Israeli ya Kale

Israeli ya Kale ni jina la watu au taifa walioitwa taifa teule katika Tanakh au Biblia ya Kiebrania (kwa hiyo pia katika Agano la Kale lililo sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kihistoria waliishi katika nchi iliyoitwa Kanaani, halafu Israeli (baadaye pia Palestina) kuanzia mnamo 1200 KK hadi mnamo mwaka 70 BK Waroma wa Kale walipovamia na kuharibu Yerusalemu, ambao tena mwaka 135 waliwafukuza wote kutoka nchi yao.

Wenyeji walijiita mwanzoni Wanaisraeli na baadaye pia Wayahudi.

Map Israel Judea 926 BC-fr
Ramani ya Israeli ya Kale mnamo mwaka 926 wakati wa kugawiwa kwa ufalme wa pamoja
kijani nyeusi: Ufalme wa Israeli na makabila yake (kaskazini)
ijani nyeupe: Ufalme wa Yuda na makabila yake (kusini);
Philiste: nchi ya Wafilisti

Mwanzo na mwisho wa historia ya Israeli ya Kale

Historia ya Israeli ya Kale inaanza tangu kupatikana kwa taifa hilo katika nchi yake inayoitwa Israeli. Kufuatana na masimulizi ya Agano la Kale taifa la Israeli lilianzishwa na Wanaisraeli waliotoka Misri chini ya uongozi wa Musa na kuvamia Kanaani mnamo mwaka 1200 KK chini ya Yoshua.

Wataalamu wengine wa kisasa wanaona ya kwamba taifa lilitokea hasa ndani ya nchi kwa kuungana kwa vikundi mbalimbali.

Muungano huo wa vikundi na makabila ukawa taifa na kuunda ufalme wa kwanza wa Israeli wakati wa mfalme Sauli aliyefuatwa na Daudi na mwanae Suleimani.

Baada ya kifo cha Suleimani likatokea farakano na jina la "Israeli" likatumiwa na ufalme wa kaskazini, wakati mji mkuu wa kale Yerusalemu ukaendelea kama mji mkuu wa ufalme wa Yuda.

Falme zote mbili zilishindwa katika vita na kuanzia mwaka 587 KK hapakuwa tena na dola la kujitegemea, bali eneo lilikuwa chini ya falme mbalimbali kama vile Babiloni, Uajemi na Ugiriki wa Kale.

Lakini harakati za Wamakabayo za kurudisha uhuru uliweza kuwafukuza Wagiriki na kuanzisha ufalme wa Kiyahudi kati ya 140 KK hadi 4 KK.

Hata hivyo kuanzia mwaka 63 KK ufalme huo uliwekwa chini ya ulinzi wa Dola la Roma na polepole kugawiwa na hatimaye kuwa jimbo la Kiroma (tangu 70 BK).

Maangamizi ya Yerusalemu mwaka 70 BK huhesabiwa kama mwisho wa Israeli ya Kale. Wataalamu wengine wanaona tayari uvamizi wa mji wa 587 KK na Wababeli kama mwisho wa kipindi hiki na kuangalia kipindi kati ya 587 KK hadi 70 BK kama kipindi kipya.

Israeli wakati wa Yesu

Wakati wa Agano Jipya, mji wa Yerusalemu, pamoja na nchi ya Israeli/Palestina, vilikuwa chini ya Dola la Roma, ambalo lilitawala maeneo yote yanayozunguka bahari ya Mediteranea. Mkuu wa Dola alikuwa na cheo cha "Kaisari" akikaa mjini Roma (Italia).

Waroma walidai utiifu na kodi za mataifa na makabila yote yaliyokuwa chini yao. Lakini hawakuwa na neno juu ya utamaduni na dini za nchi hizo.

