Israel

Kwa maana mbalimbali za jina Israeli katika Biblia tazama Israeli (maana)

מדינת ישראל
Medīnat Yisrā'el
دولة إسرائيل
Dawlat Isrā'īl

Israel
Bendera ya Israel Nembo ya Israel
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: -
Wimbo wa taifa: Hatikvah ("Tumaini")
Lokeshen ya Israel
Mji mkuu Yerusalemu1
{{{latd}}}°{{{latm}}}′ {{{latNS}}} {{{longd}}}°{{{longm}}}′ {{{longEW}}}
Mji mkubwa nchini Yerusalemu
Lugha rasmi Kiebrania, Kiarabu
Serikali Jamhuri, serikali ya kibunge
Reuven Rivlin
Benjamin Netanyahu
Uhuru
Tangazo la uhuru

14 Mei 1948 (05 Iyar 5708)
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
20,770 km² (ya 153)
~2
Idadi ya watu
 - Desemba 2016 kadirio
 - 2008 sensa
 - Msongamano wa watu
 
8,602,0002 (ya 96)
7,412,200
391/km² (ya 35)
Fedha Shekel (₪) (ILS)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
IST (UTC+2)
(UTC+3)
Intaneti TLD .il
Kodi ya simu +972
1 Haujatambuliwa kama mji mkuu na nchi nyingi duniani.
2 pamoja na raia wa Iaraeli kwenye maeneo ya Palestina, Yerusalemu ya Mashariki na Golan.


Israel (kwa Kiebrania: מדינת ישראל - Medinat Yisra'el; kwa Kiarabu: دَوْلَةْ إِسْرَائِيل - dawlat Isrā'īl) ni nchi ya Mashariki ya Kati kwenye mwambao wa mashariki wa Mediteranea.

Imepakana na Lebanon, Syria, Yordani, Misri na maeneo yaliyo chini ya mamlaka ya serikali ya Palestina.

Historia

Nchi ya kisasa ilianzishwa tarehe 14 Mei 1948 lakini nyuma kuna historia ndefu, ambayo kwa sehemu muhimu inasimulia na Biblia kama kiini cha historia ya wokovu.

Mji mkuu umekuwa Yerusalemu tangu mwaka 1950 lakini nchi nyingi hazikubali kuwa hivyo kwa sababu hali yake kadiri ya Sheria ya kimataifa haieleweki.

Watu

Takriban 74.9% za wakazi ni Wayahudi ambao wengi wao wanafuata dini ya Uyahudi, na 20.7 % ni Waarabu ambao wengi ni Waislamu (16%) lakini pia Wakristo (2% za raia wote: kati ya Wakristo hao karibu 80% ni Waarabu). Wahamiaji wengi wasiopata uraia ni Wakristo.

Lugha rasmi ni Kiebrania na Kiarabu. Lugha nyingine zinazotumika sana nyumbani ni Kirusi, Kifaransa na Kiamhari, mbali ya Kiingereza.

Tazama pia

Viungo vya nje

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Kirgizstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
BlankAsia Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Israel kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Asia ya Magharibi

Asia ya Magharibi (inalingana kwa kiasi kikubwa na jina la Mashariki ya Kati) ni sehemu ya magharibi-kusini ya bara la Asia. Inatajwa kati ya kanda za dunia ya UM.

Bahari ya Mediteranea

Bahari ya Mediteranea (pia: Bahari ya Kati) ni bahari ya pembeni ya Atlantiki kati ya mabara ya Afrika, Ulaya na Asia ya Magharibi. Eneo lake ni takriban milioni 2,5 km². Kina chake kirefu ni 5,267 m. Ina kanda ya hali ya hewa ya pekee pamoja na mimea na wanyama.

Neno "Mediteranea" limetokana na lugha ya Kilatini likiunganisha maneno ya "medium" (inamaanisha "kati ya, katikati") na "terra" (inamaanisha "bara"). Kwa hiyo neno lenyewe linamaanisha "Bahari katikati ya bara".

Katika lugha ya Biblia Kiebrania iliitwa "Bahari ya Magharibi" au "Bahari Kuu"; Waroma wa Kale waliotwala nchi zote zinazopakana na Bahari ya Mediteranea waliita "mare nostrum" yaani "bahari yetu". Waarabu na Waturuki wanaiita "Bahari Nyeupe" (kwa Kituruki: Akdeniz; kwa Kiarabu: البحر الأبيض al-baHr-al-abyaD)

Galilaya

Galilaya (kutoka Kiebrania הגליל (ha-galil), yaani "mzunguko" au "mkoa"; kiasili "galil ha-goyim - mkoa wa wapagani")

ni mkoa maarufu kihistoria upande wa kaskazini mwa Israeli au Palestina.

