Kabila la Efraimu

Kabila la Efraimu ni nusu ya kabila la Yosefu; nusu ya pili inaitwa kabila la Manase. Jumla ya makabila ya Israeli ni 12, yanayotokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli.

Kadiri ya Kitabu cha Mwanzo, kabila hilo lilitokana na Efraimu, mmojawapo wa watoto wawili wa Yosefu. Mtoto wa kwanza aliitwa Manase, na ndiye asili ya nusukabila nyingine.

Bible.malmesbury.arp.jpg Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kabila la Efraimu kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Abdon

Abdon (kwa Kiebrania עַבְדּוֹן, ‘Aḇdōn, "Mtumishi" au "Utumishi") alikuwa mmojawapo kati ya Waamuzi wa Biblia.

Kadiri ya Waamuzi 12:13-15 alikuwa wa kabila la Efraimu akaongoza Israeli kwa miaka 8.

Alikuwa na watoto wa kiume 40 na wajukuu wa kiume 30, ambao kila mmoja alikuwa na punda wake. Hii inaonyesha alikuwa tajiri.

Elishama

Elishama alikuwa kiongozi wa kabila la Efraimu (Israeli) anayetajwa katika Biblia ya Kiebrania, ambayo ni sehemu ya Biblia ya Kikristo (Agano la Kale), katika kitabu cha Hesabu, sura ya 2, mstari wa 18.

Kabila la Manase

Kabila la Manase ni nusu ya kabila la Yosefu; nusu ya pili inaitwa kabila la Efraimu. Jumla ya makabila ya Israeli ni 12, yanayotokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli.

Kadiri ya Kitabu cha Mwanzo, kabila hilo lilitokana na Manase, mmojawapo wa watoto wawili wa Yosefu. Mtoto wa pili aliitwa Efraimu, na ndiye asili ya nusukabila ya pili.

Kabila la Yosefu

Kabila la Yosefu ni mojawapo kati ya makabila ya Israeli ambayo kwa jumla ni 12, kutokana na watoto wa kiume 12 wa Yakobo Israeli. Liligawanyika pande mbili: kabila la Manase na kabila la Efraimu.

Yosefu (babu)

Yosefu (kwa Kiebrania יוֹסֵף, Yossef au Yôsēp̄; kwa Kiarabu, kwa mfano katika Qur'an, jina hilo linaandikwa يوسف, Yūsuf) ni jina la mtoto wa kiume wa kumi na mmoja wa Yakobo Israeli na babu wa kabila mojawapo la Israeli lililoitwa kwa jina lake mwenyewe, au kwa kawaida zaidi liligawanyika pande mbili: kabila la Manase na kabila la Efraimu kufuatana na majina ya watoto wake wawili wa kiume.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.