Utawala wa Kiroma ulirahisisha biashara na uchumi pamoja na mawasiliano katika maeneo haya yote. Waroma hawakuwa na mitambo ya injini lakini walikuwa wataalamu wa uhandisi. Walikuwa hodari sana kujenga barabara na nyumba za ghorofa. Majengo kadhaa waliyoyajenga husimama mpaka leo. Magofu ya miji yao yanaonekana leo hii kuanzia Misri na Algeria hadi Ujerumani na Asia. Wasanii wao walichonga sanamu za mawe za kudumu.

Israeli/Palestina ilikuwa na serikali yake ya Kiyahudi lakini pia na liwali au gavana wa Kiroma. Waroma walizima kwa ukali majaribio yote ya kupindua utawala wao. Wayahudi katika Israeli walijaribu mara mbili kuwafukuza Waroma nchini: miaka 66-73 na 135 BK. Kila safari Waroma walilipiza kisasi, wakichoma moto miji na vijiji na kuwafanya wananchi kuwa watumwa au kuwaua kabisa.

Viungo vya Nje

Daudi (Biblia)

Daudi (kwa Kiebrania דוד, Daud, kwa Kiarabu داوُد, Dāwūd) alikuwa mfalme wa pili wa Israeli ya Kale mnamo 1010 KK-970 KK. Alimfuata mfalme Sauli akafuatwa na Suleimani.

Alizaliwa na Yese mjini Bethlehemu mnamo 1040 KK.

Kama kijana alipelekwa kwenye jumba la mfalme Sauli alipopanda ngazi na kuwa kiongozi wa kijeshi.

Kati ya matendo yake yaliyokumbukwa zaidi ni ushindi juu ya Mfilisti Goliathi.

Pamoja na makosa yake, Daudi akabaki kielelezo cha mfalme wa Israeli, ambaye awe tofauti na watawala wengine wote kwa kuwa hasa mtumishi mnyenyekevu wa Mungu bila ya kuyumba kwa kuelekea miungu mingine.

Hagia Sophia

Hagia Sophia ni jina la Kigiriki la kanisa kubwa mjini Istanbul - Konstantinopoli lililobadilishwa kuwa msikiti tangu 1453 na halafu kuwa makumbusho mwaka 1934.

Jina linatokana katika Kigiriki Ἅγια Σοφία ("hekima takatifu") na kwa Kituruki inaitwa Ayasofya.

Ujenzi wa kanisa ulianzishwa mwaka 532 na Kaisari Justiniani I mtawala wa Roma ya Mashariki au Ufalme wa Byzanti. Alitaka kuwa na kanisa kubwa kuliko yote duniani akafaulu kwa sababu Hagia Sofia ilikuwa ukumbi mkubwa duniani hadi mwaka 1520. Jengo lilikamilishwa baada ya miaka mitano na Justiniani alipoingia mara ya kwanza aliita "Suleimani nimekushinda", akimfikiria mfalme Suleimani wa Israeli ya Kale aliyejenga hekalu la Yerusalemu.

Mwaka 1453 Waturuki Waislamu waliteka mji wa Konstantinopoli na kuifanya mji mkuu wa Dola la Osmani. Hapo Hagia Sofia likabadilishwa kuwa msikiti na Waturuki wakatamka jina la kigiriki kama "Ayasofya". Jengo la kanisa likaongezekwa minara minne ya mtindo wa Kiislamu.

Baada ya anguko la Waosmani katika vita kuu ya kwanza ya dunia kiongozi wa taifa Kemal Atatürk akaamuru jengo liwe makumbusho.

Hekalu la Yerusalemu

Hekalu la Yerusalemu lilikuwa kitovu cha ibada za dini ya Uyahudi wakati wa Israeli ya Kale.

Kwa jumla kulikuwa na majengo mawili yaliyofuatana kwenye mlima wa hekalu mjini Yerusalemu.

Imani ya Kiyahudi inategemea kujengwa kwa hekalu la tatu pamoja na kuja kwa Masiya wakati ujao.

Katika imani hiyo sehemu ya Patakatifu pa Patakatifu ndani ya hekalu ilikuwa mahali ambapo Mungu mwenyewe aligusa dunia.