Upande wa mashariki mpaka wake ni mto Yordani, ambao sehemu hiyo unaunda ziwa Genesareti (pia: bahari ya Galilaya).

Waisraeli walipotoka Misri na kuteka nchi ya Kanaani, katika mkoa huo walihamia watu wa makabila ya Dan, Zebuluni, Isakari na Naftali.

Galilaya ndio mkoa ambapo alikulia na kuanza utume wake Yesu, mwanzilishi wa Ukristo.

Kati ya miji na vijiji vya Galilaya vilivyotajwa katika Injili kuna:

Bethsaida

Kafarnaumu

Kana

Korozain

Nain

Nazareti

Tiberia

Kiarabu

Kiarabu (ar.: العَرَبِيَّة‎‎, al-ʻarabiyyah, kwa kirefu al-luġatu al-ʿarabiyya ) ni lugha ya Kisemiti inayotumiwa na watu milioni 206 kama lugha ya kwanza na milioni 246 wa ziada kama lugha ya pili. Ilhali kuna lahaja nyingi, Kiarabu sanifu (ar. الفصحى fuṣḥā) ni lugha rasmi ya nchi 22 za Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na ya Mkutano wa Kilele wa Kiislamu na mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Mataifa. Kuna pia matumizi kama lugha ya kidini katika Uislamu.

Hivyo Kiarabu ni mojawapo ya lugha muhimu sana duniani ikisomwa kwa viwango tofauti na mamilioni ya waumini Waislamu wakielekea kujifunza na kuelewa kitabu cha Korani. Kama lugha ya kidini ina athari na taathira kubwa juu ya lugha nyingi ulimwenguni na juu ya ustaarabu na utamaduni wa watu na makabila tofautitofauti walio Waislamu.

Kiarabu kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiarabu.

Ni lugha yenye utajiri mkubwa wa misamiati (maneno), ufasaha mkubwa wa misemo na udhibiti mkubwa wa sarufi na nahau.

Ni lugha iliyokusanya aina nyingi za mithali na mafumbo, na ina utamaduni mkubwa wa nyimbo, mashairi na misemo, nayo inakubaliwa na watu wengi duniani kuwa lugha yenye utamu wa matamshi na uzuri wa lafudhi.

Kwa kuwa Qurani Tukufu na Hadithi za Mtume Muhammad na Mashairi ya zama za Ujahili ndio yenye kudhibiti lugha hii isitetereke wala kubadilika na kupotea kama lugha nyingine nyingi, leo, baada ya miaka zaidi ya elfu, imebaki thabiti kama ilivyokuwa wakati ilipoandikwa Qurani, na mabadiliko yoyote yaliyotokea hayana uhusiano na lugha yenyewe ya Kiarabu, bali yana uhusiano na lahaja na vilugha mbalimbali zinazotumika na Waarabu wa sehemu fulani ya nchi au mji. Ama lugha rasmi ya Kiarabu basi imedhibitika kulingana na Qurani na Sunnah, ili maandishi hayo yaendelee kufahamika milele.

Leo, Kiarabu ni lugha ya sita ulimwenguni kwa wingi wa wanayoitumia kila siku katika maisha yao, baada ya Kichina, Kihindi, Kihispania, Kiingereza na Kibengali.

Umuhimu wa lugha hii unazidi kukua kila siku kwa sababu ya kutumika kwenye maeneo ya katikati ya ulimwengu baina ya mabara ya kale (Afrika, Asia na Ulaya) na mabara mapya ya ulimwengu (Amerika ya Kaskazini na Kusini).

Kiebrania

Lugha ya Kiebrania (עברית ‘Ivrit, matamshi ya kisasa ?) ni moja ya lugha za kisemiti na moja kati ya lugha mbili za kitaifa nchini Israel (pamoja na Kiarabu). Ni kati ya lugha za kale zaidi duniani.

Kiebrania kwa kawaida huandikwa kwa herufi za Kiebrania. Mwandiko huu ni wa konsonanti hasa, kwa kuwa mara nyingi vokali haziandikwi kutokana mfumo wa lugha yenyewe.

Kiebrania ni lugha iliyotumika kuandikia Torati na sehemu kubwa ya maandiko mengine ya Biblia ya Kiebrania. Sehemu hiyo ya Kiebrania pamoja na sehemu ndogo ya Kiaramu huitwa "Tanakh" katika mapokeo ya Kiyahudi na imo katika Agano la Kale ya Biblia ya Kikristo.

