Jenasi

Jenasi (kutoka Kigiriki Γένος genos / Kilatini genus "nasaba, ukoo, familia, aina")[1] ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi unaopanga viumbehai (mimea, wanyama) katika vikundi kulingana na nasaba zao.

Jenasi moja huwa na spishi ndani yake. Jenasi kwa pamoja hupangwa katika familia.

Katika jina la Kisayansi la kiumbehai ni lazima kutaja jenasi. Kwa mfano paka anaitwa "Felis silvestris catus". Felis ni jina la jenasi. Jenasi huandikwa kwa herufi kubwa.

Uainishaji
Ngazi za uainishaji katika biolojia; ngazi ndogo za kati hazionyeshwi

Maelezo

  1. kwa uwingi wa jenasi kuna pia neno "jenera" ambayo ni uwingi wa Kilatini unaotumiwa pia kwa Kiingereza
Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Jenasi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Alcelaphinae

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Alcelaphinae ni nusufamilia ndogo katika familia Bovidae. Spishi zake zinafanana na kongoni. Nusufamilia hii ina jenasi nne ndani yake:

Alcelaphus (Kongoni)

Beatragus (Hirola)

Connochaetes (Nyumbu)

Damaliscus (Nyamera na Sasabi)

Angiospermae

Angiospermae (yaani mimea inayochanua maua; kwa Kiingereza: angiosperms; pia Magnoliophyta) ndilo kundi kubwa zaidi la mimea ya nchi kavu (Embryophyte) likiwa na oda 64, familia 416, jenasi 13,000 na spishi zinazojulikana 300,000 hivi.

Binadamu

Binadamu (pia mwanadamu) ni neno linalomaanisha "Mwana wa Adamu", anayeaminiwa na dini za Uyahudi, Ukristo na Uislamu kuwa ndiye mtu wa kwanza.

Bubalus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bubalus ni jenasi katika nusufamilia Bovinae. Spishi zake zinafanana na nyati-maji. Jenasi hii ina spishi sita ndani yake:

B. arnee (Nyati-maji wa mwitu)

B. bubalis (Nyati-maji)

B. depressicornis (Anoa)

B. mephistopheles (Nyati-maji pembe-fupi)

B. mindorensis (Tamarau)

B. quarlesi (Anoa-milima)

Carl Linnaeus

Carl Linnaeus (tamka: Karl Lineus; pia kwa umbo la Kilatini Carolus Linnaeus na baadaye Carl von Linné; 23 Mei 1707 – 10 Januari 1778) alikuwa mwanasayansi nchini Uswidi aliyeweka misingi ya biolojia ya kisasa kwa kuunda utaratibu wa taksonomia au uainishaji wa mimea na wanyama katika vikundi mbalimbali na kuvipa majina ya kisayansi.

Cervidae

Kulungu (jina la kisayansi: Cervidae) ni jina la kawaida wa wanyama wa Ulaya, Asia au Amerika wanaofanana na kulungu.

Familia (biolojia)

Familia ni ngazi katika uainishaji wa kisayansi wa viumbehai. Familia ya wanyama au mimea hujumlisha spishi mbalimbali zilizo karibu.

Kwa mfano paka-kaya ni spishi mojawapo pamoja na spishi 41 nyingine ndani ya familia ya Felidae inayojumlisha paka pamoja na chui, simba, tiger n.k.

Ndani ya familia kuna jenasi mbalimbali (zinazojumlisha spishi za karibu zaidi); kila familia ni sehemu ya ngazi ya juu zaidi inayoitwa oda. Familia ya Felidae (wanyama wanaofana na paka) ni sehemu ya oda ya Carnivora au wanyama wala nyama.

Kwa kawaida majina ya kisayansi ya kila familia huishia kwa

- "idae" kama ni familia ya wanyama au

- "aceae" kama ni failia ya mimea.

Familia kubwa sana zinaweza kugawiwa katika nusufamilia; vilevile oda kubwa sana inaweza kuwa na familia kubwa za kujumlisha ngazi ya familia.

Korongo (Bovidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Korongo au kolongo ni spishi ya kawaida zaidi ya jenasi Hippotragus katika familia Bovidae. Spishi nyingine inaitwa palahala au mbarapi. Hawa ni wanyama wakubwa ambao wanatokea savana za Afrika zenye miti. Rangi ya madume ni kahawia hadi nyeusi, rangi ya majike ni kahawia. Kuna mabaka meusi na meupe kichwani, lakini hayaonekani sana kwa korongo buluu; tumbo ni jeupe. Dume na jike wana pembe ndefu zilizopindika kuelekea nyuma ambazo urefu wao unaweza kufika mita moja au zaidi lakini fupi zaidi kwa jike. Wanyama hawa hula manyasi marefu kiasi.

Kuro (jenasi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kuro ni spishi ya kawaida zaidi ya jenasi Kobus katika familia Bovidae. Spishi nyingine za jenasi hii zinaitwa lechwe, mraye na sheshe. Kuna nususpishi mbili za kuro: (kuro) ndogoro na kuro singsing. Spishi zote zinatokea karibu na maji na hutorokea maji wakitishwa na mnyama mbua. Rangi ya spishi nyingi ni ya mchanga lakini rangi ya kuro na spishi nyingine kadhaa ni kahawia hadi kijivu au nyeusi. Mara nyingi iko rangi ya nyeupe kuzunguka macho na pua na matako. Wanyama hawa hula manyasi.

