Jiwe

Jiwe (wingi: mawe) ni kitu chochote kigumu kitokanacho ardhini, kama vipande vidogovidogo ambavyo vinatokana na kuvunjika au kumeguka kwa miamba. Hutengenezwa kwa madini mbalimbali yanapochanganyika kwa mvua na joto kali hukausha maji au hata pia mkandamizo.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Jiwe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.

Moelen
Mawe.
Graviti

Graviti (kutoka Kiingereza: "gravity"; pia: kani ya mvutano, kanimvutano, nguvu ya uvutano, nguvu mvutano) ni kani ya uvutano iliyopo kati ya magimba yote ya ulimwengu. Kila gimba lenye masi linavuta magimba yote mengine yenye masi.

Hii ndiyo sababu tunatembea ardhini ilhli hatuwezi kuelea hewani: kwa sababu masi ya Dunia inatuvuta kuelekea kitovu chake. Inavuta kila kitu chenye masi kuelekea kitovu chake. Na sisi pia tunaivuta Dunia, lakini kani hii ni ndogo mno kulingana na masi kubwa mno ya Dunia. Dunia yetu imeshikwa na mvuto mkali wa graviti ya Jua na hii ndiyo sababu ya Dunia kubaki karibu na Jua katika obiti na haiwezi kutoroka kwenda mbali na Jua.

Tukitupa jiwe hewani litaanguka chini. Hii ni kwa sababu ingawa kani ya mkono ilipeleka jiwe kwenda juu lakini kani ya graviti ya Dunia inapunguza kasi ya jiwe na hatimaye inalirudisha jiwe ardhini.

Tabia ya kuvutana inaonekana vema kati ya Dunia na Mwezi. Dunia ni kubwa, inauvuta Mwezi na kuushika kwenye njia yake ya kuzunguka Dunia. Lakini wakati huohuo Mwezi unavuta pia Dunia na hii inaonekana baharini katika mabadiliko ya maji kupwa na maji kujaa kila siku. Maji ya bahari huvutwa na Mwezi kiasi kwamba kwenye sehemu ya Dunia inayotazama Mwezi, maji ya bahari yaliyo moja kwa moja chini ya Mwezi huinuliwa kiasi nusu mita juu ya wastani wa usawa wa bahari yote.

Isaac Newton anajulikana kama mtaalamu aliyeweza kueleza graviti kwa mara ya kwanza kama utaratibu wa kimsingi wa sayansi.

Kalenda ya Gregori

Kalenda ya Gregori ni kalenda ambayo leo inatumiwa zaidi kimataifa. Jina limetokana na Papa Gregori XIII aliyeamua kutumia kalenda hiyo tangu tar. 15 Februari 1582 badala ya Kalenda ya Juliasi.

Kinole

Kinole ni kata ya Wilaya ya Morogoro Vijijini katika Mkoa wa Morogoro, Tanzania yenye Postikodi namba 67202. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 11,944 walioishi humo.

Kwa jumla watu wa Kinole ni wakarimu sana. Wengi wao walikuwa wakitokea Amini: ndio walioanzisha jina la Kinole ambalo limetokana na jiwe la kunolea panga, visu na mundu.

Lugalo

Lugalo (pia: Rugaro) ni kata ya Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa nchini Tanzania yenye Postikodi namba 51313. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,359 waishio humo.Lugalo iko karibu na barabara kuu ya TANZAM, takriban kilomita 45 kutoka Iringa kwenda Dar es Salaam.

Lugalo ni mahali pa kihistoria kutokana na kwamba ilikuwa sehemu ya mapigano mnamo mwaka wa 1891 kati ya jeshi la kikoloni la Kijerumani na mtemi Mkwawa kiongozi wa Wahehe. Kuna jiwe kubwa la kumbukumbu mahali ambako Wahehe walishinda kikosi cha Kijerumani kilichoongozwa na Emil von Zelewski.