Israel

Kwa maana mbalimbali za jina Israeli katika Biblia tazama Israeli (maana)

Israel (kwa Kiebrania: מדינת ישראל - Medinat Yisra'el; kwa Kiarabu: دَوْلَةْ إِسْرَائِيل - dawlat Isrā'īl) ni nchi ya Mashariki ya Kati kwenye mwambao wa mashariki wa Mediteranea.

Imepakana na Lebanon, Syria, Yordani, Misri na maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya serikali ya Palestina.

Israeli (maana)

Israeli ni jina linalotaja

Nchi ya Israeli ya kisasa

Israeli ya Kale ambayo ni nchi au pia jumuiya ya watu ambao historia yao husimuliwa katika Biblia.Watu wa Biblia wanaotajwa katika Tanakh au Biblia ya Kiebrania; kwa hiyo pia katika Agano la Kale tena katika Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo

Yakubu mwana wa Isaka mwana wa Ibrahimu (Abrahamu) alipewa jina la Israeli baada ya kushindana na Mungu (tazama Mwanzo (Biblia) 32,29 "maana umeshindana na Mungu na watu nawe umeshinda")

jina la pamoja kwa ajili ya makabila 12 waliotokana na wana 12 wa Yakobo-Israeli, mara nyingine kwa umbo la Wanaisraeli

jina la milki ya kaskazini ya Israeli (milki) iliyoanzishwa baada ya kifo cha mfalme Suleimani kando ya milki ya Yuda; historia ya hizo mbili kwa jumla hujadiliwa chini ya jina "Israeli ya Kale".

Baada ya maangamizi ya milki ya kaskazini katika vita dhidi ya Waashuri jina lilitumiwa kwa ajili ya watu wa milki ya kusini yaani watu wa milki ya Yuda

Baada ya maangamizi ya milki hiyo pia jina lilitaja Wayahudi kama jumuiya ya kidini na taifa lililokaa katika sehemu mbalimbali (linganisha matumizi katika Agano Jipya kwenye Waraka kwa Waroma 9,6 na 11,25)

Kwa kutaja Wayahudi jina latumiwa katika Qurani mara nyingi kama "wana wa Israeli"

Kwa watu wanaoitwa taifa teule katika Agano la Kale tazama kwa jumla Israeli ya KaleIsraeli ni pia jina la kawaida la mwanamume kati ya Wayahudi hadi leo

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Habakuki

Habakuki ni jina la nabii wa Israeli ya Kale na pia la kitabu kinacholeta habari zake katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), na kwa hiyo pia katika Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme

Kitabu cha Kwanza cha Wafalme ni sehemu ya Tanakh (Biblia ya Kiebrania na ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo. Hugawiwa katika sura 22.

Kuhani mkuu

Kuhani mkuu ni cheo kikuu cha kuhani katika dini zenye ngazi mbalimbali ya ukuhani. Kwenye mahekalu makubwa yenye makuhani wengi, mmoja aliweza kuwa na nafasi ya kiongozi na kuitwa kuhani mkuu.

Katika dini za Sumeri, Babeli na Misri ya Kale walikuwepo pia makuhani wakuu waliokuwa viongozi wa dini kwa ufalme wote. Katika Babeli kulikuwa pia na makuhani wakuu wa kike.

Mashariki ya Kati

Mashariki ya Kati (kwa Kiingereza Middle East) ni namna ya kutaja sehemu kubwa ya Asia ya Magharibi pamoja na Afrika ya kaskazini-mashariki, hasa Misri.

Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa humo:

Nchi za Bara Arabu, zikiwa pamoja na Saudia, Yemen, Oman, Falme za Kiarabu, Katar na Kuwait,

Nchi za Shamu ya kihistoria, zikiwa pamoja na Syria, Lebanon, Israel na Palestina, Yordani

Iraq

Uajemi

Uturuki

Misri (ambayo iko upande wa Afrika isipokuwa rasi ya Sinai)Nchi hizo zinatajwa pamoja kwa sababu zina historia ya pamoja na utamaduni wa karibu.

