Jioni

Jioni (yaani "kwenye jio" la usiku) ni kipindi cha siku karibu na machweo ambako mwanga wa mchana unazidi kupungua hata kuingia kwa giza la usiku.

Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati wa kuacha shughuli mbalimbali na kujiandaa kwa usingizi, ingawa uenezi wa taa umebadilisha sana ratiba ya watu wengi.

Katika dini mbalimbali, ni wakati muhimu wa sala.

Katika kalenda ya Kiyahudi na kalenda ya Kiislamu jioni ni mwisho wa siku na kuanzia machweo ni mwanzo wa siku mpya, tofauti na hesabu sabifu ya kimataifa inayohesabu siku mpya kuanzia "katikati ya usiku" yaani saa sita usiku (24.00 h au 0.00 h)

24 (msimu wa 8)

Msimu wa nane, pia hujulikana kama Siku ya nane, ya televisheni ya Marekani ya kipindi cha 24 ilianza kutayarishwa mnamo 27 Mei 2009, na itaonyeshwa kwa mara ya kwanza tarehe 17 Januari 2010, kufuatia muundo wa kipindi hiki tangu msimu wa nne.

Alasiri

Alasiri (kutoka Kiarabu) ni kipindi cha mchana kati ya adhuhuri na jioni, wakati ukali wa mwanga wa jua unapozidi kupungua.

Kwa kawaida wakati huo kwa binadamu unafuata mlo: hivyo utendaji wake unapungua pamoja na umakinifu wake. Ndiyo sababu ajali nyingi huwa zinatokea wakati huo.

Dini mbalimbali zenye ratiba ya sala, kwa mfano Ukristo na Uislamu, zina kipindi maalumu kwa alasiri.

Anga

Anga (mara nyingi pia: mbingu) ni uwazi ule mkubwa tunaoona juu yetu tukiinua kichwa nje ya jengo. Tukisimama kwenye tambarare au juu ya mlima kwenye mchana bila mawingu unaonekana kama nusutufe yenye rangi ya buluu. Ile buluu inaongezeka tukitazama juu zaidi kulingana na sehemu karibu na upeo. Wakati wa usiku anga ni jeusi lakini limejaa nuru za nyota.

Kwa lugha nyingine anga ni eneo la angahewa au upeo unaojaa hewa juu ya uso wa ardhi. Sehemu hiyo imejaa molekuli za gesi za angahewa hasa nitrojeni na oksijeni; ni molekuli hizo zinazoakisisha nuru ya jua na kusababisha rangi ya buluu ya anga wakati wa mchana. Bila hewa, anga lingekuwa jeusi muda wote jinsi lilivyo mwezini (linganisha picha).

Wakati wa mchana tunaona jua angani lisipofunikwa na mawingu. Wakati wa usiku tunaona mwezi na nyota zinazoonekana pia asubuhi na jioni ambako nuru ya jua haina nguvu bado au tena.

Mengine yanayoonekana angani ni mawingu, upinde wa mvua, ndege au eropleni.

Asubuhi

Asubuhi (kutoka Kiarabu: صباح) ni kipindi cha siku ambacho kinaleta mwanga wa kwanza wa mchana baada ya giza la usiku.

Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati wa kuamka kwa kutoka usingizini ili kuanza shughuli mbalimbali.

Katika dini mbalimbali, ni wakati muhimu wa sala.

Igagala

Igagala ni jina la kata ya Wilaya ya Kaliua katika Mkoa wa Tabora, Tanzania yenye postikodi namba 45709 . Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 23841 waishio humo.Kata hii imepiga hatua sana kimaendeleo,wakazi wake hujishughulisha sana na biashara, kilimo cha Tumbaku ambacho huwapatia fedha nyingi sana,Kijiji hiki hakina umeme lakini wakazi walio wengi hutumia umeme wa 'solar'. Kwa hiyo muda wa jioni watu huwa kwenye mishemishe ya hali ya juu.