Madini

Madini (kwa Kiarabu: معدن, ma'adan; kwa Kiingereza: mineral) ni dutu mango inayopatikana duniani kiasili. Madini huwa na tabia maalumu ya kikemia, si mata ogania na mara nyingi huwa na muundo wa fuwele (kristali). Kwa lugha nyingine: Madini ni elementi au kampaundi ya kikemia inayoonyesha umbo la fuwele na ambayo imejitokeza katika mchakato wa kijiolojia.

Kuna takriban madini 4,000 yaliyogunduliwa duniani. Miamba yote yanaundwa na madini na kuna hasa madini 30 yanayounda sehemu kubwa ya miamba duniani. Miamba kwa kawaida huwa na madini mbili au zaidi ndani yake.

Madini yapo kila mahali. Katika mazingira yetu kila jiwe limeundwa na madini. Ardhi ya shamba ina kiwango kikubwa cha madini ni punje za mchanga ambao ni mawe yaliyosagwa. Tukiwasha taa kuna madini kwenye uzi ya kuwaka na umeme umefika kwenye taa kupitia shaba ya waya; na shaba hiyo ni madini. Seli za mwili wetu huhitaji madini na hivyo ni muhimu kwamba chakula chetu kina kiasi kidogo cha madini ya lazima kama chuma au kloridi.

Madini kadhaa hupendwa kama vito (johari, mawe ya thamani) au pia dhahabu.

Madini ni kati ya vitu vigumu vilivo vya kawaida katika Dunia. Ni vitu viundanishavo mawe ya Dunia. Kuna baadhi ya madini huundwa na elementi moja tu. Nyinginezo huundwa na zaidi ya elementi mbili au zaidi.

Marumaru

Marumaru (pia: marmar - kutoka Kiarabu مرمر, ing. marble) ni mwamba wa gange uliobadilika kutokana na joto na shindikizo ndani ya ganda la dunia katika kipindi cha miaka milioni kadhaa. Kikemia ni hasa CaCO3.

Ni jiwe gumu sana linalopatikana katika rangi mbalimbali.

Hupendwa sana kama jiwe la ujenzi, hasa kama ni nyeupe. Kama ni haba katika eneo fulani hutumiwa kama mapambo tu, kama vile kwa kufunika kuta.

Jiwe lenye rangi mbalimbali hutumiwa kwa sakafu katika majengo muhimu au kama mapambo ya kuta za ndani.

Tangu kale marumaru ilitumiwa pia kwa kuchonga sanamu.

Mungu

Mungu ni jina lenye asili ya Kibantu linalotumika kwa yeyote anayesadikiwa katika dini mbalimbali kuwa na uhai wa hali ya juu.

Kati ya wafuasi wa dini hizo, wengi wanaona kuwa Umungu, kwa jinsi ulivyo au unavyofirika, haukubali mgawanyiko. Hasa katika Uyahudi, Ukristo na Uislamu wanasisitiza umoja wa Mungu kuwa ndio msingi wa imani yao. Kwao Mungu ni wa milele, anafahamu yote na kutaka hasa uwepo wa viumbe. Tena kwa hiari yake alipenda kujifunua kwa binadamu; kielelezo ni Ibrahimu/Abrahamu aliyefanywa rafiki yake na baba wa waamini wote.

Kuna dini nyingine zinazokubali kuwepo kwa miungu mbalimbali (wawili au zaidi). Hasa dini nyingi za jadi zinaamini wingi wa miungu. Dini kubwa duniani inayosadiki miungu mingi ni Uhindu. Pia katika sehemu za Afrika ya Magharibi ibada za miungu mingi zinaendelea hadi leo.

Mwamba (jiolojia)

Mwamba katika jiolojia ni namna ya kutaja mawe au zaidi mchanganyiko au mkusanyiko wa mabao ya aina moja au zaidi ya madini ulio imara katika hali asilia. Jiwe ni kipande cha mwamba.

Takriban madini 30 hufanya sehemu kubwa ya miamba ya dunia, ni hasa silikati na kabonati.