Lebanoni

Lebanoni (kwa Kiarabu: لبنان ) ni nchi ndogo ya Mashariki ya Kati katika Asia ya Magharibi kando ya Bahari ya Mediteranea.

Imepakana na Syria na Israel.

Makabila ya Israeli

Makabila 12 ya Israeli (kwa Kiebrania בני ישראל, Bnai Yisraʾel, yaani Wana wa Israeli) waliunda taifa la lugha ya Kisemiti katika Mashariki ya Kati, wakiishi katika sehemu kubwa ya nchi ya Kanaani kati ya karne ya 15 KK na karne ya 6 KK), halafu wakawa wanaitwa Wayahudi na Wasamaria.

Biblia inaeleza kuwa makabila hayo yalitokana na wana wa kiume 12 wa babu Yakobo, bin Isaka na mjukuu wa Abrahamu. Ni Yakobo aliyepewa kwanza jina la Israeli.

Majina ya watoto hao na ya makabila yaliyotokana nao ni: Reubeni (babu), Simeoni (babu), Lawi (babu), Yuda (babu), Dan (babu), Naftali (babu), Gad (babu), Asheri (babu), Isakari (babu), Zebuluni (babu), Yosefu (babu) (wazao waligawanyika katika makabila mawili, kutokana na watoto wake Manase (babu) na Efraim (babu)), Benyamini (babu).

Mashariki ya Kati

Mashariki ya Kati (kwa Kiingereza Middle East) ni namna ya kutaja sehemu kubwa ya Asia ya Magharibi pamoja na Afrika ya kaskazini-mashariki, hasa Misri.

Kwa kawaida nchi zifuatazo huhesabiwa humo:

Nchi za Bara Arabu, zikiwa pamoja na Saudia, Yemen, Oman, Falme za Kiarabu, Katar na Kuwait,

Nchi za Shamu ya kihistoria, zikiwa pamoja na Syria, Lebanon, Israel na Palestina, Yordani

Iraq

Uajemi

Uturuki

Misri (ambayo iko upande wa Afrika isipokuwa rasi ya Sinai)Nchi hizo zinatajwa pamoja kwa sababu zina historia ya pamoja na utamaduni wa karibu.

Palestina

Palestina (kwa Kiarabu: فلسطين‎ filasṭīn, falasṭīn; kutoka Kilatini: Palaestina; kwa Kiebrania: פלשתינה Palestina) ni jina la eneo lililoko upande wa Mashariki wa Bahari ya Mediteranea kati ya mkingo wa bahari hiyo na mto Yordani.

Syria

Syria au Siria (kwa Kiarabu: سوريا au سورية ) ni nchi ya Mashariki ya Kati au Asia ya Magharibi.

Imepakana na Lebanon, Israel, Yordani, Iraq na Uturuki.

Kuna pwani kwenye bahari ya Mediteranea.

Nchi inatajwa pia kwa jina la "Shamu" katika maandiko ya Kiswahili, ingawa neno hili lamaanisha zaidi eneo la kihistoria ambalo lilikuwa kubwa kuliko Syria ya leo.

Uyahudi

Uyahudi ni mojawapo kati ya dini za kale za binadamu, lakini jina hilo lilienea baada ya makabila mengi ya Israeli kutoweka, hata wakabaki karibu watu wa kabila la Yuda tu.

Uyahudi (Yuda) ni pia jina la kihistoria la sehemu ya kusini ya nchi ya Palestina au Israel.

Kwa jumla kuna namna mbili za kuangalia Uyahudi: ama kama dini au kama taifa. Namna zote mbili huchanganyikana na kutumiwa pamoja mara kwa mara.

Kuna Wayahudi wanaojitazama raia wa nchi fulani na Uyahudi wao ni katika imani tu. Kuna Wayahudi wengine wanaosema hawafuati dini ya Kiyahudi wala hawaamini lakini wanajisikia kuwa Wayahudi kwa sababu ya ukoo na pia desturi za utamaduni wao.

Wafuasi wa dini hiyo huitwa "Wayahudi" hata wasipokuwa na asili ya taifa hilo.

Hata wakati ambapo idadi yao ilikuwa ndogo duniani, imani yao ilikuwa na athira kubwa. Wataalamu wengine huuita "dini mama" ya Ukristo na Uislamu.

Siku hizi wako karibu milioni 15 duniani kote, hasa nchini Israel na Marekani.