Juma kuu

Juma kuu (kwa Kilatini: Hebdomas Maior, lakini kwa kawaida zaidi Hebdomas Sancta yaani "Wiki Takatifu"; kwa Kigiriki: Ἁγία καὶ Μεγάλη Ἑβδομάς, Hagia kai Megale Hebdomas, "Juma Takatifu na Kuu") ni juma la mwaka ambalo Wakristo wanaadhimisha kwa namna ya pekee matukio makuu ya historia ya wokovu kadiri ya imani yao, kuhusiana na mwisho wa maisha ya Yesu huko Yerusalemu, uliofuatwa na ufufuko wake.

Katika madhehebu mengi ya Ukristo, juma hilo linaanza na Jumapili ya matawi ambapo linaadhimishwa kwa shangwe tukio la Yesu Kristo kuingia huo mji mtakatifu kama mfalme wa Wayahudi huku akipanda punda na kushangiliwa na umati wa wafuasi wake, waliofurahia hasa alivyomfufua Lazaro wa Betania.

Lakini Yesu alieleza kuwa ufalme wake si wa dunia hii, na kuwa yeye hakuja kutumikiwa bali kutumikia na kutoa uhai wake uwe fidia ya umati.

Hivyo siku zilizofuata, hasa Ijumaa Kuu, alikabili kwa hiari mateso na kifo kutoka kwa wapinzani wake waliopitia mamlaka ya liwali Ponsio Pilato ili apewe adhabu ya kifo kwa kusulubiwa, na hatimaye akafufuka mtukufu usiku wa kuamkia Jumapili.

Kabla ya hapo Yesu alijumlisha hayo matukio yajayo katika karamu ya mwisho aliyokula pamoja na mitume wake 12, akiwaachia agizo la kufanya daima karamu ya namna hiyo kama ukumbusho wake.

Basi, kuanzia Alhamisi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni Wakristo wanaadhimisha siku tatu kuu za Pasaka, zinazofanya ukumbusho wa Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka kama ifuatavyo:

Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni: siku ya Kristo mteswa

Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni: siku ya Kristo mzikwa

Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni: siku ya Kristo mfufuka.Kuhusiana na Pasaka ya Kiyahudi, ni lazima Juma kuu litokee mwishoni mwa Machi au kabla ya wiki ya mwisho ya Aprili.

Ushahidi wa kwanza kuhusu ibada za pekee za Wakristo wakati huo unapatikana katika "Katiba za Mitume" (kwa Kiingereza: "Apostolical Constitutions", 18, 19), zilizoandikwa katika nusu ya pili ya karne ya 3 hadi karne ya 4. Humo ulaji wa nyama unakatazwa wiki nzima, na mfungo kamili unaagizwa kwa siku za Ijumaa na Jumamosi Kuu.

Barua ya Denis wa Aleksandria (260 BK) inaonyesha taratibu hizo zimeshakuwa desturi.

Kalenda ya Gregori

Kalenda ya Gregori ni kalenda ambayo leo inatumiwa zaidi kimataifa. Jina limetokana na Papa Gregori XIII aliyeamua kutumia kalenda hiyo tangu tar. 15 Februari 1582 badala ya Kalenda ya Juliasi.

Liturujia ya Vipindi

Liturujia ya Vipindi ni sala rasmi ya Kanisa kama inavyoadhimishwa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo, lakini ni jina hasa la mpangilio unaofuatwa na Kanisa la Roma baada ya Mtaguso wa pili wa Vatikano (kwa Kilatini jina ni Liturgia Horarum).

Kwa njia yake wakleri, watawa na waamini wote wa Yesu wa madhehebu hayo wanaungana naye katika sala yake ya kudumu, na wanasaidiwa kuishi kitakatifu saa zote za siku kwa kumkumbuka Mungu mara kwa mara.

Inaitwa hivyo kwa sababu inafanyika kwa vipindi mbalimbali kadiri ya mwendo wa siku (usiku na mchana): muhimu zaidi ni vipindi vya asubuhi (Masifu ya asubuhi) na jioni (Masifu ya jioni), lakini kuna pia vipindi vya usiku kati au alfajiri (Kipindi cha masomo), mchana (Sala ya kabla ya adhuhuri, Sala ya adhuhuri na Sala ya baada ya adhuhuri) na kabla ya kulala (Sala ya mwisho).