Moabu

Moabu (kwa Kiebrania מוֹאָב Mo'av au Môʼāḇ, "Mbegu ya baba"; kwa Kigiriki Μωάβ Mōav; kwa Kiarabu مؤاب) ni jina la kihistoria la eneo la milimani upande wa mashariki wa Bahari ya Chumvi ndani ya nchi ya kisasa ya Yordani. Ilikuwako kati ya Edomu upande wa kusini na Amoni upande wa kaskazini.

Zamani eneo hilo lilikuwa ufalme wa Wamoabu. Mji wake mkuu uliitwa Diboni na maghofu yake yapo karibu na mji wa Dhiban wa kisasa.

Kati ya shuhuda za kiakiolojia za kabila hilo, muhimu zaidi ni Jiwe la Mesha, linaloeleza ushindi wao dhidi ya mwana wa mfalme Omri wa Israeli.

Sawa na Isreli Moabu ilikuja chini ya mamlaka kwanza ya Ashuru na baadaye ya milki ya Babeli. Mwaka 582 KK mfalme Nebukadnezzar II wa Babeli alifanya Moabu kuwa sehemu ya milki yake; hivyo ilikuwa sehemu ya ufalme wa Uajemi baadaye. Wakati wa utawala wa Kiajemi Moabu ilipotea kama taifa la pekee. Makabila ya Waarabu walianza kuingia na kukalia sehemu kubwa za nchi na wakazi waliacha lugha yao wakatumia Kiaramu badala ya lugha yao ya awali.

Nabii Obadia

Nabii Obadia (jina la Kiebrania lenye maana ya "Mtumishi wa YHWH) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale baada ya Yerusalemu kutekwa na kuteketezwa na Wababuloni (586 KK hivi).

Alitoa utabiri wa mistari 21 tu dhidi ya Edomu ambayo inaunda kitabu cha nne kati ya 12 vya Manabii Wadogo.

Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 19 Novemba.

Nabii Yoeli

Nabii Yoeli (kwa Kiebrania יואל, Yoel, maana yake YHWH ni Mungu) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale, labda katikati ya karne ya 4 KK.

Ujumbe wake unapatikana katika gombo la Manabii Wadogo la Biblia, kwa jina la Kitabu cha Yoeli.

Anaheshimiwa kama mtakatifu. Sikukuu yake huwa tarehe 19 Oktoba.

Sinagogi

Sinagogi (au sunagogi) ni nyumba ya dini na ya jamii ya Wayahudi inayotumika hasa kusali.

Ufalme

Ufalme ni mfumo wa utawala ambako mfalme, malkia au mtu mwingine aliyerithi cheo chake ni mkuu wa dola. Vyeo vingine vya mkuu katika ufalme ni pamoja na kaisari, shah, tenno, sultani, amiri au mtemi. Kwa kawaida mfalme amerithi cheo chake kutoka kwa babake au mamake kwa hiyo alizaliwa kama mfalme mteule na ataendelea kuwa na cheo hiki hadi kifo chake. Lakini kama mfalme aliyetangulia hakuwa na mrithi inawezekana ya kwamba mfalme mpya amechaguliwa. Mfano wa dola lenye mfumo wa ufalme ambako mkuu anachaguliwa mara kwa mara ni Vatikani ambao Papa ni mkuu wa dola.

Neno ufalme hutumiwa pia kwa kutaja nchi inayotawaliwa na mfalme au malkia, kwa mfano Ufalme wa Maungano, Ufalme wa Uswazi na kadhalika.

Kiwango cha madaraka cha mfalme huwa na tofauti kubwa. Leo hii karibu wafalme wengi wako chini ya katiba ya nchi na mara nyingi wana madaraka machache; nafasi yao ni ya heshima na desturi. Lakini kuna falme kadhaa ambako mfalme bado ana madaraka makubwa habanwi na katiba wala bunge wala serikali kama vile Omani au Saudia.

