia (H2CO3 carbonic acid).

Kabonati zinapatikana kote katika mazingira yetu, hasa katika miamba kwa mfano gange. Viumbehai wengi wana viunzi vinavyofanywa na kabonati, hasa chokaa.

Chem template.svg Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kabonati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Carbonate-3D-balls
Muundo wa kabonati
Gange

Gange au mawe chokaa (ing. limestone) ni aina ya mwamba mashapo inayotokana na madini ya kalsiti (calcite) inayofanywa na kabonati ya kalisi CaCO3.[1]

Kabonati ya kalisi inatengenzwa na viumbehai vinavyojenga kiunzi cha kujikinga au kuimarisha miili yao, kama kiunzi cha matumbawe au sifonji, lakini pia kiunzi cha mifupa ya wanyama wakubwa. Matumbawe hujenga matabaka manene ya mwamba chokaa, mabaki ya viumbe vingine katika maji hutiririka chini ambako yanajenga matabaka ya kalsiti inayokandamizwa na shinikizo ya mata inayokaa juu yake, jinsi ilivyo na mwamba mashapo wote.

Matabaka ya gange yalitokea chini ya bahari katika muda wa kiaka mamilioni hata mabilioni. Yalikua hadi kuwa na unene wa kilomita kadhaa. Gange ni takriban silimia 10 ya miamba mashapo yote duniani.

Pale ambako gange iliathiriwa na joto na shinikizo kubwa sana imebadilika kuwa mwamba metamofia, kwa mfano marumaru.

Gange ni muhimu sana kwa jamii za binadamu kama kifaa cha ujenzi. Gange si ngumu mno hivi iliwahi kukatwa tangu miaka mielfu na kutumiwa kwa majengo. Piramidi za Misri zilijengwa kwa kutumia gange.

Saruji inatengenezwa kwa kuchoma gange.

Keki

Keki ni chakula kinachotengenezwa kwa kuoka unga wa nafaka, maji au zaidi maziwa, sukari, soda ya kuokea pamoja na shahamu (k.m. siagi), na nyongeza nyingine kama vile mayai.

Jina latokana na neno la Kiingereza "cake" .

Keki zilianza kama mkate wa pekee ulioongezwa sukari au asali, baadaye pia shahamu au mafuta.Ilhali mwanzoni keki na mkate hazikutofautishwa sana baadaye mbinu za kuoka keki tamu ziliongezeka sana. Tangu karne ya 18 mafundi wa Ualya waliacha kutumia hamira kama mbinu wa kupata keki laini badala yake walitumia yai lililopigwa hadi kuwa pofu; katika karne ya 19 elimu ya kemia iliunda matumizi ya soda ya kuokea ambayo ni kabonati natiri (magadi) inayotoa gesi wakati wa kuoka na hivyo kuunda nafasi ndani ya kinyunga.Siku hizi kuna aina maelfu za keki.

Madhara ya ongezeko la joto duniani

Madhara ya ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya hali ya hewa ni mada muhimu sana, hasa kwa mazingira na maisha ya binadamu. Ushahidi unaoonyesha mabadiliko ya hali ya hewa ni pamoja na rekodi muhimu ya kipimo joto, kupanda kwa maeneo ya bahari, na kupungua kwa kiwango kilichofunikwa na theluji katika ulimwengu. Kulingana na Ripoti ya Uchunguzi ya Nne ya IPCC, "nyingi" kati ya maongezeko ya vipimo vya joto vya wastani duniani tangu katikati ya karne ya 20 huenda ikawa ni kwa sababu ya ongezeko tunaloliona la wingi wa gesi ya hewaukaa inayotokana na binadamu". Inatibiriwa kuwa mabadiliko ya hali ya anga katika siku za usoni yatahusisha ongezeko la joto duniani zaidi, kupanda kwa kiwango cha maji baharini, na uwezekano wa kupanda wa wingi wa matukio ya hali mbaya ya hewa. Mazingira huonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Mifumo ya kibinadamu huonekana kama yenye kubadilika katika uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ya siku za usoni. Ili kupunguza hatari ya uwezekano mkubwa wa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa katika siku za usoni, nchi nyingi zimebuni sera zinazolenga kupunguza uzalishaji wao wa gesi chafu.

Mapinduzi ya Viwandani

Mapinduzi ya Viwandani yalikuwa kipindi kutoka karne ya 18 hadi karne ya 19 ambapo yalitokea mabadiliko makubwa katika kilimo, utengenezaji wa bidhaa, uchimbaji wa madini na uchukuzi yakiwa na matokeo makubwa kwa hali ya kiuchumi, ya kijamii na ya kitamaduni.