Katika Kanisa la Kilatini hiyo sala ya Kanisa inategemea hasa Biblia ya Kikristo kwa kutumia Zaburi na masomo kutoka kwake.

Matini yake yote yamekusanywa pamoja katika kitabu kimoja ambacho kwa sababu hiyo kilizoeleka kuitwa breviari (yaani: "matini kwa ufupi", badala ya kuzagaa katika vitabu mbalimbali kama zamani).

Magharibi

Magharibi ni moja kati ya mielekeo minne mikuu ya dira. Mwelekeo wake ni upande wa machweo ya jua.

Magahribi ni pia neno la kutaja saa ya sala ya jioni ya Waislamu na sala hii yenyewe.

Jina "magharibi" limetokana na neno la Kiarabu مَغْرِب maghrib linalomaanisha sehemu upande wa machweo.

Magharibi kawaida huwa upande wa kushoto kwenye ramani. Tanzania iko upande mwa magharibi ya Bahari Hindi, Burundi iko upande wa magharibi ya Tanzania, na nchi ya Malawi iko upande mwa magharibi ya Msumbiji.

Kwa maana ya kiutamaduni kuna uzoefu kutaja utamaduni wa Ulaya pamoja na Marekani (ambayo ni mtoto wa utamaduni wa Ulaya) kama "magharibi", kinyume chake ni "mashariki" kwa maana ya Asia.

Wakati wa vita baridi magharibi ilikuwa kifupi cha nchi za kibepari zilizofuata mtindo wa demokrasia kinyume na mashariki iliyomaanisha nchi za kikomunisti.

Masifu ya jioni

Masifu ya jioni ni kipindi muhimu zaidi cha Sala ya Kanisa katika madhehebu mbalimbali ya Ukristo.Ni sala rasmi inayofanyika wakati wa jua kuelekea kutua ili kumshukuru Mungu kwa siku inayokaribia kwisha.Katika utaratibu wa Kanisa la Roma, unaofuatwa na majimbo karibu yote ya Kanisa Katoliki la Kilatini, sehemu kuu za sala hiyo, kati ya utangulizi na baraka ya mwisho, ni utenzi, zaburi mbili (au moja ndefu iliyogawiwa pande mbili), wimbo kutoka Nyaraka za Mitume au kitabu cha Ufunuo, somo fupi au refu kutoka Agano Jipya, kiitikizano, wimbo wa Bikira Maria, maombezi, Baba Yetu na sala ya kumalizia.

Kati ya sehemu hizo, kilele ni maneno ya Injili (wimbo wa Bikira Maria na Baba Yetu).

Mchana

Mchana ni kipindi chote cha siku ambapo nuru ya jua inaangaza sehemu fulani ya dunia.

Kinyume chake ni usiku.

Kwa wakati mmoja, jua linaangaza karibu nusu ya dunia. Huko ni mchana, kumbe katika nusu ya pili ni usiku.

Kwa binadamu na wanyama wengi ndio wakati wa utendaji mwingi zaidi.

Morris O'Brian

Morris O'Brian ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika unachezwa na Carlo Rota.

Kama jinsi inavyoonekana katika Siku ya 6 (kuanzia saa 11 jioni hadi saa saa kumi na mbili magharibi), Morris anaonekana anaweza kuongea na kusikia kidoogo lugha ya Kirusi.

Muda sanifu wa dunia

Muda sanifu wa dunia (kufupi cha kitaalamu ni UTC kwa "universal time coordinated") ni utaratibu wa kulinganisha saa na wakati kote duniani. Unarejea wakati kwenye longitudo ya Greenwich karibu na London na longitudo hii huitwa pia meridiani ya sifuri.

Nguzo tano za Uislamu

Nguzo tano za Uislamu (kwa Kiarabu: أركان الإسلام arkan al-islam, pia أركان الدين arkan ad-din yaani nguzo za dini) ni ibada au matendo yanayoaminiwa kuwa ya kimsingi katika Uislamu. Zimepata hadhi maalumu kwa sababu zinatajwa katika "hadith ya Jibril". Kwenye masimulizi ya hadith ile malaika Jibril alimwuliza Mtume Muhammad "Uislamu ni nini?" na huyu alijibu kwa kutaja matendo matano yafuatayo.