Utumwa

Utumwa ni mfumo unaotoa fursa kwa binadamu kummiliki binadamu mwenzake kama mali yake. Binadamu anayemilikiwa anakuwa na hadhi sawa na chombo au kifaa chochote kinachoweza kuuzwa.

Mfumo huu ulianza kabla ya uandishi kubuniwa, ukawa maarufu hasa kabla ya harakati za ukoloni duniani, mathalani kuanzia karne ya 15, ambapo watumwa walihitajika katika shughuli za kilimo na uchimbaji madini katika sehemu mbalimbali za ulimwengu, hasa Amerika, ingawa katika sehemu nyingine, hasa Uarabuni, walitafutwa hasa watumwa wanawake kwa ajili ya uasherati.

Mfumo huu huunda matabaka ya "mabwana" ambao humiliki watumwa na "watwana" ambao ni watumwa wenyewe.

Wanaisraeli

Kwa maana mbalimbali ya jina Israeli tazama Israeli (maana)

Wanaisraeli ni namna ya kutaja watu wa Agano la Kale waliokuwa wazawa wa Yakobo aliyeitwa pia Israeli, mmoja wa mababu wa taifa la Israeli ya Kale pamoja na babu yake Abrahamu na baba yake Isaka.

Kadiri ya kitabu cha Mwanzo Yakobo alipewa na Mungu jina la "Israeli" baada ya kushindana naye kwenye mto Yaboki.

Alizaa wana wa kiume 12 waliokuwa mababu wa makabila 12 ya Israeli ya Kale.

Katika maandiko ya Biblia ya Kiebrania (Tanakh) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo makabila haya mara nyingi huitwa "Waisraeli", "wana wa Israeli" au pia "watu wa Israeli".

Kwa historia yao angalia Israeli ya Kale.

Wayahudi

Wayahudi (kwa Kiebrania יְהוּדִים, Yehudim) ni kundi la kikabila na la kidini lenye asili yake katika eneo la Israeli ya Kale (Mashariki ya Karibu). Kabila la Kiyahudi, taifa la Kiyahudi na dini ya Kiyahudi yote yana uhusiano wa karibu sana, kwa sababu Uyahudi ndio dini ya jadi ya watu wa taifa la Kiyahudi

Wanaobadilika kuwa Wayahudi, ambao hadhi yao kama Wayahudi katika kabila la Kiyahudi ni sawa na wale ambao wamezaliwa kuingia kabila hilo, wameingizwa ndani ya kundi la watu wa Kiyahudi tangu jadi.

Katika utamaduni wa Kiyahudi, ukoo unarudi nyuma hadi kwa mababa wa Biblia kama vile Abrahamu, Isaka na Yakobo katika milenia ya 2 KK.

Wayahudi wamefurahia enzi tatu za uruhu wa kisiasa katika nchi yao ya nyumbani, Nchi ya Israel, mara mbili wakati wa historia ya kale, na mara nyingine tena, kuanzia mwaka wa 1948, wakati ambapo taifa la kisasa la Israeli lilipoanzishwa. Enzi ya kwanza ilianza mnamo mwaka wa 1350 hadi 586 KK, na ilijumuisha vipindi vya Mahakimu, Milki iliyoungana na Miliki zilizogawanywa za Israeli na Yudea, na ilisha wakati wa kuharibiwa kwa thehebu la kwanza la Solomoni.

Enzi ya pili ilikuwa kipindi cha Milki ya Hasmonea iliyoanza mnamo mwaka wa 140 hadi mwaka wa 37 KK. Tangu kuharibiwa kwa Thehebu la Kwanza, nchi geni ndizo zimekuwa kama nyumbani kwa Wayahudi wengi wa Dunia. Isipokuwa katika taifa la kisasa la Israeli, Wayahudi ni wachache katika kila nchi wanamoishi, na mara nyingi wameteswa katika kipindi chote cha historia, kusababisha idadi yao kupanda na kushuka katika karne zilizopita.

Yesu

Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).

Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.

Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.