Wayahudi

Wayahudi (kwa Kiebrania יְהוּדִים, Yehudim) ni kundi la kikabila na la kidini lenye asili yake katika eneo la Israeli ya Kale (Mashariki ya Karibu). Kabila la Kiyahudi, taifa la Kiyahudi na dini ya Kiyahudi yote yana uhusiano wa karibu sana, kwa sababu Uyahudi ndio dini ya jadi ya watu wa taifa la Kiyahudi

Wanaobadilika kuwa Wayahudi, ambao hadhi yao kama Wayahudi katika kabila la Kiyahudi ni sawa na wale ambao wamezaliwa kuingia kabila hilo, wameingizwa ndani ya kundi la watu wa Kiyahudi tangu jadi.

Katika utamaduni wa Kiyahudi, ukoo unarudi nyuma hadi kwa mababa wa Biblia kama vile Abrahamu, Isaka na Yakobo katika milenia ya 2 KK.

Wayahudi wamefurahia enzi tatu za uruhu wa kisiasa katika nchi yao ya nyumbani, Nchi ya Israel, mara mbili wakati wa historia ya kale, na mara nyingine tena, kuanzia mwaka wa 1948, wakati ambapo taifa la kisasa la Israeli lilipoanzishwa. Enzi ya kwanza ilianza mnamo mwaka wa 1350 hadi 586 KK, na ilijumuisha vipindi vya Mahakimu, Milki iliyoungana na Miliki zilizogawanywa za Israeli na Yudea, na ilisha wakati wa kuharibiwa kwa thehebu la kwanza la Solomoni.

Enzi ya pili ilikuwa kipindi cha Milki ya Hasmonea iliyoanza mnamo mwaka wa 140 hadi mwaka wa 37 KK. Tangu kuharibiwa kwa Thehebu la Kwanza, nchi geni ndizo zimekuwa kama nyumbani kwa Wayahudi wengi wa Dunia. Isipokuwa katika taifa la kisasa la Israeli, Wayahudi ni wachache katika kila nchi wanamoishi, na mara nyingi wameteswa katika kipindi chote cha historia, kusababisha idadi yao kupanda na kushuka katika karne zilizopita.

Yerusalemu

Yerusalemu (mara kwa mara pia Kudisi) (kwa Kiebrania ירושלים, Yerushalayim, kwa Kiarabu: القدس, al-Quds) ni mji wa Mashariki ya Kati wenye pande mbili. Kwa upande mmoja ni mji mkuu wa Israel. Kwa upande mwingine Yerusalemu ya mashariki inatazamiwa kuwa mji mkuu wa Palestina, ingawa imetawaliwa na Israel pia tangu 1967. Israel imetangaza tangu mwaka 1980 Yerusalemu yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi za dunia hazikubali azimio hilo, hivyo balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Yerusalemu.

Yerusalemu ina historia ndefu sana.

Yesu

Yesu (kwa Kiebrania יֵשׁוּעַ, Yeshua, kifupisho cha יהושע‎, Yeoshua, yaani "Mungu anaokoa") alikuwa Myahudi mwanamume aliyeishi miaka 2000 hivi iliyopita (labda 6 KK - 30 BK).

Alizaliwa na bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, huko Bethlehemu ya Uyahudi. Maisha yake yalikuwa ya pekee kwa kuwa alifahamu vitu vingi kwa mfano: sheria hata kuwazidi walimu wa sheria japokuwa hakusomea sheria. Alifanya pia maajabu mengi.

Ndiyo maana leo hii zaidi ya nusu ya wanadamu wote wanamuamini kuwa Mwana wa Mungu (ndio wanaoitwa Wakristo) au walau nabii (hasa Waislamu).

Kutokana na umuhimu wake katika historia ya binadamu, kwa kawaida miaka yote inahesabiwa kuanzia ujio wake (ulivyokadiriwa na Denis Mdogo kimakosa katika karne ya 6).

Yordani

Yordani (pia: Jordan, Jordani; kwa Kiarabu; الأردنّ "al-urdun") ni ufalme wa Kiarabu katika Mashariki ya Kati.

Jina la nchi limetokana na mto Yordani ambao ni mpaka wake upande wa magharibi na Israel na eneo la Palestina ya leo.

Jina rasmi ni Ufalme wa Kihashemi wa Yordani (kwa Kiarabu: المملكة الأردنية الهاشمية ) kutokana na familia ya kifalme.

Imepakana na Syria, Iraq, Saudi Arabia, Palestina na Israeli.