Kwa kawaida hizi nguzo tano zinafundishwa katika madhehebu ya Wasunni jinsi inavyoonyeshwa hapo chini.

Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi wa nguzo tano, halafu wanaongeza "wilayat" yaani kukubali uongozi wa Maimamu kama nguzo ya tano.

Shahada: (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili: Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu.

Salat: (Kiarabu: صلاة‎) ni sala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya wudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na dua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari.

Zakat: (Kiarabu: زكاة‎‎) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri.

Funga/Saumu: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mwezi Ramadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo.

Hajj (Kiarabu: الحجّ alhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijja Maka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni.

Sabato

Sabato (kwa Kiebrania: שבת, shabbāt, yaani pumziko kwa Kiswahili) ni siku ya pumziko ya kila juma katika Uyahudi kwa ujumla na hasa katika nchi ya Israeli.

Msingi wa desturi hii ni masimulizi ya Biblia jinsi Mungu alivyomaliza kuumba mbingu na nchi akaona vema kupumzika siku ya saba.

Wayahudi tangu kale walijaribu kufuata mfano huu wakipumzika siku ile ya saba. Sabato husheherekewa kila Jumamosi kuanzia saa za jioni kwenye Ijumaa hadi jioni ya Jumamosi.

Wayahudi wakifuata dini huanza kwa sala ya jioni kwenye sinagogi halafu kwa chakula cha pekee.

Siku

Siku ni muda wa saa 24 ambamo tunaona vipindi viwili: kile cha mwanga wa mchana na kile cha giza la usiku.

Siku tatu kuu za Pasaka

Siku tatu kuu za Pasaka ndizo kiini cha mwaka wa Kanisa.

Zimekusudiwa kumuadhimisha Yesu mteswa, mzikwa na mfufuka, yaani:

siku ya kwanza (Alhamisi kuu jioni hadi Ijumaa kuu jioni) inaadhimisha mateso yake kuanzia karamu ya mwisho hadi kifo chake juu ya msalaba;

siku ya pili (Ijumaa kuu jioni hadi Jumamosi kuu jioni) inaadhimisha maiti yake kubaki kaburini na roho yake kushukia kuzimu;

siku ya tatu (kuanzia Jumamosi kuu jioni hadi Jumapili ya Pasaka jioni) inaadhimisha ufufuko wake mtukufu.Siku hizo tatu ni kama bawaba kati ya Kwaresima na kipindi cha Pasaka. Ingawa tarehe zinabadilika kila mwaka, zinaangukia daima kati ya Machi mwishoni na Aprili mwishoni.

Uislamu

Uislamu (kwa Kiarabu: الإسلام al-islam) ni dini inayotokana na mafunzo ya Mtume Muhammad.

Wafuasi wa imani hiyo huitwa "Waislamu" na wanakadiriwa kuwa milioni 1,400 hivi. Hivyo ni dini ya pili duniani yenye wafuasi wengi baada ya Ukristo wenye wafuasi milioni 2,200.

Uislamu ni ile imani kuwa muumba ni mmoja tu kwa dhati na sifa zake. Nguzo nyingine za imani zinajengwa juu ya imani ya Mungu mmoja wa kweli, imani juu ya maisha baada ya kifo, imani juu ya Malaika wa Mungu, vitabu vyake na kudra na tafsiri ya vitendo ya imani hii ni: Sala, Zakah, Saumu na Hija.

Usiku

Usiku ni kipindi cha siku kilichopo kati ya machweo na macheo na hasahasa kipindi cha giza kinachotokea baada ya machweo ambapo mwanga wa jua hauonekani tena angani hadi muda mfupi kabla ya macheo yaani kabla ya jua kuonekana juu ya upeo wa anga.

Kinyume chake ni mchana.

Kutokana na kupoteapotea kwa nuru ya jua, nyota zinaonekana usiku (pasipo mawingu).

Watu wengi pamoja na wanyama wengi hulala usiku, lakini kuna wanyama wengine wanaofanya shughuli zao usiku kama vile bundi, popo na wadudu wengi.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.