Lama (mnyama)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Lama ni mnyama wa kufugwa wa spishi Lama glama katika familia Camelidae, anayeishi Amerika Kusini. Lama ametumiwa kwa upana na watu wa milima ya Andes tangu kabla ya historia, kwa nyama yake na kubeba mizigo.

Muhogo

Muhogo (Kiing. cassava) ni mmea wa jenasi Manihot na chakula muhimu katika Afrika, Amerika Kusini na nchi za Asia Kusini. Sehemu ya kuliwa ni hasa viazi vyake (mizizi minene au mahogo) vilivyo na wanga nyingi halafu pia majani yake yenye protini na vitamini.

Mwaridi

Mwaridi ni mti, kichaka au mtambaa wenye miiba na maua yanukiayo vizuri. Kwa asili jina hili limetumika kwa Rosa x damascena, lakini siku hizi hutumika kwa spishi zote za jenasi Rosa. Jenasi hii ni jenasi-mfano ya familia Rosaceae. Maua huitwa mawaridi au halwaridi.

Nyamera (jenasi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyamera ni wanyamapori wakubwa wa jenasi Beatragus na Damaliscus katika familia Bovidae. Kwa asili jina hili lilitumika kwa nususpishi D. korrigum topi, lakini siku hizi spishi na nususpishi zote huitwa nyamera mara nyingi. Majina mengine ni hirola, jimela, sasabi na tiang. Wanatokea savana za Afrika tu. Rangi yao ni ya mchanga inayoelekea nyekundu au kijivu mara nyingi. Wana mabaka meusi mwilini, miguuni na kichwani, isipokuwa hirola, na nyamera baka-nyeupe ana baka nyeupe kwa pua na paji. Kichwa chao ni kirefu kama kile cha kongoni lakini pembe zao hazina umbo wa zeze. Wanyama hawa hula manyasi.

Orangutanu

Orangutanu ni spishi za sokwe katika jenasi Pongo. Orangutanu wanaishi katika misitu ya mvua ya Borneo na Sumatra, visiwa vikubwa vya Indonesia.

Pofu (jenasi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pofu, mbungu au mbunju ni wanyamapori wa jenasi Taurotragus katika familia Bovidae. Wanatokea savana zenye miti katika Afrika. Wanyama hawa ni wakubwa kuliko spishi nyingine za Bovidae za Afrika. Rangi yao ni kahawianyekundu, kahawia, hudhurungi au kijivu na mara nyingi wana milia ya wima mbavuni. Wana ngozi ndefu chini ya koo lao. Pembe zao ni ndefu kiasi, zile za jike ndefu kuliko zile za dume.

Shomoro

Shomoro ni ndege wadogo wa jenasi Passer katika familia ya Passeridae ambao wana rangi ya nyeusi, nyeupe, majivu na kahawia. Ndege hawa huitwa korobindo pia, lakini jina hili litumiki afadhali kwa kuita ndege wa jenasi Petronia. Shomoro wenye kichwa kijivu huitwa jurawa. Ndege hawa wana domo fupi na nene lifaalo kula mbegu, lakini hula wadudu wadogo pia hasa wanapokuwa vifaranga. Kwa asili shomoro wanatokea Ulaya, Afrika na Asia, lakini watu wamewaletea Australia na Marekani.

Spishi

Spishi (kutoka Kilatini "species", yaani: aina, maumbile) katika biolojia ni jina la kutaja kundi la wanyama au mimea wa aina moja. Spishi ni kitengo muhimu katika uainishaji wa kisayansi.

Kwa kuhesabiwa katika spishi ileile haitoshi kama viumbe vinafanana sana, ni lazima waweze kuzaliana na kuwa na watoto ambao wanaweza kuzaa tena.

Kwa mfano, farasi na punda ni spishi mbili tofauti zinazoweza kuzaliana lakini watoto wao, wanaoitwa baghala, hawazai tena. Mbwa wote ni spishi moja, hata kama wanaonekana na maumbile tofauti kutokana na historia ya ufugaji wa kuteua sifa kadhaa tu kwa kuzaana. Lakini hata mbwa mkubwa kabisa anaweza kuzaliana na mbwa mdogo na watoto wao wanazaa tena.

Spishi za karibu hupangwa pamoja katika jenasi.

Mfano: mbwa, mbweha, mbweha wa Ethiopia na koyote wa Marekani wote ni spishi mbalimbali za jenasi inayoitwa "Canis".

Uainishaji wa kisayansi

Uainishaji wa kisayansi (ing. biological classification, taxonomy) ni jinsi wataalamu wa biolojia wanavyopanga viumbehai kama mimea na wanyama kwa vikundi kwenye ngazi mbalimbali. Inaweza kuitwa pia taksonomia.

Tangu muda mrefu watu walitambua ya kwamba wanyama au mimea mbalimbali wanafanana kati yao kwa namna moja au nyingine. Wataalamu walijaribu kupanga aina hizo kwa vikundi vyenye tabia za pamoja. Carolus Linnaeus alianza kuzipanga kwa muundo ulioeleweka kulingana na tabia za maumbile yao.

Mfumo wa Linnaeus uliendelezwa baadaye kulingana na nadharia ya Charles Darwin inayoona ya kwamba spishi mbalimbali huwa na chanzo cha pamoja, kwa hiyo inawezekana kupanga uhai wote kama mti yenye matawi makubwa, tena madogo yanayotoka kwenye makubwa.

Ujuzi wa kisasa kutokana na utafiti wa DNA ndani ya seli za viumbehai unaendelea kuongeza ujuzi wetu kwa hiyo katika mengi uainishaji ni utaalamu unaozidi kubadilika.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.