Yalianzia Uingereza na hatimaye kuenea Ulaya nzima, Amerika ya Kaskazini na mwishowe duniani kote.

Mwanzo wa Mapinduzi ya viwanda ulidokeza mabadiliko muhimu katika historia ya binadamu; karibu kila kipengele cha maisha ya kila siku hatimaye yaliathirika kwa njia fulani.

Mwanzo wa wakati wa mwisho wa karne ya 18 mabadiliko katika baadhi ya sehemu za Uingereza yalianza na kazi ambazo hapo awali zilikuwa za mkononi na uchumi uliotumia wanyama kuendesha kazi kulibadilishwana uundaji bidhaa uliotegemea mashine. Ilianza na utumizi wa mashine katika viwanda vya nguo, uundaji kwa mbinu za kutengeneza chuma na kuzidi kutegemea makaa ya mawe yaliyosafishwa. Upanuzi wa biashara uliwezeshwa na kuanzishwa kwa mifereji, uboreshaji wa barabara na reli. Kuvumbuliwa kwa nguvu za mvuke kuliowezeshwa hasa na makaa ya mawe, utumizi mwingi wa gurudumu la maji na mashine za nguvu (hasa katika kutengeneza nguo) kulisisimua kuongezeka kukubwa wa uwezo wa uzalishaji. Kuundwa kwa vifaa vya mashine ambavyo vilikuwa vya chuma pekee katika miongo miwili ya kwanza ya karne ya 19 kuliwezesha kutengenezwa kwa mashine zaidi za kuunda vifaa katika viwanda vingine. Matokeo yalienea kote katika Ulaya ya Magharibi na Marekani ya Kaskazini wakati wa karne ya 19, na hatimaye kuathiri karibu Dunia yote, mchakato ambao unaendelea katika kuenea kwa viwanda. Athari ya matokeo kwa jamii ilikuwa kubwa sana.Mapinduzi ya Viwanda ya Kwanza, ambayo yalianza katika karne ya 18, yaliingia katika Mapinduzi ya Pili ya Viwanda mnamo mwaka wa 1850, ambapo maendeleo ya kiteknolojia na kiuchumi yalizidi kuendelea huku meli zinazotumia mvuke, reli, na baadaye katika karne ya 19 injini ya mwako ya ndani na uzalishaji wa nguvu za umeme. Urefu wa Mapinduzi ya Viwanda unatofautiana na wanahistoria mbalimbali. Eric Hobsbawm anasisitiza kwamba 'yalianza' nchini Uingereza katika miaka ya 1780 na hayakuonekana kikamilifu hadi miaka ya 1830 au 1840, ilhali T. S. Ashton anaamini kwamba ilifanyika, kwa kukadiria, kati ya mwaka wa 1760 na 1830.Baadhi ya wanahistoria wa karne ya ishirini kama vile John Clapham na Nicholas Crafts wamedokeza kuwa mchakato wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yalifanyika hatua kwa hatua na kuwa neno mapinduzi halifai kuelezea yaliyofanyika. Hii bado ni mada inayojadiliwa na wanahistoria. Mapato ya Kijumla ya Nchi ya kila mtu kwa upana yalikuwa imara kabla ya Mapinduzi ya Viwandani na kuibuka kwa uchumi wa kisasa wa kibepari. Mapinduzi ya viwanda yalianzisha zama za ustawi wa kiuchumi na unatalenga mapato ya kila mtu katika nchi zenye uchumi wa kibepari. Wanahistoria wanakubaliana kwamba Mapinduzi ya Viwandani yalikuwa mojawapo ya matukio muhimu sana Kihistoria.

Mwamba (jiolojia)

Mwamba katika jiolojia ni namna ya kutaja mawe au zaidi mchanganyiko au mkusanyiko wa mabao ya aina moja au zaidi ya madini ulio imara katika hali asilia. Jiwe ni kipande cha mwamba.

Takriban madini 30 hufanya sehemu kubwa ya miamba ya dunia, ni hasa silikati na kabonati.

Oksijeni

Oksijeni (en:oxygen) ni elementi simetali yenye namba atomia 8 na uzani atomia 15.9994 kwenye mfumo radidia. Alama yake ni O.

Ni kati ya elementi zilizopo kwa wingi ulimwenguni ikishika nafasi ya tatu baada ya hidrojeni na heli. Kwenye dunia yetu asilimia 28 za masi yake ni oksijeni; ni elementi iliyopo kwa wingi kabisa katika ganda la dunia.

Hutokea ama kama mchanganyiko wa elementi nyingine au pekee yake kama gesi isiyo na rangi wala herufi. Pekee yake hupatikana hasa kama molekuli ya O2 yaani mchanganyiko wa kikemia wa atomi mbili. Kuna pia oksijeni ambayo ni molekuli ya atomi tatu unaoitwa ozoni (O3).