Nishati

Nishati inamaanisha uwezo wa kufanya kazi na kusababisha mabadiliko. Katika sayansi nishati hupimwa kwa kipimo cha SI joule.

Katika sayansi ina mtazamo wa pekee. Ni aina ya kani/nguvu/uwezo ambapo kazi ikifanyika kama kusogeza kitu, basi tunasema nishati imetumika.

Saruji

Saruji (pia: simiti, simenti) ni mata laini kama ungaunga unaotengenezwa kutokana na chokaa, udongo wa mfinyanzi, mchanga, chuma na mengine. Kwa kawaida huonekana kama unga wa rangi ya kijivu.

Hukorogwa na maji kuwa na hali kati ya ujiuji ila baada ya muda inaanza kuganda na kuwa imara kama jiwe.

Saruji imekuwa muhimu sana katika shughuli za ujenzi. Awali ilitumiwa kwa kushika mawe au matofali ya ukuta vikae pamoja.

Baadaye ikagunduliwa ya kwamba saruji ikichanganywa na mchanga ma mawe madogo (kama kokoto) kuwa zege inaweza kumwagwa kati ya bao mbili na kuwa imara ndani yake. Kwa njia hiyo imewezekana kujenga haraka sana kwa kumwaga mchanganyiko wa zege ya saruji katika nafasi zilizoandaliwa awali. Hapo nondo za chuma zinaingizwa ndani ya ukuta au sakafu ya saruji kwa kusudi la kuongeza uimara.

Sayansi

Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.

Mara nyingi Galileo Galilei anahesabiwa kuwa baba wa sayansi ya kisasa.

Sisimizi

Sisimizi ni familia ya wadudu wadogo wanaoishi katika jamii. Jamii hizi zinaweza kuwa na sisimizi makumi kadhaa tu au kuwa na mamilioni kulingana na spishi mbalimbali.

Makazi yao yapo mara nyingi chini ya ardhi au mahali pengine panapohifadhiwa kama chini ya jiwe kubwa au katika nafasi ndani ya miti. Wanatumia udongo na nyuzi za mimea kwa ujenzi.

Jenasi kadhaa kama vile siafu (Dorylus spp.) hawana makazi ya kudumu bali wanahamahama.

Mchwa hawako karibu na sisimizi hata kama wanafana nao katika mengi na kuitwa kwa Kiingereza "white ants" lakini wako katika nasaba nyingine pamoja na kombamwiko.

Tofali

Tofali ni nyenzo inayotumiwa katika ujenzi wa majengo. Kimsingi ni kama jiwe linalotengenezwa na binadamu kutokana na udongo unaofaa hasahasa udongo kinamo.

Matofali hutengenenzwa kwa kutumia udongo unaopatikana ambao huchanganywa na maji ili kuweza kushikamanisha udongo huo ili kupokea umbo linalotakiwa.

Ufufuko wa Yesu

Ufufuko wa Yesu ndio tukio kuu lililotangazwa daima na Kanisa lake lote kuhusu mwanzilishi wake, Yesu Kristo, kuanzia ushuhuda wa Mitume wa Yesu na maandiko ya Agano Jipya, hususan Injili, hadi leo.

Kadiri ya imani hiyo, siku ya tatu baada ya kuuawa msalabani Ijumaa kuu, Yesu alifufuka mtukufu akiacha kaburi lake na vitambaa vyote vilivyotumika kumzikia.

Tangu Jumapili hiyo na kwa muda wa siku arubaini (kadiri ya Matendo ya Mitume 1:3), yeye aliendelea kuwatokea mara kadhaa wanafunzi wake, hadi alipoonekana nao akipaa mbinguni huku akiwabariki.

Tukio hilo linaadhimishwa kila mwaka kwenye Pasaka ya Kikristo na kila wiki kwenye Dominika.

Kwa Wakristo, ufufuko wa Yesu ndiyo sababu na kielelezo cha ufufuko wa waadilifu wote siku ya kiyama.