Ina pwani fupi kwenye Ghuba ya Aqaba ya Bahari ya Shamu.

Mji mkuu ni Amman.

Yordani (mto)

Yordani (kwa Kiebrania: נהר הירדן nehar hayarden; kwa Kiarabu: نهر الأردن nahr al-urdun) ni mto mdogo katika Mashariki ya Kati lakini ni kati ya mito inayojulikana sana duniani kwa sababu imetajwa mara nyingi katika Biblia.

Hivyo katika dini za Uyahudi na Ukristo Yordani ina maana ya pekee: kwa Wayahudi unakumbusha tukio la Yoshua kuwaongoza babu zao kuuvusha pakavu wakati wa kuvamia nchi ya Kanaani. Kwa Wakristo unakumbusha pia ubatizo wa Yesu kwa mikono ya Yohane Mbatizaji.

Kwa sehemu kubwa ya njia yake uko chini ya usawa wa bahari na ni mpaka kati ya ufalme wa Yordani upande wa mashariki na maeneo ya Palestina na Israel upande wa magharibi.

Chanzo cha Yordani ni mito minne inayobubujika karibu na mlima Hermoni mpakani kwa Israel, Lebanon na Syria.

Mito ya chanzo inaungana katika Israel ya kaskazini.

Yordani hupita eneo la Galilaya inapounda ziwa Genesareti na baada ya kutoka hapo inatelemka kwa kupindapinda mara nyingi hadi Bahari ya Chumvi.

Mdomo wake uko m 400 chini ya usawa wa bahari, hivyo Yordani ni mto wa pekee kabisa duniani.

Kiasi cha maji kwenye sehemu ya kusini ya mto kimepungua sana kwa sababu Israel inavuta sehemu kubwa ya maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu katika miji yake.

Bonde la Yordani ni sehemu ya kaskazini ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki linaloendelea katika bonde la Araba na kupita Bahari ya Shamu hadi kuonekana tena Eritrea.

Yuda (ufalme)

Ufalme wa Yuda (kwa Kiebrania מַמְלֶכֶת יְהוּדָה, Mamlekhet Yehuda) ulikuwa nchi ya Mashariki ya Kati katika karne ya 10 KK hadi karne ya 6 KK.Mara nyingi unaitwa ufalme wa Kusini kwa sababu ulitokana na mgawanyiko wa Ufalme wa Israeli ulioendelea upande wa kaskazini.

Ufalme huo uliongozwa daima na ukoo wa Daudi, isipokuwa miaka 6 (842 KK - 837 KK) aliposhikwa utawala malkia Atalia, binti au dada wa mfalme wa Israeli Ahabu. Hata hivyo kwa muda mrefu watawala wa Yuda walikuwa vibaraka wa Ashuru au nchi nyingine za jirani.).

Hatimaye, chini ya mfalme Sedekia, mfalme Nebukadneza II wa Babuloni aliangamiza ufalme huo na mji mkuu wake, Yerusalemu, mwaka 587, akihamisha kwa awamu tatu wakazi wake hadi Mesopotamia.

Mwaka 539 Koreshi Mkuu, mfalme wa Persia, aliteka Babuloni na kuruhusu Wayahudi warudi kwao, si tena kama ufalme, bali kama wilaya iliyoitwa Yehud, chini ya Zerubabeli, kitukuu wa Yekonia, wa pili kuanzia mwisho kati ya wafalme wa Yuda.

Ziwa

Ziwa ni gimba kubwa la maji linalozungukwa na nchi kavu pande zote. Tofauti na bahari ni ukubwa na kutobadilishana maji na bahari kuu. Lakini maziwa kadhaa yamepewa pia jina la "bahari" hasa kama yana maji ya chumvi au kama watu wa eneo lake hawajui magimba makubwa zaidi ya maji. Mfano wake ni Bahari Kaspi katika Asia ambayo ni kubwa sana lakini hali halisi ni ziwa lenye maji ya chumvi.

Mara nyingi mito inaingia au kutoka katika ziwa.

Maziwa mengi yana maji matamu kama maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki kwa mfano Viktoria Nyanza au Ziwa Nyasa au maziwa makubwa ya Amerika Kaskazini.

Lakini kuna pia maziwa yenye maji ya chumvi kama Bahari ya Chumvi kati ya Yordani na Israel au Bahari ya Kaspi kati ya Urusi na Uajemi.

Lugha zingine

This page is based on a Wikipedia article written by authors (here).
Text is available under the CC BY-SA 3.0 license; additional terms may apply.
Images, videos and audio are available under their respective licenses.