Umuhimu wake duniani ni hasa kuwepo katika maji na katika hewa ya angahewa na kwa ujumla kwa ajili ya uhai. Karibu viumbe vyote duniani hutegemea oksijeni. Wanaipata ama kwa kupumua hewani au kwa kuichukua kwenye maji. Oksijeni tupu ni sumu kwa ajili ya viumbe vingi.

Kama atomi ya pekee ya oksijeni inakutana na atomi mbili za hidrojeni zinakuwa H2O (maji).

Soda

Soda inahusu:

a kemikali iliyo na sodiamu

Kabonati ya sodiamu kuosha soda au unga wa soda

Kabonati ya sodiamu kuoka soda

Hidroksidi ya sodiamu caustic soda

Sodiamu

Vinywaji laini

Maji ya soda maji yenye dioksidi

soda ya barafu dessert sahani

Salsola soda mti wa saltwort, kihistoria ni chanzo cha vumbi la soda

Milima ya Soda mashariki mwa Jangwa la Mojave katika California, USA

Soda Stereo Huko Argentina kuna mwamba pia unayojulikana kama "Soda"

Soda (Jumuia) maarufu kwa mfululizo kwa jumuia za Ubelgiji Philippe Tome na Bruno Gazzotti

Soda, pia inajulikana kama Slate, na tabia ya kutoka Jet Set Radio video mchezo mfululizo

Tom "Soda" Gardocki, mmoja wa wapiga muda gitaa katika bendi Wax punk (rock band)

Soda cracker

Soda Popinski, kutoka Punch-Out!!mfululizo wa michezoSoda inaweza kumaanisha:

ACM-SIAM Kongamano katika mchanganuo wa Diskret

Maendeleo ya Maombi ktika huduma

Kozi fupi katika Taasisi za masuala ya barabara (kawaida Soda), misafara ya barabarani katika kuidhinisha mwili katika Marekani

Mgawanyo wa kutoa huduma

Kauli inayoonesha Uwezo

Ziwa Magadi (Kenya)

Ziwa Magadi lipo kusini mwa Kenya katika eneo la Bonde la Ufa, kaskazini mashariki kwa Ziwa Eyasi.

Ni ziwa la chumvi na kiwango chake cha uchumvi kinazidi asilimia 30. Limepokea jina lake kutokana kiasi kikubwa cha magadi (kabonati ya sodiamu) ndani ya maji yake; wakati wa kiangazi maji ya ziwa hupungua na % 80 ya eneo lake hufunikwa na chumvi hii. Wakati wa msimu wa mvua chumvi huwa inafunikwa tena kwa maji, kisha uzidi tena maji yanapokauka na kuacha chumvi nyeupe.

Ni maarufu kwa aina mbalimbali za ndege wanaoishi kandokando ya ziwa hilo, kwa mfano flamingo.

Ziwa Magadi lina ukubwa wa kilomita mraba 100 na huwa limejaa maji iliyokolea kabonati ya sodiamu ambayo huwa na kiasi kikubwa cha madini ya trona. Asili ya chumvi hii ni chemchemi moto zinazopatikana katika bonde la Ufa. Chemchemi hizo huwa kaskazini magharibi na kusini mwa ziwa hili.

Kuna aina moja tu ya samaki kwenye ziwa hili: cichlid Alcolapia grahami. Samaki huyu anaishi kwenye chemchemi moto zilizo kwenye ufukwe wa ziwa hili.

Ziwa Magadi hapo awali halikuwa na kiwango kikubwa cha chumvi. Miaka elfu kadhaa iliyopita (kipindi cha Pleistocene) na katikati ya kipindi cha Holocene lilikuwa na samaki wengi na kiwango cha chumvi kilikuwa cha chini. Kuna muda wa kihistoria ambamo Ziwa Magadi na Ziwa Natron yalikuwa yameshikamana kuwa ziwa moja kubwa.

Mji wa Magadi upo kwenye pwani ya mashariki ya ziwa hili. Kiwanda cha soda Magadi kinapatikana kwenye mji huu.

Ziwa la chumvi

Ziwa la chumvi (kwa Kiingereza: salt lake) ni ziwa ambalo maji yake huwa na kiwango kikubwa cha chumvi ndani yake. Kwa kawaida karibu kila mahali maji yanayopatikana duniani huwa na kiwango fulani cha chumvi ndani yake. Binadamu, wanyama na mimea mingi huhitaji maji matamu ambayo kiwango cha chumvi kipo chini ya asilimia 0.1 au gramu moja ya chumvi katika kila lita ya maji.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.