Ukumbusho

Ukumbusho ni jambo, jengo au tendo lililokusudiwa kufanya watu wakumbuke mtu au tukio.

La kawaida zaidi ni jiwe au msalaba kaburini ambapo limeandikwa jina la marehemu aliyezikwa kaburini mle, mara nyingi likiwa pamoja na tarehe ya kuzaliwa na kufa kwake.

Pengine wafiwa wanaunda mfuko maalumu wenye jina la marehemu ambao usaidie watu wenye shida, kwa mfano wanafunzi wasiojiweza.

Wagweno

Wagweno ni kabila la watu wenye asili ya Kenya wanaoishi Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro, upande wa Kaskazini wa Milima ya Ugweno.

Lugha yao ni Kigweno.

Zama za Mawe

Zama za Mawe zilikuwa kipindi kirefu cha historia ya kale ya binadamu. Watu walitumia vifaa vya mawe kwa shughuli zao za kila siku.

Ziwa Kingili

Ziwa Kingili ni kati ya maziwa madogo ya Tanzania.

Linapatikana katika mkoa wa Mbeya, mpakani mwa Busokelo na Kyela, likizungukwa na vijiji vya Ntaba kwa upande wa kaskazini na kijiji cha Kingili kwa upande wa kusini.

Lina uzuri wa aina yake kutokana na mandhari iliyo nalo ikiwa ni pamoja na uzuri wa maji yake meupe na samaki safi waliomo ndani yake.

Ziwa Kingili linasifika kwa kuwa na maji safi na salama kwa shughuli zote za binadamu kama kunywa, kuoga, kupikia pamoja na shughuli za ufugaji.

Ziwa Kingili ni moja kati ya maziwa yenye samaki wengi na safi kwa ajili ya kula kama kitoweo pamoja na shughuli za biashara: samaki hao ni pamoja na kambale, perege (tilapia), dagaa (usipa), chilingali (rhamphochromis) na wengine wengi.

Ziwa Kingili ni ziwa la pekee sana kutokana na kutokuwa na mto hata mmoja unaoingiza maji ndani yake (tributaries/inlets) pamoja na kukosa mto unaotoa maji kwenye ziwa hili (distributaries/outlets). Ziwa Kingili hutegemea sana maji ya mvua kwa kiasi kikubwa, hii ni kwa sababu ziwa hili kina chake hupungua sana wakati wa kiangazi kutokana na jua kali la kuanzia mwezi Agosti hadi Desemba, na wakati huohuo kina chake huongezeka maradufu zaidi ya kiangazi wakati wa masika au kipindi cha mvua za mwezi Februari hadi Mei na kutengeneza mlango wa kutolea maji kutoka kwenye ziwa hilo kwenda kwenye mashamba ya mpunga yaliyoko upande wa mashariki wa ziwa hilo.

Mifereji hiyo hukauka pindi tu mvua za masika zinapokatika. Ziwa Kingili ni ziwa lililozungukwa na vilima vidogovidogo vilivyofunikwa na misitu myepesimyepesi ambayo ni hifadhi ya wanyamapori aina ya ngedere au tumbili.

Ziwa Kingili ni ziwa lenye mawe mengi makubwa kwa madogo ndani ya maji na kando yake ambayo yamekuwa kivutio kwa wageni na wenyeji wa eneo hilo, hasa lile jiwe kubwa lenye rangi ya chungwa (orange au nkesela kama wenyeji waiitavyo) lililopo upande wa kusini magharibi mwa ziwa hilo, pamoja na mchanga kwa kiasi kikubwa.

Ziwa Kingili lina sifa ya kuwa na maji ya moto au uvuguuvugu wakati wa asubuhi na maji ya baridi wakati wa mchana.

Ziwa Kingili ni moja kati ya maziwa yanayopokea watalii wengi mkoani Mbeya. Ziwa Kingili huzungukwa na vijiji vya Kingili (Kyela) pamoja na Ntaba (Busokelo) na wakazi wake ni Wanyakyusa.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.